Sunday, July 13, 2014

NCHINI ZANZIBAR WANAO JIITA POLISI WANAWAGONGEA WAZANZIBARI MAJUMBANI MWAO USIKU WAKIWASHIKA NA KUWASAFIRI NCHI JIRANI TANGANYIKA FAMILIA ZA WATU WALIO CHUKUKULIWA HAWAJUWI WAHAI AU.......

Kamishna wa Polisi Zanzibar, Hamdan Omar Makame
Kamishna wa Polisi wa nchi ya  Zanzibar, Hamdan Omar Makame je habari unazo kuwa rai wako na mwezi huu mtukufu wa ramadhani wanakamatwa majumbani mwao kabla ya kula daku kisha wanapakiwa ndani ya denge usiku na kupelekwa nchi ya jirani Tanganyika na mpaka sasa familia zao hawajuwi waume na watoto wao wako wapi wahai au washauliwa...? je Hamdan Omar Makame wewe unazo tarifa hizo......?? maana wanao kwenda kuwashika wazanzibari kwenye majumba ni polisi na wewe Hamdan Omar Makame ni............????


Nchini Zanzibar: Kumeibuka kamata kamata ya watu atii wanaotuhumiwa kuhusika na milipuko ya mabomu katika maeneo mbalimbali ya Mji Mkuu wa nchi ya Zanzibar na baadaye wahusika husafirishwa nyakati za usiku kisiri siri kwenda nchi ya jirani nchi ya Tanganyika imefahamika nchini Zanzibarmambo hayo jana.
Madai hayo yametolewa na familia za watu hao wakati walipozungumza na waandishi wa habari Kikwajuni Welesi mjini hapa nchini Zanzibar na kudai watu kadhaa wameshakamatwa na kusafirishwa kwa siri siri usiku kwa ndege chini ya ulinzi mkali na kupelekwa nchi ya jirani Tanganyika.
Aisha Othman mkazi wa Tomondo, alisema mume wake Hassan Bakar Suleiman alikamatwa usiku wa manane akiwa amelala.
“Niliwasikia watu usiku wakiita jina la mume wangu na kumtaka atoke nje kwamba ana wageni wake, tulipochungulia dirishani tulibaini kuwa ni polisi waliokuwa na silaha,” alisema Aisha.
Anasema mume wake aligoma kutoka kwa kuhofia usalama wake, lakini alikubali baada ya kushawishiwa na jirani yake ambaye naye aligongewa mlango na polisi hao.
Aisha alisema Naibu Sheha alitumika kumshawishi mume wake atoke nje kwa kumuhakikishia usalama wake lakini alipotoka alitiwa pingu na kuingizwa katika gari la polisi.
Swalha Hamid Hemed naye alisema mume wake, Nassor Hamad Abdallah na mke mwenzake, Salma Khamis walisema mume wao alichukuliwa usiku kwa kishindo kilichoambatana na kupigwa risasi hewani.
 je serekali ya mapinduzi inayajuwa haya na kama inayajuwa anasemaje kuhusu rai wake wanakuja wakichukuliwa majumbana mwao usiku usiku na kusafirishwa kisiri siri kwenda nchi jirani je huko wanafanywa nini..? wanao kuja kuwachukuwaa ni polisi je kwa nini usiku usiku...?

No comments:

Post a Comment