Tuesday, October 14, 2014

NCHINI ZANZIBAR WANASHERIA NA WANASIASA NA WANANCHI WA NCHI YA ZANZIBAR WAMEUNGA MKONO MSIMAMO WA MAALIM SEIF SHARRIF HAMADNchini Zanzibar: Wanasheria na Wanasiasa na Wananchi wa nchi ya Zanzibar, wameunga mkono msimamo wa Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad wa kupiga kampeni ya hapana kupinga Katiba iliyopendekezwa kupitishwa na wananchi kwa sababu imelenga kufuta hadhi ya Zanzibar kuwa nchi.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti jana mjini nchin Zanzibar, wanasheria na wanasiasa hao walisema hatua ya Maalim Seif kupinga Katiba hiyo ni haki yake kwa mujibu wa sheria kama kiongozi au mtu binafsi.
Rais wa Chama cha Wanasheria wa nchi ya Zanzibar (ZLS), Awadh Ali Said alisema anaunga mkono msimamo wa Seif kwa sababu Katiba inakuja kuondoa hadhi ya nchi ya Zanzibar kuwa nchi na mamlaka ya kikatiba ya Rais wa nchi ya Zanzibar ya kugawa mipaka ya wilaya na mikoa yake.
“Bahati mbaya tangu kupatikana kwa Uhuru, Watanganyika na Zanzibar watu wa nchi hizi mbili hawajawahi kuwa na Katiba inayotokana na wananchi bali wamekuwa wakiongozwa na Katiba zinazotokana na watawala wa Zanzibar na Tanganyika,” alisema Awadhi.

No comments:

Post a Comment