Saturday, August 30, 2014

VIDEO-KAMATI YA MARIDHIANO SIX PART 1/5 ZLS PRESS CONFRNCE 27th AUG 2014 ON LAW/COURT JURISDICTION

PART 1
PART 2

PART 3
PART 4
PART 5
KAMISHNA WA POLISI NCHINI ZANZIBAR AJIUZULU NA ASHTAKIWE KWA KUVUNJA KATIBA YA NCHI YA ZANZIBAR JAJI SEPETU AJIUZULU NA ASHATAKIWE KWA KUKANA NDANI YA MAHAKAMA KUWA KATIBA YA NCHI YA ZANZIBAR HAIKUVUNJWA,SHEIN AJIUZULU POLISI WOTE WALIO HUSIKA KUWAKAMATA WAZANZIBARI USIKU KATIKA NYUMBA ZAO NA KUSHIRIKIANA NA WENGINE KUWASAFIRISHA WAZANZIBARI MPAKA KWA MKOLONI MWEUSI TANGANYIKA NAO WAFUKUZWE KAZI NA KUSHTAKIWA PIA SHEHA WALIO SHIRIKIANA NA POLISI KUGONGA NYUMBA ZA WAZANZIBARI NA KUWAPA FURSA NZURI POLISI KUWASHIKA WAZANZIBARI USIKU WA MANANE KINYUME CHA SHERIA WAJIUZULU USHEHA NA WAO PIA WASHTAKIWE ILI LIWE SOMO KWA WATU WENGINE WOTE WANAO TUMIA MADARAKA VIBAYA NA KUVUNJA KATIBA YA NCHI YETU YA ZANZIBAR BILA YA KUJALI NA KUJIONA KUWA WAO SHERIA HAITA WAGUSA.

KILA MZANZIBARI ATAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO HAITAKUFA SIKU HIYO.

Friday, August 29, 2014

ASKARI MAKIMA JAJI MKUSA ISAAC SEPETU SOKWE VIONGOZI WA SEREKALI MAGORILA SISI WAZANZIBARI WAANADAMU TUTAPONA KWELI...????


HUYU NDEYE MKUSA ISAAC SEPETU AKITOA UAMUZI WA KESI

Nchini Zanzibar. Mahakama Kuu ya nchi ya Zanzibar imesema mashtaka atii ya ugaidi yanaweza kufunguliwa katika mahakama yoyote baina ya pande mbili za Muungano feki wa Tanganyika na Zanzibar kama ilivyotokea kwa Wazanzibari 14 waliokamatwa nchini Zanzibar na kufunguliwa mashtaka yao Tanganyika.
Akitoa uamuzi katika kesi ya maombi iliyofunguliwa dhidi ya viongozi wa Polisi wa nchi ya Zanzibar na washtakiwa hao 14 wanaopinga kukamatwa nchini Zanzibar na kufunguliwa mashtaka Tanganyika, Jaji wa Mahakama Kuu ya nchi ya Zanzibar, Mkusa Isaac Sepetu alisema hakuna sheria wala Katiba iliyovunjwa.
Jaji Sepetu alisema baada ya kusikiliza hoja za pande zote mbili, Mahakama Kuu imejiridhisha kuwa Sheria ya Ugaidi Namba 2 ya mwaka 2002, iliyotumika kuwafungulia mashtaka inatoa uwezo wa kukamata na kufungua mashtaka katika eneo lolote la Jamhuri ya Muungano feki wa Tanganyika.
Jaji Sepetu alisema ombi la Wazanzibari hao la kuitaka Mahakakama Kuu ya nchi yao ya Zanzibar itoe amri kwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ya Mkoloni Mweusi Tanganyika kuwaachia huru watuhumiwa hao ni sawa na kuingilia uhuru wa mahakama nyingine iliyopo katika upande mmoja wa Muungano feki ambayo inatakiwa ifanye kazi bila ya kuingiliwa na upande mwingine.
Jaji Sepetu alisema ombi lililofunguliwa na walalamikaji halina nguvu za kisheria kwa vile limefunguliwa nje ya wakati huku watuhumiwa wakiwa wamefikishwa mahakamani siku tisa kabla Wazanzibari hao kuwasilisha maombi yao Mahakama Kuu ya nchi ya Zanzibar ya kupinga kushtakiwa Tanganyika.
Jaji huyo alisema Mkurugenzi wa Mashtaka wa nchi ya Tanganyika (DPP mashuzi) aliwafikisha watuhumiwa mahakamani mnamo Julai 17 wakati maombi ya Wazanzibari hao ya kupinga kukamatwa na kufunguliwa mashtaka yao huko nchini Tanganyika yalifunguliwa Julai 28, mwaka huu.
“Kama waombaji wanapinga uamuzi huu, wanaweza kufungua maombi yao katika Mahakama Kuu ya nchi ya Tanganyika kupinga wateja wao kushtakiwa upande wa pili wa Muungano feki,” alisema Jaji Sepetu.
Vilevile, alisema Mahakama Kuu ya nchi ya Zanzibar haina mamlaka wala uwezo wa kuchukua hatua ya kuingilia uhuru wa mahakama nyingine hasa kwa kuzingatia watuhumiwa hao hawapo tena mikononi mwa Polisi, wapo ndani kwa amri ya Mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu ya Mkoloni Mweusi Tanganyika na kushikiliwa katika Gereza la Segerea la Mkoloni Mweusi Tanganyika.
Hata hivyo, Jaji Sepetu alilitaka Jeshi la Polisi la Mkoloni Mweusi Tanganyika liliopo nchini Zanzibar kutekeleza majukumu yake kwa kufuata sheria na taratibu ili kuepuka malalamiko yasiyokuwa ya lazima hususan suala la ukamataji na kuepuka kukaa na watuhumiwa nje ya wakati kwa mujibu wa sheria bila ya kuwafikisha mahakamani.
Kwa mujibu wa hati ya kiapo, Wakili Abdallah Juma alisema wateja wake walikamatwa na kufunguliwa mashtaka kinyume na Kifungu cha 56 a(1)(3) kinachotoa mamlaka pekee kwa Mkurugenzi wa Mashtaka wa nchi ya Zanzibar kufungua na kushughulikia mashtaka yoyote ya jinai dhidi ya mtu yeyote mbele ya mahakama yoyote isipokuwa ya kijeshi.
Alisema kitendo cha kuwakamata na kutowafikisha katika Mahakama za nchi yao ya Zanzibar ndani ya saa 24, kilivunja Katiba ya nchi ya Zanzibar ya mwaka 1984, Kifungu cha 14(1) na 16(1) vinavyotoa uhuru wa kila mtu kuwa na haki ya hifadhi ya maisha yake na kutonyimwa uhuru wake wa kwenda popote, haki ya kuishi katika sehemu yoyote ya nchi ya Zanzibar.
Wazanzibari hao 14 walifunguliwa mashtaka atii ya kula njama za ugaidi katika maeneo mbalimbali ya Jamhuri ya Muungano feki wa nchi ya Tanganyika ya Mkoloni Mweusi Tanganyika kinyume na Kifungu cha 21 cha Sheria atii ya Ugaidi cha Sheria Namba 2 ya mwaka 2002.

