Monday, November 10, 2014

WAZANZIBARI WAZIDI KUJUWA NA KUFAHAMU KUWA CCM SIO CHAMA CHA WAZANZIBARI BALI NI CHAMA CHA MKOLONI MWEUSI TANGANYIKA KIPO KWA JILI YA KUUWANGAMIZA WAZANZIBARI

Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad akizungumza na wanachama wa Baraza za CUF katika kijiji cha Kinyasini Kaskazini Unguja jana.
Makamo wa Raisi wa nchi ya Zanzibar na Katibu Mkuu wa chama cha  CUF, Maalim Seif Sharif Hamad akizungumza na wanachama wa Baraza za CUF katika kijiji cha Kinyasini Kaskazini Unguja jana.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa nchi ya Zanzibar, Mhe. Maalim Seif Shariff Hamad amesema amesikitishwa na hali ngumu inayowakabili wananchi wa kijiji cha Kiomba Mvua katika jimbo la Kitope kushindwa kufanya shughuli zao za kujiletea maendeleo kikamilifu, baada ya sehemu kubwa ya eneo lao kupewa mwekezaji ambaye amewawekea masharti magumu wananchi hao. Maalim Seif Shariff amesema hayo jana wakati alipotembelea Shehia hiyo, iliyopo katika jimbo la Kitope, Wilaya ya Kaskazini ‘B’ Unguja nchini Zanzibar na kupokea malalamiko mengi ya wananchi wa eneo hilo wanayofanyiwa na mwekezaji.
Wana kijiji wamemweleza Makamu wa Kwanza wa Rais kuwa hivi sasa wanashindwa kufanya shughuli zao za uvuvi, kilimo na uanikaji wa madagaa kutokana na vikwazo vya mwekezaji anayeshirikiana na baadhi ya viongozi Serikalini ya SMZ. Makamu wa Kwanza wa Rais amesema kwa nchi inayofuata Utawala Bora kama Zanzibar, migogoro ya aina hiyo ingeweza kuepukwa iwapo busara zingetumika kwa kuwakutanisha wawekezaji na wananchi, kabla ya eneo hilo kutolewa kwa uwekezaji Maalim Seif amesema azma ya kukaribishwa wawekezaji vitegauchumi hapa Zanzibar haikuwa kuleta vilio na masikitiko kwa wananchi, bali ni kuwawezesha wananchi hao pamoja na Serikali wanufaike na ajira ili waweze kupiga hatua kubwa zaidi katika kujikwamua na umasikini.
Amesema wananchi ndio wenye haki na matumizi ya maliasili na rasilimali katika maeneo yao, ikiwemo ardhi na bahari , hivyo ni lazima washirikishwe kikamilifu katika maamuzi yoyote yale yanayohusu matumizi yake. Awali katika risala yao kwa Makamu wa Kwanza wa Rais, wanakijiji hao walisema mwekezaji aliyepewa eneo hilo ambaye wanadhani anataka kufanya shughuli za Utalii, amewazuia wana kijiji kutumia bandari yao ya asili eneo la Nyanjale na sasa wanalazimika kuzunguuka hadi kijiji jirani cha Fujoni wanapotaka kwenda baharini. Sheha Mstaafu wa Shehia ya Kiomba Mvua, Mwinyishaa Sheha Abdallah amesema hivi sasa wana kijiji hao wanaishi katika hali ngumu katika nchi yao, baada ya mwekezaji huyo kuweka uzio na vizuizi na kuwapiga marufuku wasitumie eneo la bahari na ardhi kwa kilimo.
Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad akisalimiana na Sheha mstaafu wa Kiomba Mvua, Mwinshaa Sheha Abdallah kabla ya kumkabidhi rasmi kadi ya CUF.Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad akisalimiana na Sheha mstaafu wa Kiomba Mvua, Mwinshaa Sheha Abdallah kabla ya kumkabidhi rasmi kadi ya CUF.
“Tumelalamika sana kwa viongozi wetu, lakini kubwa lililofanyika walituletea askari na wananchi wengine waliwekwa ndani”, alisema Sheha huyo Mstaafu.Amesema kuwa kitendo hicho kimewavunja moyo sana wananchi wa Kiomba Mvua na kimewafanya wengi wao wahisi kuwa hawathaminiki na hivyo kuchukua maamuzi ya kujiunga na chama cha upinzani cha CUF, ambacho alisema wana matumaini kuwa viongozi wake wamedhamiria kuwatetea wananchi wa Zanzibar na kuwaondoa katika manyanyaso.Naye, Bi Rabani Ali Hassan akizungumza kwa uchungu alisema akinamama wa kijiji hicho ambao ndio wanaotoa mchango mkubwa wa kuendesha familia zao, ikiwemo kuwasomesha watoto, hivi sasa hawana la kufanya baada ya kuzuwiwa kwenda katika eneo la baharini ambako walikuwa wakifanya shughuli za upishi na uanikaji wa madagaa.
Alisema hata vijana wengi ambao zamani walikuwa wakijishughulisha na kazi hizo hawana kazi tena na kuna hatari kubwa kwa vijana hao kujiingiza katika matumizi ya dawa za kulevya kutokana na kukosa shughuli za kujipatia rizki walizokuwa wakizifanya. Katika hafla hiyo, Maalim Seif ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF aliwapokea wanachama 155 waliojiunga na CUF wengi wao kutoka chama cha  CCM cha Mkoloni Mweusi Tanganyika kilicho letwa ndani ya nchi yao ya Zanzibar ili kiwanyonyo na kuwangamiza wazaliwa wa nchi hii ya Zanzibar,pia akiwemo Sheha Mstaafu, Mwinshaa Sheha Abdallah ambaye amejiunga na CUF pamoja na familia zake.Shehia ya Kiomba Mvua ipo katika jimbo la Kitope, Wilaya ya Kaskazini ‘B’ Unguja nchini Zanzibar, jimbo ambalo Mbunge wake ni Balozi ndogo wa nchi ya Tanganyika kwa Mkoloni mweusi, Balozi Seif Ali Iddi na Mwakilishi wake ni Mhe. Makame Mshimba Mbarouk.

KILA MZANZIBARI ATAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

No comments:

Post a Comment