Tuesday, January 28, 2014

HII NI AIBU-NCHINI ZANZIBAR WANAWAKE WANAVYOTESWA NA WANAUME ZAO HAPA NCHINI ZANZIBAR


Wanawake wanachukuliwa kama ni watu wa kubaki katika ndoa kutii amri za mume hata kama amri hizo siyo za haki na usawa basi mume atajidai yeye ndio yeye wala hasemezeki, heshima  zinavunja utu wa mwanadamu.
Kwa mfano, gwiji la fasahi ya Kiswahili, marehemu Sheikh Shabaan Robert katika kitabu chake “Maisha yangu na baada ya miaka hamsini” katika ukurasa wa kumi anatoa wasia kwa bintiye kwa kumwambia;
“Fanya kila hali, la mume kulikubali, ila lisilo halali, kukataa si hatia” Hapa anampa ujasiri mwanawe wa kike kutokubali mambo ya ovyo kutoka kwa mume, ana mjengea uwezo wa kuwa mwanamke na mama shupavu katika maisha ya ndoa yake na kuweza kukabiliana na familia.
Matukio ya kutendewa isivyo wanawake wetu siyo mageni, wanawake wamekuwa wakipata vipigo, kuteswa na wengine kufikia hata kujeruhiwa hapa nchini Zanzibar.
Wanawake wetu hapa nchini  Zanzibar wamekuwa wakifanya kazi ngumu kama punda, wana mzigo wa kuhudumia familia, wanafanya biashara, wanafanya kazi ofisini huku wakisubiriwa kupika, kuchota maji, wanabeba mimba na kujifungua na wakati mwingine hata hayo matunzo ya mama mjamzito hayapati hasa wanawake wa vijijini. Wakati mwanamume au mume yeye anacheza bao,karata,keraam,mpira usio na mshahara N.K.
Katika sehemu za mashamba Unguja na Pemba, hapa nchini Zanzibar wanawake wanalima, wanapanda, wanapalilia, wanachuma karafuu huku wengine wakianguka na wasipofikisha vyakula vinavyotakiwa katika meza au mkeka basi, anapata matusi na hatimaye kuambulia kipigo cha nguvu je hivi ndivyo tunavyo wapenda wake zetu...? je hivi ndivyo ulivyo muambia wakati unamuowa kuwa utatafuta kila kitu na kama hukuleta utapata kichapo cha nguvu...??
Katika utafiti uliofanywa na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanganyika (TAMWA) katika Wilaya ya Mjini, Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, kati ya Novemba hadi Desemba mwaka jana, nchini Zanzibar kuna matukio kadhaa ya wanawake kupata vipigo kutoka kwa waume zao.
Ijapokuwa TAMWA katika utafiti huo wanasema kwamba hulka ya kuwapiga wanawake siyo matukio maarufu sana, ukweli ni kwamba wanawake wengi wa nchini Zanzibar ni wasiri mno, hata akipigwa au kuteswa hawi wazi kutangaza.
Mathalan mmoja ya wanawake aliyehojiwa Mtaa wa Kwamtipura, analalamikia hulka ya mumewe ya kumpiga mara kwa mara hasa pale anapodai huduma muhimu kama chakula na ikiwa akimweleza upungufu basi inakuwa nongwa na sababu ya kuanza kupokea vipigo..!!!!
Mwanamke huyu hivi karibuni alipokea kipigo pale aliposema kiwango cha chakula alichoachiwa ni kidogo na hakiwezi kumtosha, ndipo mume wake alianza kumfokea kwa maneno machafu na kuanza kumpiga jambo ambalo lilimfanya mwanamke huyo kukimbilia kwa Sheha (jina kapuni) kwenda kujisalimisha.
Wanawake wanaopata vipigo kwa hakika ni wengi, lakini wamekuwa wakitofautiana kutokana na sehemu hadi sehemu. Wapo wanaopigwa kwa madai ya kudai haki za msingi za mke ikiwamo kupatiwa huduma za mahitaji ya chakula, mavazi,usaidizi wa kulea watoto na hata kufanya kazi.
Miongoni mwa sababu za kushamiri kwa vitendo vya kupigwa wanawake na waume zao ni pamoja na wivu wa mapenzi, ulevi, kugombania watoto na mali na kuporomoka kwa maadili katika jamii. Akizungumzia hilo, Sheha (jina kapuni) anasema mara nyingi chanzo cha kipigo ni wanaume ambao wanawapiga wake zao wanapolalamikia haki zao.
Lakini anakitaja chanzo chengine ni ulevi, na hili limejitokeza sana katika Shehia yake ambapo amekuwa akilalamikiwa mara nyingi na wanawake kupigwa kwa sababu ya ulevi wa waume zao
Maelezo hayo yanasadikiwa pia na Makadhi wa Mahakama za Kadhi wilaya, Afisa wanawake na watoto wilaya na hata Polisi ambao wote kwa nyakati tofauti wanaeleza sababu za wanawake kupigwa katika ndoa na hata wale wasiokuwa katika ndoa.
Sababu kubwa inayozifanya kesi hizi zisiripotiwe ni wanawake kuona aibu, na upigaji huo kuchukuliwa kama adabu ya kawaida tu anayopewa mwanamke kwa sababu ya kukosea.
Pia wanawake licha ya kuwa wanaumizwa vibaya lakini wanakataa kutoa taarifa kwa kuogopa kuvunjika kwa ndoa zao. Hapa hatupaswi kuwatupia lawama wanawake kwani ni mfumo ndio uliowafikisha hapo walipo wanawake kuonekana kuwa hawana sauti katika jamii.
Katika utafiti huo wa TAMWA, ripoti inasema kwamba katika kipindi cha kuanzia mwezi Juni mwaka 2011 hadi Machi mwaka 2012 kuna matukio matano ya wanawake kupigwa na waume zao na kuripotiwa Polisi lakini wanawake waliofikwa na mkasa huo wapo wengi isipokuwa hawafiki katika vyombo vya kisheria na kutowa habari hizo za upigwaji.
Mbali ya hao wanaokwenda vituo vya Polisi na baadhi ya wakati kesi hizo kumalizwa kienyeji, wengine wanakwenda katika Mahakama ya Kadhi kudai talaka baada ya kuchoshwa na vipigo na janadume levi.
Kuna kesi 10 zimeorodheshwa katika mahakama hizo ambapo walalamikaji(wanawake) wanataka kuvunja ndoa wakiepusha miili yao kugeuzwa ngoma na waume zao.
Wakizungumzia kadhia wanayopata wanawake hapa nchini Zanzibar kwa mtazamo wa kidini, viongozi wa dini tafauti wanasema kwamba dini haijatoa ruhusa kwa wanaume kumpiga mkewe bali wanaume wanapaswa kuishi na wake zao kwa mapenzi na huruma kwani wao ndio walinzi na walezi wa familia.
Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA), Dk. Sheikh Issa Ziddy r anasema “Uislamu haujaruhusu kwa hali yoyote udhalilishaji ingawa suala la kumpiga mwanamke limetajwa katika Quraan na mafunzo ya Mtume kuna hadithi zinazokataza mtu kumdhuru mwenzake”
