Thursday, May 29, 2014

NI LINI MWANANCHI WA KAWAIDA NCHINI ZANZIBAR NA YEYE ATAKULA MANONO MNAYO KULA NYINYI WAKUU.....???

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akiwaongoza baadhi ya wajumbe wa Baraza la Wawakilishi na watendaji wengine katika chakula alichokiandaa, baada ya  kupitishwa kwa bajeti ya ofisi yake
Makamu wa Kwanza wa Rais wa nchi ya  Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akiwaongoza baadhi ya wajumbe wa Baraza la Wawakilishi na watendaji wengine katika chakula alichokiandaa, baada ya kupitishwa kwa bajeti ya ofisi yake
 Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akijumuika pamoja na baadhi ya watendaji katika chakula alichokiandaa baada ya kupitishwa kwa bajeti ya ofisi yake
Makamu wa Kwanza wa Rais wa nchi ya Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akijumuika pamoja na baadhi ya watendaji katika chakula alichokiandaa baada ya kupitishwa kwa bajeti ya ofisi yake
Baadhi ya watendaji wa ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais, wakijipatia chakula katika dhifa maalum iliyoandaliwa na Makamu wa Kwanza wa Rais, baada ya  kupitishwa kwa bajeti ya ofisi yake
Baadhi ya watendaji wa ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa nchi ya Zanzibar, wakijipatia chakula katika dhifa maalum iliyoandaliwa na Makamu wa Kwanza wa Rais, baada ya kupitishwa kwa bajeti ya ofisi yake
MABEMBE, MIHOGO, MAJIMBI, N.K YAMETUCHOSHA WANANCHI.

Tuesday, May 27, 2014

MAENDELEO YA SMZ MAPINDUZI DAIMA NDIO HAYA MIAKA 50 AMAA KWELI TUME ENDELEA

1898112_805451202803250_564609920_n
maendeleo ya miaka 50 ya mapinduzi daima ndio haya dari la hospitali pia linamatundu kama jumba la kufungia njiwaa astahafiruh allah.
1888498_805451209469916_247403218_n
kama hukuja na shuka lako mwenyewe la kujifunika na kutandika basi ujuwe utalalia uvundo

2011_253_2011-09-10T182103Z_01_AFR13_RTRIDSP_0_TANZANIA-FERRY
ccm oyeeee hospitali tunala chini hata vitanda hatuna lakini ccm ooyeee madaktar hatuwaoni lakini ccm ooyeee madawa hakuna lakini ccm ooyeee hospitali inanuka lakini ccm ooyeeee ndio maendeleo haya ya miaka 50 ya mapinduzi ya zanzibar ndio maana tunasema ccm ooyeeee vijijini njaa kali na hata tukiumwa basi hatuwezi kuja mjini kutibiwa kwa kuwa hakuna hospitali huko mjini lakini ccm ooyeeee.

WANAMACHO ILA HAWAONI WANAMASIKIO ILA HAWASIKII WANAMOYO ILA HAWAHISI
SERA YAO NI MAPINDUZI DAIMA.
AKILI YANGU INAWASHANGAA SANA WATU WASHAMBA UNGUJA. KUIPENDA CCM WAKATI WATU WASHAMBA NDIO WENGI WENYE KUATHIRIKA NA MAGONJWA PAMOJA NA UKOSEFU WA PESA NA UCHUMI WA MTU MMOJA MMOJA LAKINI BADO MACCM.

Friday, May 16, 2014

NCHINI ZANZIBAR 1964 HAYA NDIO MUNAYAITA MAPINDUZI MATUKUFU NYIEE...??

MAITI ZA WAZANZIBARI WALIO PINGWA RISASI 1964 LEO HII WANASEMA YALIKUWA MAPINDUZI MATUKUFU ASTAHAFIRU ALLAH
JOHN OKELLO NA WAUWAJI WENZAKE WAKIPIGA PICHA ZA KUFURAHIA KUWAUWA WAZANZIBARI SIO NA HATIA NA KUWAPINDUWA KATIKA NCHI YAO
JOHN OKELLO AKIENDELEA KUPINGWA PICHA YEYE NA WAUWAJI WENZAKE NCHINI ZANZIBAR BAADA YA KUWAUWA WAZANZIBARI
HAWA NI BADHI YA WAZANZIBARI WALIO KUSANYWA NA KUONGOZWA KWENYE MAFICHO AMBAYO WALIPINGWA RISASI NA NDIO ITAKUWA MWISHO WA MAISHA YAO M.MUNGU AWALAZE PEMA PEPONI KWA KUDHULUMIWA ROHO ZAO
HAWA NI BADHI YA MAMIA YA WAZANZIBARI WALIO ULIWA KATIKA HAYOO LEO YANAITWA MAPINDUZI MATUKUFU.... ASTAHAFIRU ALLAH KISHA MUNAJITA WAISLAMU.
HAWA NI BADHI YA MAMIA YA WAZANZIBARI WALIO ULIWA KATIKA HAYOO LEO YANAITWA MAPINDUZI MATUKUFU.... ASTAHAFIRU ALLAH KISHA MUNAJITA WAISLAMU.
MTAKWENDA MWAMBIA NINI NYINYI M,MUNGU....?
MNAKA MUKIHARIBU MAPESA CHUNGU MZIMA ATI MNAFURAHI KULIWA KWA WATU
WAZANZIBARI WALIO ULIWA NA KUFUKIWA KATIKA KABURI MOJA MWAKA 1964 AMBAYO LEO WATU WANASHEREHEKEA NA KUYAITA MAPINDUZI MATUKUFU.
HIVI KWELI NYINYI MNA AKILI KWELI..??
HAWA NI WAZANZIBARI WANAO JARIBU KUKIMBIA KWA JIA YA BAHARI NA VIBOTI NA NGARAWA ILI WASIULIWE NA HAO WAWAJI LEO WANASEMA NI MAPINDUZI MATUKUFU ASTAHAFIRU ALLAH
HIZI NI MAITI ZAWAZANZIBARI KATIKA FUKWE ZA BAHARI AMBAO HAWAKUWAHI KUKIMBI NA MABOTI  WALA NGARAWA NA KUULIWA KATIKA FUKWE  HII M.MUNGU AWALAZE PEMA PEPONI
JOHN OKELLO BAADA YA KUMALIZA MAUWAJI YAKE NA UKIRITIBWA WAKE AKIWA TAYARI KUMKABIDHI NCHI MZEE KARUME NA BABU HAKUJUWA KUWA NA YEYE ATATIMULIWA KAMA KUKU
JOHN OKELLO BAADA YA KUWAUWA WAZAZI WETU NA KUWANAJISI MAMA,DADA,ANTI ZETU AKAMKABITHI MZEE KARUME NA BABU NAO WAKAMGEUKA MAANA WALIKUWA HAWANA HAJA NAE TENA NA KUMDANGANYA ANAITWA NA NYERERE ALIPOFIKA DAR ES SALAAM AKISHIKWA NA POLISI WA TANGANYIKA NA NYERERE KUMPA MASAA ATOKE KABISA KATIKA NCHI YAKE YA TANGANYIKA HII NI PICHA KUONYESHA SIKU HIYO ALIYO SHIKWA NA KUTIMULIWA NJE YA NCHI YA TANGANYIKA
BWANA MKUBWA ANAYE YAITA MAPINDUZI MATAKUFU HUYO KULA ULUWA WAKO TU WA HARAMU NA KUSHEREHEKEA MAUWAJI YA WAZANZIBARI WASIO NA HATIA KISHA SIKU YA IJUMAA UNAJIDAI KUFUNGA SWALA.
M.MUNGU ANAKUTIZAMA TU FIRAUNI YUKO WAPI..? HITLER YUKO WAPI..? MZEE KARUME MWENYEWE YUKO WAPI....? ITAKUWA WEWE.
SIKU YA MSIBA WAO WANASEMA NI SIKU YA FURAHA NA KUSHEREHEKEA KULIWA KWA WAZANZIBARI WASIO NA HATIA SIKU MUKINGIA MAKABURINI MWENU MTASHEREHEKEA VIZURI KABISA NA SIKU YA KIYAMA NDIO KABISA.
AKITOWA HUTUBA YA KUYASIFU MAUWAJI YA WAZANZIBARI AMBAYO YEYE ANAYEITA MAPINDUZI MATUKUFU UTUKUFU KUUWA WATU WASIO NA HATI..?? UTUKUFU KUWANAJISI WANAWAKE..? UTUKUFU KUWACHUKUWA WARI WAWATU BILA ITHINI ZA BABA ZAO NA KUJIDAI NI WAKE ZENU..? UTUKUFU KUIBA MALI ZA WATU NA KUWAUWA..? UTUKUFU KUNYANGANYA MASHAMBA YA WATU NA KUYAKATA HEKA..? UTUKUFU KUWAVUWA WATU NGUO NA KUWANIKA BARABARANI..? UTUKUFU KUWANYOWA WATU NDEVU NA NYWELE NA KUWAPIGA MIKWAJU BARABARANI UCHI WA MNYAMA AU UCHI MBELE YA FAMILIA ZAO NDIO NYINYI MUNAITA MAPINDUZI MATUKUFU..?SMZ JE MUNAWAJUWA HAWA ABDALLAH KASSIM HANGA,ABDULAZIZ TWALA,SALEH SAADALLA,OTHMAN SHARIFF, MDUNGI USSI NA JAHA UBWA...MAKABURI YAO YAKO WAPI....??????

