Wednesday, June 11, 2014

SH 150,000 KWA SIKU MBALI MSHAHARA SH 4.5 MILLIONI KWA MWEZI KWA KILA MJUMBE WA BARAZA LA WAWAKILISHI NA WALA HAWAHUTHURI VIKAO NA NCHI INANUKA
Nchini Zanzibar. Kikao cha Baraza la Wawakilishi nchini Zanzibar (BLW), kimeahirishwa kwa mara ya pili kutokana na idadi ya wajumbe kutokuhudhuria vikao na kushughulikia miradi yao kwa mujibu wa kanuni za uendeshaji wa chombo hicho cha kutunga sheria,nchini Zanzibar.
Kikao hicho kiliahirishwa na Naibu Spika, Ali Abdallah Ali jana saa kumi na moja jioni baada ya Mwakilishi wa Mji Mkongwe (CUF), Ismail Jussa Ladhu kutoa hoja kutokana na mahudhurio ya wajumbe kutokamilika.
Jussa alisema BLW Zanzibar linaendeshwa kwa kuzingatia kanuni na suala la kukamilika kwa idadi ya wajumbe wanaotakiwa limepewa uzito na chombo hicho na kumtaka Naibu Spika kutoa hoja kutokana na hali iliyojitokeza.
“Mheshimiwa Naibu Spika, chombo chetu kinaongozwa na kanuni, idadi ya wajumbe iliyopo ni ndogo kimuonekano na hesabu yake, naomba kutoa hoja na kupendekeza kikao kiahirishwe kutokana na upungufu huo,” alisema Jussa.
Baada ya kuwasilisha hoja hiyo, Naibu Spika aliungana na Jussa na kuahirisha kikao hicho hadi leo asubuhi.
Baraza hilo lilikuwa liketi jana jioni kama kamati ya matumizi kupitia na kupitisha vifungu vya matumizi ya Wizara ya Uwezeshaji, Ustawi wa Jamii, Vijana, Wanawake na Watoto ya Sh7.5 bilioni ambayo yaliwasilishwa na Waziri wake, Zaynab Omar Mohamed.
Mara ya kwanza kuahirishwa kwa kikao hicho kutokana na akidi ya wajumbe wake 82 kutokuhudhuria katika vikao  ilikuwa Mei 26, mwaka huu. Hadi kikao hicho kinaahirishwa kulikuwa na wajumbe 26 na wengine hawajulkani waliko wala wamefikwa na nini wala hawajaeleza ni kwa nini hawakuhudhuria vikao.
Baadhi ya wajumbe wa BLW nchini Zanzibar wamekuwa wakitumia usafiri wa daladala kwenda na kurudi kutoka kwenye kikao hicho na wengine kutofika kwa muda mwafaka tangu kufanyika kwa mabadiliko ya vituo vya usafiri huo katika Manispaa ya Mji wa nchi ya  Zanzibar ati hicho ndio kisingizio.
Wajumbe wa Baraza hilo kila mmoja hulipwa posho ya kikao ya Sh150,000 kwa siku mbali na mshahara wa Sh4.5 milioni kwa mwezi.
sibora basi hiyo mishahara yao ikatwe na pesa zinunuliwe vitanda vya hospitali au tuanzishe umeme wetu wenyewe au maji safi lakini wapi nchi hii kama iliyo laniwa astahafiri allah.

No comments:

Post a Comment