Anasema kuna masharti yamewekwa kabla ya mume kufikia hatua ya kumwadabisha mkewa, lakini kabla ya kufikia hatua ya kumpiga kipigo kisichodhuru mume anatakiwa kutimiza mambo matano ambayo ni kuwa mume haruhusiwi kumpiga mkewe kwa kosa lolote hadi kosa hilo liwe kubwa na uzito wa pekee.
Pia kabla ya hatua ya kumpiga anapaswa kwanza kumpa nasaha mkewe kwa kosa alilotenda na sharti la pili ni kumpa mawaidha amma yeye mwenyewe au atafute mtu aje kumpa mawaidha. Sharti la tatu ni kumkumbusha mara kwa mara huku sharti la nne kumhama malazi yaani kumuacha akalala peke yake sio mume utoke nyumba ukalale kwengini laaa nyumba hiyo hiyo ila usilale nae kitanda kimoja, sharti la tano kwenda kushitaki kwa wazee au katika vyombo vya sheria ikiwemo kwa Kadhi na viongozi wa dini na la sita ndio kumpiga, lakini kipigo ambacho hakitomdhuru huku sharti la kumpiga mwanamke hutakiwi kumpiga ukiwa na hasira.
“Ukishawekewa masharti kama hayo matano sharti la mwisho ikiwa mke hasikii ndio umeruhusiwa kumpiga lakini unatakiwa usimpige ukamuumiza wala usimpige ukiwa na hasira lakini hapo hapo unaambiwa hupaswi kumdhuru mwengine basi ndio baadhi ya wanazuoni husema kupiga haijaruhusiwa kwa mantiki hiyo” aliongeza Sheikh Ziddy.
Hakuna mwanamke ambae amehojiwa akasema kuwa mumewa kabla ya kufikia kumpiga amefuata maagizo hayo ya dini kwa upande wa waumini wa kiislamu zaidi ya kujiona wao ndio wenye uwezo wa kufanya watakalo kwa kumpiga mwanamke kwa nguvu na kumuumiza vibaya.
Kwa upande wa dini ya Kikristo, Father Emmanuel Masoud wa Kanisa la Anglikan anasema kuwa hakuna andiko linalofundisha kwamba mwanamme ampige mke wake bali wanaume wanahimizwa kuwapenda na kuwatunza wake zao kama wanavyojipenda wao wenyewe na kumpa mke heshima ili maombi yao yakubalike kwa Mola.
Father Emmanuel anasema tatizo la kupiga wanawake ndani ya wakristo lipo kutokana na mapokeo ya kimila hasa mfumo dume na mfumo jike, kuna baadhi ya makabila kama mume hampigi mkewe anaonekana hampendi au anaambiwa ametawaliwa na mkewe.
Father Emmanuel anasema wakristo wanaungozwa na kitabu kitakatifu cha Biblia na wamekatazwa kuwapiga wanawake na wamesisitizwa kuishi nao kwa wema ili waombi yao yakubaliwe.
Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, moja ya mambo ambayo yanawaumiza wanawake karibu kote duniani ni ukiukwaji wa haki za binadamu wanazofanyiwa na matokeo ya hayo ni maumivu ya kimwili na kisaikolojia wanayopata wanawake.
Wanawake wanateseka katika vita, katika matukio ya nchi nyengine serekali haziwajali wanawake kama nchi yetu ya Zanzibar haiwajali wanawake kabisa, wengine wanakufa kwa njaa, kwa kukosa maji na huduma nyengine. Inakisiwa kuwa asilimia 80 ya wakimbizi wote ni wanawake waliokimbia machafuko ya kisiasa, vita na matukio mengine.
Huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo(DRC) Mapigano yameacha athari kubwa kwa jamii, wakina mama na watoto ndio wanaopatwa na majanga kama hayo yanayosabishwa na vita wengi wao hivi sasa wanaishi katika maisha ya dhiki wakiwa wakimbizi, huko nchini Somalia nako pia Mapigano yanaendele kuathiri kukubwa kwa jamii, wakina mama na watoto ndio wanaopatwa na majanga kama hayo yanayosabishwa na vita wengi wao hivi sasa wanaishi katika maisha ya dhiki wakiwa wakimbizi.
Nchi ya Zanzibar nayo haikuwa nyuma katika masuala ya kuathirika kwa wanawake na matukio ya machafuko ya kisiasa. Mwaka 2001 wanawake kadhaa walifanyiwa vitendo vya kikatili, wengine walikimbia nchi kwenda Shimoni Mombasa nchini Kenya kunusuru maisha yao.
Ni Wanawake hao hao wanaowapa vipigo hapa nchini Zanzibar ndio wanaokuwa mstari wa mbele katika kuwachagua viongozi mbalimbali wa kisiasa na matumbo yao makubwa kama majungu ya biriyani ya tausii, kwenye mikutano ya vyama vya kisiasa ni wanawake ndio wanaojaza uwanja.
Wanawake wa nchi ya Zanzibar walijitolea mali na maisha yao kuunga mkono, juhudi za kisiasa na kijamii, wengi wao ama hawajulikani kabisa au wamewekwa kwenye kapu la sahau kwa makusudi au kwa bahati mbaya iwapo viongozi wakishaingia madarakani basi huwapiga mateke. Hawakuwa wanaume tu waliosimama mstari wa mbele katika mapambano ya kudai uhuru, bali kulikuwa na wanawake shupavu, hodari na mahiri ambao walikuwa sehemu ya kuanzishwa kwa vuguvugu la madai ya kisiasa, lakini mambo yanapokuwa mazuri wanawake wanaelezwa kazi yao ni jikoni.....!!!!!
Wengi wetu tunafahamu kwamba historia ya mapambano ya wanawake inakwenda mbali zaidi, wakati wa kutafuta uhuru ni wanawake waliojitokeza kwa wingi kwenye mikutano ya vyama vya ukombozi, wengine wakasimama kwenye majukwaa kupaza sauti za ukombozi wakiwashinda wanaume woga hata hivi sasa katika kudai mamlaka kamili ya nchi yetu ya Zanzibar wangaliye wanawake wanavyo jaza viwanja na maholi au mahali popote panapofanywa mkutano wa kutaka kuikombowa nchi ya Zanzibar katika makucha ya mkoloni mweusi Tanganyika ni wanawake huku midume mejoga ikibanza pembeni.
Katika matukio mengi ya kisiasa husikii kabisa kutajwa kwa mchango wa wanawake katika harakati za mapambano ya kudai uhuru. Hili linafanywa kwa makusudi kwani ni aina ya wanaume wanaowapiga wanawake ndio hao hao wengine wanajitumbukiza katika masuala ya kisiasa na kuhodhi madaraka.
Jambo la muhimu kwa kila mwana jamii ni kuhakikisha haki, maslahi na wajibu wa kila mmoja unatimizwa na kuheshimiwa. Elimu zaidi inahitajika kwa ngazi zote kuona kwamba wanawake waishi katika dunia ya amani na yenye kuwaheshimu Wanawake wa nchi yetu ya  Zanzibar na kwengineko ulimwenguni.

