Saturday, January 31, 2015

NCHI YA TANGANYIKA NA NCHI YA ZANZIBAR SIO NCHI ZINAZO FATA DEMOKRASI NI UDEKTETA TU,PIGA TU,WAUWENI TU,WAFUNGENI JELA TU,WATESENI TU,WALAWITINI TU,WATIENI CHUPA NA MAJITI SIHEMU ZAO ZA NYUMA TU,WAPENI MAISHA MAGUMU TU,HAMNA MAJI WALA UMEME KWA RAI WABAKI HIVYO HIVYO TU,TUIBE MAMILLIONI WAKITUSHTUKIA SIUNAJIUZULU TU ILI CCM ENDELE KUBAKI MADARAKANI TUSakata la kupigwa na kudhalilishwa kwa Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba na wafuasi wengine wa chama cha CUF, limeibua mapya, baada wabunge wa upinzani kuja juu wakitaka Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe wawajibike au Bunge liwawajibishe. Wengine, ambao wabunge wanataka wawajibike ni Mkuu wa Jeshi la Polisi, Inspekta Jenerali (IGP), Ernest Mangu, naibu wake (DIGP), Abdukrahman Kaniki, Kamishna wa Operesheni na Mafunzo wa jeshi hilo, Paul Chagonja pamoja na wote waliohusika na kadhia hiyo. Pia wametaka viongozi wengine wa polisi waliohusika ama kutoa amri au kutekeleza unyama huo wachukuliwe hatua za kisheria na jeshi hilo lifumuliwe na kuundwa upya.
PINDA WAPIGWE TU NASEMA WAPIGENI
PINDA HII NDIO DEMOKRASI YAKO..?
Walisema hayo kwa nyakati tofauti wakati wakichangia bungeni mjadala kuhusu hoja iliyohusu jambo la dharura, iliyotolewa na Mbunge wa Kuteuliwa (NCCR-Mageuzi), James Mbatia na kauli ya serikali, kuhusiana na yaliyotokea Januari 27, mwaka huu, Mbagala, Dar es Salaam nchini Tanganyika. Katika mjadala huo, Waziri Chikawe pamoja na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), George Masaju walipatwa na wakati mgumu wakijaribu ama kutoa hoja za kuzuia mjadala kuhusu suala hilo kufanyika bungeni au kuwatetea polisi na kumkandamiza Profesa Lipumba. Kila viongozi hao walipozungumzia mambo hayo, wabunge wa upinzani walikuwa wakipaza sauti zinazoashiria kuwapinga, kuwakejeli na kuzomea.
LISSU
Wa kwanza kuchangia mjadala huo ulioruhusiwa na Spika wa Bunge, Anne Makinda kwa sharti la kutokutoa kauli zinazoingilia mhimili mwingine wa dola, alikuwa ni Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu. Lissu kwanza alikosoa kauli ya Masaju ya kulishauri Bunge liache kujadili kadhia hiyo kwa kuwa kuna kesi iko mahakamani, akisema yeye siyo mshauri wa Bunge na kwamba, kama linahitaji kushauriwa kisheria litashauriwa na Katibu wa Bunge na wanasheria wake na siyo AG. Alisema kauli ya serikali kuhusiana na madhila yaliyotendwa na askari wa Jeshi la Polisi dhidi ya Profesa Lipumba na wafuasi wengine wa CUF, iliyotolewa bungeni jana na Waziri Chikawe, imejaa uwongo Alisema kauli ya Waziri Chikawe, imewapa ufahamu kuwa ile kauli iliyowahi kutolewa bungeni na Waziri Mkuu, Pinda ya kuamuru kila anayekaidi amri ya polisi kupigwa, ni ya serikali nzima, haikuwa ya bahati mbaya na pia ni ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