KILA MZANZIBARI ATAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO HAITAKUFA SIKU HIYO.

ZAHOR MAZRUI AWAPA JESHI LA POLISI LA MKOLONI MWEUSI TANGANYIKA LILIOPO NCHINI ZANZIBAR VITENDA KAZI TUNAKUKUMBUSHA ZAHOR MAZRUI USISAHAU KUWALETEA MAJITI NA CHUPA PIA NI VITENDA KAZI ILI WAWATHIBU VIZURI WAZANZIBARI

Bwana Zahor Mazrui akimkabidhi radio call kamishna wa Jeshi la Polisi Zanzibar Hamdan Omar.
Jeshi la Polisi la Mkoloni Mweusi Tanganyika liliopo nchini Zanzibar limesema litaendelea kuthamini jitihada za wasamaria wema wenye nia ya kulipatia jeshi hilo msaada wa vitu mbali mbali kama vitendea kazi.
Kauli hio imetolewa na Kamishna wa Jeshi la Polisi la Mkoloni Mweusi Tanganyika liliopo nchini Zanzibar Hamdani Omar Makame, wakati alipokuwa akipokea msaada wa vitu mbali mbali kwa ajili ya kupeleka mbele harakati za Jeshi hilo kukabiliana na Wazanzibari wote wanao pigania haki ya nchi yao kuwa huru na kujivuwa katika mikono ya Mkoloni Mweusi Tanganyika pia aina mbali mbali kama kuwatharaulisha Masheikh,Wazanzibar kwa ujumla Nchini huko makao makuu ya Polisi Ziwani nchini Zanzibar.
Hamdan ameleza kuwa msaada huo uliotolewa na Katibu mtendaji wa jumuia ya Zanzibar Cheretable Society Bwana Zahor Mazrui umekuja kwa wakati muafaka kutokana na changa moto kadhaa zinazolikabili Jeshi la Polisi la Mkoloni Mweusi Tanganyika liliopo nchini Zanzibar.
Akibainisha miongoni mwa Changamoto zinazolikabili Jeshi la Polisi la Mkoloni Mweusi Tanganyika hapa nchini Zanzibar Kamishna huyo amesema ni uhaba wa majengo sambamba na vitendea kazi.
Hivo ametoa wito kwa wasamaria wema wenye moyo kama wa Bwana Zahor Mazrui kujitokeza kwa ajili ya kulisaidia jeshi hilo la Mkoloni Mweusi Tanganyika ili liweze kufanya kazi zake kwa ufasaha wa kuwathibiti Wazanzibari wote wao taka nchi yao kuwa huru.
Mara baada ya kukabidhi msaada huo wa Computer 10 radio call 30 printer 2 pamoja na calculate 90,Mkurugenzi mtendaji wa Zanzibar Cheretable Society Bwana Zahor Mazrui amesema ameamua kutoa msaada huo kwa jeshi la polisi ili wawe na nyenzo imara za kufanyia kazi ili kudhibiti wahalafu nchini Zanzibar.
Amebaisha kuwa msaada huo kwa jeshi hilo la Mkoloni Mweusi Tanganyika hautokuwa wa mwanzo na ataendelea kila pale anapopata wasaa kwani si jambo baya kusaidia Polisi.
”Wako watu wananishangaa sana kwa nini nawapa msaada jeshi la polisi la Mkoloni Mweisi Tanganyika lakini sitosita kwa sababu msaada utawafanya watende kazi zao kwa uadilifu”alieleza Bwana Mazrui.
Sambamba na hayo ametoa shukrani zake kwa jeshi hilo la Mkoloni Mweusi Tanganyika kupokea hicho kidogo alichokitowa na amewataka wasimchoke pale anapohitaji kutoa msaada mwengine zaidi.

KILA MZANZIBARI ATAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO HAITAKUFA SIKU HIYO.

Saturday, August 23, 2014

WAZANZIBAR UMEFIKA MDAA WA KUMG'OAA MADARAKANI SHEIN KWA MAADAMANO MAKUBWA HANA HAKI YA KUBAKI MADARAKANI HATA SECONDE MOJA

KULAWITIWA KWA MASHEIKH NA WAZANZIBARI WALIO TEKWA NYARA NA JESHI LA MAKABURU WEUSI LA KUTOKA KWA MKOLONI MWEUSI TANGANYIKA WAKULAUMIWA KUHUSU HILI  SHEIN..


