Monday, October 27, 2014

SHEIN HATA MWENYEZI MUNGU BASI HUMUOGOPI......???Rais wa Kisonge na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, jana alihutubia mkutano wa hadhara mjini hapa huku akiwataka Wazanzibari kuipigia kura ya ndiyo Katiba mpya inayopendekezwa na CCM wasaka tonge.
Dk. Shein ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar, alihutubia mkutano huo uliofanyika katika uwanja wa Demokrasia Kibanda Maiti na kuhudhuriwa na wanachama wa CCM na kusema kuwa katiba hiyo inabeba maslahi ya Wazanzibari.(tunakuliza maslahi yapi ya kuifanya Zanzibar isiwe nchi tena...???)
Alisema katiba hiyo ni nzuri,...!!!!!!!!!  kisha ya waliosusa Bunge Maalum la Katiba bila ya sababu za msingi na kudhani kuwa kususa kwao katiba haitapatikana. “Walidhani tukiwa peke yetu tutashindwa mawe, tumeweza tena kwa ufanisi mkubwa sana na kusifiwa na nchi za nje jinsi tulivyofanikiwa,” alisema Dk Shein.(tutajie hizo nchi zilizo wasifia usisema tu nchi kila nchi ina jina taja majina basi) kisha ati unaswali wewe astahafiruh allah.
Alisema katiba hiyo haina walakini wala mushkeli, ni katiba safi na nzuri kabisa kilichobaki kwa wananchi ni kuipigia kura ya ndio. ((hahahahahaahhahahahahahahahaahaha unaumwa na akili nini wewe..?)) Alisema mambo yote ya Zanzibar kuhusu Muungano na yasiokuwa ya Muungano ikiwemo kero za Muungano yameelezwa katika katiba hiyo na kupatiwa majawabu kama koti ndo limevuliwa na wala halibani tena.
Alisema anashangazwa na wanaosema katiba hiyo ni ya CCM wakati rasimu imeandikwa na Tume ya Jaji Joseph Warioba na chama hicho tawala kilikuwa na mapendekezo yake ya serikali mbili. “Nawashaangaa CUF wanaosema katiba hawaitaki, mimi napata mashaka ndo tunataka kuendelea hivyo, wezetu bara wanachimba gesi wanaingiza fedha nyingi, leo wanasema katiba hawaitaki hivyo kweli mafuta tutayachimba na tutapata maendeleo?” alihoji na kuongeza: “Lazima tukubaliane tupige kura ya ndio katiba hii ili kuweza kupata maendeleo.
”(( miaka 50 na sasa munawadanganya wananchi munaleta maendeleo wakati maendeleo munayo leta ni yenu nyinyi na wake zenu na mahawara wenu na watoto wenu wa halali na waharamu pia ndio wanao pata maendeleo wananchi wanaumia tu ndio leo muanalete maendeleo na katiba mkoloni mweusi....?))
“Nataka niwahakikishieni katiba hii itapigiwa kura za ndiyo na nimwambie Katibu Mkuu wa CUF (Maalim Seif) aseme na wanachama wake na siyo Wazanzibari wote, mimi ndiye nina mamlaka ya kuwaambia Wazanzibari wote kwani mimi ndiye waliyenichagua niwambie wanachama wake wa CUF,” alisema.
Swali: Kwa maana hiyo unataka kusema kuwa Karume alikupigia simu ukazungumze na Maalim Seif kwa kuwa Dk. Shein hakushinda uchaguzi?
Jibu: Ndiyo maana yake, wewe ni mtumzima umeniuliza swali la kiutu uzim, ndiyo maana yake.
Swali: Je, Dk. Shein naye hakukuita?
Jibu: Ndiyo maana nilitaka nikuonyeshe picha. (Anaonyesha picha akiwa anateta jambo na Dk. Shein huku upande mwingine akionekana mkewe Dk. Shein, Mwanamwema na nyuma yao ni maafisa wengine wa Serikali).
