Friday, August 29, 2014

ASKARI MAKIMA JAJI MKUSA ISAAC SEPETU SOKWE VIONGOZI WA SEREKALI MAGORILA SISI WAZANZIBARI WAANADAMU TUTAPONA KWELI...????


HUYU NDEYE MKUSA ISAAC SEPETU AKITOA UAMUZI WA KESI

Nchini Zanzibar. Mahakama Kuu ya nchi ya Zanzibar imesema mashtaka atii ya ugaidi yanaweza kufunguliwa katika mahakama yoyote baina ya pande mbili za Muungano feki wa Tanganyika na Zanzibar kama ilivyotokea kwa Wazanzibari 14 waliokamatwa nchini Zanzibar na kufunguliwa mashtaka yao Tanganyika.
Akitoa uamuzi katika kesi ya maombi iliyofunguliwa dhidi ya viongozi wa Polisi wa nchi ya Zanzibar na washtakiwa hao 14 wanaopinga kukamatwa nchini Zanzibar na kufunguliwa mashtaka Tanganyika, Jaji wa Mahakama Kuu ya nchi ya Zanzibar, Mkusa Isaac Sepetu alisema hakuna sheria wala Katiba iliyovunjwa.
Jaji Sepetu alisema baada ya kusikiliza hoja za pande zote mbili, Mahakama Kuu imejiridhisha kuwa Sheria ya Ugaidi Namba 2 ya mwaka 2002, iliyotumika kuwafungulia mashtaka inatoa uwezo wa kukamata na kufungua mashtaka katika eneo lolote la Jamhuri ya Muungano feki wa Tanganyika.
Jaji Sepetu alisema ombi la Wazanzibari hao la kuitaka Mahakakama Kuu ya nchi yao ya Zanzibar itoe amri kwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ya Mkoloni Mweusi Tanganyika kuwaachia huru watuhumiwa hao ni sawa na kuingilia uhuru wa mahakama nyingine iliyopo katika upande mmoja wa Muungano feki ambayo inatakiwa ifanye kazi bila ya kuingiliwa na upande mwingine.
Jaji Sepetu alisema ombi lililofunguliwa na walalamikaji halina nguvu za kisheria kwa vile limefunguliwa nje ya wakati huku watuhumiwa wakiwa wamefikishwa mahakamani siku tisa kabla Wazanzibari hao kuwasilisha maombi yao Mahakama Kuu ya nchi ya Zanzibar ya kupinga kushtakiwa Tanganyika.
Jaji huyo alisema Mkurugenzi wa Mashtaka wa nchi ya Tanganyika (DPP mashuzi) aliwafikisha watuhumiwa mahakamani mnamo Julai 17 wakati maombi ya Wazanzibari hao ya kupinga kukamatwa na kufunguliwa mashtaka yao huko nchini Tanganyika yalifunguliwa Julai 28, mwaka huu.
“Kama waombaji wanapinga uamuzi huu, wanaweza kufungua maombi yao katika Mahakama Kuu ya nchi ya Tanganyika kupinga wateja wao kushtakiwa upande wa pili wa Muungano feki,” alisema Jaji Sepetu.
Vilevile, alisema Mahakama Kuu ya nchi ya Zanzibar haina mamlaka wala uwezo wa kuchukua hatua ya kuingilia uhuru wa mahakama nyingine hasa kwa kuzingatia watuhumiwa hao hawapo tena mikononi mwa Polisi, wapo ndani kwa amri ya Mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu ya Mkoloni Mweusi Tanganyika na kushikiliwa katika Gereza la Segerea la Mkoloni Mweusi Tanganyika.
Hata hivyo, Jaji Sepetu alilitaka Jeshi la Polisi la Mkoloni Mweusi Tanganyika liliopo nchini Zanzibar kutekeleza majukumu yake kwa kufuata sheria na taratibu ili kuepuka malalamiko yasiyokuwa ya lazima hususan suala la ukamataji na kuepuka kukaa na watuhumiwa nje ya wakati kwa mujibu wa sheria bila ya kuwafikisha mahakamani.
Kwa mujibu wa hati ya kiapo, Wakili Abdallah Juma alisema wateja wake walikamatwa na kufunguliwa mashtaka kinyume na Kifungu cha 56 a(1)(3) kinachotoa mamlaka pekee kwa Mkurugenzi wa Mashtaka wa nchi ya Zanzibar kufungua na kushughulikia mashtaka yoyote ya jinai dhidi ya mtu yeyote mbele ya mahakama yoyote isipokuwa ya kijeshi.
Alisema kitendo cha kuwakamata na kutowafikisha katika Mahakama za nchi yao ya Zanzibar ndani ya saa 24, kilivunja Katiba ya nchi ya Zanzibar ya mwaka 1984, Kifungu cha 14(1) na 16(1) vinavyotoa uhuru wa kila mtu kuwa na haki ya hifadhi ya maisha yake na kutonyimwa uhuru wake wa kwenda popote, haki ya kuishi katika sehemu yoyote ya nchi ya Zanzibar.
Wazanzibari hao 14 walifunguliwa mashtaka atii ya kula njama za ugaidi katika maeneo mbalimbali ya Jamhuri ya Muungano feki wa nchi ya Tanganyika ya Mkoloni Mweusi Tanganyika kinyume na Kifungu cha 21 cha Sheria atii ya Ugaidi cha Sheria Namba 2 ya mwaka 2002.

KILA MZANZIBARI ATAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO HAITAKUFA SIKU HIYO.

No comments:

Post a Comment