ZANZIBAR SIO NCHI WALA HAINA RAISI-NDUGU ZETU MULIO NJE KUTOWA NI MOYO SIO UTAJIRI TUMSAIDIYE NDUGU YETU MANSOOR.

IMG_5343
FREE ZANZIBAR PEOPLE FROM MKOLONI MWEUSI
Tunasikitika sana na serekali yetu ya Wauwaji wa Wazanzibari kuwa haina hata habari jinsi inavyo uwa rai wake na hata kuwajali haiwajali. Serekali hii ni domo kaya tu mapinduzi daima smz ukwakwasi. Serekali ya kitaifa uvundo mtupu hamuna lolote washenzi wakubwa kazi kujirundikia mali na wake zenu na watoto wenu basi huku watoto wa Kizanzibari na taifa la kesho linazidi kuangamia.  kwa kujivuna tu serakali hii imepindukia mpaka inaleta maendeleo hebu someni hii stori ya huyu kijana mutuonyeshe hayo ndio maendeleo...? kijana anataka millioni ishirini tu makelbu nyie ndani ya baraza la wawakishi mamillioni mangapi mumejirundika millioni ishirini kwa nyinyi ni kama elfu mbili tu lakini wapi nyinyi sio watu wala binadamu nyinyi ni wanyama hatari na nyoka wenye sumu kali sana ndio maana mumekazania mapinduzi daima makelbu nyieee. Mumeharibu mabillioni mangapi kwa sherehe zenu za mapinduzi watu kufanya laana na machafu usiku kucha huku mambo muhimu kama haya utasikia serekali hai pesa kelbu wakubwa nyiee.muko bizi kuhonga na kulisha watu mavyakula na ukiritibwa kwenye jimbo la kiembesamaki pesa munazivuruga huyu kijana na wenzake wengine wengi na rai wengi wanalala na njaa na kuteseka na maradhi nyinyi sio wetu nyinyi astahafiru laaa hata sijuwi niwaite nini midubwana nyiee.
Salma Said, 
Ni mwenye furaha usoni mwake, huwezi kuamini kama ni mgonjwa huwezi kukubali kama ana machungu ndani ya moyo wake kwa kuwa sura yake ni ya kutabasamu wakati wote na kuonesha matumaini ya kuishi kwa amani lakini utagundua tu pale utakapomsikiliza kwa umakini sana katika maelezo yake na ukimtulizia jicho ndipo utakapogundua kama kweli kijana Mansoor Hamad Saleh (21) ana majonzi na maumivu makali anayoyapata katika kiwiliwili chake.
Ni miaka mitatu sasa tokea Mansoor alipoanza kulala kitandani kutokana na matatizo ya kupooza miguu yake yote miwili chanzo chake khasa cha ulemavu huo kilikuwa ni kuanguka juu ya mnazi huko Maangwe Wete Pemba alipokuwa amepanda kwa ajili ya kuangua nazi kwa ajili ya matumizi ya nyumbani kwao.
Mansoor ni mwanafunzi wa kitatu cha pili ambaye alikuwa akijitayarisha na kufanya mitihani lakini kwa bahati mbaya sana kabla ya kuanza tarehe za mitihani alipata mtihani mkubwa wa kuanguka kutoka juu ya mnazi hadi chini na kusababisha matatizo makubwa ya kumlaza kitandao hadi leo hii akiwa hana matumaini tena katika maisha yake.
Hata hivyo Mansoor anajipa moyo kwamba iwapo atatibiwa na atafanikiwa kupata fedha za kumfikisha nchini India ataweza kurejea katika hali yake ya kawaida na amekuwa akiomba apate matibabu hayo ili aweze kurejea shuleni kuendelea na masomo yake kama kawaida.
Awali Mansoor alipoanguka kutoka juu ya mnazi miaka mitatu iliyopita alikimbizwa katika hospitali ya Chake Chake Kisiwani Pemba na alilazwa hapo kwa muda wa mwaka mmoja chini ya uangalizi wa Daktari Shaaban wa hospitali hiyo kabla ya kusafirishwa na kuletwa Unguja katika Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja kwa amtibabu zaidi lakini licha ya matibabu hayo ya mwaka mzima hakuweza kupata nafuu na bado yupo kitandani.
Kwa kuwa ni kijana mdogo hapendi kulala muda wote na amekuwa akipenda sana kujishughulisha ingawa hawezi lakini anajilazimisha kukaa ingawa kwake yeye ni vigumu kukaa katika kiti muda mrefu lakini amekuwa akijaribu kukaa na kulala mara kwa mara.
“Napenda niendelee kusoma lakini siwezi kwenda skuli na hiki kigari changu kwa sababu kila wakati naumia sana mgongo wangu kwa hivyo inanibidi kila wakati nilale kidogo ninyanyuke nikae kidogo nikale kidogo hivyo hivyo kutwa nzima na nikijilazimisha basi naumia sana” alisema huku akionesha kukunja uso kwa maumivu.
“Sehemu ya kiuno hadi miguu kwenye nyayo iliathirika na kutofanya kazi na Ex Rays zinaonesha kuwa ameumia maeneo ya uti wa mgongo” imesema ripoti yake ya hospitali.
Licha ya matibabu aliyofanyiwa Mansoor alipatiwa madawa mbali mbali ya kuamsha hisia za mwili wake na kuondosha maumivu, kulazwa katika sehemu maalumu ili kunyoosha mgongo wake vile vile kufanyiwa mazoezi mepesi ya kusimamishwa ili viungo vyake viweze kufanya kazi katika kipindi chote cha kuumwa kwake lakini matibabu hayo hayajaweza kuleta mafanikio.
Mansoor baada ya kufanyiwa vipimo vya Computer Tomography Scan (CT SCAN) vinaonesha athari aliyoipata katika mgongo wake anahitajika kusafirishwa na kupelekwa India kwa matibabu kwani ameumia katika uti wake wa mgongo.
Kwa mujibu wa maoni ya madaktari wameshauri Mansoor kupelekwa India kufanyiwa operesheni kwa kuwa operesheni yake haiwezi kufanyika hapa ncini Tanzania na hivyo kila anapoendelea kukaa madhara yanaweza kuongezeka zaidi.
Mansoor anahitaji kusafirishwa kupelekwa nchini India kwa matibabu na kwa mujibu wa madaktari waliomchunguza wanasema ni jumla shilingi millioni 20 zinahitajika kwa makisio ya matibabu yake ya kumfikisha nchini humo.
Makisioa ya fedha hizo ni pamoja na gharama za usafiri kutoka Zanzibar hadi India, vipimo vya uchunguzi, matibabu na gharama za malazi na fedha ya kufuatana na Daktari dhaZ Q1 mana atakayeweza kuondoka naye hapa nchini hadi India.
Matatizo yake makubwa kwa sasa Mansoor ni kuwa hawezi kusimama kwa vile amepata athari katika viungo vyake vya chini (Nyayo) kukosa hisia na pia hawezi kuzuwia choo kutokana na kuathirika kwenye uti wa mgongo.
Wazazi wa Mansoor wamekuwa wakitafuta misaada mbali mbali kutoka kwa watu lakini bado hawajafanikiwa kukusanya kiasi chochote cha fedha licha ya kuandika barua kadhaa kwa wafadhili “Sisi wazee wake Mansoor baba na mama wazazi sote ni masikini sana hatuna uwezo wa kumsafirisha mtoto wetu kwa ajili ya matibabu, mtoto wetu anakabiliwa na ulemavu wa kudumu, tunaleta kilio chetu kwa lengo la kupata msaada wa tiba ya mtoto wetu huyu wa kwanza” imesema moja ya barua yao ya maombi wazee hao ya hivi karibuni ambayo iliandikwa 15/9/2013.
Bi Farashuu Mansoor Mohammed ni mama mzazi wa Mansoor mwenye familia ya watoto wanane kati yao ni wanawake wawili na Mansoor ndio mtoto wake wa kwanza anashukuru kuona mwanawe upo hai bado licha ya hali mbaya na ya kusikitisha kutokana na maumivu ayapatayo mwilini mwake.
“Mwanangu alikuwa akijitayarisha na mitihani ya darasa la kumi na mbili lakini akapata mtihani huu maana na huu ni mtihani mwengine mkubwa zaidi ya huo mtihani wake wa darasani” alisema Mama Mzazi wa Mansoor, Bi Farashuu
Bi Farashuu mwenye watoto saba kati ya hao wanawake ni wawili anasema amefanya juhudi mbali mbali za kutafuta misaa kwa ajili ya kumuokoa mwanawe ili aweze kurejea katika afya yake lakini ameshindwa kutokana na familia yao kuwa masikini sana na haina uwezo wa kuchangishana fedha kwa ajili ya matibabu ya mwanawe huyo.
“Jamaa zangu wanataka kunisaidia lakini jambo kubwa wamenambia wao hata familia nzima ikichangishana haitaweza kupata hata milioni tano na ndio maana nakuwa napata wakati mgumu na wakati mwengine nachanganyikiwa nikimuona mwanangu anavyoteseka na maumivu” alisema huku akiwa na uso wa huzuni sana.
Bi Farashuu anasema mwanawe amekuwa akitaja mara kwa mara kufanya kazi iwapo atakosa matibabu na kushindwa kuendelea na kusoma hivyo angependelea kufanya kazi gereji kutengeneza magari.
Mansoor anapoletewa supu kwa ajili ya kunywa ili kurejesha afya yake amekuwa akisema bora hao kuku anaoletewa kwa ajili ya supu apewe mwenyewe aweze kuwafuga waweze kuendeshea maisha yao yeye na ndugu zake wengine.
“Mwanangu ameshakata tamaa kama baba yake na ndio maana nakhisi kama hatokuwa tena na akili ya kuendelea na masomo na ndio maana anakuwa anataja sana kutaka kufanya kazi gereji kutengeneza magari” alisema Bi Farashuu.
Ameongeza pia kusema “Aanapoletewa supu anywe basi anawaambia nileteeni hao kuku nitafuga mwenyewe kwa sababu akifuga atapata pia kuuza na watazaa wengine na hivyo atapata kuendeleza mifugo na pia atasaidia ndugu zake” alisema ambapo hivi sasa ameshapata makoo wawili kwa ajili ya kuwafuga.
Mansoor anahitaji kupata banda la kuku dogo ili aweze kuwaweka kuku wake ambao wameletewa na jamaa zake baada ya kukataa kupikiwa supu kwa ajili ya kuimarisha afya yake “Nikifuga kuku nitapata kuchinja nipate supu lakini pia nitapata pesa kwa ajili ya kuwasaidia wenzangu” alisema Mansoor.
Baadhi ya majirani wanasema maisha ya Bi Farashuu na Mume wake Bwana Hamad Saleh ni magumu wakati mume hana kazi ya kufanya Bi Farashuu anahangaika na kupika maandazi kwa ajili ya kuendeleza maisha yake na familia yake.
“Mwanadishi ngoja mimi nikuambie ukweli maana yeye mwenyewe anaona aibu kusema kwa kweli maisha yake ni magumu sana kuliko unavyomuona hapa maana ananunua unga na kukanda maandazi 20 kila siku na maandazi hayo 10 anauza na maandazi 10 anakula na wanawe kila mtoto anakula andazi moja” alisema Sada Hamed Rashid ambaye ni jirani yake.
Kufuatia hali yao ngumu ya maisha na wanataka kumtibu mtoto wao wameamua kuuza nyumba yao kwa tahamani ya shilingi millioni 30 lakini tokea wameanza kutangaza bei hadi leo hii haijanunuliwa huku baadhi ya jamaa zao wakikataa nyumba hiyo isiuzwe kutokana na kuwa watapata tabu na kukosa sehemu ya kuishi.
“Jamaa zangu wengi wamenishauri tusiiuze nyumba yetu wanasema tutapata tabu ya makaazi ya kujisitiri mimi na wanangu lakini hali ndio ngumu mtoto anateseka kwa hivyo lazima tutafte namna ya kutatua tatizo hili lakini pia ni mtihani maana hiyo nyumba pia hatujapata mteja” alisema Bi Farashuu.
Idadi ya watu wenye kupata ulemavu imekuwa ikiongezeka kufuatia kuanguka juu ya minazi lakini zaidi wanaoanguka juu ya mikarafuu ambapo baadhi yao huvunjika viungo vya miili yao na wengine kupooza na kuwa walemavu.
Kwa mujibu Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko, Nassor Ahmed Mazrui amesema ni kweli wapo watu ambao huanguka mikarafuu lakini idadi haifiki 200 kwani baadhi yao kati ya hao wanaotajwa ni wameanguka mikarafuu, Minazi na wengine wamepata ajali mbali mbali ikiwemo Vespa na Gari hivyo ndio maana idadi inaonekana ni kubwa zaidi lakini katika kipindi cha mwaka jana wizara yake imeshuhudia watu watatu walioanguka mikarafuu ambao wamepata majeraha na ulemavu.
Msomaji wa Makala hii kumbuka kwamba kutoa ni moyo na sio utajiri kwa hivyo utakachoweza kutoa wewe toa tu na kitasaidia hata kama ni shilingi elfu tano (5,000) utakuwa umemsaidia Mansoor katika matibabu yake kwani hii ni sadaka yako na utakuwa unamkopesha Mwenyeenzi Mungu na bila ya shaka utakikuta mbele ya safari Inshallah.
Mtu ambaye ataguswa na matatizo ya Mansoor awasiliane na Mwandishi wa Makala hii Salma Said kwa email muftiiy@yahoo.com au simu +255777477101 au Tigo Pesa  +255715477101