SIKU NYERERE ALIPO MUADHIRI KASSIM HANGA KINARA WA MAPINDUZI YA NCHI YA ZANZIBAR VIWANJA VY MNAZI MMOJA MBELE YA KIBARUA BAR NYUMA YA UKUMBI WA ARNATOUGLO, KASSIM HANGA KINARA WA MAPINDUZI YA NCHI YA ZANZIBAR ALITOLEWA JELA UKONGA NA KULETWA HAPA MAKHSUSI KWA JILI YA SHUGHULI HII YA KUADHIRIWA MBELE ZA WATU, BAADA YA SIKU HII HANGA HAKUONEKANA TENA.SASA HUYO MSAKA TONGE ANAYE JIDAI NA MTOTO WA HANGA NA KUJIDAI ATAMSHATAKI LISSU KABLA HUJAMSHATAKI LISSU NA KUIBIKA HEBU SOME HII STORI KISHA JIULIZE BABA YAKO ALIKUWA MAKAMO WA RAISI IKIWA ATAKUFA KIFO CHA KAWAIDA IWEJE ISITANGANZWE KUWA MAKAMO WA RAISI KAFA HATA MAHALI PAMOJA IWEJE MAZIKO YAKE YASIONEKANI WAKATI WA MAZIKO WAKATI ALIKUWA KIONGOZI MKUBWA JE UNAKILI WEWE AU NDIO CCM ISHAKUNUNUWA MSAKA TONGE...???


Siku Nyerere Alipomuadhiri Hanga Viwanja Vya Mnazi Mmoja
Mbele ya Kibarua Bar Nyuma ya Ukumbi wa Arnatouglo
Hanga Alitolewa Jela Ukonga Kuletwa Pale Makhsusi kwa Shughuli Hiyo
Baada ya Siku Hii Hanga Hakuoenekana Tena