“Na kwa sababu ni kauli ya serikali, mtu mwingine, mbaye hapaswi kuendelea kubaki katika nafasi yake kwa dakika moja zaidi, ni Waziri Mkuu, Mizengo Pinda,” alisema Lissu. Alisema Jeshi la polisi limetekwa nyara na viashiria vya ufashisti, ambazo zinaungwa mkono na kubebwa na viashiria vya aina hiyo ndani ya CCM na serikali. “Kumbe tunapigwa siyo kwa sababu tuna makosa, tunapigwa kwa sababu kuna mafashisti ndani ya polisi, kuna mafashisti ndani ya serikali, hawa ambao wamesema tupigwe tu,” alisema Lissu. Alisema katiba ya nchi imetamka wazi kuwa (Tanzania) Tanganyika ni nchi ya kidemokrasia yenye kufuata mfumo wa vyama vingi vya siasa. Pia alisema sheria ya vyama vya siasa imeeleza wazi kwamba, moja ya haki za vyama hivyo ni pamoja na kufanya maandamano na mikutano ya hadhara.
“Na sheria ya Jeshi la Polisi mheshimiwa Spika anayoizungumzia huyu waziri (anamuonyesha Chikawe) asiyepaswa kuwapo hapo tena, imewapa polisi mamlaka ya ku-regulate (kudhibiti) mikutano ya hadhara na maandamano, siyo kuyapiga marufuku,” alisema Lissu. Aliongeza: “(sheria hiyo) inawaruhusu kukwambia usifanye leo (maandamano), fanya kesho, usitumie njia hii, tumia njia ile. Haiwapi mamlaka ya kukataza maandamano na mikutano ya hadhara.” Alisema viongozi wote wa vyama vya siasa hakuna asiyekuwa na majeraha, makovu, ambaye hajakamatwa na kunyanyaswa na Jeshi la Polisi. Lissu alisema wengi wa wanasiasa wana kesi nyingi za uwongo zilizotungwa na Jeshi la Polisi na kwamba, (Watanzania) Watanganyika wengi wameuawa na jeshi hilo.
Alisema pia aliyekuwa mwakilishi wa kituo cha televisheni ya Channel ten, mkoani Iringa, Daudi Mwangosi aliuawa na jeshi hilo kwa amri ya aliyekuwa Kamanda wa Polisi mkoani humo, Michael Kamuhanda ambaye amepandishwa cheo na hivi sasa yuko makao makuu ya jeshi hilo, Dar es Salaam. “Watu wetu wameuawa Arusha 2011, wakauwa Arusha 2012 na 2013, wameuawa Morogoro, wameuawa Nzega na Jeshi la Polisi. Serikali hii na jeshi lake imetekwa nyara na fashistic elements (viashiria vya ufashisti),” alisema Lissu. Aliongeza: “Profesa Lipumba amepigwa siyo kwa sababu alikataa (kutii) amri (ya polisi), alitamka, imeonekana dunia nzima kwenye televisheni. Waziri mzima unakuja kudanganya umma hapa.” Hivyo, akasema katika mazingira ambayo Jeshi la Polisi limetekwa nyara na viashiria vya kifashisti, serikali inasema “wapigwe tu” na jeshi hilo limebadilisha hata namba za magari yake kutoka STK kuwa PT ‘Piga Tu’, Bunge lazima lichukue hatua. Pia IGP Mangu, DIGP Kaniki, Chagonja na wote wanaohusika, wawajibike.
Alisema pia yanahitajika mabadiliko makubwa ya kimfumo wa jeshi hilo na kwamba ili yapatikane, inahitajika sera na sheria za nchi zilizopo kuhusu ulinzi na usalama wa raia zitamke wazi wazi kuwa Jeshi Polisi halina mamlaka ya kuzuia maandamano wala mikutano ya hadhara. Kutokana na hali hiyo, alisema umefika wakati wa kuwafukuza kazi wakuu wa wilaya na wakuu wa mikoa kwenye kamati za ulinzi na usalama akisema hao ndiyo wamekuwa chanzo cha wapinzani na raia wengine kupigwa. “(Hao) ni makada wa CCM, ni wajumbe wa vikao vyote vya CCM kwenye ngazi za wilaya, kwenye ngazi za mikoa ndiyo wanaowaamuru ma-OCD (wakuu wa polisi wilaya) watupige, ndiyo wanaowaamuru ma-RPC (makamanda wa polisi mkoa) watupige,” alisema Lissu. Alisema (Tanzania) Tanganyika haiwezi kujiita nchi ya mfumo wa vyama vingi halafu ikaendekeza mambo ya kikatili, ya kifashisti yaliyofanyika Januari 27, mwaka huu.
Alisema (Watanzania) Watanganyika hivi sasa wanaelekea kwenye uchaguzi mkuu, lakini kwa ushahidi uliokwishaonekana kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa wa Jeshi la Polisi kupiga watu bure, kama kelele hazitapigwa sasa, basi maafa makubwa yanawasubiri Aprili, wakati wa kura ya maoni na Oktoba wakati wa uchaguzi huo.
MNYAA
Mbunge wa Mkanyageni (CUF), Mohammed Habib Mnyaa, alisema CUF ilitoa taarifa kwa Jeshi la Polisi kuhusu maandamano hayo tarehe 22 na siyo 26 kama ilivyoelezwa na Chikawe, bungeni. Hata hivyo, alisema jeshi hilo halikujibu lolote hadi tarehe 27 asubuhi siku, ambayo maandamano yalipangwa kufanyika, ndiyo waliipelekea CUF barua ya kuwaarifu kuzuia mkutano wa hadhara na maandamano hayo. Alisema polisi walifanya hivyo wakati CUF wakiwa wamekwishafanya maandalizi makubwa gharama nyingi zikiwa zimetumika, ikiwamo kukodi redio na televisheni kwa ajili ya kurusha matangazo ya shughuli hizo.
Hata hivyo, alisema Profesa Lipumba kwa kutii amri ya polisi alikwenda Temeke Mwisho na kuanza kutoa matangazo ya kuzuia maandamano kufanyika na kuwatawanya wananchi. Alisema kitendo cha Waziri Chikawe, kwenda bungeni kueleza kitu tofauti ni jambo linalosikitisha na kutia aibu kwa Bunge, ambalo linadanganywa, huku wabunge wakipiga kimya. Aliungana na Lissu kutaka Pinda ajiuzulu kutokana na kauli yake “wapigwe tu” vinginevyo, arudi bungeni kwenda kuifuta na pia jeshi la polisi livunjwe.
MKOSAMALI
Mbunge wa Muhambwe (NCCR-Mageuzi), Felix Mkosamali alisema hashangazwi na Jeshi la Polisi kuwatendea hayo raia, kwani ripoti ya Jumuiya ya Madola imeeleza bayana kuwa bado lina mifumo ya wakoloni ya kuhakikisha wanabaki madarakani.
NASARI
Mbunge wa Arumeru Mashariki (Chadema), Joshua Nasari alisema Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora ilipendekeza polisi wachukuliwe hatua, lakini hadi leo hakuna aliyechukuliwa hatua.
MASOUD
Mbunge wa Tumbe (CUF), Masoud alisema Profesa Lipumba ni sawa na Rais Jakaya Kikwete, kwa kuwa wote ni wenyeviti wa vyama vya siasa, hivyo anawashangaa polisi kushindwa kumpa heshima inayostahili na kuwa Waziri Chikawe hafai kuongoza Jeshi la Polisi, hivyo akae pembeni.
SALIM
Mbunge wa Mtambile (CUF), Masoud Abdallah Salim aliitaka serikali kueleza amri ya kumshughulikia Profesa Lipumba na wananchi inayoelezwa kuwa ilitoka juu, ni sehemu gani?
MBOWE
Mbunge wa Hai (Chadema), Freeman Mbowe kwa kuwa Rais na waziri mkuu wameshindwa kuchukua hatua dhidi ya polisi wanaowafanyia madhila wananchi, iundwe kamati teule ya Bunge kushughulikia tatizo hilo.
SHEKIFU
Mbunge wa Lushoto (CCM), Henry Shekifu alisema vurugu zote zinazotokea chanzo chake ni watu kuvunja sheria na kwamba amebaini kuwapo na njama za kutaka kulitumia Bunge kama chombo cha kubadilisha mambo.
Hivyo, akasema kamwe hawawezi kukubali kuona amani inavunjika, badala yake watapambana. Hata hivyo, alisema kama kuna polisi waliotumia nguvu kubwa, basi wachukuliwe hatua.
NKUMBA
Mbunge wa Sikonge (CCM), Said Nkumba alishauri wahusika wote kuchukuliwa hatua kwani hakuna mbunge anayeweza kutetea maovu.
KASSIM
Mbunge wa Chwaka (CCM), Yahya Kassim Issa aliwalaumu CUF kutaka kufanya maandamano hayo kukumbuka watu waliouawa kwa kupigwa risasi na polisi nchini Zanzibar, Januari 27, 2001 huku wakishindwa kufanya hivyo kwa askari polisi aliyechinjwa katika tukio nilo.

SADIFA
Mbunge wa Donge (CCM), Sadifa Juma Khamisi alisema haki ya kuandamana ipo kwenye katiba, lakini haipaswi kutumiwa vibaya, kwani katiba hiyo hiyo inaeleza kuwa hakuna haki isiyokuwa na mipaka.
Kauli hiyo nusura ichafue hali ya hewa bungeni baada ya wabunge wa CUF kumjia juu kutaka kumshughulikia kabla ya Spika Makinda kuingilia kati na kumtaka afute kauli yake hiyo.
LUSINDE
Mbunge wa Mtera (CCM), Livingstone Lusinde alipinga hoja ya kutaka viongozj nao kujiuzulu kwa madai kwamba, kitendo cha polisi kimeonyesha uimara ilionao serikali ya CCM, ambayo mara kwa mara wapinzani wamekuwa wakiita dhaifu.
Awali, akisoma kauli ya serikali, Waziri Chikawe alisema yaliyomkuta Profesa Lipumba, yametokana na kukaidi amri ya polisi iliyozuia kuandamana.
Wakati Chikawe akisoma kauli hiyo ya serikali, wabunge wa upinzani walikuwa wakizomea na kumwita mwongo. Hata hivyo, alisema katika Jeshi la Polisi kuna kitengo cha malalamiko, hivyo kama kuna mtu ana malalamiko, ayawasilishe huko.
Hali ya kuzomea na kutoa maneno ya kumpinga, ilijitokeza wakati Masaju aliposimama bungeni na kulishauri Bunge kwamba, halipaswi kujadili suala hilo kwa kuwa liko mahakamani na kwamba kufanya hivyo, ni kukiuka katiba ya nchi.

