Sunday, June 15, 2014

MCHANGO WA WAISLAMU KUPIGANIA UHURU WA NCHI YAO TANGANYIKA NI MKUBWA SANA LAKINI KWA NINI LEO WAO NDIO WANAO ATHIBIWA...???

WAZEE WA TANU
Waliokuwa Katika Picha Hii ni Wazee wa TANU waliopigania uhuru wa Tanganyika wa Kristo ni wawili 2 kwenye list hii.
Kila anaye kata kuto kuikubali Tanganyika au kuto kuizungumzia Tanganyika anaogopa haya maana anajuwa wakizungumza kuhusu Tanganyika itakuwa je nani walio gombea uhuru wakitajwa wengi wao huwa hawafurahi wataje kwa kuwa ni waislamu au kwa sababu zao nyengine wenyewe wanazijuwa wenyewe ndio ukaona wanashika bango la nyerere weee nyerere weee wakati nyerere mwenye alipojiunga na TANU watu walikuwa tayari washagombania uhuru kwa miaka mingi nyuma kabla yeye toka enzi za chama cha TAA na kabla ya chama cha TAA waislamu walikuwa wakidai uhuru leo hii wamekuwa kama wageni kaika nchi yao au mayatima.
1. Abdallah Shomari (Tandamti No. 3)
2. Nassoro Kalumbanya (Simba)
3. Said Chamwenyewe (Aggrey/Congo)
4. Mtoro Ally (Muhonda)
5. John Rupia (Misheni Kota)
6. Julius Nyerere (Pugu Sekondari)
7. Said Chaurembo (Congo/Mkunguni)
8. Jumbe Tambaza (Upanga)
9. Sheikh Suleiman Takadir (Mafia/Swahili)
10. Dossa Aziz (Mbaruku/Somali Kipande)
11. Mshume Kiyate (Tandamti)
12.Juma Sultani (Kitchwele Karibu na Kanisa Dogo)
13. Maalim Shubeti (Masasi/Likoma)
14. Rajab Simba (Kiungani)
15. Waziri Mtonga (Kilosa 18, Ilala)
16. Mwinjuma Mwinyikambi (Mwananyamala)
17. Makisi Mbwana (Aggrey/Congo)
18. Usia Omari (Sungwi, Kisarawe)
19. Sheikh Issa Nasir (Bagamoyo).
Hakuna shaka kuwa mchango wa waislamu katika harakati za kupigania uhuru wa nchi ya Tanganyika ulikua mkubwa lakini baada ya uhuru na mpaka leo hii jee waislamu walithaminiwa au kanisa lilichukua mkondo wake....????

1 comment:

  1. Tena wazaramo, na watu wa pwani Leo ukarimu wao wamegeukiwa.

    ReplyDelete