Thursday, June 12, 2014

HATA BARABARA HII PIA BASI TUNASUBIRI MAMLAKA KAMILI CUF.....????


Hii ni barabara ya Mtendeni mjini magharibi kabisa, inayopitwa na wananchi na viongozi wengi, hususan Makamo wa Kwanza wa Rais wa nchi ya Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad.
Mtendeni, kabla, ilikuwa ndani ya Jimbo la Mlandege lililokuwa chini ya uongozi wa Mh Kamal Basha Pandu na Bi Fatma Said Ali. Ambao kwa miaka mingi walikuwa mawaziri waandamizi wa serikali zote mbili.
Mwaka 2005, Mtendeni ilijumuishwa ndani ya Jimbo la Mji mkongwe, chini ya uongozi Mh Ibrahim Sanya na Mh Fatma Ferej na Mh Ismail Jussa.
Lakini barabara hii ni maarufu kwa kuwa ndio inayoelekea Makao makuu ya Chama cha Wananchi – CUF. Leo barabara hii inapitwa angalau kila wiki mara moja na Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar. Sio jambo la kushangaza kusikia ving’ora vikilia pale Makamo anapokwenda ofisini kwake.
Lakini kuna tofauti gani ya ubora wa barabara hii baina ya kipindi kile cha uongozi wa CCM na sasa chini ya uongozi wa CUF...??

No comments:

Post a Comment