Friday, November 28, 2014

MAHAKAMA YA KISUTU BAADA YA KUPATA PIGO KUWA HAIAMINIWI NA WANANCH NA MAHAKI WAO PIA YA AMUUWA KUJISAFISHA NA KUMFUTIA SHEIKH MPONDA KESI HALI WANAJUWA KUWA TOKA MWANZO KULIKUWA HAKUNA KESI BALI KUBABIKIZIWA TU


Nchini Tanganyika Dar es Salaam. Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam imemtakasa Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanaanyika, Sheikh Issa Ponda dhidi ya hukumu ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu iliyomtia hatiani katika kesi ya jinai iliyotokana na mgogoro wa ardhi wa Chang’ombe Markazi. Uamuzi huo ulitolewa jana na Jaji Agustine Shangwa baada ya kuridhika na hoja za rufani za Sheikh Ponda kupitia kwa Wakili wake, Juma Nassoro kupinga hukumu na hatia ya Mahakama ya Kisutu. Mbali na kumfutia hatia hiyo, pia Jaji Shangwa alimshauri Sheikh Ponda kufungua kesi ya madai dhidi ya Baraza Kuu la Waislamu Tanganyika (Bakwata), pamoja na Kampuni ya Agritanza Ltd iliyonunua eneo la Chang’ombe Markazi. Ponda alikata rufani mahakamani hapo akipinga hukumu ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu iliyomtia hatiani katika kesi ya jinai namba 245 ya mwaka 2012, iliyokuwa ikimkabili yeye na wenzake 49. Katika rufaa hiyo, Sheikh Ponda kupitia kwa wakili wake, Nassoro aliwasilisha jumla ya hoja sita za kupinga hukumu hiyo. Hoja hizo zilikuwa ni pamoja na ya kudai kuwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ilikosea kumtia hatiani kwa kuwa hapakuwa na ushahidi wa kutosha kumtia hatiani kwa kosa hilo la kuingia kwa nguvu katika eneo hilo la mgogoro. Pia alidai kuwa mahakama ilikosea kumtia hatiani na kuwaachia huru washtakiwa wenzake. kwa kutumia ushahidhi huohuo, na kwamba kesi hiyo ilikuwa ikihusu mgogoro wa ardhi hivyo Polisi walipaswa kumshauri mlalamikaji akafungue kesi ya madai katika Mahakama ya Ardhi. Hata hivyo katika hukumu yake Jaji Shangwa alijikita katika hoja moja tu kama kulikuwa na ushahidi wa kutosho kumtia hatiani mrufani.
Akijibu hoja hiyo katika hukumu yake, Jaji Shangwa alikubaliana na Wakili wa mrufani kuwa hapakuwa na ushahidi wa kutosha kumtia hatiani mrufani bila kuacha mashaka. Jaji Shangwa alisema kuwa hakuna ushahidi kuwa mrufani aliwashinda mkono au kuwahamaisha wale watu aliokuwa akishitakiwa nao kwenda katika eneo hilo, bali wale watu walikwenda pale wenyewe baada ya kutangaziwa katika misikiti yao kuwa kuna ujenzi wa msikiti wa muda katika eneo hilo. “Kama hakufanya hivyo utasema kuwa aliingia kwa nguvu..???? Nakubaliana na hoza za wakili wa mrufani, Nassoro kuwa hakuna ushahidi wa kutosha mahakama kumtia hatiani mrufani bila kuacha mashaka.”, alisema Jaji Shangwa. Alisema kuwa hata katika maelezo ya Onyo, ya baadhi ya waliokuwa wakishtakiwa pamoja, hakuna hata mmoja aliyesema kuwa alipelekwa katika eneo hilo na Sheikh Ponda na kwamba walikwenda kwa utashi wao baada ya kutangaziwa kuwa kuna ujenzi wa msikiti. “Hivyo ninatengua hukumu ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, ilioyomtia hatiani kwa kosa la kuingia kwa nguvu katika eneo la Chang’ombe Markazi na kumwachia kwa masharti.”, alisema Jaji Shangwa. Hata hivyo licha ya kumfutia hatia hiyo Jaji Shangwa alimshauri Sheikh Ponda asiende kudai hilo eneo kwa njia nyingine isipokuwa kwa njia ya mahakama. Alisema kuwa hadi sasa kuna mkataba kuwa Bakwata waliiuzia Agritanza kwa Sh150 milioni pamoja na eneo lingine la hekari 40 Kisarawe.
Alisema kwa kuwa wanadai kuwa eneo hilo ni mali ya Waislam lililowekwa wakfu na hivyo halikustahili kuuzwa, basi washauriane na wakili wao ili wafungue kesi ya madai dhidi ya Agritanza na kuliunganisha Bakwata, kupinga kuuzwa kwa eneo hilo. Katika kesi ya msingi, Ponda na wenzake walikuwa wakikabiliwa atii mashtaka ya kula njama, wizi wa mali yenye thamani ya Sh 59.6 milioni na kuingia kijinai kwa nia ya kujimilikisha isivyo halali eneo la ardhi inayomilikiwa na Kampuni ya Agritanza Ltd. Ponda na mwenzake Mukadamu Swaleh kwa pamoja walikuwa wakikabiliwa na shtaka linguine zaidi, la uchochezi. Mahakama ya Kisutu katika hukumu yake iliyotolewa na Hakimu Mkazi Victoria Nongwa, Mei 9, 2013, ilimtia hatiani Ponda peke yake kwa kosa la kuingia kijinai katika eneo la ardhi ya Agritanza Ltd, lakini ikawaachia huru washtakiwa wengine wote. Hata hivyo licha ya kumtia hatiani Ponda, mahakama hiyo ilimwachia huru kwa masharti ya kutokutenda kosa lolote katika kipindi cha miezi 12 (mwaka mmoja), chini ya kifungu ncha 25 (g) cha Sheria ya Kanuni za Adhabu (Penal Code- PC). Hata hivyo licha ya kushinda rufaa hiyo Sheikh Ponda alirudishwa mahabusu kutokana na kesi nyingine ya jinai inayomkabili katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro, ambapo dhamana yake imefungwa na Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP). Katika kesi hiyo jinai namba 128 ya mwaka 2013 Morogoro, Ponda anakabiliwa na mashtaka ya kufanya uchochezi katika maeneo mbalimbali mjini Morogoro na kukaidi amri ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, kumtaka asifanye kosa lolote katika kipindi cha miezi 12. Kutokana na hukumu hiyo Wakili wake, Nassoro alisema sasa watawasilisha nakala ya hukumu hiyo katika Mahakama ya Morogoro na kuomba afutiwe shtaka hilo la kukaidi amri ya Mahakama ya Kisutu.

KILA MZANZIBARI ATAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

No comments:

Post a Comment