Naomba nikuwekeeni kitu kuhusu Kassim Hanga katika yale niliyoyajua katika
udogo wangu hapa Dar es Salaam nikumuona Hanga akija mtaani kwetu kuja
kucheza bao na watu wa kawaida sana:
KUULIWA KWA ABDALLAH KASSIM HANGA
KUULIWA KWA ABDALLAH KASSIM HANGA
Leo hii asubuhi katika Bunge la Bajeti Mheshimiwa Tundu Lissu kamtaja Kassim Hanga kuwa aliuliwa…
In Sha Allah tunatayarisha kitu kwa kumbukumbu ya Hanga na wenzake waliopoteza maisha baada ya kuipindua serikali ya Sheikh Mohamed Shamte…serekali halali ya wananchi wa Zanzibar.
Fuatilia ukurasa huu…
Haya hapa chini ni baadhi ya maneno aliyosema Mheshimiwa Lissu Bungeni kuhusu kuuliwa kwa Abdallah Kassim Hanga, Abdulaziz Twala, Saleh Saadalla, Othman Shariff, Mdungi Ussi na Jaha Ubwa…
”Swali kuu ambalo sisi tuliozaliwa ndani ya Muungano tunataka lijibiwe kwa ukweli kabisa ni ‘waasisi’ hawa wengine wa Muungano, akina Abdallah Kassim Hanga, Abdulaziz Twala na Saleh Saadalla Akida kwa upande wa Zanzibar; na Oscar Kambona, Bhoke Munanka na Job Lusinde kwa upande wa Tanganyika walipotelea wapi...?? na kwanini hawatajwi katika historia rasmi ya Muungano na waasisi wake...?? Kassim Hanga alikuwa Waziri Mkuu na baadaye Makamu wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar; wakati Twala alikuwa Waziri wa Fedha wa Serikali hiyo na Saleh Saadalla alikuwa mjumbe wa Baraza la Mapinduzi. Kwa upande wa Tanganyika, Oscar Kambona alikuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ulinzi wakati wa Mapinduzi ya Zanzibar na baadaye wakati wa kuzaliwa kwa Muungano; Bhoke Munanka alikuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais mwenye dhamana ya masuala ya usalama, na Job Lusinde alikuwa Waziri wa Serikali za Mitaa. Katika Kwaheri Ukoloni, Kwaheri Uhuru!, Ghassany ameonyesha jinsi ambavyo akina Hanga, Twala na Saadalla pamoja na viongozi wengine waandamizi katika Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kama vile Othman Shariff, Mdungi Ussi na Jaha Ubwa waliuawa na kuzikwa katika handaki moja katika sehemu inayoitwa Kama, nje kidogo ya mji wa Zanzibar. Sisi wa kizazi cha Muungano tunataka kujua ukweli juu ya makosa waliyoyafanya hawa waasisi wa Muungano hadi wakauawa na kuzikwa katika kaburi au handaki moja. Tunataka kujua ukweli kama walifanya makosa walishtakiwa katika mahakama gani iliyowahukumu adhabu ya kifo. Aidha, tunataka kuambiwa ukweli kwanini mchango wao katika kuzaliwa kwa Muungano umefichwa kwa muda wote wa nusu karne ya Muungano huu.”
Wakati Dk. Harith Ghassany anaandika kitabu chake, ”Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru,” siku moja usiku kanipigia simu kutoka Washington. Wakati ule mimi naishi Tanga. Dk. Ghassany akaniuliza kuhusu Hanga nadhani katika mazungumzo yetu siku za nyuma nilipata kumweleza kuwa nikimjua Hanga katika utoto wangu. Baada ya kumpa kisa hiki sikumaliza akanikatisha na kunambia angependa anirekodi katika kinasa sauti ili atumie maelezo yangu kwenye kitabu. hapa chini ndiyo niliyosema kuhusu Hanga na ndivyo yalivyo katika kitabu:
”Mimi nikiishi na baba yangu mtaa wa Somali, namba 22. Klabu ya mwanzo maarufu ya Kilwa Jazz Band ilikuwa kwenye nyumba ya mama yake Abdu Kigunya. Mbele ya nyumba yao ikifika kama saa tisa, kumi, laasiri, wazee walikuwa wanaweka jamvi pale, wanacheza bao. Sasa hivi ukenda pamejengwa majumba ya maghorofa. Hanga akija pale mtaa wa Gogo, kona na Mtaa wa Mchikichi, nyumba ya kona barazani wazee wametandika majamvi wanacheza bao. Mimi nilimjuwa Hanga kwa sababu nikimuona kwenye magazeti. Na wakati ule mawaziri wakitembeya na yale magari meusi yakiitwa “Humber.” Sikumbuki kumuona Hanga kuja pale na gari. Basi ikapita, mapinduzi Unguja yakatokeya sisi wadogo, hatujui nini kinachotokea. Mwaka 67 nadhani, pale Mnazi Mmoja, Dar es Salaam, Anatoglou Hall, tukicheza mpira wa miguu pale. Mambo yalianza Mnazi Mmoja katika mkutano wa hadhara. Hanga katolewa jela Ukonga kaletwa pale kuadhiriwa na Nyerere. Sisi ni watoto, mambo yale na nyimbo zile lazima tujumuike. Hanga akaletwa pale. Namuona Hanga mimi kwa macho yangu ya kitoto na miwani yake ile.
Hanga alikuwa mwembamba na mrefu na alikuwa na thick hair. Alikuwa mtu mwenye kupendeza. Kaja pale na uso ulionyongonyeya. Lakini sisi hatujui kinachotendeka. Watoto wa Kiswahili miaka 14, 15, 16, ni wadogo. Hatujui kinatendeka nini. Lakini mimi najua kuwa yule pale Hanga namuona kuwa ni mfungwa. Hanga miwani iko puani uso umemparama kama jiwe la kiama, madevu yamemjaa. Anaadhiriwa! Jua la saa sita mchana linampiga vizuri. Kwa pale kukaa na kajiinamia nilijuwa kuwa mambo si mazuri. Nyerere pale anazungumza na wote wanasikiliza. Nyerere unajua. Nyerere alikuwa ni orator. Na kuna kumuuwa mtu kiungwana. Nakumbuka incident moja Nyerere anamuonyesha kidole Hanga anasema “hili, hili, hili. Hana lolote. Hakuna lolote anaweza kufanya huyu. Afadhali huyu mwanzake [Babu].” Ukitizama kwenye Tanganyika Standard, wakati ule bado halikuchukuliwa na serikali, wakati ule editor ni yule Muingereza, Brandon Grimshaw. Utakuta full page. Mimi kwa jicho langu nimeona kwa sababu baba yangu mimi akinunua lile gazeti. Picha ya Hanga iko mbele na madevu na miwani yake ile. Si mimi tu, watu wengi wanakumbuka hiki kisa. Mimi baba yangu rafiki zake walikuwa Jaha Ubwa, Twala…Wakitembeleyana zamani wakati wa Easter…baba yangu alikuwa memba wa band ya Black Birds ya Bwana Ally Sykes.
Siku Nyerere Alipomuadhiri Hanga Viwanja Vya Mnazi Mmoja
Mbele ya Kibarua Bar Nyuma ya Ukumbi wa Arnatouglo
Hanga Alitolewa Jela Ukonga Kuletwa Pale Makhsusi kwa Shughuli Hiyo
Baada ya Siku Hii Hanga Hakuoenekana Tena
Nadhani kule ndo walikofanya urafiki na hawa jamaa wa Zanzibar. Picha yangu mimi ya Mzanzibari, wakija kule nyumbani, unamuamkia na suala lilikuwa “wewe umeshahitimu wewe.” Na ile ”sophistication” za wake zao wakija nao pale, yale mavazi, mabuibui, uturi ule, vile vyakula wakiandaa nyumbani pale. Hi ndo picha yangu ya Mzanzibari. Palikuwa na picha pale ukutani ya marahemu father wangu na kina Jaha Ubwa. Ile picha ikapotea pale ukutani. Ikawa haionekani tena. Lakini palikuwa mzee akizungumza habari za akina Twala alikuwa akinong’ona. Nahisi mzee alikuwa ana khofu. Ile ni dalili ya woga. Kitu kibaya kimetendeka. Lakini lazima aulize. Vipi mkewe. Watoto vipi? Lakini hawezi kusema kwa sauti. Siku nilipokuja kukutana na Ali Nabwa aliponielezeya habari za Zanzibar, nikamwambia mimi baba yangu alikuwa ana masikilizano na akina Twala na yeye akaanza ku open up sasa. Nikasema duu! Alipotoka jela Ali Nabwa alikuja pale mtaa wa Narungombe na Skukuu. Pale palikuwa na baraza maarufu sana ya Saigon Football Club. Nabwa alikuwa anakuja pale. Tukitoka tukikaa pembeni tukizungumza chamber. Nilijua baadaye sana kuwa kumbe alikuwa ametoka jela. Pale ndo nilipoanza kuwaona Wazanzibari kwa sura nyingine sasa. Kumbe zile bashasha zinadanganya?