Sunday, January 26, 2014

VUAI ALI VUAI NA MBIO ZAKE ZA KUMCHAFUA MAALIM SEIF SHARRIF HAMAD-JE VUAI UNA MUONA MAALIM SEIF USINGIZINI UKILALA NDIO MAANA HUISHI KUMTAJA..?

Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, akimfariji Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai alipofika katika kijiji cha pongwe kuhudhuria maziko hayo.
Makamo wa Kwanza wa Rais wa nchi ya Zanzibar Maalim Seif Sharrif Hamad, akimfariji Muhafidhina Naibu Katibu Mkuu wa CCM nchini  Zanzibar Vuai Ali Vuai alipofika katika kijiji cha pongwe kuhudhuria maziko hayo pembeni ni Abu Jahal Borafya Jahal la Kizanzibari.

UKIFUNGUA wavuti ya google.co.tz kwenye intaneti na kuandika “Vuai Ali Vuai,” halafu ukabonyeza kitufe cha kutafuta, zitakuja taarifa zinazomhusu mtu mwenye jina hilo.
Vuai Ali Vuai ni mwanasiasa wa miaka ya kati ambaye kwa sasa anashika wadhifa wa Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha (Mapinduzi) Wauwaji wa Wazanzibari (CCM) upande wa Zanzibar.
Lakini ukishafungua na ukaangalia eneo lenye picha zake huyu mwenye asili ya kijiji cha Pongwe, Wilaya ya Kati, Mkoa wa Kusini Unguja, picha ya pili utakayoiona, baada ya ile aliyopigwa akiwa amevalia shati ya rangi kijani, ya CCM, inamuonesha Vuai akisalimiana kwa kupeana mikono na Maalim Seif Shariff Hamad kama unavyo iona hapo juu.
Picha hii imepigwa kijijini kwao tarehe 5 Novemba mwaka 2013, siku ya maziko ya baba yake mzazi, Mzee Ali Vuai. Hiyo ina maana Maalim Seif, Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), na Makamu wa Kwanza wa Rais wa nchi ya Zanzibar, alikuwa mmoja wa viongozi wa kitaifa waliohudhuria maziko ya baba yake Vuai, kijijini Pongwe Pwani.
Katika picha hii, unamuona Vuai anaitika mkono wa salamu kwa Maalim Seif kwa moyo mkunjufu kabisa, roho tulivu (roho kwatu), na usoni kwake akijenga sura yenye tabasamu kubwa. Pamoja na ukweli kwamba ile kwake ilikuwa siku ya msiba mkubwa, kwa kuondokewa na mmoja wa wazazi wake, Vuai anaonesha kama vile ni mtu aliyekutana na mtu anayemheshimu sana.
Katika hali ya kawaida, huwezi kusema kama Vuai atakuwa na shaka katika kiwango cha kumheshimu Maalim Seif. Hampati kwa umri. Hampati kwa ujuzi, uzoefu na ufundi katika siasa. Hampati hata kwa umbo. Maalim ni mrefu kwa kimo na mng’avu kwa rangi kuliko alivyo Vuai.
Vuai kwa Maalim Seif kwa mambo mengi ni kama unapozungumzia kichuguu na mlima Kilimanjaro. Vitu viwili tofauti. Vuai ni wa daraja dogo mno kwa hali hizo akilinganishwa na Maalim Seif.
Lakini amekuwa akijitokeza kama mtu anayejua sana kila jambo mbele ya Maalim Seif. Ukunjufu wa moyo aliouonesha alipokuwa akishikana mkono na Maalim Seif siku ya msiba wa baba yake kijijini Pongwe Pwani, huwezi kuupata kamwe unapomkuta akimtaja Maalim Seif kwenye medani ya siasa.
Nathubutu kusema Vuai anamuona Maalim Seif adui mkubwa. Kwa hali hiyo, pengine Vuai wala hakutarajia kuwa anayesalimiana naye mazikoni ni, Maalim Seif, angethubutu kufika Pongwe Pwani kwa lengo la kuhudhuria maziko ya baba yake.
Isitoshe, picha ya Vuai na Maalim Seif iliyopigwa kutoka kwenye uwanja wa maziko siku hiyo, kwenye mtandao huo wa google, imetangulia picha aliyopiga Vuai siku hiyohiyo na kiongozi mkubwa wa chama chake – CCM,  Ali Mohamed Shein.
Hii inawezekana isiwe na maana yoyote kwani bila ya shaka kihadhi katika jamii,  Shein ni raisi wa Kisonge na Maalim Seif ni Makamu wa Raisi wa nchi ya Zanzibar.
Kama kuhusu hadhi nyengine, poo simo; wewe msomaji utaamua mwenyewe.
Uadui aliouweka Vuai dhidi ya Maalim Seif si wa kutafuta kwa tochi. Ukimsikia Vuai akizungumza mchana kweupe, hafichi chuki yake kwa kiongozi huyo msikivu na ambaye Wazanzibari wamempa imani kubwa.
Nataka kuamini kuwa kwa Vuai, ni haramu kukamilisha hutuba yake popote anapokuwa katika medani ya siasa, bila ya kumtaja Maalim Seif. Hata pasiwe na sababu, ataitafuta tu, almuradi ataje jina la Seif Shariff Hamad.
Kwa kuwa hata waandishi wanaomtii Vuai wanalijua hili, hata asipomtaja kwa jina kamili, vikaragosi wake watalitaja tu.
Mwenendo huu inawezekana umewaambukiza viongozi wa Jumuiya ya Vijana ya CCM (UV-CCM), ambao nao ni kama vile wameapa kuishi na jina la Maalim Seif, iwe usiku iwe mchana, iwe jua iwe mvua.
Ni nani hajawahi kusikia viongozi wa UV-CCM kama Shaka Hamdu Shaka na Sadifa Juma wakimsema ovyo Maalim Seif majukwaani..? Tena mara kadhaa maneno ya vituku na vilembwe wa CCM hawa wanapomtaja Maalim Seif huwa ni makali yanayochoma moyo na kuumiza mapafu kwa anayeyasikia lakini nathani wao wanaumiya zaidi kwa kumuona Maalim Seif ndio maana hurupoka ili kupunguza maumivu walio nayo kumbe hawajuwi ndio wanazidisha maumivu ndani ya mili yao.
Wazanzibari wameyazoea sana maneno ya wajuku na vilimbwe wa CCM dhidi ya Maalim Seif. Wamekuwa wakiyachukulia kama upuuzi mtupu kwa sababu huwa mara nyingi yamekosa heshima na haya malengo wala faida yoyote kwa nchi ya Zanzibar na hata kwa Wazanzibari wenyewe pia.
Ni maneno yasiyo na maana. Ni kama yamesemwa na mtu aliyeuchapa ulevi usiku kuchaa kisha siku ya pili akakurupuka na kuhubiria watu nini unatarajia katika hutaba hiyoo..? jibu nalo wewe msomaji.
Lakini wakati sina uthibitisho kama viongozi hao wa UV-CCM huwa wanalewa kabla ya kupanda jukwaani na kuanza kumtusi Maalim Seif, inajulikana wanatema maneno yanayoashiria matusi ya nguoni kama mashangingi au majimama yanayo imbaa nyimbo za mipasho.
Vuai yeye hamtukani Maalim Seif. Sijawahi hata mara moja kusikia akimtukana. Hatoi matusi kwa maana ile ya wanavyofanya wasaidizi wake hao wa UV-CCM. Lakini kauli zake naye zinaonesha sura yake halisi Vuai kisiasa na kiumantiki.