Hapa Bwawani (hotel) tumekwenda kusikiliza matokeo ya urais. Usiku walikuja askari wa Polisi wakasema, mzee unatafutwa uende Bosnia (kule kwa Maalim Seif, Maisara). Kumbe kule wameshaambiwa kuwa matangazo ya urais yasitangazwe mpaka Mzee Moyo awepo.
Nikaendea mimi kule Maisara, nikakuta vijana wa Usalama wa Taifa wakanipokea na magari mawili tukaongozana mpaka Bwawani. Tumefika na kukaa, huyu mimi, yeye na mkewe.
Unaona hapo kwenye picha tunanong’onezana? Kila nikiiangalia hii picha namshukuru sana mpiga picha huyu amefanya kazi kubwa.
Alikuwa akiniuliza. Leo nasikia Rais Karume alikupigia simu asubuhi akasema utazungumza na Maalim Seif. Nikamwambia ni kweli alinituma na matokeo ya mazungumzo yetu utayasikia hapa.
Mimi ni Mngoni, siogopi kitu. Basi yakatangazwa matokeo pale akawa ameshinda. Akatoa hotuba pale na wakasema ushindi huu ni wetu sote. Halafu anasema leo hanitambui!
Chaguzi ngapi zimefanywa hapa Zanzibar mimi nilikwenda? Lakini siku ile Amani alisema lazima Mzee Moyo awepo. Kwa sababu anajua kazi yangu, nchi hii imetulia kwa sababu ya uongozi wangu.
Hii picha unayoiona ni kamati yetu ya maridhiano ambayo tulikwenda Ikulu kumtembelea Rais Shein. Hapa bado alikuwa akiitambua. Uchaguzi umefanyika hakuna mtu hata aliyevunjiaka ukucha.
Nilimwambia hii ndiyo kamati ya maridhiano, je tuivunje maana iliundwa na marais wengine. Akasema kwa nini muivunje na kazi mmeshafanya? Basi tukaondoka.
Mara ya pili tukaenda tena kupeleka taarifa ya kamati yetu. Akasema vizuri nitaisoma. Hajatuita mpaka leo. Mpaka katangaza hadharani kuwa haitambui kamati yetu… kasema hadharani, mimi mtu mzima siwe kumsingizia rais wangu.
Basi sisi hatuna haja naye, tunakwenda upande wetu na yeye upande wake, tutakutana tu.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano feki wa mkoloni mweusi Tanganyika), Samia Suluhu Hasan, alisema endapo katiba iliyopendekezwa kama haitapigiwa kura ya ndiyo, Wazanzibar wataendelea kunung’unika katika mambo ya Muungano.((ahaa msaka tonge unajitahidi kumfurahisha mkoloni mweusi Tanganyika kwa kuipigia debe katika feki endelea tu)) Wanachama hao na wapenzi wa chama tawala walitoka maeneo mbalimbali ya mikoa minne ya Zanzibar ambao waliaanza kukusanyika asubuhi.
Mkutano huo ambao ni wa kwanza CCM kufanyika Zanzibar hapa baada ya Bunge Maalum la Katiba kupitisha Katiba hiyo ya CCM inayopendekezwa, ulihudhuriwa na viongozi wakuu wa Chama hicho na waliokuwa wajumbe wote wa bunge hilo kutoka Zanzibar waliopiga kura ya ndiyo wasaka tonge.
Miongoni mwa Wasaka Tonge waliohudhuria ni Makamu wa Pili wa Rais wa Kisonge pia ni balozi mdogo wa nchi ya Tanganyika, Balozi Seif Ali Iddi; Spika wa Baraza la Wawakilishi, Pandu Ameri kificho; Mwenyekiti wa CCM mkoa wa mjini Magharibi, Borafya Silima; Shamsi Vuai Nahodha; Naibu katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai; Ali Ameri Muhammed na wajumbe wote wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) na mke wa Rais wa Kisonge, Mwanamwema Shen.

KILA MZANZIBARI ATAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

No comments:

Post a Comment