Kuwa Hanga ndiye aliyekuwa kinara wa Mapinduzi ya Zanzibar hili si jambo lenye utata tena. Ikiwa hivyo ndivyo Hanga hatoweza kuutua mzigo wa roho zilizopotea katika mapinduzi hayo. Ikiwa Hanga atalaumiwa kwa vifo vya maelfu ya Wazanzibari nani alaumiwe kwa mauti yaliomfika Hanga tena kwa kuuliwa kishenzi kwani hapana neno zaidi ya hilo linaloweza kutosheleza kuelezea jinsi Hanga alivyouliwa. Kichekesho kikubwa ni kuwa wale waliopoteza roho na kutangulia mbele ya haki yao yalikuwa yamekwisha. Lakini kwa wale wajane na mayatima waliobakia nyuma na kuhangaika, kifo cha Hanga na wenzake katika wale waliofanikisha mapinduzi kuuliwa kwao kulikuwa miujiza ya aina yake, uchawi usioelezeka nani fundi wake. Ilikuwa vigumu kueleza. Ingeeleweka vyema endapo kisasi cha kuitoa roho ya Hanga kingetimizwa kwa mikono ya maadui zake waliopinduliwa. Haikuwa hivyo.
Wale wajane na mayatima walililipiziwa kisasi na watu waliokuwa maadui wakubwa wa hao waliopinduliwa. Vipi Hanga kiongozi mkuu wa mapinduzi aje kuwa adui wa mapinduzi yenyewe kiasi cha kuwa hukumu ya kumtosheleza haikuwa kifo tu bali kifo cha kishenzi? Fikra za Hanga zilikuwaje pale alipokuwa peke yake ndani ya selo Ukonga Prison…usiku ukimpita bila ya hata lepe la usingizi akiwaza yanayomkabili. Nini kilikuwa kikimpitikia katika ubongo wake wakati wauaji wake walipomtoa katika selo yake na yeye akawakabili ilhali akijua kuwa walikuwa wamekuja kuitoa roho yake. Fikra yake ilikwenda wapi? Ilikwenda kwa Sultan Jamshid bin Abdullah na Masultani wengine waliopita ambao wameiaga dunia mikono yao ikiwa haina damu, au kwa Abeid Amani Karume aliyeingia madarakani kwa mapanga ya Wamakonde wakata mkonge kutoka Sakura na Kipumbwi? Fikra ya Hanga ilielekea wapi? Kwa Nyerere aliyemsaliti?
Hakika ni wazi hakutegemea mapinduzi aliyoyaasisi yangemgeukia na kuwa sababu ya yeye kutolewa roho kwa kuuliwa kishenzi. Jambo la kusikitisha ni kuwa hadi pale alipokamatwa na kuwekwa jela Ukonga na kufikishwa mbele ya mkutano wa hadhara na kuadhiriwa na Julius Nyerere tayari alikuwa keshapoteza kila kitu achilia mbali dira ya mapinduzi aliyokusudia ingeongoza Zanzibar. Hanga hakuwa kamwe na uwezo wa kumfanya Karume lolote kwani Karume tayari alikuwa chini ya mbawa za Nyerere, ngome ambayo Hanga asingeweza kuitikisa achalia mbali kuibomoa. Muungano baina ya Tanganyika na Zanzibar ilikuwa hirizi tosha ya kumkinga Karume. Katika mkasa wa kuuliwa kwa Hanga ndipo msemaji mmoja akasema, “Maiti toka makaburini mwao walionyesha ujuzi wa kufanya miujiza na uchawi wao kwani laiti kifo cha Hanga kingesababishwa na wale waliyopinduliwa kisasi chake kingekuwa cha kutisha. Ilibidi Hanga kwa miujiza ya maiti zile auliwe na wale wale aliowaweka madarakani watu ambao hapakuwepo na sababu ya wao kumuona adui. Halikudondoka chozi kwa kifo cha Hanga. Kila aliyepata mnong’ono wa kuuliwa kwake alikuwa kimya kama vile ile taarifa ya kifo haimuhusu.”
Hebu tumsome Dk. Ghassany ameandika nini katika kitabu chake Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru kuhusu Hanga wakati yuko nyumbani kwa Oscar Kambona anajitayarisha kurejea Tanzania:
”Nnavokumbuka mimi Oscar akatwambia sikilizeni bwana. Mimi nimekwiteni hapa mje mseme na ndugu yenu na mzee wenu huyu, Abdalla Kassim Hanga amekuja hapa na anataka kurudi nyumbani. Hajataja pahala. Na mimi nimemkataza. Nimemwambia huu si wakti mzuri ni bora yeye asiende. Ama angelibaki huko huko West Africa anokotoka kwa mkewe, au abaki hapa London lakini kakataa, anataka lazma arudi. Na mie na hofu maisha yake kuwa akifika kule hatoweza kupata salama. Kwanza kuwa yeye amefikia kwangu, anajulikana yeye na mimi ni rafiki, Nyerere atajuwa zaidi/uzuri hayo kuwa mimi tangu tuko kule tunasikilizana mimi na ndugu huyu Abdalla. Kwa hali hiyo mimi namwambia. Na yeye Abdalla anasema hana ugomvi na Nyerere.
Sasa mimi nimekwiteni mzungumze naye, mseme naye. Akatuchukuwa akatupeleka kwenye chumba akasema “Abdalla, hebu zungumza nao hawa jamaa wamekuja kukuamkia.” Tukaingia sie chumbani akatuacha mimi na Ahmed [Rajab] na Abdalla. Peke yetu watu watatu. Ndivo navokumbuka mie na ndivo anavokumbuka Ahmed [Rajab].
Mimi sikumbuki ile nilikwenda railway station. Kile mimi sijakumbuka. Kama ulivosema, mimi nyumba nilikuwa naijuwa, sina haja ya Kasembe kunpeleka. Lakini inaweza kuwa nimekwenda mimi na Kasembe kumpokea Ahmed Rajab. Yeye Ahmed kafkiri tu na mie ni mgeni. Hajajuwa kuwa mimi na Kambona tunajuwana na jirani, na nyumba yangu mie na yake si mbali.
Ahmed Rajab ndo anosema, tumefika alofunguwa mlango ni Oscar Kambona, na akatuonyesha chumba. Hajaeleza nini Kambona katwambia. Lakini mimi nakumbuka Kambona katwambia kwanza, “semeni naye.” Yeye kazungumza moja kwa moja, sisi tumekaribishwa tumekwenda kwa Abdalla. Yeye Ahmed amekumbuka mambo mimi sijayakumbuka. Kwa sababu, kasema tulipofika Abdalla Hanga katwambia skizeni: nyinyi ni vijana, watoto kwa sasa, lakini kesho nyie ndo mtakuwa viongozi. Nna maneno nnataka kukwambieni. Tukawa sasa tumekaa tunamsikiliza nini atasema.
Anasema nataka kukwambieni juu ya habari ya mapinduzi yetu ya Zanzibar. Kuna mabaya ambayo tuliyafanya na kabla sijasema lolote nnakutakeni jambo moja muhimu mlikumbuke. Msije mkakubali kufata siasa za ukabila.4 Siasa za ukabila ndizo zinotuletea matatizo na ndizo zitozidi kutuletea matatizo. Hilo ni jambo la mwanzo ambaye yeye Hanga katwambia. Akasema mimi (Hanga) nilivoondoka Zanzibar kupelekwa Dar es Salaam, kuwa Waziri wa kule, badili ya kuwa Vice-President [Makamo wa Rais] huku na Mzee Karume, alivopelekwa bara, anasema jambo moja katika mambo aloyafanya ni kuwasaidia Wazanzibari walokimbia kutoka Zanzibar wakakaa pale, wale ambao wataalamu, kuwatafutia kazi. Akataja majina. Akamtaja Maalim Salim Sanura, na akawataja wengine, mimi siwakumbuki. Kuwatafutia kazi na wakapewa kazi serkalini. Hata ikafika akaanza kusemwa, akalaumiwa, kuwa Abdalla, mbona unakwenda kinyume sasa? Hawa si ndo tuliowapinduwa, mbona wewe sasa hapa unawasaidia? Unawapokea? Akasema bwana, hapa mimi naona ni Mzanzibari tu hapa. Hawa wote ni Wazanzibari bwana. Na hawako nchi nyengine. Wako na sisi pamoja hapa. Kwa hali hiyo yeye anasema ule ndo uzi anataka sisi tuufate. Tusibaguwane.
