Wednesday, June 4, 2014

RAISI MPYA WA NCHI YA MALAWI KIBOKO YA WATANGANYIKA SIO SHEIN KILA KITU HEWALA BWANA TANGANYIKA


PEOPLES’ POWER
Dar es Salaam nchini Tanganyika. Wingu jeusi limeanza kutanda kuhusu hatima ya mzozo wa Ziwa Nyasa kutokana na msimamo wa hivi karibuni wa kiongozi wa Democratic Progressive Party (DPP), Peter Mutharika ambaye sasa ni Rais mpya wa nchi ya Malawi.
Hiyo inatokana na msimamo wa Mutharika ambaye ni Profesa wa Sheria wa kupinga kuendelea kujadiliana na nchi ya Tanganyika kuhusu nani mwenye haki ya kumiliki ziwa hilo alioutoa wakati alipowatembelea wananchi wa Chipoko, kando ya ziwa hilo miezi michache kabla ya uchaguzi mkuu ambao ulimwigiza madarakani.
Pamoja na kwamba mazingira ya msimamo huo yanaweza kutofautiana na hali halisi ya sasa, tofauti za kisiasa baina yake na mtangulizi wake, Joyce Banda zinaweza kuongeza msukumo mpya wa kutaka kutoendelea na mazungumzo ya mpaka wa ziwa hilo.
Akizungumza na wananchi hao, Profesa Mutharika aliwatoa wasiwasi na kuwataka kuendelea na shughuli zao kama kawaida kwa maelezo kuwa ziwa hilo lipo kwenye himaya ya nchi ya Malawi na kwamba kuendelea kujadiliana na nchi ya Tanganyika ni kupoteza muda.
“Hakuna haja ya kuendelea kujadiliana, Ziwa Malawi ni mali ya Malawi na litaendelea kuwa la Malawi daima,” alisema Mutharika ambaye pia amewahi kufundisha sheria Chuo Kikuu cha Dar es Salaam nchini Tanganyika.
Alimshutumu Banda na kudai alikuwa dhaifu kiasi cha kutoa fursa kwa Tanganyika kutumia udhaifu huo kutaka kupora ziwa hilo.
“Ziwa hili letu ila Tanganyika inatumia tu udhaifu wa Serikali iliyopo kwani wenyewe wanajua ndani ya mioyo yao kuwa hawana chochote katika ziwa hilo. Tutakaporejea serikalini mwakani haya mambo yote yasiyo na kichwa tutayamaliza. Nataka niwahakikishie kwamba tutapeleka meli zaidi kwenye ziwa hili ili kuinua shughuli zetu za kiuchumi na kutengeneza ajira kwa vijana wetu.”
Hata hivyo, wiki iliyopita Serikali ya Tanganyika ilitoa msimamo wake kuhusu mzozo huo wa mpaka na kudaia kuwa itaendelea kujadiliana na nchi ya Malawi.
Akizungumza bungeni wakati akiwasilisha Bajeti ya wizara yake, Waziri wa Mambo ya nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe alisema Tanganyika ilikuwa ikifuatilia kwa karibu uchaguzi wa Malawi na kwamba iko tayari kufanya kazi na serikali yoyote itakayoingia madarakani.
Nishara kuwa nchi ya Tanganyika ishajuwa kuwa Raisi wa mara hii wa Malawi sio mtu wa kuchezea ndio maana wakajidai wako tayari kufanya kazi, kazi gani....??

1 comment:

  1. Mutharika ni mtoto mdogo sana kwa Tanganyika na majeshi yake, uzuri tulifundishwa adabu na nyerere ya kumuheshimu mwafrika mwenzetu ila kama ata leta USENGE utaona kitakacho mkuta maaana uwezo tunao na nia tunayo atapigwa tu, kwa kuwa kama umeshawai kufika malawi ni kwamba ana kajeshi kadogo na dhaifu ambacho akana ata Air force kamandi

    ReplyDelete