Thursday, October 30, 2014

WAMEONA KUJA KWA MELI WANACHELEWA SASA WANATAKA KUJENGA DARAJA KABISA MUUNGANO WA DARAJA UNAINYEMELEA NCHI YETU YA ZANZIBAR


DAR ES SALAAM NCHINI TANGANYIKA MPAKA NCHINI ZANZIBAR

JENGENI VIWANDA NA MAOFISI MUWAJIRI HAWA WAACHE KUJIUZA

WATUHUJENGA NYUMBA ILI RAI WAO WAISHI VIZURI SIO DARAJA ILI MUJE ZANZIBAR

BAADA YA ndoto ya kuziunganisha nchi mbili za Tanganyika na Zanzibar kuwa zina fifia sasa wanakuja na mbinu mpya ya jiji la Dar es Salaam na Kigamboni kwa daraja lenye umbali wa mita 680, Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), linaangalia uwezekano wa kujenga daraja atii la kihistoria zaidi, litakalounganisha Dar es Salaam na bandari ya Malindi nchini Zanzibar. Kwa sasa, uongozi wa shirika hilo upo katika mazungumzo na wataalamu mbalimbali ili kuangalia uwezekano wa kujenga daraja hilo kutoka bandari ya Dar es Salaam kwa upande wa Tanganyika na Unguja nchini Zanzibar.
Umbali kati ya Dar es Salaam nchini Tanganyika na nchi ya Zanzibar ni kilomita 74.43 sawa na meli 45.62 hivyo kuwepo kwa mradi huo ni jambo linalowezekana, kwani kuna madaraja marefu zaidi duniani yanayounganisha upande mmoja wa bahari na mwingine chajabu rai wao hali zao tabani hata mlo moja unawashinda na pahali pa kuishi kwa nini wasiwajenge nyumba za kuish rai wao wa Tanganyika wanakimbilia kujenga dara kutoka dar nchini Tanganyika mpaka nchini Zanzibar kwa nini...?mifuko ya sementi na mchanga na kila kitu vitakavyotumika kujenga daraja hilo kwa nini wasiwajenge rai wao wakawa na nyumba za kuishi.
Kwa sasa, daraja refu zaidi duniani ni lile la Danyang-Kunshan, lililopo nchini China, ambalo linaumbali wa kilomita 165, sawa na meli 102.4. Daraja hilo lilifunguliwa mwezi wa Juni, mwaka 2011. Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Dk Ramadhan Dau wakati alipokuwa akijibu swali la Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii, Said Mtanda ambaye alitaka kufahamu, kama kuna matarajio ya kujenga daraja kubwa zaidi, ikiwezekana kati ya Dar es Salaam nchini Tanganyika mpaka nchini Zanzibar. Akijibu swali hilo alisema wapo katika mazungumzo na wataalamu mbalimbali ambapo mazungumzo hayo yakienda sawa, ujenzi wa daraja hilo huenda isiwe ndoto, bali ukweli.
“Hilo wazo lipo mheshimiwa na tayari tumeshaanza mazungumzo ya awali…kwa hivyo hilo wazo lipo na sisi tulilifikiria,” alisema Dk Dau. Kamati hiyo ilifanya ziara katika miradi mikubwa mitatu ya shirika hilo ambayo ni daraja la Kigamboni, ujenzi wa nyumba za Mtoni Kijichi na ‘Dege-Eco village’ ambao una nyumba zaidi ya 7,000. Akizungumza wakati wa kuhitimisha ziara hiyo, Mtanda alisema kamati yake imeridhishwa na miradi ya NSSF ambayo inaendelea, huku akitaka kuongezwa kwa kasi ili watanganyika waanze kunufaika na miradi hiyo. “Muangalie na hilo la ujenzi wa daraja la kutoka Dar es Salaam nchini Tanganyika hadi nchini Zanzibar alisistiza na mradi wa makazi bora na salama ambao utaweza kubadili taswira ya jiji la Dar es Salaam,” alisema Mtanda.
Alisema kamati yake isingependa kuona changamoto zozote ambazo zinaweza kukwamisha miradi hiyo na kwamba serikali kupitia Wizara ya Ujenzi, itaangalia namna ya kuunganisha miundombinu karibu na miradi hiyo.“Lakini pia tumesikia kuwa serikali inadaiwa na mifuko ya hifadhi…tunashauri serikali kulipa mifuko hii ili kuifanya kuwa na nguvu na kuweza kuleta maendeleo,” alisema Mtanda..

KILA MZANZIBARI ATAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

No comments:

Post a Comment