Friday, October 3, 2014

HAMAD RASHID AWAKEJELI WAZANZIBARI WENYE UCHUNGU NA NCHI YAO KUMEZWA NA MKOLONI MWEUSI TANGANYIKA ASEMA KATIBA HAIPO KUBANDA MAITI


Mjumbe wa Bunge la Katiba Hamad Rashid alizidi kujipalilia msumari wa moto zaidi ya  Wazanzibari jana baada ya kupitishwa kwa katiba iliyopendekezwa na Bunge. Hamad Rashid alichaguliwa mahsusi kuwa mjumbe wa kwanza kutoa maoni yake kabla ya wabunge wengine,na hivi ndivo hali ilivokuwa ili azidi kuwatukana Wazanzibari na kuwakejeli:
BAADA YA KUMALIZA KUJITEKINYA WENYEWE KWA WENYEWE
Walitangaza matokeo hayo, ukumbi mzima ulilipuka kwa shangwe, vifijo na vigelegele, huku wabunge wengi wakiinuka kutoka kwenye viti vyao na kujimwaga katikati ya ukumbi kushangilia, wakiimba na kucheza nyimbo na mitindo ya aina mbalimbali.
Hali hiyo ilisababisha shughuli za BMK GININGI kusimama kwa zaidi ya dakika 20 ambapo wajumbe walikuwa wakikumbatiana kwa maana ya kupongezana kwa kupitisha katiba isiyo takiwa na wananchi wa nchi hizi mbili Tanganyika na Zanzibar lakini matumbo yao watakula vizuri na familia ndicho wanacho kijali wabunge hawa,ndipo wapoanza kucheza na kuimba nyimbo mbalimbali hususan taarab. Baada ya wajumbe hao kutulia, Mwenyekiti wa BMK, alimwita Mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge ambaye alikuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Uandishi ili atoe hoja ya kupitisha Katiba inayopendekezwa na wao sio wananchi.
Baada ya hoja kutolewa na Chenge, kabla ya kuwahoji wajumbe, Mwenyekiti alitoa nafasi ya kusema neno kwa baadhi ya wajumbe na nafasi ya kwanza akapewa Mbunge wa Wawi, Hamad Rashid awakejeli Wazanzibari na naam alifanya hivyo.
Mjumbe Hamad Rashid alisema kuna baadhi ya watu walisema wao wana kura za Wazanzibari na kuwa walipendekeza Serikali ya mkataba. Hata hivyo, alisema, matokeo yaliyotolewa ndiyo yamebainisha nani ni Wazanzibari na Serikali gani wanaitaka.“Katiba inapatikana kisheria, ndiyo maana tumekuwa hapa kuifanya kazi hiyo. Sasa hawa wenzetu waendelee kupiga kelele wenyewe. Sasa ni wazi kuwa sauti ya watu wa Kibanda Maiti imesikika katika matokeo haya,” alisema Rashid.
Rashid alisema kuwa kwa mara ya kwanza katika historia ya ((Tanzania)), ((watanzania)) wamepata fursa ya kukaa pamoja kuandika katiba, hivyo akawaomba watanzania kutumia fursa hiyo kuipokea na kuikubali Rasimu ya Katiba ili kudumisha amani na utulivu wa taifa. Alisema kuwa wapo baadhi ya watu waliosema kuwa katiba haitapatikana wakidhani kuwa wanamiliki kura za wazanzibar, lakini kwa ushindi uliopatikana umeonyesha kuwa kura za wazanzibar ni wale waliokuwa ndani ya Bunge.
“Wako watu walisema kuwa wao ni wazanzibari kuliko wazanzibari wengine, waliwataka wazanzibar hao wapate mafuta yao, lakini waliwatetea Kibanda Maiti, walitaka wazanzibari wapate mikopo wakope bila matatizo, lakini waliwatetea kibanda maiti, walitaka wazanzibar rais wetu atambuliwe katika Jamhuri ya Muungano kama ilivyokuwa kwenye hati ya Muungano lakini walifanya hayo Kibanda Maiti, lakini nawambia wazanzibar halisi wanaowatetea wapo ndani ya nyumba hii na wataendelea kuwatetea mpaka mwisho,” alisema Hamad Rashid.

KILA MZANZIBARI ATAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

No comments:

Post a Comment