Saturday, September 6, 2014

MWANASHERIA MKUU WA NCHI YA ZANZIBAR AJIUZULU (KATIBA IANDIKENI KISHA TANGANYIKA HAINA KATIBA TUMIYENI NYINYI HIYO KATIBA MUWE NA NCHI YENU TANGANYIKA NA HIYO ITAKUWA NDIO KATIBA YENU TANGANYIKA)


Mwanasheria Mkuu wa nchi ya Zanzibar ajiuzulu Kamati ya Uandishi, asema sababu aulizwe Mwenyekiti wa Bunge, Sitta,Saba,Nane,Tisa, akataa kuzungumzia kwa hikma alizo nazo.Giningi inayo wauwa Wazanzibari Dodoma. Kuna dalili ya hali halisi si shwari ndani ya Bunge Maalumu la Katiba baada ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya nchi ya Zanzibar  Othman Masoud Othman kujiuzulu ujumbe wa Kamati ya Uandishi wa Katiba inayopendekezwa.
Habari za uhakika zilizopatikana jana bungeni mjini Giningi Dodoma, zinaeleza kuwa kigogo huyo wa nchi ya Zanzibar amemwandikia barua Mwenyekiti wa Bunge hilo, Samuel Sitta akimwarifu juu ya uamuzi wake huo wa kujiuzulu.Kamati hiyo ndiyo moyo wa Bunge hilo katika kuandika vifungu, ibara na sura za rasimu kulingana na mapendekezo ya kila kamati na baada ya majadiliano na mwisho inawajibika kuandika Katiba itakayopendekezwa kwa wananchi kwa ajili ya kupigiwa kura ya maoni.
Kujiengua kwake ni pigo kwa Bunge Maalumu, kwani kunapunguza uhalali wa Katiba itakayopendekezwa kwani Othman akiwa Mwanasheria Mkuu wa upande huo wa Muungano feki ndiye anayepaswa kuwa kinara wa kulinda masilahi ya nchi ya Zanzibar wakati wa uandishi wa Katiba inayopendekezwa.Jana Mwanasheria huyo Othman alilithibitishia Muandishi wetu wa siri wa Free Zanzibar People From Mkoloni Mweusi Tanganyika aliyepo Giningi Dodoma kuhusu kujiuzulu kutoka kwenye kamati hiyo, lakini akakataa kueleza zaidi sababu zilizomsukuma kuchukua uamuzi huo akitaka Mwenyekiti wa Bunge Maalumu atafutwe kwani barua yake ya kujiuzulu ameikabidhi kwake.
Mwanasheria huyo wa nchi ya Zanzibar alisema “Ni sahihi kwamba nimejiuzulu…hizo sababu ndiyo siwezi kukutajia maana kwa mujibu wa taratibu za Bunge Maalumu zinapaswa kuzungumzwa na Mwenyekiti maana barua yangu ya kujiuzulu anayo yeye,”alisema Othman alipozungumza na muandishi wetu.Hata hivyo, Sitta,Saba,Nane,Tisa alipotafutwa jana, alikataa kuzungumza lolote juu ya taarifa hizo akisema hawezi kufanya mahojiano na mwandishi asiyemfahamu kwa njia ya simu. ilibidi mwandishi wetu acheke kwanza hahahaahah
Sita akiendelea kusema kwenye simu “Kwanza sikujui halafu unataka nifanye mahojiano kwenye simu...?? Mimi sipo (Dodoma), nipo Dar es Salaam ninarudi Jumatatu niliondoka huko (Dodoma) mara tu baada ya kipindi cha asubuhi,” alisema Sitta.Kwa upande wake, Katibu wa Bunge Maalumu, Yahya Khamis Hamad, alipotafutwa alisema hajaiona barua hiyo ya Othman, lakini kwa utaratibu, mjumbe anayetaka kuchukua uamuzi kama huo humwandikia barua mwenyekiti ndipo ishuke chini.“Mimi bado sijapata taarifa hiyo, labda atakuwa amewasilisha kwa mwenyekiti akishaipata ndiyo inaletwa huku kwangu,”alisema Hamad.Alisema kwa sababu nafasi hizo ni uteuzi unaofanywa na mwenyekiti na kanuni ziko kimya kuhusiana na idadi ya wajumbe katika kamati, mwenyekiti ndiye mwenye uamuzi wa kuteua mtu mwingine ama kuacha.
ZANZIBA KWANZA ZANZIBA KWANZA ZANZIBAR KWANZA