KILA MZANZIBARI ATAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

Friday, January 30, 2015

VIDEO-WAPIGWE TU KAULI YA PINDA YAMKUTA PROF LIPUMBA NA WAFUASI WA CUF NCHINI TANGANYIKA MARA HII


KAULI YA PINDA YAENDELEA KUFANYA KAZI NCHINI TANGANYIKA WAPIGWE TU

IKIWA KIONGOZI MKUBWA KAMA HUYU ANADHALILISHWA NAMNA HII HIYO DEMOKRASI IKO WAPI....? KAULI YA PINDA YAENDELEA KUFANYA KAZI NCHINI TANGANYIKA WAPIGWE TU

WAPIGWE TU
ATI ANATAKA AGOMBE URAISI WA NCHI YA TANGANYIKA ILI AWAPIGE VIZURI KABISA HEBU MSIKILIZE
WAPIGWE TU AU SIO PINDA
BAADA YA KUDHALILISHWA PROF LIPUMBA KASHESHE LAZUKA KATIKA BUNGE LA NCHI YA TANGANYIKA

KILA MZANZIBARI ATAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

Friday, January 23, 2015

VIDEO-BAADA YA UCHANGUZI WA 2010 KUMALIZIKA HAYA NDIO YALIYOKUWA YAKITOKEA

KILA MZANZIBARI ATAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

VIDEO_DELETE FUTA KABISA HUYU 2015 HAJI OMARY KHEIRI NA SERA ZILE ZILE ZA TV MOJA KIJIJI KIZIMA WAMPE KILA MTU TIVI YAKE KAMA KWELI.

KILA MZANZIBARI ATAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

Saturday, January 17, 2015

ABDALLAH SHARIA AMEIR MBUNGE WA DIMANI CCM BADALA YA KUWALETE WAZANZIBARI MAENDELEO UNAWALETE KASHFAA KWA HALI HII DELETE FUTA KABISA .


ABDALLAH SHARIA AMEIR MBUNGE WA DIMANI CCM APATWA NA KASHFAA GININGI DODOMA NCHINI TANGANYIKA

MWENYE BUIBUI NA HIJABU NI HAWA KUNDANI ANAYESEMA KUWA AMEZAA NA KUTELEKEZWA NA MBUNGE WA DIMANI,ABDALLAH SHARIA AMEIR,AKIWA CHINI YA ULINZI WA POLISI HUKO DAR ES SALAAM NCHINI TANGANYIKA BAADA YA KUVAMIA KIKAO CHA KAMATI YA BUNGE LA KATIBA,KILICHOKUWA ATII KIKIJADILI  SHERIA NA UTAWALA KILICHOKUWA KIKIFANYIKA.


Nchini Tanganyika jijini Dar es Salaam. Mwanamke aliyetambulika kwa jina la Hawa Kundani amezua taharuki kwenye kikao cha Kamati ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala, baada ya kuvamia ghafla na kupiga kelele akidai kutelekezwa na mumewe ambaye ni Mbunge wa Dimani (CCM) kutoka nchi ya Zanzibar, Abdallah Sharia Ameir.
Tukio hilo la aina yake lilitokea jana kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere, na mwanamke huyo akiwa ameongozana na mtangazaji wa kituo kimoja cha redio, Joyce Kiria aliingia na kusababisha mshtuko kwa wajumbe wa kamati hiyo na viongozi wa dini ya Kikristo waliokuwa wamealikwa hapo. Wakati huo walikuwa wakijadiliana suala la Mahakama ya Kadhi...!!!!!!!!!!!!!!!
Hawa akizungumza na magazeti tafauti na muandishi wetu wa siri akisikiliza kunani Hawa alisemaa kwamba Ameir ni mume wake walifunga ndoa mkoani Arusha mwaka 1999 na kuzaa naye watoto wanne, lakini mmoja alifariki dunia. “ Nashangaa amebadilika ghafla amekuwa mtu wa kuoa wanawake na kuacha mara kwa mara, hadi sasa ameshaoa wanawake wanne na kuwaacha mimi nipo tu, alinioa bado mdogo,” alisemaa Hawa. Huku akiendelea kusemaa kuwa watoto wengine wawili, mkubwa ana miaka tisa na mwingine miaka sita walichukuliwa na mumewe huyo akawapeleka kulelewa na mwanamke aliyemuoa jambo ambalo alidai linamuuma.
“ Naumia wanangu sijui wanaishi vipi, huyu niliyembeba ni mlemavu, hamtaki amekuwa akininanga kwa maneno mengi sana, mimi nimetoka naye mbali nilibadili dini kwa ajili yake, leo hii ananitesa, hanitaki anipe haki yangu ili niishi mwenyewe,” alisema Hawa. Kwa upande wa mbunge hiyo Ameir alidai kwamba kesi yao ipo kwenye Mahakama ya Kadhi, akidai kwamba mwanamke huyo amekuwa akimdhalilisha kwa kupitia mtoto huyo mlemavu ambaye alikiri ni mwanaye. “ Huyu ni mwanangu sishindwi kumhudumia, lakini sitaki fedha ziende kwa huyu mwanamke atazitumia kwa mambo yake mengine, mimi nilimpeleka kwa mama yake mzazi akakae naye huko lakini yeye hataki,” alisema Mbunge Ameir.
Akizungumzia tukio hilo Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Gosbert Blandes alisema ni tukio ambalo limewafedhehesha kwa kuwa hawakulitarajia. “Tulivamiwa na wanawake kama wanne na wanaume wawili nafikiri mmoja alikuwa ni mpiga picha, mwanamke mmoja akawa anapiga kelele, tulitaharuki kwa sababu maaskofu walikuwa wameanza kutoa maoni yao,” alisema. Alisema kwamba waliomba msaada kwa maofisa usalama wa ukumbi na walifika na kuwachukua wahusika hao, kisha kuwapeleka polisi kwa hatua zaidi.