Jambo la pili akasema, sisi Mungu atusamehe, tumefanya mambo mengi ambayo mabaya, tumedhulumu, tumechukuwa watoto na wake za watu, na Mwenye Enzi Mungu ndiye anojuwa. Basi mimi namuomba Mweye Enzi Mungu anisamehe na ninajuta kwa haya nlioyafanya. Ahmed Rajab akamuuliza suala. Akamwambia, mzee, lakini wewe na Janab [Babu] mnaskizana vipi kisiasa? Akamwambia, mimi na Babu sote wawili ni Marxists lakini Babu si tishio kwa Karume. Mimi ndo tishio. Mimi ndo ni tishio juu ya Karume, lakini Babu is not [si tishio]. Hiyo tafauti yangu mimi na Babu, anasema. Kwa Unguja. Sasa ndio tukamuuliza, Vipi ikawa wewe ndo tishio? Yeye Ahmed Rajab ndo anamuuliza.
Rome ilijaribu kuingia kati katika ugomvi wa Oscar na Nyerere na ilishindwa. Kambona alinieleza. Hata makanisa yamejaribu. Ugomvi ulikuwa mkubwa na hiyo akijuwa yeye zaidi Kambona ndo mana akahofu Abdalla asirudi. Ile imani yake ilikuwa kubwa kuwa Nyerere hatomdhuru. Na yeye akiona watu wangapi wamepotea lakini hajafikiria atakuja kuwa yeye.
Tukasema naye tukamwambia kweli hayo maneno anayoyasema Oscar inaonyesha ni bora usirudi kwa sasa. Akasema hapa kuna mambo mawili. Moja, kuna kutosikilizana baina ya Oscar Kambona na Mheshimiwa Nyerere, Raisi Nyerere. Sasa huyu bwana akisema mimi nisirudi anazungumzia kule kutosikilizana baina yake yeye na Raisi Nyerere. Sasa anahisi mie nikirudi labda kwa sababu mimi nimefikia kwake au ni rafki yake Nyerere anaweza akachukuwa hatuwa. Mimi nimeshafanya kazi na Nyerere na namjuwa uzuri mzee Nyerere, mimi na yeye hatuna ugomvi wowote. Abdalla Kassim Hanga anasema kuwa yeye na Nyerere hawana ugomvi. Na yeye ikiwa anarudi harejei kwa Zanzibar. Atarudi anakwenda zake akakae nyumbani Dar es Salaam. La pili alisema, kuna ukweli wa kuwa mimi na Mzee Abedi Amani Karume kuwa hatuskizani na kusema kweli si makosa yangu. Akasema Abdalla, jambo dogo sana limemfanya Mzee Abedi anichukie mimi hata ikawa mimi nikienda Zanzibar sasa siwezi kukaa nikalala Zanzibar. Lazima siku ileile nirudi Dar es Salaam.
Na hili jambo anasema, mimi nilivokuwa niko Tanzania Bara na Dar es Salaam ni mmoja katika Mawaziri, nilikuwa nnakwenda Zanzibar mara kwa mara. Na nikenda nikifia katika nyumba ilioko Migombani ambayo niliwahi kukaa nilivokuwa Makamo wa Raisi. Wakati mmoja nafikiri baada ya mapinduzi, President wa Zanzibar alikuwa ni Karume na Makamo alikuwa Hanga. Sasa ile nyumba ya Migombani ikawa yeye bado Hanga hajairejesha serikalini kila akienda Zanzibar anafikia pale. Siku katika siku alizokuweko pale anasema yeye kaja kafikia nyumbani pale Migombani na kila akenda watu wakipata habari kuwa Abdalla kaja, watu, jamaa, ndugu na marafiki, walikuwa wanakwenda kumuona na kuzungumza naye, na wengineo wanakuwa nayo mahitajio yao wanakwenda kumuomba awasaidie. Sasa sku moja hiyo Mzee Karume anatokea njia ya uwanja wa ndege kwenda zake mjini akapita pale Migombani akaona magari, akauliza. Kuna nini hapa, mbona magari mengi? Akaambiwa basi lazim Mzee Abdalla Kassim Hanga kaja. “Ala, sasa yeye kila akija lazma iwe namna hii?” Akaambiwa, yeye akija watu wanakuja hapa kumuamkia na kuonana naye. Basi jambo hilo anavosema Abdalla Kassim Hanga ndilo liloanzisha ugomvi baina yake na Mzee Karume. Karume akawa hataki tena na ikawa na yeye Abdalla akenda Zanzibar hafikii tena katika nyumba ile. Akakataa kabisa.
Lakini inaskitisha kuwa tangu wakati ule yeye yupo pale London habari zishafika Cairo. Walioko Cairo maambassador wa pale wameshapeleka habari Tanzania kwa Mzee Nyerere. Ikawa serikali ninavosikia wamekaa wakimngojea arejee tu. Yeye Hanga hajajuwa, wala sisi hatujajuwa.”
Ukimsoma Dk. Ghassany anavyoeleza jinsi Hanga alivyoonywa asirejee Tanzania na yeye akakaidi unaweza kusema kuwa kifo kilikuwa kinamwita. Hebu sikiliza na kisa hiki kilichotokea uwanja wa ndege wa Dar es Salaam siku Hanga alipotua kutoka London kwa Egypt Air. Mpashaji habari wangu anasema:
”Wakati ule mimi nilikuwa meneja wa shirika moja la ndege. Nilikuwa uwanjani nikamuona Bi. Mkubwa. Huyu alikuwa mkewe Hanga, mwanamke wa Kingazija. Nikamuuliza mbona yuko pale akanambia kuwa alikuwa amekuja kumpokea Hanga. Nilishtuka sana. Mimi ni Mzanzibari na nikijuana na Hanga kwa miaka mingi na nilikuwa nasikia mengi. Hanga alipofika nilikwenda kumlaki na tukatoka sote nje ya uwanja na hapo nikamualika yeye na mkewe chakula cha mchana hapo hapo uwanja wa ndege. Wakati tunatoka nje ya uwanja nilimuuliza Hanga iweje karejea nchini wakati kama ule. Hanga akanijibu kuwa hapana kitu. Mimi sikuridhika. Tulipomaliza kula na tukawa tanazungumza nilitaka kwa mara nyingine niufungue moyo wangu kwa Hanga. Sikumbuki nilifanya nini lakini niliweza kumtoa mkewe pale mezani tukabaki sie wawili, mimi na Hanga. Hapo nikamwambia Hanga kuwa ni vyema kama akirejea London na ndege ile ile aliyokujanayo. Hanga hakuniskiliza. Jioni mimi nikamtafuta Ali Nabwa wakati ule anafanyakazi Tanganyika Standard. Nikampa habari kuwa Hanga yuko mjini. Tulimtafuta mji mzima mwisho tukampata Oyster Bay kumbe kafikia kwenye nyumba ya Kambona. Tukaja hadi Magomeni kwa Maalim Matar tukafanya dua. Ali Nabwa kumbe alikuwa amewaambia Tanganyika Standard wasubiri habari muhimu wachelewe kidogo kuchapa gazeti. Siku ya pili Tanganyika Standard ikachapa habari ukurasa wa mbele kuwa Hanga amerejea nchini. Haikuchukua siku Hanga akakamatwa.”
Tukirudi kwa Mheshimiwa Samia Hassan labda ni wa kuonewa huruma tu kwani mzigo alioubeba si makamu yake lakini ndiyo yuko kazini na kama yuko kazini ana wajibu wa kutoa majibu kwa vifo vile.
Tusimlaumu kwa kushindwa kutoa majibu.
Mimi binafsi katika shughuli zangu za utafiti nimezungumza na wengi wakubwa kutoka Zanzibar na moja katika mambo yawayowapa shida ukiwauliza ni haya mauaji baada ya mapinduzi.