Mwanasiasa anayechoka na asiyejitambua.
Wakati kauli za wenzake huashiria matusi ya nguoni, Vuai zake ni za kebehi na upotoshaji wa mambo. Kauli za Vuai wakati mwingine zinawataka wananchi kuamini jambo lisilokuwepo, ingawa kwake labda huwa ndio jitihada za kumbomoa Maalim Seif.
Tatizo hapa, Vuai hajajua namna ya kumbomoa kisiasa Maalim Seif. Hajapata maneno ya kutumia kumbomoa kiongozi huyu. Badala yake, anapodhani anambomoa, kwa hakika huwa anamjenga au anazindi kumjengea taswira nzuri kwa rai au wananchi wa Zanzibar.
Wiki kadhaa nyuma, Vuai aliwahi kusema Maalim Seif ni msaliti wa Wazanzibari kwa kuwashawishi wavunje Muungano wa nchi ya Tanganyika na nchi yetu ya Zanzibar.
Kwamba Vuai anasema, Maalim Seif amewalaghai Wazanzibari kuwa chini ya mfumo wa Muungano wa Serikali Tatu ndio watapata mamlaka.
Kama ninakosea, ingia ujikumbushe utakapofungua mtandao ule wa jina la Vuai Ali Vuai, ukute habari inayoeleza dhana hii.
Wakati fulani Vuai aliwahi kumtuhumu Maalim Seif kuunga mkono viongozi wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu (JUMIKI).
Kauli yake ilikuwa inajenga imani watu kwamba Maalim Seif anapalilia au kushadidia vurugu zilizokuwa zikitokea Zanzibar na CCM kutuhumu kuwa zikifanywa na Uamsho.
Vuai alikuwa anasema isingekuwa hivyo, Maalim Seif angekuwa amekanusha na kukemea viongozi wa Uamsho ambao yeye na wakubwa zake yumkini humshutumu kuwa anawasaidia katika harakati zao za kutetea haki za Wazanzibari, ambazo wao kina Vuai, wanasema ni kuvunja amani.
Vuai anamaanisha kuwa Maalim Seif akiwapa nguvu Uamsho wafanye vurugu. Vuai anajua fika kwamba hakuna hata mara moja viongozi wa Uamsho wamethibitishwa kuhusika na vurugu.
Hakuna mpaka leo hii. Wanachoendelea kukiamini kina Vuai ni propaganda yao ya kuwachafua viongozi wa Uamsho ambao wanaamini kwa kazi waliyoifanya, wamefanikiwa kuwaamsha Wazanzibari kwa kiwango cha kupigiwa mfano katika kuhimiza kutambua na kudai haki zao.
Sasa safari hii, Vuai, akiwa jukwaani tena kupokea walichoita wenyewe matembezi ya vijana wa CCM, anasema kwa njia ya kuwakampeni Wazanzibari, wasimchague Maalim Seif. Anasema hachaguliki.
Vuai anajua wazi hakuna uchaguzi kwa sasa. Kwa Zanzibar, hakuna kabisa uchaguzi ambao unahusisha ushiriki wa Maalim Seif. Kilichopo ni kampeni za uchaguzi mdogo wa kuwania kiti cha ujumbe wa Baraza la Wawakilishi, jimbo la Kiembesamaki, Wilaya ya Mjini Unguja nchini Zanzibar.
Kiti hicho kimekuwa wazi tangu mwakilishi wake, Mansour Yussuf Himid alipokosa sifa za kuwa mwakilishi katika chama cha CCM na baada ya kuvuliwa uanachama wa CCM kutokana na tuhuma za kusaliti chama kama wanavyosema wenyewe CCM.
Kwa nchi ya Tanganyika, kuna uchaguzi wa serikali za mitaa. Kama ni ushiriki, basi Maalim Seif atakuwa anashiriki kupigia kampeni wale walioomba kugombea nafasi mbalimbali katika uchaguzi huo kupitia CUF.
Sasa kama sote tunakubaliana kwamba kwa sasa hakuna uchaguzi wowote unaomhusisha mwanasiasa anayeitwa Maalim Seif Shariff Hamad, Vuai anataka watu wasimchague kwa uchaguzi upi...? Kuna kinyang’anyiro gani kinachofanyika na ambacho ameingia kugombea..?
Hakuna uchaguzi. Hakuna uwaniaji wowote kwa sasa. Lakini Vuai si mpumbavu. Ana akili. Tena, anajua anachokifanya. Na hicho anachokifanya, anajua kuwa ni cha haramu na dhulma kwa Maalim Seif. Kumchafua.
Anafanya hivyo kwasababu ya ukweli kwamba Vuai ni mwanasiasa anayechoka kwa kasi wakati Maalim Seif anazidi kung’ara na kuaminiwa. Vuai hataki kufikiri kwa akili yake. Kama anaitumia akili, basi anafikiri vibaya.
Vuai kampeni za uchaguzi hazijafika bado. Angeacha kufikiri vibaya na akatuliza akili yake na kutafuta namna vya kukiokoa chama chake na hatari ya kuanguka kibudu.
Vuai achangamke kunusuru chama chake, kwa sababu akifanya hivyo atakuwa pia anajinusuru yeye na anguko la kisiasa vilevile. Uanasiasa wake unahatarishwa na vile anavyokataa kukubali haki ilipo.
Vuai anaamini siasa za kulazimisha mambo. Siasa hizi ajuwe hazina nafasi tena zama hizi. Anaamini siasa za ulaghai, hazina nafasi. Anaamini siasa za upotoshaji, hazina nafasi na hazifai leo, siasa za chuki na kuwabaguwa watu hazina nafasi tena, siasa za kudanganya watu huku watu wakirudi majumbani wanakula mihogo yeye anachakaza pilau na biriani hazina nafasi.
Nionavyo kwa hatua hii, Vuai anachokifanya kingine ni kuinua sauti za wahafidhina wenzake wanaoshikilia mfumo wa serikali mbili uendelee. Hapa ndipo Vuai anapomchukulia Maalim Seif kama adui kwa kuwa amekuwa mstari wa mbele kuutilia shindo mfumo wa serikali tatu kama sera ya CUF tangu kilipoundwa mwaka 1992.
Bali Maalim Seif ameutaka mfumo huu kwa kuja na kitu kipya alichokiita “Muungano wa Mkataba,” akitaka washirika wawili wa Muungano, Zanzibar na Tanganyika wakae na kukubaliana upya maeneo ya ushirikiano na kuyaandikia mkataba.
Vuai na wenzake wanaamini mfumo wa serikali mbili bado unanguvu. Ni sawa yaweza kuwa hivo, lakini, kweli unauimarisha muungano kwa maana ya kuukomaza kwa wananchi kwamba unawaletea maendeleo au unazidisha kero ambazo zimekuwepo kwa miaka yote 50 ya Muungano....? yako vuai yanakuende wanao wanasoma vizuri nyumba nzuri magari pesa za kubadili mchuzi kama kawa huku mtaani watu bado wanakula ngumu wewe bado unawapa bla bla bla ungelikuwa wewe ungekubali vuai...?
Vuai anasema Maalim Seif anawashawishi Wazanzibari wavunje Muungano. Anajua hata mara moja Maalim Seif hajasema muungano uvunjwe au labda angependa kuona muungano unavunjika, isipokuwa ndio kile ninachosema, Vuai hataki mdomo wake ukauke kulitaja jina la Seif Shariff Hamad.

