Friday, June 13, 2014

NCHI YETU YA ZANZIBAR TULIKUWA TUKILALA MLANGO WAZI LEO HII NI KAMBI YA MAJAMBAZI WENYE SILAHA ZA MOTO (AKA 47,BASTOLA n.k)

Msikecorner199
Kutoka kwenye kulala mlango wazi mpaka sasa tunamageti na pia hatuna tena salama katika nchi yetu ya Zanzibar na hii yote inasababishwa na kutokuwa na kizuizi cha ingia toka katika mwambao wa visiwa vyetu vidogo vidogo na nchi yetu Zanzibar kwa ujumla watu wanaingia tu kama vile jalalani maana hata choo pia kinahishima yake maana lazima ugonge mlago ujuwe kama kuna mtu utasubiri kama hakuna ndio utaingia lakini jaani unakwenda tu na kutupa uwoza wako ndio nchi yetu ya Zanzibar ilivyo fanywa na wahafidhini ganga njaa ya matumbo yao,
 ile sifa na haiba ya Amani na Utulivu katika visiwa au nchi yetu ya Zanzibar imeondoka na sasa imebakia ni kisiwa cha Majambazi na vitendo vya Uharamia wakutisha hata wizi wakutumia silaha za moto (Risasi) sasa limekuwa ni jambo la kawaida good jobb asha bakari makame na balozi mdogo wa tanganyika.
Huko Nyuma Wananchi wa nchi ya Zanzibar hatukuzowe kuona haya na hivi sasa ni hali ya kawaida tu katika nchi yetu ya Zanzibar kuyaona haya au kusikia vitendo hivi vikifanyika ndani ya nchi yetu ya Zanzibar.
Hali hii ni yakujaa Zanzibar na sio utamaduni ulozoweleka kwa Wananchi wa nchi ya Zanzibar.
Hivi sasa akina mama wanashindwa kutembea peke yao ikingia kiza tu kwa kuogopa na hofu ilotanda wakati ilikuwa baada ya maghari mama zetu huka barazani na kupunga upepe wa marashi ya karafu sasa kuna jipepo la majambazi nje hakukaliki ,ukenda badhi ya maeneo kama vile Masokoni majumba yalokua yamejengwa hayaja malizika kuna makundi ya wageni wenye kulala lala ovyo Serekali haina ijuwala zaidi ya fitina na ubaguzi na chuki basi wananchi wa nchi yako hawana raha wao habari hawana kazi kuiba mapesa na kupandikiza chuki.  
Wengi wao wanakua ndio hao majambazi na wenye kupora watu wamo katika majumba ambayo hayajamalizwa ndimo wanamo lala na kupanga jinsi gani ya kuwahujumu rai na wananchi wa nchi ya Zanzibar.tumulize Shein lile jeshi lako la polisi lililokwenda kuwapinga watu msikitini kwajili yakuwaombea watu walio zama na meli linafanya kazi gani...? au ile ndio kazi yao kuwahujumu wananchi wa Zanzibar kama wanavyo hujumiwa na hawa majambazi...?
Serekali ya majambazi Smz hebu wambiyeni hao majambazi wenu watafute kwengine kwa kwenda la sivyo yatakayo wakuta musije kuwalaumu Wazanzibari na nyinyi SUK nilazima iwe na operation malumu ya walala lala ovyo musituzinguwe.

No comments:

Post a Comment