KILA MZANZIBARI ATAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

Friday, January 16, 2015

SHEIN AMRISHA SHAKA ATOLEWE KATIKA VIKAO VYA CCM NA AEKWE CHINI YA ULINZI


Habari za mwaka mpya ndio hizi mupo salama wazenji ulimwenguni kote......bukheri wa afya........Mtu wangu karibu zaidii amenijuza haya yaliyojiri katika Kikao cha kwanza CCM kisiwandui ambapo mwekiti wake alikuwa Rais wa Maskani ya Kisonge Shein. Kikao hichi ni kufuatia vikao 2 ambavyo vimefanyika huko huko nchini Zanzibar baada ya sherehe za Mapinduzi ya kuuwauwa Wazanzibari kuadhimishi miaka 51 ya mapinduzi ya kuwapinduwa  Wazanzibari na kuingeuza nchi ya Zanzibar kuwa kimoja cha kijiji katika vijiji vya nchi ya Tanganyika Mkoloni Mweusi Tanganyika ambapo vikao hivi 2 Mwenyekiti wake alikuwa Raisi Jakaya mrisho Kikwete Raisi wa nchi ya Tanganyika.
Shein ambaye ni Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi alimtoa nje ya ukumbi Shaka Mwenyekiti Vijana CCM nchini Zanzibar na Raisi wa Maskani ya Kisonge Shein kuagiza awe chini ya ulinzi. Hii ilitokana na kikao hicho Baada ya Mwenyekiti wa Kikao hicho Rais Shein kuanza kutaja matarajio na tathmini ya chama chao 2015 kuelekea uchaguzi mkuu. Shein alisema “Napenda nipongeze juhudi zinazochukuliwa na chama chetu kwa viongozi wa chama chetu kukiimarisha chama hichi na kua imara zaidi kuliko changuzi za miaka iliyopita mara hii kukuwa kwa kasi zaidi na kuwa na matarajio makubwa ya ushindi mkubwa wa chama chetu. Ambapo Shein alisema matarajio ya chama Cha Mapinduzi kushinda katika uchaguzi ujao ni kuanzia 52% hadi 58% kwa Zanzibar hivyo ni faraja kubwa. Baada ya kusema hayo alisema kikao kimefunguliwa na mkutano uko wazi wajumbe kuchangia’’.
Akaanza kusimama Dr Hussuen Mwenyi Waziri wa Afya na kumtaka Shein pia afafanue mpasuko uliopo ambao unaonekana wazi kukiathiri chama cha Mapinduzi nchini Zanzibar kuhusu Katiba Feki mpya na kuhusu viongozi wa Jumuia ya Uamsho ambao wamefunguliwa mashtaka nchi jirani Tanganyika kwa Mkoloni Mweusi Tanganyika Baraza jambo ambalo kwa kiasi kikubwa limeonekana kukiathiri chama chao kwa watu walio wengi kuchukizwa na jambo hilo kwa upande wa nchi ya Zanzibar.

Baada ya hapo alisimama ndugu Shaka Mwenyekiti vijana wa CCM na neno la kwanza alisema ‘’Mhe Rais chama chetu kimekufaaaa. Akaendelea kusema ‘’Chama chetu kimekufa na aliyekiuwa chama hichi weweeee. (poleni wasomaji lakini inabidi nicheke kidogo hahahahaha)
Ndio aliposimama Shein na kumwambia Shaka mbona wewe huna heshima maneno gani hayo unayosema kuniambia mimi. Unapaswa kuniheshimu na viongozi na maraisi wote wa Zanzibar mumekuwa mukiwa na heshima lakini mimi munakuwa munanivunjia heshima. Na ndio nyinyi mnaosema mimi sigombanii tena Uraisi wa Zanzibar na hali mimi mwenyewe sijatamka jambo hilo. Maraisi wote waliopita wa Zanzibar haijawahi kutokezea mtu CCM kusema kiongozi huyo hagombanii tena baada kumaliza kipindi cha miaka 5 isipokuwa mimi tu.
Naomba mara moja utoke nje na nitakuchukulia hatua kwa kunivunjia heshima na nitakuweka ndani.  ndipo Shaka alipotolewa nje chini ya ulinzi. Ndipo sasa Aliposimama Asha Bakari kutaka kumtuliza na kumburudisha Shein mjumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar akaanza kumpongeza raisi kwa juhudi za chama zilipofikia na kupiga hatua zaidi katika kuleta Maendeleo, na pia kumtaka Rais aweze kumsamehe Shaka amchukulie kama mtoto amekosea na mtoto akikosea kiganja hakikatwi bali huoshwa na akachukua ahadi watamwita ndugu Shaka ili kumuonya mara ya pili asirudie tena.  ((KIMENUKA CCM CHAMA CHA MKOLONI MWEUSI TANGANYIKA HAPA ZANZIBAR KIMENUKA MTAKE MSITAKE))

KILA MZANZIBARI ATAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

MARAISI WENGI WA AFRIKA WANABADILI KATIBA ILI WABAKI MADARAKANI ILA NCHI YA TANGANYIKA INABADILI KATIBA ILI IMEZE NCHI YA ZANZIBAR NA KUIPOTEZA KATIKA RAMANI YA DUNIA.


 BENDERA YA NCHI YA TANGANYIKA KATIKA UWANJA WA TAIFA  ZILIPOFANYIKA SHEREHE ZA UHURU WA NCHI YAO YA TANGANYIKA.


Leo tunalazimika kuzungumzia utamaduni ambao sasa unaendelea kuota mizizi barani Afrika, utamaduni wa viongozi  au Maraisi wengi barani Afrika kubadili katiba za nchi zao ili kujiongezea muda wa kubaki madarakani.
Vyombo vingi vya habari zimekuwa vikitawaliwa na habari za Maraisi wa nchi mbalimbali barani Afrika kutumia mbinu za kila aina kubadili katiba kwa kisingizio kwamba wananchi wengi wanawataka waendelee kubaki madarakani kwa sababu ya ‘uongozi na utumishi wao uliotukuka’.lakini ukweli wa mambo ni kuwa utamu,uluwa wakuwa madarakani umewalevya mpaka wanakuwa na hali ngumu ya kuwachia ngazi. Utamaduni huo wa Maraisi kutumia hila na ghiliba kuendelea kubaki madarakani kumelifanya bara letu la Afrika kuwa kichekesho mbele ya jumuiya ya kimataifa. Kati ya Maraisi hao, wengi wametumia ujinga na umaskini wa wananchi wao kubaki madarakani huku wao wakijitajiri kwa kuiba serekalini na kujinemesha wao na wake zao na watoto wao na mahawara wao na kila waziri au mbunge na jeshi na polisi wanao msapoti yeye kubaki madarakani basi nao wanakula mpaka wana nenepeyana.
Wametumia kila njia kufifisha demokrasia kwa kukwaza asasi za kiraia zinazosaidia wananchi kutambua haki zao za msingi. Matokeo yake uchumi katika nchi hizo umekwama, kwani demokrasia na maendeleo ya kiuchumi haviwezi kupatikana katika mazingira yanayowanyima wananchi haki hizo. Matokeo ya Maraisi kubadilisha katiba ili kubaki madarakani ni maafa, kwa maana ya vurugu, umwagaji damu na wakati mwingine vita ya wenyewe kwa wenyewe. Pengine ni vyema tukajikumbusha matukio yaliyosababisha vurugu kama hizo hivi karibuni katika baadhi ya nchi barani Afrika. Nchini Burkina Faso, iliyopo Afrika Magharibi, Rais Blaise Campaore ambaye alitawala nchi hiyo kwa miaka 27, hivi karibuni aliondolewa madarakani kwa nguvu ya umma alipotaka kubadili katiba ili aendelee kubaki madarakani.
Pamoja na kuondolewa madarakani kwa aibu na kukimbilia nchi jirani ya Ivory Coast, aliacha nyuma maafa makubwa, kwani wananchi wengi walipoteza maisha, majengo na miundombinu muhimu kama Bunge na Ikulu yaliteketezwa, huku maelfu ya wananchi wakijeruhiwa na kuachwa bila makazi. Kwa upande wa kusini mwa Afrika, ni Rais Yoweri Museveni wa Uganda na Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe ndio pekee wamefanikiwa kubadili katiba za nchi zao na kuendelea kuwa madarakani. Museveni ametawala kwa miaka 25 na Mugabe miaka 29 sasa. Lakini aliyekuwa Rais wa Namibia, Sam Nujoma alijaribu kubadili katiba kiujanjaujanja bila mafanikio, kama ilivyokuwa kwa waliokuwa Maraisi wa Zambia, Kenneth Kaunda na Frederick Chiluba.
Itakumbukwa kwamba aliyekuwa Rais wa Malawi, Bakili Muluzi naye alijaribu kufanya hivyo, lakini akakabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa wananchi na asasi za kiraia. Hivi sasa hali imezidi kuwa siyo shwari nchini DRC, ambako Rais Joseph Kabila anataka kubaki madarakani wakati muda wa utawala wake utakapomalizika, huku nchini Burundi tayari kukiwako machafuko na hali ya wasiwasi kutokana na Rais Pierre Nkurunziza kutaka kubadilisha katiba ili aendelee kuwako madarakani. Hali ni kama hiyo nchini Rwanda ambako Rais Paul Kagame pia anataka kubadili katiba ili aendelee kutawala, wakati aliishatamka kwamba ataachia madaraka baada ya miaka 14 ya utawala wake kwa mujibu wa Katiba. Maraisi wengine wengi barani Afrika wamejaribu kubadili katiba ili wabaki madarakani.
Pamoja na aliyekuwa Rais wa nchi ya Zanzibar, Salmin Amour kujaribu kubadili Katiba bila mafanikio, dunia na Wazanzibari bado wanaiangalia nchi ya Tanganyika kama nchi ambayo viongozi wake wanaheshimu ukomo wa madaraka. Raisi wa nchi ya Tanganyika wa kwanza Nyerere aliwambia viongozi kuheshimu Katiba kwa kupokezana kijiti cha uraisi. Hili ni jambo zuri kwa nchi zote za afrika linatakiwa kulindwa na kuendelezwa kwa kuwa litaendelea kulinda amani na umoja katika nchi za afrika pia ni vizuri kwa Watanganyika na Wazanzibari kwa maingiliano tuliao nayo na kwa nchi ya Tanganyika iliojijengea kwa miaka 53 ya Uhuru.
Athari za vitendo hivyo tumeziona na Ni jambo jema kwamba Rais Jakaya Kikwete amesema amejiandaa kukabidhi madaraka atakapomaliza muda wake baadaye mwaka huu wa nchi yake ya Tanganyika ila bado kuna kamchezo kanachezwa ili kulazimisha katiba mpya ili ije imeze nchi ya Zanzibar na hilo Wazanzibari washalijuwa vizuri sana kuwa hii katiba sio katiba bali ni mpango mzima wa kutaka kuipoteza nchi ya Zanzibar katika ramani ya dunia nchi nyingi zinabadilisha katiba ili Raisi aliyekuwepo abaki madarakani ila nchi ya Tanganyika inabadili katiba ili imeze kabisa nchi ya Zanzibar na ndio maana wamesusa mpaka leo hawataki kujadili huo wanaita Muungano na kila anaepaza sauti kuhusu hilo anaishia jela au anapotea katika mazingira ya kutatanisha je ndio Demokrasia hiyo....???