MAKUBALIANO YA (MoU) YATIWA SAINI KATI YA NCHI YA ZANZIBAR NA SHELL JE PESA ZITAKAZO PATIKANA ZITAJENGEWA NCHI YA ZANZIBAR AU ZITAKWENDA KWA MASULTANI WEUSI TANGANYIKA KAMA ZA TRA ZINAVYOKWENDA HUKO NA NYENGINEZO..???

mafuta_shell_nl
Wawakilishi kutoka Kampuni ya Shell International Exploration na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wakiwa katika mkutano Hague Uholanzi

Kufuatia kusainiwa kwa Mkataba wa Makubaliano (MoU) kati ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na kampuni ya kimataifa ya utafiti na Uzalishaji wa gesi (Shell) tarehe 28 Agosti 2013, wawakilishi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Shell walikutana huko The Hague, Uholanzi kwa ajili ya uzinduzi wa kamati ya utekelezaji (JIC) tarehe 19 na 20 Januari 2014.Wakati wa mkutano huo, majadiliano muhimu yalifanyika katika maeneo ya kujenga uwezo, uwekezaji wa jamii na maendeleo katika mafuta na sekta ya gesi.
JIC ilianzishwa kwa lengo la utekelezaji wa makubaliano. Makubaliano yameainisha ushirikiano kati ya Shell na Zanzibar katika mafuta na sekta ya gesi na inaelezea shughuli za awali.
“Tunategemea ushirikiano wa muda mrefu na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar juu ya maendeleo ya sekta za mafuta na gesi Zanzibar,” alisema Axel Knospe, mwakilishi Shell visiwani Zanzibar. “

Friday, January 24, 2014

NCHI YA ZANZIBAR HAITAMBULIKI KATIKA UMOJA WA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI EAC IMO NDANI YA TUMBO LA MKOLONI MWEUSI TANGANYIKA.


SERIKALI ya Wauwaji (Mapinduzi) ya Zanzibar imesema kuwa msimamo wake katika suala la uwanachama wa  Jumuiya ya Afrika ya Mashariki ni ule ule uliotolewa na Rais wa Jamhuri ya Tanganyika Dkt Jakaya Mrisho Kikwete wakoloni weusi Tanganyika.
Waziri wa Nchi Afisi ya Rais Ikulu na Utawala Bora Dkt Mwinyihaji Makame Mwadini aliwaambia wajumbe wa baraza la wawakilishi katika kikao kilichoanza jana huko Chukwani nje kidogo na Mjini Magharib wa nchi ya  Zanzibar.
Akijibu suali la mwakilishi wa nafasi za wanawake (CCM) Mgeni Hassan Juma, Waziri huyo alisema kuwa nchi ya  Zanzibar ni sehemu ya Jamhuri ya Mungano na nchi ya Tanganyika msimamo wake katika suala hilo ni ule ule wa Tanganyika  uliotolewa na Rais Kikwete wa nchi ya Tanganyika.
“Serikali ya Jamhuri ya Tanganyika tayari imeshatowa msimamo wake kuhusu mambo yaliyojitokeza hivi karibuni juu ya uwanachama wake wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, msimamo ambao ulitolewa na Rais Kikwete Raisi wa nchi ya Tanganyika katika hotuba yake aliyoitowa katika bunge la nchi yao mjini Dodoma Nchini Tanganyika ((Giningi ya kuuliwa na kufukuzwa viongozi wa nchi ya Zanzabar wasio tii amri ya MKOLONI MWEUSI TANGANYIKA)) Novemba 7 mwaka jana hivyo sisi nchi ya Zanzibar hatuwezi kwenda kinyume chake”, alisema Waziri.((Wazanzibari mnasiki kama sio ukoloni ni nini..?))
Alisema kuwa katika msimamo huo Rais Jakaya Raisi wa nchi ya Tanganyika alisisitiza kuwa Jamhuri ya Tanganyika haijajitowa na wala haina lengo na kujitowa katika mtangamano wa  Jumuiya ya Afrika Mashariki hivyo mambo yaliojitokeza yatamalizwa kwa njia ya kidiplomasia.
Mwakilishi huyo alitaka kujua Wazanzibari na nchi yao ya Zanzibar wanaelezwa nini kuhusiana na suala zima la Afrika Mashariki ambapo hivi karibuni kumekuwepo na hisia kuwa uwanachama wa nchi ya Tanganyika katika Jumuiya hiyo unayumba na kuwa kumeshakuwa na mikutano mbali mbali inayohusisha wanachama wake wa EAC ikiendelea wakati nchi ya Tanganyika haihusishwi  na kwa kuwa nchi ya Zanzibar inaingia katika Jumuiya hiyo  chini ya kivuli cha MKOLONI MWEUSI TANGANYIKA.
Aidha alitaka kujuwa iwapo nchi ya Tanganyika itajitowa  kwenye Umoja huo nchi Zanzibar itakuwa na nafasi gani katika kutoa ushauri na katika kuendeleza malengo na dhamira ya umoja huo wakati nchi ya Zanzibar haitambuliki katima umoja huwo imefichwa ndani ya tumbo la MKOLONI MWEUSI TANGANYIKA.