“Mheshimiwa tunalazimishwa kutoa maelezo wanayoyataka wao, wanatuingilia kinyume cha maumbile, wanaingiza majiti, chupa, wengine wanavuja nyuma, kama unaweza hakimu twende faragha nikakuonyeshe”
“Askari ameniingilia kisha akaniingiza jiti mpaka likakatika, kungekuwa na sehemu ningekuonyesha, Jeshi la Polisi la kwanza kuvunja sheria, waliofanya madhila haya wanawatukanisha Watanganyika na kufanya waonekane wabaya”ni moja katika wazanzibari akieleza mahakamani.
Umeshawahi kumuona Ngo’mbe akimuingizia Ng’ombe mwenzake jiti katika sehemu za siri..?? Watu wanadhalilishwa jamaniiii.Watu wanaingiziwa!!! Haki zao ziko wapi..?? Ndio watu wanavyohojiwa hivi..?? Hizi ndio faida za Muungano ee!!!!!!
Watu wanachukuliwa tu kinyemele nyemela, kisha mambo wanayoenda kufanyiwa hata hayasemeki. Serekali yetu ipo, imekaa tu ndio Muungano huo ndio Muungano huo eebooo. Muungano wa kutiana majiti na chupa mpaka wakakojoa damu na kuvuja kama Kistula. Duuuh!!
TUMEZISIKIA MALALAMIKO kutoka Mahakamani ya Mkoloni Mweusi Tanganyika Mashekh wetu wakilalamika kuhusu vitendo vya ushenzi wanavyofanyiwa na askari wa nchi ya Tanganyika, vinavyoungwa mkono na viongozi wa CCM na serikali ya Zanzibar.
Itakumbukwa wakati Samuel Sitta na Samia Suluhu walipoleta rasimu nchini Zanzibar, watu walipopata nafasi ya kuchangia, na kuchambua kwa kutoa maoni Sheikh Farid, aliichana rasimu ile, hadharani.
Samia Suluhu alisema waliyochana rasimu ile si Masheikh bali ni wahuni. Kinachotokea sasa dhidi ya Masheikh wetu, ni mkakati maalum uliopangwa na Serikali ya Zanzibar na Tanganyika Mkoloni Mweusi wa kuwaadhibu, kuwadhalilisha na kuwatesa. Wanalipa kisasi.
Katika awamu zote za Serikali zilizotawala nchini Zanzibar, hii awamu ya saba ya Shein, imefurutu adda kwa ukatili dhidi ya raia wake, ukatili dhidi ya uislamu.
Shein mbona haonekani kuwa ni kiongozi wa Zanzibar, haonekani kuwa na imani wala huruma wala mapenzi kwa Wazanzibari, anaowaongozo…kweli huyu ni ..... au ADUI wa Wazanzibari.....??
Hivyo Shein tumuhesabu vipi...?? Mbona anaizamisha nchi ya Zanzibar, au ndiyo anatekeleza jukumu na kazi aliyotumwa kutoka kwa MKOLONI MWEUSI TANGANYIKA...?? Sijui kuhusu sheria na taratibu za uchaguzi za nchi ya Zanzibar, zinasemaje.
Mtu ambaye sheria haimruhusu kupiga kura nchini Zanzibar, inakuwaje yeye akaweza kupigiwa kura na kuwa rais wa nchi ya Zanzibar, ilhali yeye mwenyewe hawezi kupiga kura yake ya kujichagua au kumchagua mwingine. Mtu huyo kweli atakuwa na imani ya waliyomchagua...??
Haya yanayotokea sasa dhidi ya Masheikh na watu wengine, bila ya kutafuna ulimi yana Baraka kwa asilimia mia moja za Shein akiwa shauri moja na Balozi Seif Ali Iddi na kundi zima la akina Samia Suluhu na viongozi wa nchi ya Tanganyika Mkoloni Mweusi kupitia mwenvuli wa Muungano Feki.
Sijui watu wanafuatilia kwa kiasi gani kauli za Shein. Kuna siku kwa shikio langu nilimsikia akisema kuwa yeye hawezi kupingana na matakwa ya Kikwete na Mkapa:
Anasema: “Mimi nimefanyakazi kama Makamu wa Rais kwa miaka mitano na Mkapa…nimefanyakazi nikiwa Makamu wa rais na Kikwete…nawaheshimu nawaogopa na niko pamoja nao katika suala la chama chetu kuhusu mfumo wa Muungano,” eti huyo ndiyo ........ wa watu wa nchi ya Zanzibar, asilimia 60 wanaotaka Muungano wa Mkataba.
......... huyu huyu, Shein ndiye aliyesema hadharani kuwa yeye haitambui ile ‘Kamati ya Maridhiano’ inayoongozwa na Mzee Hassan Nassor Moyo. Huyu kweli anafaa kuwa kiongozi kwa kuwaongoza Wazanzibari. Sasa ni wakati mwafaka wa watu kutafakari.
Tangu siku aliyokaa madarakani watu wamekuwa wakisumbuliwa kwa kukamatwa ovyo-ovyo hasa Masheikh, Wapemba na wapinzani, kwa kuwekwa ndani kwa kesi za kubambikiziwa uongo.
Kiongozi wa nchi aliyekula kiapo cha kuitumikia nchi ya Zanzibar na raia wote wa nchi ya Zanzibar, hivi kweli ndiyo anawalinda na kuwatumikia. Shein, bila kumchambua sana ana chuki ndani ya moyo wake dhidi ya Wazanzibari.
Moja kwa moja namuunganisha na kauli za Kikwete, kuhusu ubaguzi dhidi ya Wapemba. Pia namuunganisha na kauli ya Lukuvi, dhidi ya Uislamu ndani ya Zanzibar. Na juhudi za viongozi wa aina hiyo kuhusu kuindoa nchi ya Zanzibar, ndani ya Dunia utafikiri wao ndio walio iyumba hii nchi ya Zanzibar.
Shein si kiongozi wa kumpa muda wa kuendelea kuwa ..... wa Zanzibar. Umefika wakati wa kumg’oa madarakani kwa maadamano makubwa.
Laiti kama ungekuwepo ushujaa kwa vijana wa nchi ya Zanzibar, ni kufanya kama walivyofanya wa Egypt, (Misri) walipoamua kumg’oa madaraka Hosni Mubarak kwa maadamano ya Tahrir Square. Wiki mbili tu, alifunga virago.
Kama bado watu wanakhofu ya kufa, kiama kitashuka unyanyasaji wa raia wa nchi ya Zanzibar, chini ya akina Kikwete, Shein, Dk Bilal, Mkapa, Ali Hassan Mwinyi, Nahodha, Lukuvi, Wassira, Kinana Samia, Vuai Ali Vuai, Uso wa sokwe na wengineo.
Umefika muda kwa raia wa nchi ya Zanzibar, kutafakari na kuachana na utegemezi wa vyama vya siasa, kuanza kutengeneza mtandao wa kuratibu maandamano endelevu kwa watu wa rika zote wa nchi ya Zanzibar, wanaume kwa wanawake na walemavu, kumg’oa madarakani Rais Feki wa Zanzibar, kwa sababu yanayotendeka ya kushikwa watu,kubambikiwa kesi watu,na hili sasa la kulawitiwa Wazanzibari katika jela ya Mkoloni Mweusi Tanganyika yanabaraka zake Shein. Hawatendei haki kabisa Wazanzibari.
Hayo ndiyo maoni yangu, ndiyo ninavyoona na si dhani kuwa kuna njia mbadala kwani juhudi za kuleta mshikamano, ili Wazanzibari waishi kwa furaha, waishi kwa kupendana, viongozi waliyoko madarani huanzisha chokochoko na uonevu bila sababu.
Watu wamechoka na uonevu wa CCM wa kila siku.....