ABDALLAH KASSIM HANGA MAKAMU WA RAISI MBONA ALIPO KUFA HAKUPEWA HASHIMA YA MAZISHI KAMA VIONGOZI WENGINE..?? IKIWA NI KWELI HAKUWAWA

n2
Kutoka kushoto kwenda kulia ni Abdulaziz Twala (Msaidizi Waziri katika Ofisi ya Rais), Aboud Jumbe (Waziri wa Siha na Majumba), Hasnu Makame (Waziri wa Fedha na Maendeleo), Othman Shariff (Waziri waElimu na Mila), Abdulrahman Babu (Waziri wa Mambo ya Nje na Biashara), Abeid Karume (Rais wa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar), Abdallah Kassim Hanga (Makamu wa Rais), Saleh Saadalla (Waziri wa Kilimo), Idris Abdul Wakil (Waziri wa Kazi, Njia na Nguvu za Umeme) na Hassan Nassor Moyo (Msaidizi Waziri wa Kazi, Njia na Nguvu za Umeme).Abdalla Kassim Hanga
Kuwa Hanga ndiye aliyekuwa kinara wa Mapinduzi ya Zanzibar hili si jambo lenye utata tena. Ikiwa hivyo ndivyo Hanga hatoweza kuutua mzigo wa roho zilizopotea katika mapinduzi hayo. Ikiwa Hanga atalaumiwa kwa vifo vya maelfu ya Wazanzibari nani alaumiwe kwa umauti uliomfika Hanga tena kwa kuuliwa kishenzi kwani hapana neno zaidi ya hilo linaloweza kutosheleza kuelezea jinsi Hanga alivyouliwa. Kichekesho kikubwa ni kuwa wale waliopoteza roho kwa hiyo kutangulia mbele ya haki, yao yalikuwa yamekwisha. Lakini kwa wale wajane na mayatima waliobakia nyuma wakihangaika, kifo cha Hanga na wenzake katika wale waliofanikisha mapinduzi kuuliwa kwao kulikuwa muujuza wa aina yake, uchawi usioelezeka nani fundi wake. Ilikuwa vigumu kueleza. Ingeeleweka vyema endapo kisasi cha kuitoa roho ya Hanga kingetimizwa kutoka katika mikono ya maadui zake waliopinduliwa. Haikuwa hivyo.
Wale wajane na mayatima walililipiziwa kisasi na watu waliokuwa maadui wakubwa wa waume na baba zao waliopinduliwa. Vipi Hanga kiongozi mkuu wa mapinduzi aje kuwa adui wa mapinduzi yenyewe kiasi cha kuwa hukumu ya kumtosheleza haikuwa kifo tu bali kifo cha kishenzi. Fikra ya Hanga ilikuwaje alipokuwa peke yake ndani ya selo Ukonga Prison…usiku ukimpita bila ya hata lepe la usingizi akiwaza yanayomkabili. Nini kilikuwa kikipitika katika ubongo wake wakati wauaji wake walipomtoa katika selo yake na yeye akawakabili ilhali aikijua kuwa walikuwa wamekuja kuitoa roho yake. Fikra yake ilikwenda wapi? Ilikwenda kwa Sultan Jamshid bin Abdullah aliyempindua na kwa Masultani wengi waliopita ambao wameiaga dunia mikono yao ikiwa haina damu au kwa Abeid Amani Karume aliyeingia madarakani kwa mapanga ya Wamakonde kutoka Tanganyika, wakata mkonge kutoka Tanganyika wakifanya kazi mashamba ya Sakura na Kipumbwi? Fikra ya Hanga ilielekea wapi? Kwa Nyerere aliyemsaliti?
Hakika ni wazi hakutegemea mapinduzi aliyoyasisi yangemgeukia na kuwa sababu ya yeye kutolewa roho kwa kuuliwa kishenzi. Jambo la kusikitisha ni kuwa hadi pale alipokamatwa na kuwekwa jela Ukonga na kufikishwa mbele ya mkutano wa hadhara na kuadhiriwa na Julius Nyerere tayari alikuwa keshapoteza kila kitu achilia mbali dira ya mapinduzi aliyokusudia ingeongoza Zanzibar. Hanga hakuwa kamwe na uwezo wa kumfanya Karume lolote kwani Karume tayari alikuwa chini ya mbawa za Nyerere ngome ambayo Hanga asingeweza kuitikisa achalia mbali kuibomoa. Muungano baina ya Tanganyika na Zanzibar ilikuwa hirizi tosha ya kumkinga Karume.
Katika mkasa wa kuuliwa kwa Hanga ndipo msemaji mmoja akasema, “Maiti toka makaburini mwao walionyesha ujuzi wa kufanya miujiza na uchawi wao kwani laiti kifo cha Hanga kingesababishwa na wale waliopinduliwa kisasi chake kingekuwa cha kutisha. Ilibidi Hanga kwa miujiza ya maiti zile auliwe na wale wale aliowaweka madarakani watu ambao hapakuwepo na sababu ya wao kumuona adui. Halikudondoka chozi kwa kifo cha Hanga. Kila aliyepata mnong’ono wa kuuliwa kwake alikuwa kimya kama vile ile taarifa ile ya kifo haimuhu
Tuendelee kujikumbusha na Mapinduzi !
unao wanahistoria wengi makini wanaoweza kueleza mambo haya kinaganaga kuliko tunavyofanya katika makala za magazetini, lakini ama hawajapata jukwaa au hawako tayari kufanya hivyo. Namuunga mkono Issa bin Nasser kwa aliyosema katika kitabu chake, ‘Zanzibar: Kinyang’anyiro na Utumwa’. Aliandika: “Mwenyezi Mungu ndiye mjuaji wa yote.” Sentensi inayotangulia maneno hayo, ambayo ndiyo imenikopesha maneno ya kichwa cha habari ya mada hii, inatia uchungu hata zaidi inaposomeka hivi: “…Mwenyezi Mungu mwenyewe anaelewa namna ya kuihukumu dhuluma hii iliyotendeka…”
Naiandika mada hii kwa ufupi sana kutokana na ufinyu wa nafasi. Kassim Hanga alikuwa rafiki mkubwa wa kisiasa wa Oscar Kambona. Kama Kambona alivyopoteza nyadhifa zake katika siasa, ndivyo Hanga naye alipoteza nyadhifa zake katika Serikali ya Muungano wakati yalipofanyika mabadiliko makubwa ya Baraza la Mawaziri.
Hanga hakujua mambo mengi kuhusu Tnganyika (Tanzania) kama Kambona alivyojua. Baada ya kwenda Guinea, Hanga alihakikishiwa na Rais wa nchi hiyo, Ahmed Sekou Toure, na Nyerere wa Tanzania, kwamba angekuwa huru na salama akirejea nchini. Hanga alirejeshwa Tanganyika (Tanzania) kutoka Guinea.
Hanga hakuuona uhuru alioahidiwa na, badala yake, Desemba 1967 alikamatwa kwa tuhuma za uhaini. Alipohoji sababu ya kukamatwa alijibiwa kuwa alikula njama za kuwarubuni maofisa wa jeshi ili aweze kuiangusha serikali ya Sheikh Abeid Karume. Katika mahojiano aliyoruhusiwa kufanyiwa akiwa rumande, kwa mujibu wa jarida Africa Confidential, Hanga alikana kuhusika kwa vyovyote katika kula njama na maofisa wa jeshi na akasisitiza kwamba siku zote jitihada zake zilikuwa ni katika kutaka kuwapatanisha Kambona na Nyerere.
Mapema mwaka 1969, Kassim Hanga aliachiwa huru kutoka rumande. Badala ya kurejea Zanzibar, aliondoka na kwenda kuishi katika mojawapo ya nyumba zilizomilikiwa na Kambona mjini Dar es Salaam ambayo ilikuwa bado kutaifishwa.
Lakini matatizo yake na serikali za Tanganyika na Zanzibar hayakuwa yamemalizika. Kuna Watanganyika ambao hawakuridhishwa na hali ya kisiasa nchini. Miongoni mwa mengi waliyohoji ni suala la Kassim Hanga na ‘udikteta wa Zanzibar’ wakidai kuwa Karume hakutaka uchaguzi kufanyika nchini  Zanzibar.
Baada ya kupinga sana sera za serikali, Oktoba 1968, wabunge kadhaa walitimuliwa Bungeni na baadhi ya watu wengine wakakamatwa na kutiwa kizuizini. Hawa walikuwa ni pamoja na Eli Anangisye, Joseph Kasella-Bantu, Christopher Kassanga Tumbo, Ndugu Choga, Ndugu Bakampenja na Ndugu Kaneno.
Taarifa za watu kutiwa kizuizini zilipochapishwa katika gazeti Daily Nation (Okt. 2, 1968) la Kenya, serikali ya Tanganyika (Tanzania) iliamuru kukamatwa kwa mwandishi wa Kitanganyika aliyevujisha habari hizo, Melek Mzirai Kangero.