Monday, January 20, 2014

ALIVYOTAKA MZEE KARUME SIO ANAVYOFANYA SHEIN

MZEE KARUME
1)MAJI BURE
2)ELIMU BURE NA SKULI NZURI.
3)RAI WAISHI KATI NYUMBA NZURI
4)KUONDOWA UBAGUZI
5)ZANZIBAR IWE NCHI NZURI NA YENYE MAENDELEO N.K.

SHEIN
1)MAJI KWA PESA NA WALA HAYATOKI NA YAKITOKA USI W MANANE
2)ELIMU IMEKUFA SKULI ZIMEKUWA MAGHETTO NA KUJAZANA MIMBA
3)RAI MTAJIJU-MKE NA WANAGU WAWE NA MADARAKA SEREKALINI
4)UBAGUZI KAMA KAZI FITINA NDIO USISEME CCM TUKANENI MNAVYOTAKA HAKUNA WAKUWAGUSA HAPA
5)NIKIONDOKA MIMI MADARAKA BASI NA ZANZIBAR SIO NCHI TENA BALI NI KIJIJI CHA PWANI KATIKA NCHI YA TANGANYIKA


Friday, January 17, 2014

KUNANI RAISI WA NCHI YA TANGANYIKA J.M.KIKWETE KUKUTANA NA MAKAMO WA KWANZA WA RAISI MAALIM SEIF SHARRIF HAMAD WA NCHI YA ZANZIBAR FARAGHA...???

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akikutana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Ikulu jijini Dar es Salaam. Viongozi hao wamekutana na kufanya mazungumzo ya faragha kwa zaidi ya dakika 20. (picha na Salmin Said, OMKR)
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Nchi ya Zanzibar Maalim Seif Sharrif Hamad, amekutana na Rais wa Jamhuri ya Tanganyika Dkt  Jakaya Mrisho Kikwete, Ikulu leo jijini Dar es Salaam Nchini Tanganyika. Viongozi hao wamekutana na kufanya mazungumzo ya faragha kwa zaidi ya dakika 20 au tuseme wamezungumza mazungumzo ya siri peke yao kwa dakika zaidi ya 20 KUNANI.......??

DODOMA GININGI WAMEMUUWA MZEE KARUME,WAKAMFUKUZA MZEE JUMBE,MAALIM SEIF,MASOUR JE RAZA ATAPONA..????Nchini Zanzibar. Chama Cha Mmkoloni Mweusi (CCM) kimeanza kumhoji Mwakilishi wa Uzini, Mohamed Raza, kwa tuhuma atii za kugombanisha viongozi na wananchi na kushindwa kutetea misingi ya Muungano wa nchi ya Tanganyika na nchi ya Zanzibar.
Raza anatuhumiwa kufanya hayo katika matamshi anayodaiwa kuyatoa kwa waandishi wa habari kupitia mkutano wake wa Oktoba mwaka jana na mkanda wa video umetumika kama ushahidi katika kikao cha Kamati ya Siasa ngazi ya jimbo na wilaya.
Akizungumza na waandishi wa habari huko Malindi jana, Raza alisema ametakiwa kujibu hoja 16 na Kamati ya Siasa ya Jimbo la Uzini na kwamba tayari kamati imetoa mapendekezo kwa ngazi ya wilaya.
Alisema kikao cha kwanza kilikutana Oktoba 27 mwaka jana na kumtaka ahudhurie kwa madai kuwa kulikuwa na mambo muhimu aliyopaswa kuyatolea ufafanuzi kutokana na matamshi yake katika mkutano wake na waandishi wa habari.
“Niliwasilisha ombi la udhuru kutokana na kukabiliwa na safari nchini Dubai, nikaomba wanitajie maeneo ambayo hawajayafamu ili niwajibu kwa maandishi, wenzangu walikuwa wagumu na waliendelea kunijadili bila kunipa nafasi ya kujitetea,” alisema Raza.
Alisema wakati akitafakari hayo, alipokea barua nyingine ya wito kutoka Wilaya ya Kati akitakiwa ahudhurie kikao cha Desemba 13 huko Dunga na kujibu tuhuma 16. Raza aliwataja baadhi ya viongozi waliohudhuria kikao hicho kuwa ni, Hassan Mrisho Vuai, Shukuru Adam Ali, Ame Abdallah Ame, Shaaban Jabu Kitwana, Mju Silima Makame na Arada Ali Abdallah.
Wengine ni Vuai Ali Mohamed, Usi Ali Mtumwa, Salama Mussa Bilal, Khalfan Salum Suleiman, Ali Makame Usi, Mussa Ali Hassan na Haji Mkema Haji.
Raza alizitaja tuhuma zinazomkabili kuwa ni pamoja na kuzungumzia hadharani, masuala mazito na yenye utata akiwa mwakilishi wa CCM, kuhoji uhalali wa marais Dk Jakaya Kikwete na Dk Ali Mohamed Shein kuhusu kuunda Tume ya Kukusanya Maoni ya Katiba na kuitisha Bunge la Katiba.
Nyingine ni kutetea muundo wa Serikali tatu, kuwahasimisha wananchi wa nchi ya Tanganyika na wa nchi ya Zanzibar kuchukiana na viongozi wa Muungano feki.
Nyingine ni kutamka kuwa Watanganyika hawawezi kutawala nchi ya Zanzibar na kwamba wakijaribu watatawala miembe na minazi tu sio Wazanzibari.
Pia kutoa kuponda ilani ya uchaguzi inayotaka Serikali mbili akisema mwisho wake ni Kisiwa cha Chumbe.
hawa aliyo wataja Hassan Mrisho Vuai, Shukuru Adam Ali, Ame Abdallah Ame, Shaaban Jabu Kitwana, Mju Silima Makame na Arada Ali Abdallah.
Wengine ni Vuai Ali Mohamed, Usi Ali Mtumwa, Salama Mussa Bilal, Khalfan Salum Suleiman, Ali Makame Usi, Mussa Ali Hassan na Haji Mkema Haji. free zanzibar people tumegunduwa kuwa wengi wao sio Wazanzibari bali ni mitwana ya kitanganyika iliyo vaa Uzanzibari nasi tunawajulisha kabisa tukipata mamlaka kamili mutafute paa kuishi au na nyinyi mutaishia kinuwa miguuu.