KILA MZANZIBARI ATAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO HAITAKUFA SIKU HIYO.

Friday, August 22, 2014

MKOLONI MWEUSI TANGANYIKA AWATHALILISHA KIJINSIA NA KUWAPIGA WAKIWA UCHII WA MNYAMA WAZANZIBARI WALIO WATEKA NYARA NA KUWAFUNGA KATIKA JELA ZAO KINYUME CHA SHERIA

uamsho+clip
Wanachama na Wananchi wa nchi ya Zanzibar wa kundi la uamsho atii wanaotuhumiwa kujihusisha na vitendo vya ugaidi wakitoka wakiwa chini ya ulinzi wa Magereza ya Mkoloni Mweusi Tanganyika walipofikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam nchini Tanganyika jana.
Asema: “Waliotuhoji hawakutumia ustaarabu wala ubinadamu ilikuwa ni ushenzi na ukatili. Walituhoji wakati tukiwa watupu na kutupiga”(( nchi ya Tanganyika Mkoloni Mweusi Makaburu Weusi wajifanya Wamarekani nambari 2 sasa))
Nchini Tanganyika Dar es Salaam. Viongozi wa Jumuiya za Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu kutoka nchini Zanzibar (Jumiki), akiwamo Sheikh Farid Hadi Ahmed (43) wameilalamikia Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa polisi “walitumia ushenzi na ukatili” wakati wa kuwahoji.
Sheikh Farid na washtakiwa wenzake wanakabiliwa na mashtaka manne waliyobambikiwa na nchi ya Tanganyika Makaburu Weusi atii likiwamo la kuwaingiza watu nchini kushiriki katika vitendo vya ugaidi, kusaidia na kuwezesha kufanyika vitendo hivyo.
Washtakiwa hao walitoa malalamiko hayo jana kwa Hakimu Mkazi, Hellen Liwa muda mfupi baada ya Wakili wa Serikali, Peter Njike kuiomba Mahakama iwaruhusu washtakiwa saba kwenda polisi kuhojiwa kwa ajili ya upelelezi zaidi.
Baada ya wakili huyo kuwasilisha ombi hilo, Sheikh Farid aliuliza: “Wametuomba tena kwenda kuhojiwa...???? Kwanza waliotuhoji hawakutumia ustaarabu wala ubinadamu ilikuwa ni ushenzi na ukatili. Walituhoji wakati tukiwa watupu na kutupiga”.
Sheikh Farid alidai kuwa kiongozi Mkuu wa Jumuiya za Uamsho, Sheikh Mselem Ali Mselem alimweleza watu hao walichomfanyia.
Hata hivyo, Hakimu Liwa alimkata kauli Sheikh Farid na alimwambia alimtaka kuzungumzia kile ambacho amekiona siyo cha kusimuliwa.
Sheikh Farid Aliendelea kueleza: “Walipigwa na wala hawakupewa matibabu na watu wameumizwa, utakuta wanakojoa damu wiki moja hadi mbili, tunaomba wafanyiwe uchunguzi wa afya zao.”
Mshtakiwa Salum Ali aliiomba Mahakama kupeleka daktari mahabusu kwa madai kuwa wanafanyiwa vitendo vya ‘kuingiliwa kinguvu kinyume cha maumbile’ na kuhoji kwa nini wamekamatwa nchini kwao Zanzibar na kusafirishwa mpaka nchini Tanganyika na kushtakiwa katika nchi ya Tanganyika wakati waliokamatwa Arusha walishtakiwa huko huko na hawakupelekwa hata Dar es Salaam au nchini Zanzibar kwa nini sisi tufanyiwe hivi.......????
Akiendelea kutoa malalamiko yake, Sheikh Farid alidai kuwa wao wamekamatwa kwa sababu hawautaki Muungano na kwamba huo ndiyo msingi wa kesi hiyo.
Baada ya kauli hiyo, Hakimu Liwa kutaka kuziba ziba na kuwavunja moyo alisema: “Tupo kwenye mchakato wa Katiba Mpya na masuala ya muungano yanatajwa mbona watu wanasema na hawakamatwi......????”
Mara baada ya Hakimu Liwa kusema hayo, Sheikh Farid alisema ni kwa sababu wao wanahubiri ukweli na watu wanaukubali.
Hakimu Liwa aliiahirisha kesi hiyo hadi Septemba 3, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa na kuangalia kama upelelezi utakuwa umekamilika au laaa.
((kwa mara nyengine tena wanapelekwa mahakamani wakati upelelezi haujakamilika ni kwa nini basi munawapeleka mahakamani au ndio munataka musikie mulichowafanyia huko jela na sisi wandishi tuandike kisha watu wengine wakisoma waogope kutetea nchi yetu ya Zanzibar ndio nia yenu sio....???))
Katika kesi hiyo, Sheikh Farid na Jamal Nooridin Swalehe (38) waliunganishwa na wenzao 18 mahakamani hapo.
Mbali na Sheikh Farid na Jamal, washtakiwa wengine wanaokabiliwa na mashtaka hayo ni Nassoro Hamad, Hassan Bakari, Ahtari Humoud, Mohamed Isihaka, Abdallah Hassan, Hussein Mohamed, Juma Sadala, Said Kassim, Hamis Amour, Abubakar Abdallah, Salum Ali, Salum Amour, Alawi Othman, Rashid Ally, Amir Hamis, Kassim Salum na Said Shehe.
Kwa pamoja wanadaiwa kuwa kati ya Januari 2013 na Juni, mwaka huu walipanga njama ya kutenda makosa hayo na kuwezesha kufanyika kwa vitendo vya kigaidi lakini ukweli wa mambo ni kuwa wanapigania nchi ya Zanzibar kuwa huru na hawautaki MUUNGANO FEKI WA MKOLONI MWEUSI TANGANYIKA NDIO MAANA WANAWASINGIZIA KESI HIZO WANAZO ZIJUWE WENYEWE MAKABURU HAWA WEUSI TANGANYIKA.
KILA MZANZIBARI ATAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO HAITAKUFA SIKU HIYO.