KILA MZANZIBARI ATAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

Thursday, January 15, 2015

KWA VITISHO HIVI HUYU HAJI OMAR KHEIR NI DELETE FUTA KABISA.NA AKHERA M.MUNGU ANAMSUBIRI


Katika Mkutano wa Chama Cha CCM cha Mkoloni Mweusi Tanganyika Jimbo la Tumbatu uliofanyika tarehe 21/12/2014, Waziri wa Tawala za Mikoa na Idara Maalumu Haji Omar kheir ambaye pia ni mwakilishi wa jimbo la Tumbatu kibaraka au unaweza kusema msaka tonge kitumwa cha Wakoloni Weusi Tanganyika alisema hivi:

“…Namuapia Mungu Wallahi laadhim kama hodari … mana mumehamasishwa nyinyi vijana…..hao Masheikh mnaowalilia huko wanavyofanywa wanavyofanywa ……mtakwenda kuwa wasaidizi wao .…”
Nadhani sote ni mashahidi jinsi Masheikh wa UAMSHO wanavyoendelea kusota katika Magereza ya nchi jiran ya Tanganyika Wakoloni Weusi Tanganyika kwa kukabiliwa na kesi atii za ugaidi na mpaka leo wanasuwasuwa mara ushahidi haujakamilika mara kinyoko kinyokoke uwonevu tu pia kwa kila mwenye akili timamu ana kila sababu ya kuamini kuwa wanachofanyiwa Masheikh hawa ni uonevu na kukosekana kwa utashi wa kutofuatwa sheria . Siyo lengo la makala hii kujadili kesi ya Viongozi wa UAMSHO.
Maneno aliyazungumza Haji Omar Kheir , ameyatoa siku chache tu baada ya Mkutano wa Chama Cha Wananchi – CUF kufanyika Tumbatu ambapo vijana 200 waliamua kuchukua kadi za chama hicho pamoja na ufunguzi wa Baraza ya Cossovo hayo yakiwa mambo yaliyomkera  pumbavu hili yana kukera nini hii ndio demokrasi kama watu wanaona chama hakina maslah na wao wanahama ndivyo ilivyo CCM sio QURAN juha wewe. 
Kwa maneno aliyoyazungumza Haji Omar Kheir yanaonesha wazi kwamba vitendo wanavyofanyiwa mashekhe wa UAMSHO vinaratibiwa na chama chake anachokinadi na kwamba yeye Haji Omar Kheir anaelewa vyema vitendo vya kuingiliwa kinyume na maumbile , kutiwa chupa za sehemu za siri,majiti na vyenginevyo vilivyoripotiwa na magazeti na mitandao kuwa wanafanyiwa mashekhe wa UAMSHO anavielewa vyema na kwamba yeye kama waziri wa Serikali ya SMZ kwa kutumia cheo chake na mamlaka yake hashindwi kuwapeleka magerezani vijana wa Tumbatu na Wazanzibari kwa ujumla kufanyiwa mambo ambayo wanafanyiwa viongozi wa dini ya kiislam kutoka nchini Zanzibar na kufanyiwa vitendo hivyo huko nchini Tanganyika kw Mkoloni Mweusi Tanganyika kwa itikadi za kisiasa kwa kuikataa CCM.

Kwa upande mwengine Haji Omar Kheir anamwakilisha vyema raisi aliyemteua kuwa waziri, na pia anawawakilisha vyema mawaziri wa CCM na viongozi wenzake kama tunavyowasikia kina Shaka Hamdu Shaka, Sadifa, Bi Asha Bakari, Salmin Awadh,Vuai ali Vuai,Balozi Mkazi A.K.A.Baloteli,Samia na Nahodha wanavyowakashifu Wazanzibari ; kwamba matokeo ya wananchi kwa muda wa miaka 50 kuipenda CCM, Kuithamini CCM, Kuilinda CCM na Kuiweka madarakani ni kuwadhalilisha wananchi kwa kuwatukana kila uchao na kwamba hawana maana yoyote mbele ya CCM na Serikali yake na zaidi ni kuwa kila asiye ipenda CCM atajumuika na Masheikh huko nchi ya Mkoloni Mweusi Tanganyika.


M.MUNGU AWAPE MOYO WA SUBIRI HUKO HUKO JELA WALIKO.
MZANZIBARI MWENYE MACHO HAMBIWI TIZAMA AMKA MZANZIBARI AMKA MZANZIBARI LA LEO LIFANYE LEO USISUBIRI KESHO.