Thursday, January 16, 2014

HUTUBA YA SHEIN KATIKA SHEREHE ZA MAUWAJI YA WAZANZIBARI


Mheshimiwa Wageni wetu, Wakuu wa Nchi na Serikali na
Mawaziri wa Nchi Rafiki mliohudhuria hapa leo,
Mheshimiwa Dk. Jakaya Mrisho Kikwete,
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania;
Mheshimiwa Dk. Mohamed Gharib Bilal,
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania;
Mheshimiwa Mizengo Kayanza Peter Pinda,
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania;
Mheshimiwa Maalim Seif Sharif Hamad,
Makamu wa Kwanza wa Rais, Zanzibar;
Mheshimiwa Balozi Seif Ali Iddi,
Makamu wa Pili wa Rais, Zanzibar;
Mheshimiwa Mzee Ali Hassan Mwinyi,
Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania;
Mheshimiwa Benjamin William Mkapa,
Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania;
Mheshimiwa Dk. Salmin Amour Juma,
Rais Mstaafu wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi;
Mheshimiwa Dk. Amani Abeid Karume, Rais Mstaafu wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi;
Viongozi Wakuu Wastaafu Mliohudhuria;
Waheshimiwa Mawaziri wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar;
Mheshimiwa Mama Anne Makinda, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania;
Mheshimiwa Pandu Ameir Kificho, Spika wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar;
Mheshimiwa Othman Chande Mohamed, Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania;
Mheshimiwa Omar Othman Makungu, Jaji Mkuu wa Zanzibar;
Waheshimiwa Mabalozi na Wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa;
Mheshimiwa Abdalla Mwinyi, Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi;
Waheshimiwa Viongozi wa Serikali na Vyama vya Siasa;
Ndugu Wananchi, Mabibi na Mabwana;
Assalaam Alaykum,
Kwa unyenyekevu mkubwa, namshukuru Mwenyezi Mungu, Muumba Mbingu na Ardhi na vyote vilivyomo ndani yake, kwa kutujaalia uhai na uzima wa afya, tukaweza kukusanyika hapa leo kuadhimisha miaka 50 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, ya tarehe 12 Januari, 1964. Namuomba Mola wetu aibariki shughuli yetu hii iwe ya mafanikio.
Kwa niaba ya wananchi wa Zanzibar, natoa shukrani zangu za dhati kwako Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dk. Jakaya Mrisho Kikwete, kwa kuungana nasi katika sherehe zetu hizi adhimu na muhimu. Vile vile natoa shukrani kwa wageni wetu wote kutoka nje ya nchi yetu akiwemo Mheshimiwa Yoweri Kaguta Museveni, Rais wa Jamhuri ya Uganda, Mheshimiwa Dk. Ikililou Dhoinine, Rais wa Muungano wa Comoro, na Mjumbe Maalum, Waziri wa Makaazi na Maendeleo Miji na Vijiji Mheshimiwa Jiang Weixin anayemwakilisha Rais Xi Jinping wa Jamhuri ya Watu wa China. Kadhalika, natoa shukrani kwa viongozi wote wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, waliopo madarakani na waliostaafu, Mabalozi wa nchi mbali mbali, Wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa, Viongozi wa dini na vyama vya siasa na wananchi wote kwa kuhudhuria kwa wingi kwenye sherehe hizi.
Kuwepo pamoja nasi wageni wetu mbali mbali kunatupa faraja kubwa sana. Kuja kwenu kunatudhihirishia kuwa Mapinduzi yetu yanaheshimika na yanapewa taadhima kubwa ndani na nje ya nchi yetu. Tuna kila sababu ya kujivunia uhusiano wetu na kuja kwenu ni uthibitisho wa juhudi zetu za pamoja za kuyaenzi Mapinduzi yetu.
Waheshimiwa Viongozi na Ndugu Wananchi,
Leo ni siku muhimu sana katika historia ya wananchi wa Zanzibar, ambapo miaka 50 iliyopita walikata minyororo ya utawala wa Kisultani na ukoloni wa Kiingereza uliodumu kwa miaka 132. Wananchi walikataa kwa vitendo kudharauliwa, kunyanyaswa, kubaguliwa na kutoheshimiwa katika nchi yao.
Ukombozi wa watu wa Zanzibar ulifanywa na Chama cha Afro-Shirazi, ambacho kilianzishwa tarehe 5 Februari, 1957, kwa madhumuni ya kuikomboa Zanzibar kutokana na madhila ya wakoloni, mabwanyenye na mabepari. Madhila haya walitendewa wananchi kwenye mambo yote muhimu katika maisha ya binadamu, kama vile kubaguliwa katika kupata elimu, huduma za matibabu, makaazi, chakula, ubaguzi kwenye kazi, ubaguzi na dhulma kwenye matumizi ya ardhi, ubaguzi katika kupata haki, na kadhalika.
1)unasema kubaguliwa je huu upemba na unguja au wale mahizbu sisi wakulima na wakwezi mbona upo mpaka leo au huu sio ubaguzi...?
2)unasema kubaguliwa katika elimu hapa hapa zanzibar watu wangapi wamefelishwa tu kwa kuwa hakuna jina la kombo,jecha,pandu,kificho,nahodha kama mtu hana jina hilo mwanzo au mwisho munamfelisha je sio ubaguzi huo wa elimu isitoshe hao wakoloni weusi tanganyika washawafelisha dungu zetu wangapi sio ubaguzi huo..?
3)unasema huduma za matibabu ikulu yako iko ubavuni mwa hospitali kubwa hapa zanzibar na unasikia au unasoma kila siku habari kuwa hakuna madawa hakuna vitanda manasi na madaktari wajeuri kupita kiasi kwa wangojwa hakuna hata chumba cha kujifunguwa wanawake wazazi sasa huo ukombozi wenu wakuwapa watu huduma ya matibabu uko wapi..? au kuwa na lili jengo tu ndio matibabu yenu...?
4)unasema makazi kweli kweli wewe kampeni zako zote umefanya vijijini hivi hukuona vibanda vya udongo wanavyo ishi watu toka uingiye madarakani ni miaka mitano inakatika umewajengea nyumba ngapi za kuishi...?
5)unasema chakula muliwandanganya watu mabembe basi mbona mpaka leo mabembe ndio namba moja isitoshe mumewatia wazanzibari ufakiri mpaka wanakula futari ramadhani ugali ugali nchi hii walikuwa watu hawali ugali watu waliokuwa wakila ugali na wanyamwezi na wamakonde na wazaramo wanaokuja kuchuma kaarafu siku za msimu wa karafu ndio watu wanawaona wanakula ugali leo hii zanzibar watu wanafutari ugali ndio maendeleo hayo..?
6)unasema ubaguzi katika kazi nyinyi mpaka leo kama sio mwana maskani hupati kazi je huo sio ubaguzi..? watu wamefukuzwa makazi kisa ni wapemba au wamejiunga na chama cha cuf je sio ubaguzi huo..?
7)unasema ubaguzi na dhulma kwenye matumizi ya ardhi daaah shein weee shein weee nyinyi muliwanyanganya watu mashamba yao 1964 kisha mukayakata heka tatu tatu kuwapa watu sawa sasa kila waziri katika baraza la wawakilishi ana heka karibu 60 kazitowa wapi..? wamewanyanganya hao masikini walio pewa na heka tatu tatu na kujiribikia wao na wake zao na watoto wao mumeuza visiwa vidogo vidogo vyote na fukwe za bahari wewe mwenyewe umeuza nyumba ngapi za shangani kisha ukawambia wazanzibari mtu halaumiwi kuza chake au sio wewe shein..?
8)unasema ubaguzi katika kupata haki, na kadhalika ni wazanzibari wangapi hawapati kitambulisho mpaka sasa..? ni wazanzibari wangapi hawapati paspoti mpaka sasa je sio haki yao..? waznzibari wangapi wamefanyiwa ukiritimbwa wasiende kusoma nje na nafasi wanapewa watoto wa mawaziri nakadhali.                                                                       
 Shein 
Kwa research yako uliyoifanya na kujenga hoja maendeleo yaliopatikana kwa miaka 50 iliyopita. Juu ya kuwa kuna counter arguments nyingi za kitaalamu kuhusu uliyoyasema, lakini tu nakuomba ufanye research nyengine ili ututhibitishie kauli yako ifuatayo:
“Hatutokubali kutawaliwa, kudhulumiwa, kubaguliwa na kudharauliwa katika nchi yetu.”
1 Kweli wananchi (Wazanzibari) wanaamini hivyo kuwa hawatawaliwi,kudhulumiwa,kubaguliwa na kudharauliwa katika nchi yao kwa wanamini hayo.....?

2 Ni kweli hatutawaliwi tena...? Maamuzi makubwa ya nchi yetu ya Zanzibar pamoja na kumteua au hata kumfukuza Rais wa nchi yanafanyika wapi pale kisonge au kisiwa nduwi...?


3 Ni kweli hatudhulumiwi tena.....? Hizo KERO ZA MUUNGANO za nini basi......?


4 Ni kweli hatubaguliwi tena......? Huu upemba na Unguja au uarabu na uafrika ni kutukana......?


5 Ni kweli hatudharauliwi tena.....? Mbali ya mifano iliyopo chungu nzima, wa juzi ya kijomba Warioba kakubali kuwa 60% ya Wazanzibari wametaka MUUNGANO WA MKATABA, fikra hizo zimehishimiwa kiasi gani......?
Ikiwa moja kati ya masuala hayo matano yatathibiti kuwa si kweli basi kauli yako “HATUTOKUBALI” tueleze wewe kama ni kiongozi wetu  umefanya nini na utafanya nini kutuyakinishia kuwa:
“Hatutokubali kutawaliwa, kudhulumiwa, kubaguliwa na kudharauliwa katika nchi yetu.”? kama si hivyo heshima yako kwa wananchi wako iko hatarini kuvunjika