Friday, September 5, 2014

CCM MUUTAMJUWA MANSOUR YUSSUF HIMID NI NANI SASA MMERAMBA MOTO KWA ULIMI WACHAA UWANGUZE SASA


Nchini Zanzibar. Siku chache baada ya kujiunga na CUF, Waziri wa zamani wa Serikali ya Zanzibar (SZ), Mansour Yussuf Himid (46), ameteuliwa kuwa mkuu wa mikakati wa kufanikisha kukiondoa madarakani Chama Cha Mapinduzi(CCM) kupitia Uchaguzi Mkuu mwakani.
Mansour alijiunga na CUF baada ya kuvuliwa uanachama wa CCM, Agosti mwaka jana kwa tuhuma za atii usaliti na kwenda kinyume na sera za chama hicho cha Mkoloni Mweusi Tanganyika kilichokuja kukiua chama cha ASP na kujipenyeza na kuwatawala Wazanzibari kwa Ukoloni wasio ujuwa kuwa ni UKOLONI, hivyo kupoteza nafasi yake ya uwakilishi wa Jimbo la Kiembesamaki.
Mkurugenzi wa Uenezi na Mawasiliano kwa Umma wa CUF, Salum Abdallah Bimani alisema Mansour ameteuliwa kushika wadhifa huo kuanzia Agosti 27, mwaka huu hadi utakapofanyika Uchaguzi Mkuu mwingine wa Taifa wa CUF mwaka 2019.
Bimani alisema majukumu ya Mansour ni kuratibu mipango na mikakati ya kisiasa na kuhakikisha CUF inafikia malengo yake ya kushika madaraka kwa njia za kidemokrasia.
Alitaja sifa za mwanasiasa huyo kuwa ni mwanaharakati, mchapakazi na mpenda mabadiliko na kwamba hivyo amekabidhiwa jukumu hilo akiaminiwa kuwa ni kiranja atakayefanikisha malengo hayo kwa weledi na ushupavu.
“Siku zote (Mansour) hufanya jambo analoliamini bila ya kusukumwa, analolisimamia basi huzaa matunda bila ya kusukumwasukumwa, ni jasiri na hodari,” alisema Bimani.
Alisema kikao cha Kamati ya Uongozi cha CUF kilichokaa hivi karibuni na kuwakutanisha wajumbe 300 wa wilaya sita za Unguja, kilitambulishwa nafasi mpya ya Mansour.
Alisema madhumuni ya mkutano huo ilikuwa ni kuwatambulisha viongozi wapya wa Kamati ya Utendaji Taifa ya CUF ambayo itafanya kazi kuelekea Uchaguzi Mkuu ujao.
Mansour alithibitisha uteuzi huo lakini hakuwa tayari kuzungumza chochote.
Mwanasiasa huyo ameshiriki katika mikakati ya kampeni za uchaguzi za vipindi vitatu akiwa CCM wakati wa Rais mstaafu, Amani Abeid Karume na kushiriki kikamilifu katika kampeni za  Shein.
KILA MZANZIBARI ATAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

No comments:

Post a Comment