MKOLONI MWEUPE ALIKUWA AKISHIKA WATU KENYA AKIWAHUKUMU UGANDA MKOLONI MWEUSI ASHIKA WATU NCHINI ZANZIBAR NA KUWAHUKUMU NCHINI TANGANYIKA NDIO TAKTIKI ZA WAKOLONI NA MAKABURU SUBR TU LINAMWISHO HILI LA KABURU MWEUSI TANGANYIKA LINAMWISHO WAKE

DSC_0219
Mawakili wa watuhumiwa waliopo kizuizini kutokana na tuhuma za makosa atii ya ugaidi kutoka nchini Zanzibar, wamedai kuwa kitendo cha Jeshi la Polisi kuwakamata na kuwapeleka Mahakama ya Kisutu, Dar es Salaam nchi jirani ya Tanganyika ni kuidhalilisha nchi ya Zanzibar kisheria.
Mawakili hao wakiongozwa na Abdallah Juma walitoa madai hayo mbele ya Jaji Mkusa Isack Sepetu wa Mahakama Kuu ya nchi ya Zanzibar wakati wakiwasilisha hati ya maombi ya dharura kufuatia wateja wao waliokamatwa nchini Zanzibar na kupelekwa nchi ya jirani Tanganyika  kushtakiwa.
Alisema watu hao wamenyimwa uhuru wao wa kikatiba kwa mujibu wa katiba ya nchi ya Zanzibar ya mwaka 1984 kifungu cha 14 (1) (2) na kifungu cha 16 (1).
Alisema kuwa kitendo kilichofanywa na Jeshi la Polisi cha kuwaweka kizuizini wateja wao kwa mienzi miwili sasa tena nje ya nchi yao ya  Zanzibar wakati Zanzibar ni nchi, ni kinyume cha sheria ya makosa ya jinai kifungu cha 28 sheria namba 7 ya mwaka 2004 ya nchi ya  Zanzibar.
“Zanzibar ni nchi tena ina mahakama yake kwa nini wateja wetu wakamatwe nchini kwao hapa Zanzibar wakawekwe katika kizuizi kisicho halali nchini Tanganyika......? alihoji, hivyo jaji huoni kitendo hicho ni kuidhalilisha mahakama yako tukufu,” alimuliza Abdallah Juma Jaji huyo.
Aliongeza kusema kuwa wateja wao wanne walikamatwa na polisi nchini Zanzibar miezi miwili iliyopita kwa kuhusishwa na tukio la mlipuko wa bomu uliotokea eneo la Darajani Juni 13, mwaka huu na kuua mtu mmoja na majeruhi tisa.
Alisema kwa mujibu wa sheria za nchi yetu ya  Zanzibar tukio limefanyika hapa hapa nchini kwetu Zanzibar, hivyo watu hao wangepaswa kuhukumiwa katika mahakama za hapa hapa nchini kwetu  Zanzibar na siyo Dar es Salaam nchini Tanganyika.
Aliendelea kusema kuwa wateja wao hawajapewa fursa ya kusikilizwa na kuiomba mahakama hiyo kufuata sheria.
Hata hivyo, upande wa mashitaka uliiomba mahakama kutupilia mbali madai hayo na Jaji Sepetu aliahirisha kesi hiyo hadi Agosti 28, mwaka huu mahakama hiyo itakapotoa maamuzi kuhusiana na maombi hayo.
Watuhumiwa hao waliokamatwa miezi miwili iliyopita kutokana na kosa la ugaidi ni Nassor Hamad Abdallah, Mohammed Ishaq Yussuf, Said Kassim Ali, Hassan Bakari Suleiman, Rashid Ali Nyange, Antar Humoud, Khamis Salum Amour na Salum Ali Salum.

