Tuesday, August 19, 2014

UJENZI WA KIWANJA CHA NDEGE NCHINI ZANZIBAR UMEANZA TENA KWA KASI BAADA YA KUSINZIA KWA MIAKA MIWILI

IMG_0572
Ujenzi ukiendelea sasa wa jengo la airport nchini Zanzibar
Hatimae ujenzi wa uwanja wa ndege wa kimataifa wa nchi yetu ya  Zanzibar uliokua umekwama kwa muda mrefu, umeanza kwa kasi huku ujenzi huo ukitarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Kisauni nje kidogo ya mji mkuu  wa nchi ya Zanzibar, Katibu Mkuu Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano, Dk. Juma Malik Akil, alisema hitilafu zilizotokea hapo awali tayari zimeshafanyiwa kazi na ujenzi unaendelea .
Alisema mradi huo uliosita miaka miwili iliyopita kwa sababu mbali mbali unaendelea tena chini ya kampuni ya Kichina ya BCEG ikisimamiwa na Mshauri Elekezi Kampuni ya ADPI kutoka Ufaransa.
Alisema juhudi za serikali katika kuwaletea maendeleo wananchi wake ikiwa na pamoja na kuwajengea miundombinu muhimu ambayo itakuwa chachu ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii kwa wananchi wa nchi ya Zanzibar itaendelea.
Alisema lengo la serikali kujenga uwanja huo ni kufikia hadhi ya kimataifa ambayo itaweza kuitangaza nchi ya
 Zanzibar na kuongeza idadi ya watalii.
Uwanja huo hadi kumalizika kwake utagharimu dola za Marekani milioni128 ambazo ni mkopo wakutoka benki ya Exim ya China na unategemewa kuchukuwa abiria milioni 1.6 kwa mwaka na kutua ndege kubwa ikiwemo Airbus A340 na Boeing 777.
Mratibu wa mradi huo,Yassir Dicosta, aliwaomba Wazanzibari kutoa hofu kuhusu jengo hilo.
Mshauri elekezi kutoka kampuni ya ADPI ya Ufaransa, Jean Mare, alisema kazi yake kubwa ni kuangalia ujenzi huo unavyokwenda.
383021_328610877162988_107665212590890_1175288_2072876772_n
Hivi ndivyo jengo litavyokua Bada ya kumaliza

No comments:

Post a Comment