KILA MZANZIBARI ATAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

Wednesday, January 14, 2015

SHEIN AJA NA MPYA YA SKULI ZIANZISHE TENA MIRADI YA KUUZA UROJO,KAIMATI NA UJII ILI ZIPATE PESA ZA KUNUNULIA CHAKI DAAAH AIBU TUPU 2015 AMA KWELI AIBU AIBU


Kwanza Hongera Rais wa Kisonge Shein na Wazanzibari woooote ambao bado hawaja elimika kuwa haya mapinduzi sio mapinduzi bali ilikuwa ni kuliwa Wazanzibari na kuchukuliwa nchi yao na kuwa kijiji katika vijiji vya Serekali ya Kikoloni ya Tanganyika Wakoloni Weusi Tanganyika kw akuadhimisha miaka 51 ya Mapinduzi ya kuwauwa Wazanzibari.
Pili, nimesikiliza kwa makini sana hotuba yote (mara mbili au tatu) aliyoitoa Shein katika kilele cha madhimisho ya sherehe za mapinduzi ya kuwauwa Wazanzibari kutimiza miaka 51, pale Amaan stadium.
Kuna kitu sikukifahamu na nitamuomba Shein atufafanulie – Je, elimu alikuwa inalipiwa hapa nchini Zanzibar....???
Kama ni hivyo, ni lini SMZ ilitangaza kuwa sasa elimu sio tena bure; au kwa lugha nyengine ya mnasaba zaidi – Je, dhana ya elimu bure iliondoshwa (lini) na ilitangazwa wapi; alikuwepo nani..??? au BLM lilipitisha hilo...? Je, wananchi tulijulishwa au…..? huna la kuwambia wananchi unabakia kuropoka tu.
Sasa kinachotolewa na wanafunzi ni kitu gani (ada au michango) iliyobuniwa na walimu wenyewe bila ya hata kupata ridhaa ya wazee au hata wizara inayohusika (yaani serikali).....?? Naomba ufafanuzi wenzangu dungu zangu.
Ninacho kifahamu mimi ni kuwa walimu walianzisha hili (kuchangia) baada ya kushindwa hata kuwa na chaki za kuandikia maskulini,na hili sio kosa lao wao ni walimu tu ni kosa lenu nyinyi viongozi musio juwa kutimiza wajibu wenu munacho juwa ni kufitinisha watu na kutisha watu na utamu wa kuiba na kujijengea maisha mazuri na familia zenu basi walio baki kufeni. Hawa walimu pesa hawana, na wizara kushindwa kutimiza haya mahitaji muhimu kwao. Hapo ndipo ilipoanza hicho kitu kinachoitwa ‘michango’ au Shein anasema ‘ada’. Ilikuwa lazima mpaka leo wanafunzi wachangie hili, nafikiri kuanzia 3000 mpaka 5000 shs….skuli nyengine kwa mwaka mpaka elfu 12, na ushei. Almuradi michango au ada zitaendelea; na walimu sifikiri kama wataridhia kauli hii ya Shein maana yeye anaropoka kisha anakwenda ikulu kuchezea biriani halitafuti ufumbuzi unafikiri walimu watafanya nini......??
Huko nyuma, Shein aliwahi kutoa amri kuwa ‘waja wazito wanaokwenda kujifungua hosp.pale mnazi mmoja – wasilipishwe’. Kauli hii pale pale ilipingwa na waziri wake mdogo wa afya, bi.sira ubwa mwamboya. Mpaka leo waja wazito wakija lazima waje na pesa tunalipa kuanzia huduma ya kunua daftari (cheti) 2015 bado tunatumia madaftari aibu tupu mpaka X-ray au utra sound, na hata kuingia pale hosp unalipia, imekuwa kama vile kuigia disco tech/ukumbi wa muzik —na ni jirani na ikulu pale hapana bure tena.
Ninavyoona ni kuwa hii ni siasa ya Shein kuelekea 2015, ili watu wamchague tena na tena. Hilo si tatizo, wewe utapata tu, ukishinda au usishinde siunajuwa jeshi la machogo la Mkoloni Mweusi Tanganyika linakulinda ndio maana pesa zote za nchi ya Zanzibar zinachukuliwa na kuinemesha nchi ya Tanganyika na Wazanzibari wanaumia na maisha na kuufa kwa thiki ya maisha wewe Shein huna wasi wasi unakula tu uluwa wako —Pia tumeshaaambiwa na akina Salmin Awadh Salmin kuwa ‘hata kama tutapiga kura mpaka vidole vikatike basi Zanzibar haitoki mikononi mwa CCM’. na lugha kama hizo……..na mengine mengi waliyosema akina Shaka, Haji Omar Kheri, Balozi Iddi n.k.
Hebu tuangalie – hali halisi ya maskuli yetu…..idadi ya wanafuzni ni kuanzia 60 na ushei, pale mwanakwerekwe, mabanda ya zamani ya maonyesho, sasa yamegeuzwa kuwa skuli — kuna mwanakwerekwe A, B, C,D….lakini kila darasa moja linasoma madarasa mawili (wanaolekea huku ni darasa la sita B, na kinyume chake wanasoma darasa la sita A — mfano). Desk moja na watu wawili, wanakaa wanne mpaka watano…..na hali ndio kama hiyo. Je, hii tutalitatua vipi Shein.............??? miaka 4 upo madaraka lipi umefanya zaidi ya mnara wako pale kisonge......????
Chengine ujenzi wa skuli — SMZ imeamua kujenga skuli kubwa hata kama hakuna wanafunzi wa kusoma, mfano — makunduchi, lakini wilaya ya magharibi pekee inahitaji skuli kama 15, ni wilaya yenye wakaazi wengi kuliko zote hapa nchini Zanzibar kwa mujibu wa sensa ya watu 2012.Nimetaja Makunduchi kwa sababu wakakti wa Maalim Haruna, kama waziri wa elimu, alilazimisha ujenzi wa skuli huko just kuvutia ‘maendeleo’ katika jimbo lake ilhali hakuhitajiki skuli. na kuzipiga panga pesa zote ambazo zilihitajika kwa wahitaji wa skuli, kwa mfano, wilaya ya magahrib. SMZ ilimuachia kukamilisha interests zake wakati nchi inaumia.
Hii ndio hali halisi ya hapa nchini kwetu Zanzibar, ubinafsi, kuvirigiza maneno (ada au michango) ya kuwazuga zuga wananchi kwa kuambiwa kuwa ‘serikali inawaonea huruma ilhali inazidi kuwaumiza na kuwamaliza kabisa huku viongozi wakijitajirisha wao na mahawara wao na kuvimba matumbo yao. Kwa fikra zangu mimi, kauli hii ya Shein kuhusu kulipia mitihani, na kufuta ‘ada/michango’ ni ya kisiasa zaidi ni turufu ya kutaka kuchaguliwa 2015, kulainisha mitambo, kuwalainisha wananchi ili wamuone ‘hodari na mwema’ baada ya mtafaruk wa maisha na kuwasafirisha Masheikh wetu na Dungu zetu kwenda kuwafunga jela ya nchi jirani ya Mkoloni Mweusi Tanganyika. Ukisikiliza ile hotuba yake, utapata picha kuwa Zanzibar ni nchi tajiri sana, na hakuna umasikini kumbe washaimaliza mpaka Mwezi Mtukufu Wa Ramadhani watu Walifuturu Ugali hapa haijapata kutokea lakini Shein mashaa allah.
Sheni alisema skuli zianzishe tena miradi ya kuuza urojo, kaimati na uji ili zipate pesa za kununulia chaki na matengenezo madogo madogo ya skuli ambazo zilitokana na michango hiyo iliyofutwa sasa ngoja tukulize katika utawala wa Mzee Karume miaka hiyo ya sitini na sabiini alipokuwa madarakani ni lini alitangaza kuwa maskuli sasa muuze urojo na kaimati na uji ili mununuwe chaki na matengenezo madogo madogo......?? Mzee Karume kajenga Nyumba za Michenzani,Kilimani N.K. kwa ajili ya wananchi masikini  je wewe Shein  unajenga Nyumba zipi kwa ajili ya masikini.....?? au ule mnara pale Kisonge.........? wakati wa Mzee Karume maji yanatoka 24 7 katika nyumba zenye mifereji leo hii nchi ya Zanzibar imerudi nyuma mpaka inatumia maji ya visima 2015 maendeleo yenu ya mdomo tu miaka 51 ya kuwanyonyo wananchi na kujitajirisha nyinyi Viongozi na Mahawara wenu na matumbo yenu basi ndio faida ya miaka 51 ila kwa rai wakawaida kwa kiswahili cha maskani tunasema KIMENUKA BABA kwa rai wa kawaida.
mengine nimeyawacha kiporo, na hasa sijajua kama ada hii ni ya ‘umma au …..’kama vile Escrow tu.
TOKA AFE KARUME TUNAYUMBA YUMBA TUNASAGA RUMBA HATUNA HATA MAJI ZANZIBAR
WAZANZIBARI HATUTAISAHAU SIKU HII
KILA MZANZIBARI ATAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