Tuesday, August 19, 2014

UJENZI WA KIWANJA CHA NDEGE NCHINI ZANZIBAR UMEANZA TENA KWA KASI BAADA YA KUSINZIA KWA MIAKA MIWILI

IMG_0572
Ujenzi ukiendelea sasa wa jengo la airport nchini Zanzibar
Hatimae ujenzi wa uwanja wa ndege wa kimataifa wa nchi yetu ya  Zanzibar uliokua umekwama kwa muda mrefu, umeanza kwa kasi huku ujenzi huo ukitarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Kisauni nje kidogo ya mji mkuu  wa nchi ya Zanzibar, Katibu Mkuu Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano, Dk. Juma Malik Akil, alisema hitilafu zilizotokea hapo awali tayari zimeshafanyiwa kazi na ujenzi unaendelea .
Alisema mradi huo uliosita miaka miwili iliyopita kwa sababu mbali mbali unaendelea tena chini ya kampuni ya Kichina ya BCEG ikisimamiwa na Mshauri Elekezi Kampuni ya ADPI kutoka Ufaransa.
Alisema juhudi za serikali katika kuwaletea maendeleo wananchi wake ikiwa na pamoja na kuwajengea miundombinu muhimu ambayo itakuwa chachu ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii kwa wananchi wa nchi ya Zanzibar itaendelea.
Alisema lengo la serikali kujenga uwanja huo ni kufikia hadhi ya kimataifa ambayo itaweza kuitangaza nchi ya
 Zanzibar na kuongeza idadi ya watalii.
Uwanja huo hadi kumalizika kwake utagharimu dola za Marekani milioni128 ambazo ni mkopo wakutoka benki ya Exim ya China na unategemewa kuchukuwa abiria milioni 1.6 kwa mwaka na kutua ndege kubwa ikiwemo Airbus A340 na Boeing 777.
Mratibu wa mradi huo,Yassir Dicosta, aliwaomba Wazanzibari kutoa hofu kuhusu jengo hilo.
Mshauri elekezi kutoka kampuni ya ADPI ya Ufaransa, Jean Mare, alisema kazi yake kubwa ni kuangalia ujenzi huo unavyokwenda.
383021_328610877162988_107665212590890_1175288_2072876772_n
Hivi ndivyo jengo litavyokua Bada ya kumaliza

MANSOUR YUSSUF HIMID MOJA KATIKA VIONGOZI WATAKAO NCHI YA ZANZIBAR YENYE MENO SIO ZANZIBAR KIBOGOYO YUPO NJE YA JELA KIDEDEYA WAZANZIBAR MKOLONI MWEUSI TANGANYIKA JITI LIMEWAKAA

Mansour Yussuf Himid akimkumbatia Mke wake Bi Asha Karume mara baada ya kutoka Mahakama kuu Vuga alipopewa dhamana
Mahakama ya Mkoa,Vuga imempatia dhamana aliekuwa waziri wa zamani wa serikali ya Mapinduzi (SMZ),Mansour Yussuf Himid anaetuhumiwa atii kwa kosa la kumiliki silaha kinyume na sheria ya nchi ya Zanzibar, baada ya kupata maelekezo kutoka Mahakama kuu.
Hakimu Khamis Ramdhani ametoa dhamana hiyo leo baada ya kutakiwa kusimamia maamuzi yakupatiwa dhamana yaliotolewa na Mahakama kuu chini ya Jaji Abraham Mwampashe kufuatia kusikilizwa kwa ombi la dhamana lililowasilishwa Mahakama hapo na mawakili wanaomtetea Mh.Mansour.
Mapema Jaji Abraham Mwampashe, akitoa dhamani hiyo, amesema Mahakama yake imeangalia hoja za kisheria zilizotolewa na pande zote mbili za muombaji na mpigaji dhamana zilizowasilishwa Mahakamani hapo na Mawakili wa pande zote mbili.
Jaji mwampashe amesema kutokana na kifungu cha sheria cha (150) kifungu kidogo cha nne(4) sheria No (7 )ya mwaka (2004) sheria ya Zanzibar,kinaipa uwezo Mahakama kuu kutoa dhamana kwa mtuhumiwa ikiwa itaridhika na hoja zilizowasilishwa.
“hakuna kosa lolote lisolokua na dhamana,kifungu kidogo cha nne (4) kiko wazi kimeeleza Mahakama kuu ina uwezo wa kutengua makosa yote yaliokuwa hayana dhamana ikiwa itajiridhisha kama yalivyoorodhesha katika kifungu kidogo cha kwanza” Alisema Mwampashe.
Amesema baada ya kuangalia hoja za kisheria pia amechanganya na akili zake mwenyewe kwa kuangalia faida na hasara za mtuhumiwa kuwepo nje na kuwepo kizuizini.
Amesema gharama za kumhudumia na kumleta Mahakamani mtuhumiwa kunaitia hasara jamii ,hivyo Mahakama hiyo haioni sababu ya mtuhumiwa kuendelea kubaki kizuizini.
Mwampashe amesema hasa akiangalia mtuhumiwa hana historia ya uhalifu,pia mtuhumiwa anamajukumu ya kuendesha biashara zake ambazo husaaidia ajira kwa vijana walioajiriwa hapo katika vitega uchumi vyake.
Amesema Mahakama hii haiwezi kumyima mtu dhamana bila ya kuambiwa sababu ya msingi kuwepo kwake nje kuweza kuathiri mwenendo mzima wa kesi yake.
Pia amefahamisha kwamba endapo Mahakama kuu itamnyima mtuhumiwa dhamana,huku kesi inaendelea na kufikia kufutwa au mtuhumiwa kushinda kesi, jamii inayomzunguka wataingia hasara ikiwemo kukosa huduma muhimu kutoka kwa ndugu wanaemtegemea.
Aidha Jaji Mwampashe ametowa masharti ya dhamana kwa mtuhumiwa huyo kutoa dhamana ya shilingi milioni tatu tasilim za Tanganyika Mkoloni Mweusi Tanganyika, wadhamini wawili wanaoaminika kwa kusaini dhamana ya milioni tano za maandishi, kwa kila mmoja.
Pia mtuhumiwa huyo alitakiwa kukabidhi Mahakamani hapo hati zake za kusafiria, pia hatoruhisiwa kutoka nje ya Nchi bila ya kuiarifu Mahakama.
Wakati huo, huo Hakimu Khamis Ramadhani alihairisha kesi mama inayomkabili mtuhumiwa huyo hadi Agosti 28,mwaka huu na mtuhumiwa yuko nje baada ya kutimiza masharti yote ya dhamana.

