Thursday, August 7, 2014

SHEIKH FARID APELEKWA MAHAKAMA YA MKOLONI MWEUSI TANGANYIKA KISUTU JE NCHI YA ZANZIBAR HAINA MAHAKAMA...????


Nchini Tanganyika jijini Dar es Salaam. Kiongozi wa Jumuiya za Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu wa nchi ya Zanzibar (Jumiki), Sheikh Farid Hadi Ahmed (43) na mwenzake Jamal Nooridin Swalehe (38), wameunganishwa na watu wengine 18 atii wanaoshtakiwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ya Mkoloni Mweusi Tanganyika wakikabiliwa atii na mashtaka manne likiwamo la kula njama ya kuingiza watu nchini kushiriki katika vitendo vya ugaidi.
Pia, wanakabiliwa na shitaka la kuwaingiza watu nchini kushiriki katika vitendo vya ugaidi, kusaidia na kuwezesha kufanyika vitendo hivyo.haya mambo haya eleweki kichwa wala miguu ila ndio Mkoloni Mweusi Tanganyika anajaribu kila mbinu ili kuwazima Wazanzibari wasidai nchi yao ya Zanzibar.
Mawakili wa Serikali, Peter Njike, Bernard Kongola na George Barasa wakiwasomea hati ya mashtaka hayo yanayowakabili washtakiwa wa kusingiziwa. hao walidai kuwa Sheikh Farid ambaye ni mfanyabiashara na mkazi wa Mbuyuni, nchini Zanzibar na Fundi Ujenzi, mkazi wa Koani nchini Zanzibar, Swalehe atii walijihusisha na makosa hayo ya ugaidi kinyume na Kifungu cha 27(c) cha Sheria ya Kuzuia Ugaidi ya 2002.
Mbali na Farid na Jamal, washtakiwa wengine wanaokabiliwa na mashtaka hayo ni Nassoro Hamad, Hassan Bakari, Ahtari Humoud, Mohamed Isihaka, Abdallah Hassan, Hussein Mohamed, Juma Sadala, Said Kassim, Hamis Amour, Abubakar Abdallah, Salum Ali, Salum Amour, Alawi Othuman, Rashid Ally, Amir Hamis, Kassim Salum na Said Shehe.swali ni kuwa hawa nchi yao ni Zanzibar sasa hko Zanzibar hakuna mahakama...? hakuna jela....? kwa nini waletwe nchi ya jirani ya Tanganyika na kuja kufungwa huko na kupelekwa mahakama za huko za Mkoloni Mweusi Tanganyika kwa nini...?
Walidai kuwa kati ya Januari 2013 na Juni mwaka huu washtakiwa hao kwa pamoja walipanga njama ya kutenda makosa hayo ya kula njama za kusaidia na kuwezesha kufanyika vitendo vya kigaidi.
Njike alidai kuwa katika kipindi hicho na maeneo tofauti nchini, Sheikh Farid aliwaingiza Sadick Absaloum na Farah Omary nchini ili kushiriki kutenda makosa ya ugaidi...!!!!!!
Pia Sheikh Farid anadaiwa  kwa makusudi na akijua, alitoa msaada kwa watu hao wa kutenda vitendo vya kigaidi kinyume cha sheria. Pia anadaiwa kuwa katika kipindi hicho akiwa anajua kuwa Sadick na Farah wametenda makosa ya kigaidi, aliwahifadhi.
Baada ya kusomewa mashtaka hayo, washtakiwa hao hawakuruhusiwa kujibu chochote kwa sababu mahakama hiyo haina mamlaka ya kuisikiliza kesi hiyo hadi Mahakama Kuu.sasa kwa nini wasipelekwe mahakama kuu moja kwa moja kwa nini wakaletwa hapa kuja kupoteza mdaa...?
Upande wa mashtaka ulidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika na kuiomba mahakama kupanga tarehe nyingine.kama haukukamilika kwa nini mukawaleta mahakamani...?mngelisubiri mpaka ukamelike ndio muwalete ziko wapi sheria munazojidai kuwa nchi ya Tanganyika inafuta sheria..? je ndio sheria zenu hizo kuwachukuwa watu wa nchi ya Zanzibar na kuwafunga katika majela yenu...? kuwapeleka mahakamani kabla ya kukamilisha uchunguzi....?
Hakimu Hellen Liwa aliahirisha kesi hiyo hadi Agosti 20, mwaka huu na kuamuru washtakiwa kupelekwa rumande kwa sababu mashtaka yanayowakabili ni miongoni mwa mashtaka yasiyo na dhamana......!!!!!!
Baada ya kusomewa mashtaka yanayowakabili, Sheikh Farid alidai mahakamani hapo kuwa anashangazwa na kitendo cha wao kukamatwa nchini Zanzibar na kushtakiwa nchini Tanganyika wakati hawana ndugu, baba wala mama katika upande huo wa ((Jamhuri ya Muungano)).kw MKOLONI MWEUSI TANGANYIKA
“Tunashangaa kushtakiwa huku nchini Tanganyika wakati Zanzibar ni nchi yenye Mwanasheria Mkuu, Jaji Mkuu na askari watiifu tu na kila kitu,” alisema na kuongeza kuwa wamekamatwa Aprili lakini hadi sasa upelelezi bado haujakamilika na kuhoji ni upelelezi gani huooooooooooooooooooooo.
KAMA WAZANZIBARI HAMJA AMKA WALA HAMTAA AMKA TENA ZANZIBAR KWANZA ZANZIBAR KWANZA ZANZIBAR KWANZA MKOLONI MWEUSI TANGANYIKA WACHIYE HURU WAZANZIBARI ULIOKUJA KUWASHIKA NCHINI KWAO ZANZIBAR.

No comments:

Post a Comment