Tuesday, January 13, 2015

VIDEO- !!! DELETE FUTA KABISA

UCHANGUZI 2015 OKTOBA SHEIN DELETE FUTA KABISA
BALOZI MKAZI A.K.A.BALOTELI DELETE FUTA KABISA
SAMIA SULU DELETE FUTA KABISA
ALI VUAI DELETE FUTA KABISA
NAHODHA DELETE FUTA KABISA
NA WENGINE WOTE WASAKA TONGE
MADALALI VITUMWA VYA MKOLONI MWEUSI TANGANYIKA DELETE FUTA KABISA.

KILA MZANZIBARI ATAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

VIDEO- TAFAUTI ZA MATUKIO YALIO TOKE KATIKA UTAWALA WA SHEIN KITUMWA CHA MKOLONI MWEUSI TANGANYIKA

ZANZIBAR NAMBA 1

MUNGU ALIUMBA DUNIA ZANZIBAR TANGU NA TANGU


HATUKUPINDUA ILI TUTAWALIWE - MZEE NASSOR MOYO

KABLA YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR RAP

TUNATAKA NCHI YETU


WAZANZIBAR WANAVYOUPOKEA MFUNGO WA RAMADHAN KWA MABOMU! ...............FAIDA ZA SHEIN ALIZO WALETEA WAZANZIBAR KUTOKA KWA MKOLONI MWEUSI TANGANYIKA.


WAZANZIBARI TUNAPOFUTWA MACHOZI KWA KUTOLEWA MACHOZI!...............FAIDA ZA SHEIN ALIZO WALETEA WAZANZIBAR KUTOKA KWA MKOLONI MWEUSI TANGANYIKA.


FAIDA ZA SHEIN ALIZO WALETEA WAZANZIBAR KUTOKA KWA MKOLONI MWEUSI TANGANYIKA.

KILA MZANZIBARI ATAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

Monday, January 12, 2015

VIDEO-JIONE KISHA TAFAKARI KISHA AMUWA WEWE SIKU YA UCHANGUZI ILA KUMBUKA SIKU YA KIYAMA UTAULIZWA UKIPIGIA .....

UBAYA WA DUBWANA MUUNGANO - UAMSHO 'ALABAMA'


KUIJUWA THAMANI YA NCHI YAKO - UAMSHO MAHONDA


NI BORA YA MNYAMA KULIKO MWENYE KUDHULUMU - UAMSHO MSIKITI NGAMIA 


HAJA YA KUWA WAMOJA ~~ UAMSHO MAKUNDUCHI '1'

KILA MZANZIBARI ATAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

VIDEO-HAJA YA KUWA WAMOJA ~ UAMSHO MAKUNDUCHI '2'KILA MZANZIBARI ATAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

VIDEO-SABABU YA KUUKATAA UMOJA HUU ~ UAMSHO KINYASINI


KILA MZANZIBARI ATAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

MANSOUR YUSSUF HIMID NA WZANZIBARI WANASONGA MBELE JE NA WEWE MSOMAJI UNASONGA MBELE AU UMEGANDA...?????