Friday, August 15, 2014

LAPTOP YA MANSOUR YUSSUF HIMID INAWATOWA ROHO POLISI WA MKOLONI MWEUSI TANGANYIKA WANATAMANI IWE YAO

Ni Mansour Yussuf Himid akiwa kwenye chumba maalumu cha kuskiliziwa kesi hapo Mahakama kuu Vuga.
MANSOUR YUSSUF HIMID AKIWA MAHAKAMANI NA TABASAMU LA NGUVU KABISA

JESHI LA POLISI LA MKOLONI MWEUSI TANGANYIKA LINALO ENDELEA NA UKABURU WAKE NCHINI ZANZIBAR,Atii linaendelea kuishikilia ‘laptop’ ya alia kuwa waziri  wa nchi ya Zanzibar Mansour Yussuf Himid aliyekamatwa na kufunguliwa mashtaka atii ya kupatikana na bunduki na risasi 407 kinyume cha sheria za MKOLONI MWEUSI TANGANYIKA.
Naibu Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai kutoka kwa MKOLONI MWEUSI TANGANYIKA ishie nchini Zanzibar ili kuwakandamiza wananchi wa Zanzibar, Salum Msangi alisema laptop hiyo iko mikononi mwa polisi, tangu ilipokamatwa Agosti 2, mwaka huu.
Msangi alisema polisi inaendelea kuifanyia upekuzi ili kujua yaliyomo ndani yake na imehifadhi vitu vya aina gani na iwapo hakutakuwa na vitu vya kuvunja sheria itarejeshwa kwa mhusika.(free zanzibar people from mkoloni mweusi tunawauliza kweli mtairijesha nyinyi watu wa porini)
Alisema endapo watabaini kuwapo kwa vitu vyovyote vya kuvunja sheria itatumika kama kielelezo na kwamba kazi ya kuipekua inaendelea:(mnapekuwa laptop wiki mbili mpaka wiki nne semani kweli hamjuwi hata inavyo washwa)                                                                                                                                                                                                                                                                                      
“Ni kweli laptop tunaendelea kuifanyia uchunguzi bado ni mapema kuwaeleza nini tumekiona na hakuna sababu ya kueleza hivi sasa kwa kuwa kazi hiyo bado haijakamilika,” alisema Msangi.(na hata ikikamilika hamtaeleza maana hakuna la kueleza nyinyi ni vibaraka tu munatumwa tu fanyeni hivi mnafanya kunyeni mnakunya basi lipi jipya..???)
Hata hivyo, alisema hatua za awali za uchunguzi zimeonyesha kuna mambo alikuwa akiyatuma kwenye mitandao ya kijamii na kushiriki hatua mbalimbali za mijadala inayohusu siasa na maendeleo ya jamii.
Alisema siyo kosa mtu kushiriki na kutoa maoni katika mitandao ya kijamii lakini kuna mambo zaidi ya hapo yanahitaji kuchunguzwa.
Mbali na hilo, Polisi walifanya upekuzi katika nyumba nyingine ya waziri huyo wa zamani iliyopo katika Kijiji cha Kiboje, kilomita 12 kutoka mji Zanzibar.
MANSOUR KUPATA DHAMANA JUMATATU 
Wakati huo huo, Jaji wa Mahakama Kuu ya Zanzibar, Abraham Mwampashi amesema kwamba Mahakama hiyo haina pingamizi ya kutoa dhamana kwa Mansour Yussuf Himid ambaye ameshtakiwa kwa tuhuma za kumiliki silaha kinyume cha sheria za nchi.
Baada ya kusikiliza hoja za kisheria kutoka pande zote mbili za mawakili wa Serikali na Utetezi, Jaji Mwampashi amesema: “Mahakama Kuu haina pingamizi na ombi la dhamana kwa Mansour kwa sababu limezingatia vigezo vyote vya kisheria,”.
Jaji Mwampashi alisema hayo jana wakati alipokuwa akisikiliza ombi la dhamana lililowasilishwa kwenye Mahakama hiyo na Mawakili wanaomtetea Mansour. Mshtakiwa huyo amerudishwa rumande.
Adha, Jaji huyo amesema ombi la dhamana hiyo litatolewa uamuzi siku ya Jumatatu, Agosti 18, mwaka huu siku ambayo pia, inatarajiwa kuanza kusikilizwa kwa kesi ya msingi ya mshtakiwa huyo.
Mansour ambaye alikuwa katika madaraka ya Serikali ya Zanzibar ya awamu ya sita na ya saba, alikamatwa na kuwekwa rumande mapema mwezi huu.
MKUTANO WA CUF KIBANDAMAITI
