Monday, November 10, 2014

SHEIN KIDAMPA AENDELE KULIPIGIA DEBE BOOK LA UBATIZO LA MKOLONI MWEUSI TANGANYIKA NCHINI ZANZIBAR MARA HII PEMBE


Rais wa Maskani ya Kisong, Ali Mohamed Shein amesema ndoto za wapinzani kutaka kuvunja Muungano kwa kutumia visingizio vya Zanzibar kuwa na mamlaka kamili, hazitofanikiwa na kuwataka kusahau mpango huo. Akizungumza na wananchi wa mikoa miwili katika mkutano wa hadhara katika Uwanja wa Gombani ya Kale, Chake Chake Pemba jana, alisema Serikali anayoiongoza yeye inafuata makubaliano ya Hati za Muungano ya mwaka 1964.
Katika mkutano huo alijaribu kutumia kufafanua atii mafanikio ya miaka minne ya kuwepo madarakani na Katiba Inayopendekeza aliyopewa na wa Wakoloni Weusi Tanganyika, Shein alisema makubaliano hayo yanahusu muundo wa Muungano wa serikali mbili. “Wapo watu wanadai Zanzibar kuwa na mamlaka kamili…huwezi kuwa na mamlaka kamili kwa mujibu wa Hati ya Muungano ya mwaka 1964…kufanya hivyo ni kuvunja Muungano,” alisema. huku akiendelea Kusema, kwa bahati mbaya, wapinzani wamekuwa wakitumia nafasi ya kupotosha wananchi wa Pemba, hata kwa mambo yenye maslahi ambayo yamelenga kuimarisha uchumi na kukuza maendeleo.((wewe acha upumbavu maendeleo maendeleo gani miaka 50 nchi inanuka nani anawpotosha wanachi kama sio wewe kibushuti..?? ))
Akiendelea kusema Shein “Mimi nashangaa sana hawa wapinzani, walikimbia katika mchakato wa Katiba na sasa wapo vichochoroni wakifanya kazi ya kupotosha ukweli uliopo,” alisema.Kwa mfano alisema kwa bahati mbaya, anasikitika kuwa baadhi ya mawaziri wake, wamekuwa wakiongoza kwa upotoshaji wa hali ya juu kwa mambo ambayo wanafahamu ukweli wake.((Tuambeye basi mambo gani...?? naona unajiuma uma tuu kila mkutano )) “Nasikitika sana wananchi… wapo baadhi ya viongozi katika Serikali ninayoiongoza ni vigeugeu wa hali ya juu, sijui kwa nini jamani,” alisema  Shein kwa masikitiko. Akifafanua, alisema wapo waliotaka muundo wa Muungano wa Mkataba, ambao umekataliwa kwa sababu hauna maslahi na unaweza kuvunja Muungano wa serikali mbili.((umekataliwa na Mkoloni Mweusi Tanganyika wanao kutuma wewe kibaraka wao sio Wazanzibari))
Alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) ipo kwa mujibu wa sheria ikiwa na mihimili yake yote mitatu, ikiwemo Rais, Mahakama na Baraza la kutunga Sheria. “Sasa huyu anayesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar haina mamlaka nani....?? Utakuwaje Rais wa Zanzibar kama huna mamlaka ya nchi....?” alihoji.(( kama unayo mbona Wazanzibari wamekuja kuchukuliwa usiku wa manane na kupelekwa kwa Mkoloni Mweusi Tanganyika na wewe hata kwii kwii hujasema UMEUFYATA. )) Aliwataka wananchi wa Pemba, kujitokeza kwa wingi kuipigia kura Katiba Inayopendekezwa wakati ukifika, kwani katiba hiyo ndiyo mkombozi kwa wananchi wa Zanzibar, itakayoimarisha umoja na utulivu na kuleta maendeleo ya wananchi wote. ((labda maendeleo ya kufungwa jela))
Dk Shein alisema kisiwa cha Pemba sasa kimebadilika kwa kiwango kikubwa, kutokana na mabadiliko yanayoletwa siku hadisiku, ikiwemo kuimarishwa kwa miundo mbinu na nishati ya umeme. “CCM ndiyo chama kinachozingatia maendeleo na kuleta mabadiliko ya wananchi wa Unguja na Pemba ambapo hata washiriki wa maendeleo wanatupongeza kila siku,” alisema. ((Miaka 50 mpaka leo maji tabu umeme tabu unasema nini wewe Miaka 50) Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kusini Pemba, Hamad Bakari Mshindo, alisema wananchi wa Pemba wapo tayari kupigia kura Katiba Inayopendekezwa wakati ukifika. “Nawaomba Wapemba wenzangu, msikubali kupotoshwa na kudanganywa na wapinzani wanaosema kwamba Katiba Inayopendekezwa haina maslahi kwa wananchi wa Zanziba…si kweli,” alisema. Alisema Katiba Inayopendekezwa imetoa fursa kubwa kwa wananchi wa Zanzibar na kufaidika katika maeneo mbali mbali ikiwemo ardhi, elimu na mambo ya uchumi.

KILA MZANZIBARI ATAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

No comments:

Post a Comment