Baadaye ikajulikana kuwa Hanga na Othman Sharif walikamatwa mjini Dar es Salaam kutokana na shinikizo la Karume aliyewataka watu hao kwa gharama zozote—hata kama ni kwa kuuvunja Muungano. Othman Sharif, msomi kutoka Chuo cha Makerere, alikuwa mmoja wa waasisi wa Afro-Shirazi na kiongozi wa chama Bungeni wakati Karume akishikilia Urais wa chama.
Mara baada ya Mapinduzi ya Zanzibar, kwa kudhani kuwa Othman alikuwa na tamaa ya mamlaka ya kisiasa na uwezekano wake wa kula njama za kuiangusha serikali yake Karume nchini Zanzibar, akisaidiwa na Nyerere, Karume alimwondosha Othman Unguja na kufanywa kuwa Balozi.
Kwanza alikuwa Balozi wa Tanganyika (Tanzania) mjini London, Uigereza, kisha akapelekwa Washington, Marekani. Wakati mmoja, inadaiwa, Othman Sharif aliporudi nchini Zanzibar kwa matembezi aliponyoka kuingia katika kucha za Abeid Karume. Karume alianza kumwandama kama simba anavyoandama windo lake. Kuona hivyo, Nyerere aliingilia kati mara hiyo hiyo akidai kwamba Othman Sharif alikuwa Balozi wa Muungano wa Tanganyika (Tanzania,) na si Balozi wa nchi ya Zanzibar. Karume alipotambua kuwa hakuwa na mamlaka kisheria ya kumdhibiti Othman, alibadili mbinu ya kumtafuta. Nyerere alipogundua hilo alijaribu kufanya kila mbinu aliyoweza ili Othman asirudi nchini Zanzibar.
Baada ya kupoteza wadhifa wa Ubalozi wa Tanganyika (Tanzania) nchini Marekani, Mwalimu Nyerere alimpatia Othman kazi nyingine kwa kumteua kuwa afisa uganga wa mifugo mkoani Iringa. Lakini hiyo haikumzuia Karume kumwandama hadi mkoani Iringa na, kwa mujibu wa kitabu ‘Conflict and Harmony in Zanzibar’, Karume aliwashawishi Wazanzibari watatu waliokuwa marafiki wa karibu sana wa Othman ili wamsaliti.
Watu hao walikubali. Wakafikishwa mbele ya Baraza la Mapinduzi, wakatoa ushahidi kwa kiapo na kudai kwamba ni kweli Othman Sharif alikula njama za kutaka kuiangusha serikali ya Karume nchini Zanzibar. Watu hao walipelekwa kwa Nyerere na kurudia madai hayo hayo. Wakati Nyerere anaelekea kuuamini huo ‘mchezo wa kuigiza’, tayari uhusiano kati yake na Karume ulianza kuingiwa na dosari nyingine. Muungano wa Tanganyika-Zanzibar ulikuwa majaribuni.
Hatimaye Nyerere akasema watu hao watapokea “hukumu ya haki” Zanzibar. Gazeti Ulimwengu (Nov. 19, 1967) katika tahariri yake liliandika kuwa lazima hukumu ya haki itolewe. Kisha likaonyesha kupinga suala la watu kuwekwa kizuizini. Kama matokeo, mhariri wa gazeti hilo, Otini Kambona, alikamatwa. Hata ndugu yake Otini, aliyeitwa Mathias, naye alikamatwa kwa sababu nyingine tofauti kwa madai ya kushiriki katika njama za kuiangusha Serikali.
Kikundi cha viongozi kutoka mkoani Iringa, ambako Sheikh Sharrif alikuwa akifanya kazi, walimsihi sana Nyerere asiruhusu watu hao wapelekwe nchini Zanzibar kwani walijua hatima yao. Jawabu la Nyerere lilikuwa hivi: “…Hili si jambo la ubishi kwa sababu halina uzito wa kubishaniwa. Lakini kama kutakuwa salama, ni vizuri tukajua watu hawa watakuwa salama kiasi gani.” Lakini historia ni shahidi. Hakukuwa na usalama wa kiasi chochote. Wanadamu hawa walinyang’anywa haki yao ya kuishi.
Baada ya kuona kuwa mambo yameshindikana, na kwa kuwa Muungano wa Zanzibar na Tanganyika (Tanzania) ndilo lililokuwa suala kuu katika akili yake, Mwalimu ‘alibwaga manyanga’. Septemba 1969 Nyerere akajikuta akiwapa idhini maofisa wake kuwatoa Kassim Hanga na Othman Sharif wakabidhiwe SMZ serekali ya wauwaji kama walivyo uwaa rai wanyonge wasio na hatia mwaka 1964 ndivyo walivyo wauwa viongozi wa kuu kama Abeid Karume alivyotaka.
Walipelekwa Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Dar es Salaam (DIA), wakipewa maneno ya kuwafariji, na kisha wakasafirishwa kwenda nchini Zanzibar. Hiyo ikawa ndiyo safari yao ya mwisho—angalau safari ya mwisho kutoka Dar es Salaam—tena, inadaiwa, wakiwa na wamefungwa pingu.
Huko ndiko walikokutana na mauti yao, pengine kwa kupigwa risasi—ingawa taarifa nyingine zilisema kuwa waliuawa kwa kuzamishwa katika maji. Lakini, kinasema kitabu ‘Conflict and Harmony in Zanzibar’, hata wale waliomsaliti Othman Sharif nao waliuawa mmoja baada ya mwingine. Machapisho mengine ya kihistoria yanaunga mkono madai hayo. Katika hotuba aliyoitoa Oktoba 1969, ukiwa ni mwezi mmoja baada ya kufanyika kwa mauaji hayo, Abeid Karume alitangaza kuwa watu wanne waliokuwa wakila njama za kuiangusha serikali yake “…wameuawa kwa kupigwa risasi.” Hili alilikiri mwenyewe. Vyanzo kadhaa vinasema kuwa Kassim Hanga, na aliyekuwa Waziri wa Elimu na Balozi wa Tanganyika (Tanzania) nchini Marekani, Sheikh Othman Sharrif, waliuawa nchini Zanzibar na utawala wa Karume akiwa Raisi wa nchi ya Zanzibar. Hata hivyo mauaji hayo hayakuwa mwisho wa mambo. Inaelekea kuanzia hapo, au kabla ya hapo, kulijengeka utamaduni wa kuwakamata watu, kuwaweka kizuizini na hatimaye wengine kuuawa.
Zaidi ya watu kuwekwa kizuizini bila kufunguliwa mashitaka, kulikuwa na madai ya kuweko kwa zile kambi za mateso. Kwa mfano katika miaka ya 1960 na mwanzoni mwa 1970, inasemwa, nchi ya Zanzibar kulikuwa na ile kambi iliyoitwa ‘Kwa Bamkwe’ au ‘Kwa Mandera’. Mkoani Mwanza kaskazini mwa Tanganyika (Tanzania) kulikuwa na (kambi ya) Kigoto. Hiyo ni moja ya kambi zilizokuwa mbaya. Baada ya kuwakamata watu kwa tuhuma za uchawi mwaka 1977 katika maeneo ya Mwanza na Shinyanga, ikijumlishwa na matendo waliyofanyiwa watu hao, ilitosha kumfanya Alhaj Ali Hassan Mwinyi kujiuzulu ‘kwa kuwajibika’.
Ingawa wengi walitarajia kuwa kuwajibika huko kungekuwa ndio mwisho wa Mwinyi katika siasa, Nyerere ‘alimpigia debe’ kuwa Rais wa nchi ya Zanzibar (Jan. 30, 1984—Okt. 24, 1985) na hatimaye Rais wa Tanganyika (Tanzania) (Nov. 5, 1985—Nov. 23, 1995) kwa kura za NDIYO. Kwa mujibu wa kitabu ‘Zanzibar: Kinyang’anyiro na Utumwa’, mwana siasa aliyekuwa Unguja wakati mambo yote hayo yakitokea, Issa bin Nasser Al-Ismaily, anaandika kuwa mwaka 1970 Wazanzibari tisa “walitiwa nguvuni na Serikali ya ASP kwa kisingizio cha kutaka kuipindua serikali hiyo ya wauwaji SMZ.” Wazanzibari hao ni Salim Ahmed Busaidi, Abdallah Suleiman Riyami, Othman Soud, Aziz Bualy, Hemed Said, Muhammed Juma, Muhammed Hamza, Musa Ali na Said Hamoud.
Bila ya kufikishwa mahakamani, Karume aliwahukumu kutupwa gerezani na kupewa kazi ya kuchunga ng’ombe katika uwanda wa “Hanyagwa-Mchana”. Baada ya kifo cha Karume Aprili 1972, “wananchi hao waliuawa wakati wa utawala wa mrithi wa Karume, Aboud Jumbe.” Kitabu hicho kinaomboleza hivi: “…Mwenyezi Mungu mwenyewe anaelewa namna ya kuihukumu dhuluma hii iliyotendeka…; kwani Mwenyezi Mungu ndiye mjuaji wa yote.” Ni kweli kwamba “Mwenyezi Mungu ndiye mjuaji wa yote” kwa sababu hakuna mwanadamu atakayejua yote yaliyotendeka, hasa yale ambayo hayatajulikana kamwe.

