Tuesday, September 23, 2014

KIONGOZI WA SKOTISHI ALITAKA RAI WAVUNJE MUUNGANO KWA KURA ZANZIBAR VIONGOZO WANATAKA MUUNGANO RAI HATUTAKI KAMA HAMUAMINI TUPENI KURA NAWALA MUZIZICHAKACHUWE MUONE


Kinana kutoa mfano kwa wascotish ni saw a na kulinganisha vitu viwili tofauti ambavyo havifanani.
Sasa kama wewe unasema waziri mkuu wao Scotland alikuwa akiwahamasisha watu kujitoa ktk mungano lakini mwisho Wa siku watu wamekataa.
Na Wazanzibari tunakushauri hivi  leteni kura ya maoni Kisha mwambieni Raisi wa Kisonge shein ahamasishe Wazanzibar waendelee na serikali 2 Kisha muwachie watu waamue kwa hakii bila kuchakachua na matokeo utakayopata ndio sasa ujisifu na kuilinganisha Zanzibar na scotland.


Tofauti Hapa petu Zanzibar Kiongozi Wa CCM wanataka watu wasijitoe ila watu wanataka kujitoa ilhali Scotland watu hawakutaka kujitoa wakati kiongozi wao alitaka wajitoe ktk mungano.Kinana amejuwa maneno haya ayaseme wapi, Tanganyika nchini kwao. Tufahamu kuwa Watanganyika wengi bado wamelala usingizi mzito wa FOFOFO sana au wamejengwa na woga mkubwa kusema dhidi ya utawala wa Makaburu Weusi CCM. Watanganyika wengi bado hawajuwi namna wanavyonyonywa na utawala huu wa kidhalimu wa Makaburu CCM. Watanganyika wengi hutuona sisi Wazanzibari ni watu wakorofi tu kwa vile hatuna kigugumizi kudai haki zetu za dola.


CCM imejenga woga mkubwa ndani ya Watanganyika kiasi ya kuwa hata mwenyekiti wa shina anaweza kumfanyia Mtanganyika matendo anayopenda yasiyo ya kisheria na aliyefanyiwa anaogopa hata kusema. Wewe tazama tu nchi ya Tanganyika jinsi ilivyobarikia na raslimali za kila aina Thahabu,Amasi,Tanzanight,Makaa ya Mawe,Mbuuga za Wanyama,Ardhi iliyo kubwa kabisa na yenye rutuba ya kuota kitu chochote,Milima mizuri mizuri, Maziwa na Mitoo isitoshe Bahari na Gasi juu N.K. na habu angalia maisha wanao ishi rai wao wa Tanganyika mpaka leo mlo moja kwa mbindee kulaleki.Qatar in Gasi tu angalia inavyo peleka dunia mchaka mchaka Gasi tu U.A.E. in petrol tu angalia inavyo ghara Saudi arabia, Kuwaiti N.K. utakuta wana kitu kimoja tu lakini wananchi wao wanaishi maisha ya juu kabisa na nchi swafii leo Mwananchi wa Tanganyika aliyekuwa akila milo mitatu wakati wakitawaliwa na Mjerumani na kisha Mgereza wakati wa utumwa leo wako HURU hata MLO moja unawashinda sasa Uhuru huu wa nini basi....?? 

Ni nchi ya ajabu sana Tanganyika kuwa nchi yenye raslimali kama vile halafu wanakubali kuja kudhalilishwa Zanzibar na CCM eti waje watie kura kuisaidia CCM halafu watapatiwa kazi hebu jiulizena Tanganyika na Zanzibar ipi ni kubwa ipi ina raslimali nyingi mukisha pata jibu jiulizeni ikiwa hapa hatupati na ndio kwetu kweli tutapata ugenini....?? Wengi wenu Mwisho wake humalizikiaje baada ya kupiga kura na kuifanya CCM ishinde huwa munamalizikiaje....??

Kudhalilika mitaani tunawaona. Tunawaamsha sana vijana wanu wa Kitanganyika lakini naona bado wamo katika usingizi na khofu kubwa kuweza kukabiliana na utawala dhalimu wa Makaburu Weusi CCM wa kudai haki zao kule Tanganyika nchini kwenu na ndio kwenu. Matokeo yake huja nchini kwetu  Zanzibar kuvaana na Wazanzibari. Wasomi wa nchi ya  Tanganyika bado hawajafanya kazi ya kuwaamsha Watanganyika. Inaoneshea Wasomi wengi wa Tanganyika wakisha kupata wao “elite” wanatoshelezeka, japo raia wa kawaida wakiwa wanateketea kwa umaskini, maradhi na njaa namna gani. Kwa hivyo CCM nchini Tanganyika wanajuwa vipi kuwadhibiti wasomi wa nchi yao ya Tanganyika kwa sababu wanajuwa wakisha kuwadhibiti wasomi wao ni rahisi kuwadhibiti raia wa kawaida ambapo jambo hili utaona ni vigumu kwa nchi yetu ya Zanzibar. Zanzibar kila mtu ana mwamko, awe msomi au raia wa kawaida.

KILA MZANZIBARI ATAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

No comments:

Post a Comment