Saturday, January 17, 2015

ABDALLAH SHARIA AMEIR MBUNGE WA DIMANI CCM BADALA YA KUWALETE WAZANZIBARI MAENDELEO UNAWALETE KASHFAA KWA HALI HII DELETE FUTA KABISA .


ABDALLAH SHARIA AMEIR MBUNGE WA DIMANI CCM APATWA NA KASHFAA GININGI DODOMA NCHINI TANGANYIKA

MWENYE BUIBUI NA HIJABU NI HAWA KUNDANI ANAYESEMA KUWA AMEZAA NA KUTELEKEZWA NA MBUNGE WA DIMANI,ABDALLAH SHARIA AMEIR,AKIWA CHINI YA ULINZI WA POLISI HUKO DAR ES SALAAM NCHINI TANGANYIKA BAADA YA KUVAMIA KIKAO CHA KAMATI YA BUNGE LA KATIBA,KILICHOKUWA ATII KIKIJADILI  SHERIA NA UTAWALA KILICHOKUWA KIKIFANYIKA.


Nchini Tanganyika jijini Dar es Salaam. Mwanamke aliyetambulika kwa jina la Hawa Kundani amezua taharuki kwenye kikao cha Kamati ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala, baada ya kuvamia ghafla na kupiga kelele akidai kutelekezwa na mumewe ambaye ni Mbunge wa Dimani (CCM) kutoka nchi ya Zanzibar, Abdallah Sharia Ameir.
Tukio hilo la aina yake lilitokea jana kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere, na mwanamke huyo akiwa ameongozana na mtangazaji wa kituo kimoja cha redio, Joyce Kiria aliingia na kusababisha mshtuko kwa wajumbe wa kamati hiyo na viongozi wa dini ya Kikristo waliokuwa wamealikwa hapo. Wakati huo walikuwa wakijadiliana suala la Mahakama ya Kadhi...!!!!!!!!!!!!!!!
Hawa akizungumza na magazeti tafauti na muandishi wetu wa siri akisikiliza kunani Hawa alisemaa kwamba Ameir ni mume wake walifunga ndoa mkoani Arusha mwaka 1999 na kuzaa naye watoto wanne, lakini mmoja alifariki dunia. “ Nashangaa amebadilika ghafla amekuwa mtu wa kuoa wanawake na kuacha mara kwa mara, hadi sasa ameshaoa wanawake wanne na kuwaacha mimi nipo tu, alinioa bado mdogo,” alisemaa Hawa. Huku akiendelea kusemaa kuwa watoto wengine wawili, mkubwa ana miaka tisa na mwingine miaka sita walichukuliwa na mumewe huyo akawapeleka kulelewa na mwanamke aliyemuoa jambo ambalo alidai linamuuma.
“ Naumia wanangu sijui wanaishi vipi, huyu niliyembeba ni mlemavu, hamtaki amekuwa akininanga kwa maneno mengi sana, mimi nimetoka naye mbali nilibadili dini kwa ajili yake, leo hii ananitesa, hanitaki anipe haki yangu ili niishi mwenyewe,” alisema Hawa. Kwa upande wa mbunge hiyo Ameir alidai kwamba kesi yao ipo kwenye Mahakama ya Kadhi, akidai kwamba mwanamke huyo amekuwa akimdhalilisha kwa kupitia mtoto huyo mlemavu ambaye alikiri ni mwanaye. “ Huyu ni mwanangu sishindwi kumhudumia, lakini sitaki fedha ziende kwa huyu mwanamke atazitumia kwa mambo yake mengine, mimi nilimpeleka kwa mama yake mzazi akakae naye huko lakini yeye hataki,” alisema Mbunge Ameir.
Akizungumzia tukio hilo Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Gosbert Blandes alisema ni tukio ambalo limewafedhehesha kwa kuwa hawakulitarajia. “Tulivamiwa na wanawake kama wanne na wanaume wawili nafikiri mmoja alikuwa ni mpiga picha, mwanamke mmoja akawa anapiga kelele, tulitaharuki kwa sababu maaskofu walikuwa wameanza kutoa maoni yao,” alisema. Alisema kwamba waliomba msaada kwa maofisa usalama wa ukumbi na walifika na kuwachukua wahusika hao, kisha kuwapeleka polisi kwa hatua zaidi.

KILA MZANZIBARI ATAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

No comments:

Post a Comment