Thursday, November 20, 2014

KADA WA CCM AELEZAYALIO MOYONI MWAKE KUHUSU CHAMA CHA MKOLONI MWEUSI TANGANYIKA CCM

iddi
BALOZI MDOGO WA NCHI YA TANGANYIKA TING TONG A.K.A BALETOLI AJIDANGANYA KUWA ATI YEYE NDIO ANAFAA KUWA RAISI WA NCHI YA ZANZIBAR 2015
• Kada wa CCM aeleza wazi kwamba hakuna njia ya kuwazuia wapinzani nchini Zanzibar kushinda Uchaguzi wa 2015.
• Asema CCM imekufa hapa nchini Zanzibar, haikubaliki tena na imekimbiwa na idadi ya wanachama wengi katika kipindi cha karibuni kutokana na mchakato wa katiba Mpya.
• Asema kwa hali ilivyo sasa ni wazi wazanzibari wanaiona CCM kuwa sio chama chao tena kinachotetea maslahi yao
• Agusia mpango wa Makamo wa pili wa raisi kutaka kumpikua Dr. Shein katika uchaguzi wa kumpata mgombea wa uraisi wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM 2015.
Kada mkongwe wa chama cha mapindizi ambae ni rafiki mkubwa wa makamo wa pili wa rais wa nchi ya Zanzibar ameamua kuzungumza yaliyo moyoni kuhusiana na mwenendo wa siasa za nchi ya Zanzibar zinavyokwenda na jinsi CCM ilivyojimaliza wenyewe katika kuendesha siasa zake.
Kada huyo maarufu asikitika akisema kwamba “CCM kwa sasa ipo katika wakati mgumu kisiasa kutokana na kukwepa maoni ya wazanzibari katika mchakato wa katiba, na nikwambie jambo moja kwa hali inavyokwenda achilia mbali wilaya zenye mabadiliko makubwa ya kisiasa hapa Zanzibar, CCM huenda ikapoteza viti viwili ndani ya wilaya ya Kati na Kusini katika uchaguzi mkuu ujao”
“Tumeshafanya vikao vya ndani vya chama na kujiridhisha kwamba matawi yetu yamekufa; ndio unaona sasa tunataka kuziingiza maskani zetu katika katiba ya chama ili kutambulika, vijana ambao ndio mwega wa kukiinua chama cha siasa wametukimbia, idadi ya wanachama wetu imepungua na hata wazee hawatutaki na wanatwambia kwamba hawana tena imani na sisi baada ya kuipitisha katiba iliyopendekezwa kule Dodoma” alieleza kada huyo kwa sharti la kutotajwa jina lake kutokana na ukaribu wake na viongozi wakubwa wa chama na serikali.
“Juzi moja nilikua nikizungumza na makamo wa pili, aliniambia wazi nia yake ya kutaka kugombea uraisi wa Zanzibar 2015, kwa kweli sijui amejipanga vipi....?? anasema kwamba rais Shein hatakiwi tena na CCM wa Zanzibar (Unguja) hasa kutokana na asili yake, ingawa kuna taarifa za Shamsu Vuai Nahodha na Dokta Mwiji Haji Makame kujiandaa kuwania nafasi hiyo, yeye anaamini atawapiku wote na kupitishwa kuwa mgombea wa CCM; 2015”
“Balozi pia amenambia kwamba anavyojua yeye huenda Shein asigombee kabisa uraisi 2015, suala hilo litamrahisishia yeye kushinda uchaguzi katika CCM, lakini mimi nadhani endapo atapitishwa CCM itajimaliza zaidi kwakua rafiki yangu hakubaliki kwa wana CCM na wazanzibari wengi hasa kwa siasa anazoziendesha”
Mbali na hayo kada huyo amesema pia kwamba CCM haiwezi kushinda Uchaguzi wa 2015 ikiwa wazanzibari wengi watajitokeza kupiga kura; kwakua hata makambi na vikosi ambavyo vinatayarishwa kwa ajili ya uchaguzi havitoweza kuhimili mabadiliko yaliyopo Zanzibar na Tanganyika, huko bara kuna UKAWA na huku Zanzibar CCM imekufa inachotegemea ni vyombo vya Dola kuisaidia katika uchaguzi ujao.
Kwa mwenendo wa mabadiliko ya kisiasa ya Zanzibar na hasa jinsi Chama cha Wananchi – CUF kinavyokwenda sambamba na mabadiliko hayo kitendo cha kubadilisha mgombea wa uraisi wa Zanzibar hakitowasaidia CCM badala yake kitawaangusha vibaya katika uchaguzi ujao, CUF imebadilika sana kisiasa na itawashangaza wengi 2015.

KILA MZANZIBARI ATAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

No comments:

Post a Comment