Baada ya Muandishi wetu kufuatilia zaidi habari hizi tulingundua kuwa mara ya mwisho,Mwanasheria Mkuu wa nchi ya Zanzibar Othman aliingia katika kikao cha Kamati ya Uandishi Jumanne na tangu siku hiyo hakuhudhuria vikao na hata jana wajumbe walikutana Ukumbi wa Pius Msekwa bila ya kigogo huyo kuhudhuria.Vyanzo hivyo vilimdokeza Mwanandishi wetu  kuwa sababu kubwa ya kujiondoa katika kamati hiyo ni kutokana na kutoridhishwa na hali ya mambo katika uandishi wa ibara za katiba kama zilivyopendekezwa na kamati 12 za Bunge Maalumu.
Habari hizo zinadai, Othman alisikika akiwatahadharisha baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo, nje ya vikao juu ya athari za wajumbe wa kamati za Bunge, kuamua kuifumua rasimu iliyopendekezwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba.“Alitahadharisha juu ya kubadili maudhui ya Rasimu ya Katiba iliyoandikwa kwa misingi ya serikali tatu na kuiandika kwa misingi ya serikali mbili kuwa itakuwa na athari huko baadaye,” alidokeza mmoja wa watoa habari.Kujiuzulu kwa Othman kumekuja wakati Bunge hilo likiwa limegawanyika vipande vipande baada ya wajumbe wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kuamua kususia vikao vya Bunge hilo tangu Aprili 16, mwaka huu.
Sababu inayotajwa na Ukawa ya kususia vikao hivyo, ni hatua ya Bunge hilo kuamua kuacha kujikita katika kujadili na kuboresha Rasimu ya Katiba na badala yake kuifumua upya ili kuingiza masilahi ya CCM wasio jali maaslahi ya Wananchi wao ni Matumbo yao na wake zao na hawara wao basi mlio baki kufani na nja miaka sasa zaidi ya 50.Hata hivyo, pamoja na wajumbe wa Ukawa kususia, Bunge hilo limeendelea na vikao vyake vya haramu huku jitihada za kutafuta maridhiano zikielekea kukwama kutokana na kila upande kushikilia msimamo wake.
Kadhalika baadhi ya wajumbe ambao pia ni makada wa CCM wakiongozwa na Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho (Nchini Tanganyika), Mwigulu Nchemba wamekuwa wakipinga kuendelea kwa Bunge hilo kwa maelezo kwamba litakosa uhalali wa kisiasa, huku kukiwa na hofu ya kutopatikana kwa idadi ya theluthi mbili ya wajumbe kutoka Nchini Zanzibar.Sitta,Saba,NaneTisa mara zote amenukuliwa akijitetea kuwa Bunge hilo halijatoka nje ya msitari na kwamba kinachojadiliwa ndani ya Bunge hilo ni Rasimu ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba na siyo vinginevyo.Kamati ya Uandishi inajumuisha wajumbe 24 wakiwamo watu wazito na inaongozwa na Mwanasheria Mkuu mstaafu, Andrew Chenge na mjumbe mwingine ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Fredrick Werema na wanasheria mbalimbali waliobobea katika taaluma ya sheria.DSC_2138
ZANZIBA KWANZA ZANZIBA KWANZA ZANZIBAR KWANZA
HATUTAKI KITU MWANASHERIA WETU ASHATOKA BASI TUPENI HAO NDUGU ZETU MULIO WAFUNGA HUKO JELA BILA YA SABABU KISHA NYINYI MUBAKI NA TANGANYIKA YENU MUANDIKE HIYO KATIBA IWE NDIO KATIKA YA NCHI YENU YA TANGANYIKA  BASI MUNA NCHI YENU NA HIYO NDIO ITAKUWA KATIBA YENU NA SISI TUNA NCHI YETU YA ZANZIBAR NA KATIBA YETU HAKUNA KUINGILIANA TUISHI KWA AMANI KAMA TUNAVYO ISHI NA WAKENYA,WAGANDA N.K.
KILA MZANZIBARI ATAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

No comments:

Post a Comment