Tuesday, May 13, 2014

WAASIA WA MAREHEMU SHEIKH ILUNGA HASSAN KAPUNGU KWA WAZANZIBARI WOTE


MAREHEMU SHEIKH ILLUNGA WAKATI WA UHAI WAKE AKITOWA DAWAA M.MUNGU AMSAMEHE MATHAMBI YAKE NA AMPE PEPO IN SHAA ALLAH

Asalamu alaikhum ndugu zangu Wazanzibari wa Ndani na Nje ya Visiwa Vyetu Adhimu.
Hutuba ya Shekh KISHKI
MAKAMO wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, MaalimSeif Sharif Hamad, alikuwamiongoni mwa maelfu ya Waislamu walioshiriki faradhi kifaya ya kumzika Sheikh Ilunga Hassan Kapungu siku ya Jumaa tatu wiki hii.
Kama alivyosema Sheikh‘Kishki’ katika nasaha zake pale msikitini TIC, Magomeni Kichangani, Maalim Seif kashiriki maziko yale kama Muislamu. Alishiriki kumzika Muislamu mwenzake kama Uislamu unavyo himiza.‘Kishki’ akatumia fursa hiyo kuwazindua viongozi wengine wa kiserikali na wanasiasa kwamba,kuwa kwao madarakani hakuwaondolei wajibu wao wa kidini. Akawataka,wasione fahari tu kujitokeza kushiriki maziko yawana muziki Bongo, ‘Bongo movies’, na mambo kama hayo, lakini vyema zaidi waone fahari kujumuika na Waislamu wenzao katika maziko kama yale ya Sheikh Ilunga.
Katika muktadha huu,pamoja na kuchukuliwa kwamba Maalim kaja kama Muislamu, na si kama kiongozi wa kisiasa au kama Mzanzibari, lakini pengine ingekuwa vyema kutumia fursa hii kusema yale ambayo Sheikh Ilunga aliyasema mwaka 2011 kama nasaha zake kwa Maalim Seif na viongozi wenzake wa nchi ya Zanzibar na Wazanzibari wote kwa ujumla. Katika muhadhara wake mmoja kule Pemba nchini Zanzibar, Sheikh Ilunga alisema kuwa kabari ya mfumo kristo imewakaba barabara Wazanzibari,hawafurukuti. Hata hivyo,pamoja na hali hiyo,Sheikh Ilunga aliwataka Wazanzibari kuto kukata tamaa, bali watumie fursa zilizopo kurejesha hadhi yao.
Fursa ya kwanza akasema ni wao kuwa Waislamu. Akawataka watizame kwanza hadhi ya Uislamu, ndio ifuatie nchi yao na dola yao. Alisema kuwa,Wazanzibari ni lazima watumie maridhiano ya kisiasa yaliyopo ili kuleta maridhiano ya Kiislamu. Kwamba amani iliyopo itumike kuimarisha udugu wa Kiislamu, watu wajitambue kwamba wao ni Waislamu kwanza kabla ya jambo jingine lolote. Ni Waislamu kabla ya CUF, Ni Waislamu kabla ya CCM na ni Waislamu kabla ya kuwepo Tanganyika (Tanzania) na Muungano wake. Akasema hilo linahitaji Da’wah ya kutosha na watu warejee katika Qur’an walonena kutafakari jinsi Mwenyezi Mungu anavyo waonya juu ya kuwafanya Mayahudi na Manasara kuwa marafiki na wasiri wao.
Akawakumbusha pia kuwa Qur’an imesema wazi kwamba chuki iliyofichwa na Manasara ndani ya vifua vyao ni kubwa mno kuliko wanayo idhihirisha na kwamba hawataridhia mpaka wawaritadishe Waislamu, japo wabakie Waislamu wa majina lakini makafiri kwa kauli, vitendo na maadili. Kufuatia kauli ya Bwana William Lukuvi Kanisani na Bungeni, bila shaka maneno haya ya Shekh Ilunga yanathibitika zaidi. Kwamba ipo chuki dhidi ya Uislamu na Waislamu. Na hiyo namna pekee ya kukabiliana nayo, ni kujitizama kama Waislamu, kama Lukuvi na waliokuwa Kanisani pamoja naye walivyo jitizama kama Wakristo kutoa hofu yao dhidi ya Waislamu walio wengi nchini  Zanzibar.
Baada ya neema ya Uislamu, na fursa ya kuwepo maridhiano na serikali ya umoja wa kitaifa ( G.N.U), shekh Ilunga alitaja fursa nyingine kuwa ni mabadiliko ya katiba yanayokuja. Akasema, ni lazima fursa hiyo itumike vizuri kuhakikisha kuwa kichaka kinachoficha mfumo kristo kinapigwa moto. Na hiyo itafanyika kwa kuwa na muungano wahaki ambapo pande mbili za Muungano, Tanganyika na Zanzibar zitakuwa na haki sawa, sio huu wa serikali ya Tanganyika kujivika joho la Serikali ya (Tanzania.)
Shekh Ilunga alimalizia kwakuwapa changamoto viongozi wa serikali ya nchi ya Zanzibar, Shein,na Makamo wake wawili, Maalim Seif Sharif Hamad na ((Balozi Seif Ali Iddi Balozi ndogo wa nchi ya Tanganyika)) kwamba wao wametoka katika migongo ya wazee wa Kiislamu na hivyo, hawawezi kukwepa jukumu la kuona hadhi ya Uislamu inarudi kama ilivyokuwa wakati wakilelewa na wazee wao. Kabla ya kutoa nasaha hizo, Sheikh Ilunga alisema kuwa mfumo wa Muungano uliopo umekuwa kama
kichaka unakojificha mfumo kristo kuiburura nchi ya  Zanzibar katika idhilali kwa kuipora nguvu zake za kisiasa na kiuchumi na kubwa zaidi kuhujumu Uislamu na Waislamu.
Aliyabainisha hayo katika kongamano lililofanyika katika eneo la Markazi Tabligh, Ole Kianga, Pemba nchini Zanzibar Jumapili Oktoba 2011. Kongamano hilo lililohudhuriwa na maelfu ya Waislamu kutoka sehemu mbalimbali za Pemba, lilijadili hatari ya mfumo kristo kwa nchi ya Zanzibar na Tanganyika (Tanzania) kwa ujumla. Awali Sheikh Ilunga Hassan Kapungu alisema kuwa, inaweza kuwa jambo lisilo eleweka ukizungumzia mfumo kristo alisema japo kwa vile takriban viongozi wote waserikali na taasisi muhimu nchini  Zanzibar ni Waislamu, Wapemba na Waunguja. Hata hivyo akasema kuwa,ile kuwa inaitwa ni serikali ya Zanzibar haina maana kuwa Serikali hiyo ni serikali inayo ongoza dola kwani mamlaka yote ya kisiasa yapo katika serikali ya muungano.
Akifafanua alisema kuwa yapo mambo ambayo Wazanzibari wangetaka kufanya au kuamua kwa masilahi ya Nchi yao ya Zanzibar. Lakini hawawezi kuyafanya kwa vile Muungano umewapora nguvu za kisiasa. Na kwamba, yale mamlaka ya kidola na kisiasa ya nchi ya Zanzibar yalizikwa nakusomewa talakini siku ASP ilipoungana na TANU ambapo CCM ilishika hatamu na maamuzi yote muhimu kuwa yanafanyika Dodoma. Akitoa mfano alitaja uchaguzi mkuu ambapo jina linalopitishwa kugombea Urais laweza kuwa lile ambalo halikupata ridhaa ya Wazanzibari. Na hata kuondoka madarakani, kiongozi anaweza kuondolewa bila ya Wazanzibari wenyewe waliompigia kura au vyombo vyao vya uwakilishi kama Baraza la Wawakilishi kuhusishwa. Akataja mfano wa Mzee Aboud Jumbe aliye kwenda mkutanoni Dodoma akiwa Rais akarudi Urais akiwa ameuacha Dodoma. Sheikh Ilunga kwa kutoa mfano huo alisema kuwa Alhaj Aboud Jumbe, yalimfika kwa sababu alihoji Muungano nakuhoji kwenyewe si kutaka kuuvunja, bali kutaka uwe wa haki.
“Yalimfika.” “Kwa nini..?”
“Kwa nini imefanywa kuwa mwiko kuhoji Muungano..?” Alisema na kuhoji Shekh Ilunga. Kabla ya kutoa jawabu, Sheikh Ilunga alirejea pia hali ilivyokuwa wakati wa Mzee Abeid Aman Karume ambaye alishaonesha kuwa koti la Muungano linambana, lakini mauti yakamfika muda mfupi kabla ya kutimiza nia yake ya kulivua. Aligusia pia yaliyo mfika Maalim Seif Sharif Hamad, hata hivyo hakutaka kufafanua bali akawataka Wazanzibari wenyewe wamuulize Maalim nini kilimkuta na kwa nini...? Katika kukamilisha hoja yake akasema kuwa Muungano umefanywa jambo nyeti na mwiko kujadiliwa kwa sababu ndio uchochoro na kichaka mfumo kristo unakopitia kuiua nchi ya Zanzibar na kuuwa Uislamu.
Katika hali hiyo akasema kuwa, Wazanzibari watakuwa wakiwalaumu na pengine hata kuwachukia bure viongozi wao, lakini nao wanashindwa kufanya yanayotakiwa na Wazanzibari kwa sababu inabidi kwanza watizame Dodoma inasema nini. Kwa maana kuwa jambo kama halijapata ridhaa yamfumo Kristo, haliwezi kuwa kama ambavyo haikuweza nchi ya Zanzibar kujiunga na OIC na hivi sasa Tanganyika (Tanzania) haiwezi kujiunga na jumuiya hiyo kwa sababu Maaskofu hawataki, mfumo kristo hautaki. Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mheshimiwa Bernad Membe aliliambia rasmi Bunge kuwa serikali haioni tatizo Tanganyika (Tanzania) kujiunga na OIC, lakini ghafla msimamo ukabadilika baada ya kuitwa na Kardinali Pengo.
JE VIONGOZI WA CCM NCHINI ZANZIBAR DINI YENU SASA NI CCM NA SIO UISLAMU TENA....????

Friday, May 9, 2014

SWALI KWA LUKUVI VITA VIKALI VYA MAKABILA INAYOENDELEA KITETO NCHINI TANGANYIKA NI KWA SABABU WAZANZIBARI WAMEDAI NCHI YAO....?


Kwa mujibu wa taarifa kupitia mitandao ya kijamii ikiwa ni pamoja na mtandao wa http://www.jamiiforums.com/ ni kwamba makabila ya wafugaji ya kimasai yanapigana vikali hivi sasa kati yao na makabila ya wakulima. Inasemekana kwamba mgawanyo wa rasilimali, upendeleo, ubaguzi na ukandamizaji kwa baadhi ya makibila dhidi ya mengine ndio uliopelekea kuzuka vita hiyo kali ambayo hadi sasa inasemekana si chini ya watu watatu (3) wameuliwa.
Mmoja kati ya waliouliwa alichinjwa kinyama kama kuku kama inavyoonekana hapo kwenye picha. Milio ya risasi na kuchomeana nyumba moto pia imetokea ktk eneo hilo huku viongozi wa kisiasa na kiserkali YA TANGANYIKA wakilaumiana kwa kuchochea mgawanyiko huo kwa njia ya kupendelea wafugaji badala ya kutenda haki. Sasa LUKUVI kazi kwako, usijeukasema wanauana kwa sababu ya serikali 3 bado tuko kwenye 2. Jee ni uamsho waloyafanya haya ya watanganyika kuchinjana kama kuku.....? lukuvi wacha kasumba zako na shughulikia Yatanganyika ya Zanzibar hayakuhusu au utakufa nacho kijiba cha roho.