Naye, Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad alisema Jumapili iliyopita kwenye mkutano wa hadhara wa Kibandamaiti, Unguja kwamba kadhia iliyomkuta Mansour, ni ishara njema:
“Njia zile zile walizompitisha Maalim Seif…Maalim Seif kwanza alifukuzwa Chama hicho hicho cha Mapinduzi…wakamtafutia shtaka halina dhamana wakamuweka jela kwa muda watakao wenyewe…ulipofika muda…wenyewe wakasema toka,” alisema Maalim Seif.
Alisema: “Tumeanzisha CUF mkutano wa kwanza tumeufanya Malindi…mimi nipo kama Makamu Mwenyekiti lakini ndiyo nimeshonwa mdomo…nikaja kwenye jukwa nikatoa mkono tu hivi basi imetosha.”
Alisema: “Wakenda wenyewe mwisho wakasema sasa kesi tunaifuta…sasa Maalim Seif yule yule ni Makamu wa Rais wa Zanzibar.”
Alisema: “Nakumbuka kulikuwa na askari wakinipeleka jela walivyokuwa wakinitukana na kuninyanyasa mie kimya mmh…mmh. Mungu si Athman wala si Mfaki…mmoja yuko Dar es Salaam sasa hivi akiniona mmnhh.”
“Kwa hivyo nasema la Mansour ni ishara njema…Hatujui huko mbele Mwenyezi Mungu kamuandikia nini…lakini najuwa kamuandikia mambo mema tu Inshaallah,” alisema na kuongeza:
“Lakini papo hapo niseme…nataka niamini kwamba Mansour hakukamatwa kwa sababu yeye si mwanachama tena wa Chama cha Mapinduzi…Nataka niamini kwamba Mansour kakamatwa kwa sababu katoka hadharani kuunga mkono Mamlaka Kamili kwa Zanzibar.”
Alisema: “Nataka niamini kwamba Mansour hakukamatwa kwa sababu kasema wazi wazi atamuunga mkono Maalim Seif mwakani katika kupigania uchaguzi.”
“Nataka niamini kwamba Mansour hakukamatwa kwa sababu kasema atagombea Jimbo la Kiembe Samaki kwa tiketi ya CUF…Nataka niamini hizo sizo sababu ambazo zilizomfanya Mansour akamatwe,” alisema Maalim Seif.
Alisema: “Nataka niamini kwamba Mansour atatendewa haki kama raia yeyote yule mwingine katika nchi hii na kwamba yale mashtaka yote yanayomkabili…lakini sheria itachukuwa mkondo wake pasipo na shinikizo za kisiasa.”
Alisema: “Mimi ilikuwa kesi yangu inaamuliwa kama kesho kwenda mahakamani kwanza watu wanakutana katika Ofisi ya Waziri Kiongozi pamoja na Hakimu aliyohusika kuzungumzia kesho tutafanya nini kwa maalim Seif…sasa nataka niamiani hayo hayatatendeka kwa Mansour.”
Maalim Seif ambaye ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, alisema Mahakama iliyohuru itaweza kabisa kabisa kusikiliza shtaka lililoko mbele yake na kuamua kwa mujibu wa sheria za Zanzibar.
Alisema: “Kwa sababu sasa hivi siyo tena mwaka 64…sasa hivi siyo tena 74 sasa hivi siyo tena 84 sasa hivi tunapiga makelele sote viongozi kwamba tunataka utawala wa sheria…hatutaki utawala kwamba Maalim Seif ni Makamu wa Kwanza wa Rais…basi aseme mkamate huyo akakamatwa tutoke huko.”
Alisema: “Huyu huyu Mheshimiwa Mansour…si wakimpigia suluti si alikuwa ni waziri si alokuwa karibu yao mwenzao sasa kama watu wamekula njama ‘wajue na wa-wajue-na-wajuee’ kwamba Mwenyezi Mungu anahukumu dunia hapa hapa akhera inakwenda hesabau…kwa hivyo yaliyomfika Mansour yanaweza kumfika mtu yeyote.”
Alisema: “Kama kuna watu mimi sijui wamekula njama kwamba Mansour akae ndani basi nasema wakati mwingine ukilitandika godoro ukalitia miba ili mwenzako aje alale basi iko siku godoro lile utalilalia wewe,”..

Thursday, August 14, 2014

VIDEO-KAMATI YA MARIDHIANO SIX PART 1-3 MISSING/5 CUF KIBANDA MAITI 10 AUGUST 2014

PART 1
PART 2
SAHAMANINI DUGU MNAO FUATILIA BLOG YETU KWA KUTO WAWEKEA PART 3 KUTOKA NA MATATTIZO YA KUINGIZA VIDEO PINDI TUKIFANIKIWA TUTAIWEKA
PART 4
PART 5

Friday, August 8, 2014

VIDEO-UBAGUZI TUUU BASI SIO MCHEZO

ANGALIA VIDEO HII HAUTAMINI MACHO YAKO UNACHO KIONA
PART 1
ANGALIA VIDEO HII HAUTAMINI UTAKACHOKIONA 
PART 2
PART 3
PART 4