MIEZI minne iliyopita, mama mzazi wa Mansour Yussuf Himid, alinukuliwa akisema kamwe msimamo wake na familia yake wa kupendelea Zanzibar yenye mamlaka kamili, hautabadilika. Alibainisha msimamo huo akisema hata kama gharama yake itakuwa ni kijana wake huyo kufungwa gerezani. Ilikuwa ni kipindi ambacho Mansour ametupwa rumande baada ya kushitakiwa mbele ya Mahakama ya Mkoa ya Vuga, akidaiwa atii kukutwa na silaha pamoja na risasi kinyume cha sheria za nchi ya Zanzibar.
Msimamo huo, ulielezwa kwa wananchi na Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Shariff Hamad kwenye mkutano wa hadhara uliohudhuriwa na umma wa watu katika uwanja wa Demokrasia, Kibandamaiti, nchini Zanzibar. Wakati huo Mansour, aliyeshika uwaziri katika Serikali ya Mapinduzi ya nchi ya Zanzibar kwa miaka 13 mfululizo tangu awamu ya uongozi ya Dk. Salmin Amour Juma, alikuwa gereza kuu la Kilimani, baada ya kesi yake kuahirishwa kwa siku 12.
Mama Jinja, mmoja wa wanawake maarufu nchini Zanzibar, amekuwa imara katika msimamo kwa sababu ameona kuna uonevu Zanzibar inafanyiwa kutokana na ushirikiano wake chini ya Muungano na Tanganyika. Na msimamo huo ndio aliouchukua na kuusimamia kinagaubaga Mansour, tangu akiwa bado serikalini na kama mmoja wa viongozi waandamizi katika CCM. Katika mazungumzo na Muandishi wetu wa Siri hili hivi karibuni, amekiri kuwa huo ndio msimamo hasa uliomchonganisha na viongozi wakubwa wa CCM.
“Wapinzani wangu waliutumia kunifitinisha ndani ya chama,” anasema.
Kwa kuwa hakushituka na mipango iliyokuwa inasukwa dhidi yake, hakutetereka. Aliendelea kuamini hajamkosea mtu yeyote kwani aliona ni wakati muafaka wa nchi ya Zanzibar kurudishiwa mamlaka yake kamili ili ipate kujiongoza na kujisimamia kikanda na kimataifa. Hapo alikuwa akitamka waziwazi kuwa msimamo wake ni kuwa nchi ya Zanzibar inahitaji na ni haki yake kupata mamlaka kamili yakiwemo ya kutumia raslimali za kiuchumi ilizonazo ili kujenga uchumi wake bila ya kulazimika kushauriana na nchi yoyote.
Mansour wakati huo alikuwa ametoka kuwa waziri anayeshughulikia sekta ya kilimo na maliasili, ambako raslimali ya mafuta na gesi asilia inayoaminika ipo ndani ya mamlaka ya nchi ya Zanzibar, ilikuwa imeshatolewa azimio la kutolewa katika orodha ya mambo ya Muungano Feki. Ndio kusema ni uongozi wake kama waziri uliofanikisha serikali kutoa azimio hilo, kwa kuwa alitekeleza uamuzi wa Baraza la Wawakilishi, uliozingatia maoni ya wajumbe kwamba nchi ya Zanzibar inahitaji kushughulikia yenyewe sekta ya mafuta badala ya kutegemea Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika ((Tanzania.))
Aliondolewa uwaziri pale ilipodhihirika kuwa amekuwa na msimamo mkali wa kupinga mwenendo wa Muungano Feki unaoinyonya nchi ya Zanzibar na kuidhoofisha kiuchumi na kutaka kuimeza kabisa. Msimamo huo ulikuwa umeingia vifuani mwa wananchi wengi wa nchi ya Zanzibar waliokuwa wakimsifia na kumpa moyo kwa kujitoa mhanga na kuinua sauti kwa kaulimbiu maarufu ya “Tuachiwe Tupumue.” Mama yake alipotokeza na msimamo imara, alijua hana chaguo isipokuwa kusimama na mwanawe kwa kuamini kuwa ni chuki binafsi tu walizonazo wapinzani wake ndani ya chama zilizomponza.
Alithibitisha hayo kwani Mansour alikamatwa na Polisi ya Mkoa wa Mjini Magharibi, tarehe 6 Agosti, 2014, akapekuliwa nyumbani kwake eneo la Chukwani, nje kidogo ya mji wa mjini magharib huko nchini Zanzibar, na hatimaye kufunguliwa mashtaka ya jinai mahakamani. Madai yaliyoko kwenye hati ya mashtaka, ni tuhuma za kumiliki silaha na risasi kinyume cha sheria za nchi ya Zanzibar. Ametolewa nje kwa dhamana iliyoidhinishwa na Mahakama Kuu nchi ya Zanzibar. Sasa baada ya kukaa bila ya kusema mwelekeo wake wa kisiasa, ambao lazima uegemee kusimamia chama cha siasa, Mansour amefanya kile kinachofaa kuitwa “kukata jongoo kwa meno.”
Amejiunga rasmi na CUF kwa kukabidhiwa kadi ya chama hicho na Katibu Mkuu Maalim Seif mbele ya umma uliohudhuria mkutano wa hadhara katika kijiji cha Paje, Wilaya ya Kusini, Mkoa wa Kusini Unguja nchini Zanzibar, wiki iliyopita. “Nimeamua kujiunga rasmi na chama hichi kwa kuwa anakiamini kuwa ndio chama kinachosimamia ukombozi wa Mzanzibari. CUF ndicho chama kinachobeba matumaini mapya ya Wazanzibari,” anasema. “Leo ile siku imefika, nimeamua kwa hiari yangu kuchukua kadi ya chama cha CUF siyo kwamba nimefanya hivyo kwa kuichukia CCM lakini naipenda CUF kwa nia yake ya kuikomboa Zanzibar. Nawaambia ninasonga mbele,” anasema.
Mansour alishaeleza kuwa utakapofika muda wa uchaguzi mkuu, atarudi jimboni Kiembesamaki, na kuomba ridhaa ya wananchi kwa tiketi ya chama kingine, si CCM, kile alichoingilia Baraza la Wawakilishi, na kuteuliwa waziri baada ya uchaguzi mkuu wa 2000. Alieleza msimamo huo alipoulizwa hatima yake kisiasa baada ya kufukuzwa CCM tarehe 23 Agosti 2013, baada ya kuvuliwa uanachama kwa kutuhumiwa kusaliti chama hicho.Mansour alianza kuonekana mpinzani ndani ya chama alipojitokeza waziwazi akishabikia mfumo mbadala wa muungano badala ya serikali mbili uliopo. Wakati akijiunga na CUF, tayari amekuwa akitekeleza majukumu mbalimbali aliyopewa baada ya kujumuishwa katika timu ya mkakati wa kuhakikisha Maalim Seif anaingia madarakani utakapofika uchaguzi ujao.
Watu wengi wanamuona Mansour kama damu mpya inayohitajika ndani ya CUF kwa kuwa itasaidia kuimarisha nafasi ya chama hicho kushika hatamu ya uongozi huku Maalim Seif atakayesimama tena kuwania urais, akiwa ametamka rasmi kuwa hatawazuia tena vijana wa CUF kudai haki yao wakiamini wamedhulumiwa.“Katika uchaguzi mkuu wa 2010 nilifanya kazi kubwa ya kuwazuia vijana wasifanye vurugu pale hoteli ya Bwawani. Mwanzo niliwatuma wasaidizi wangu waende kuwaondosha, lakini hakuna aliyesikia hadi nilipo kwenda mwenyewe. “Tena waliondoka kwa shingo upande kabisa. Kwa hivyo uchaguzi mkuu ujao sina namna yoyote tena ya kuwazuia vijana kutetea haki yao,” amewaambia wananchi kwenye mkutano wa kijijini Paje.
Maalim Seif amekumbusha kilichotokea wakati Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Khatibu Mwinchande alipokuwa akisubiriwa kutangaza matokeo ya urais yaliyocheleweshwa katika mazingira yaliyozusha hofu kwamba kura zinachakachuliwa. Kundi la wananchi walizingira geti la kuingilia Bwawani, na kutaka kuingia ndani ili wafuatilie kinachoendelea ndani ya ukumbi wa kutangazia matokeo, wa Salama. Wakati huo, kulishaenea taarifa kuwa kamati ya maridhiano ya Mzee Hassan Nassor Moyo, ilikuwa inahangaika kumshawishi Maalim Seif akubali matokeo ya ushindi wa Dk. Ali Mohamed Shein wa CCM kwa nia safi kumbe Shein anawasubiri tu wampe awatende naam katutenda sote mpaka leo Masheikh na Ndugu zetu wanateseka katika majela ya nchi ya Tanganyika kwa Mkoloni Mweusi.
Umma wa Wazanzibari, ulikuwa ukitarajia kusikia tangazo la ushindi wa Maalim Seif. Mansour yumo katika kamati hiyo, pamoja na Mohamed (Eddi) Riyami wakiwa CCM wakati huo, na Ismail Jussa Ladhu, Salim Abdalla Bimani na Abubakar Khamis Bakary kutoka CUF. Riyami alishahama CCM. Kamati hiyo ndiyo iliyofanikisha maafikiano ya siasa za maridhiano kati ya aliyekuwa Rais wa nchi ya Zanzibar, Amani Abeid Karume na Maalim Seif walioanza vikao vya siri Novemba 2009.

KILA MZANZIBARI ATAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.