Thursday, January 15, 2015

KWA VITISHO HIVI HUYU HAJI OMAR KHEIR NI DELETE FUTA KABISA.NA AKHERA M.MUNGU ANAMSUBIRI


Katika Mkutano wa Chama Cha CCM cha Mkoloni Mweusi Tanganyika Jimbo la Tumbatu uliofanyika tarehe 21/12/2014, Waziri wa Tawala za Mikoa na Idara Maalumu Haji Omar kheir ambaye pia ni mwakilishi wa jimbo la Tumbatu kibaraka au unaweza kusema msaka tonge kitumwa cha Wakoloni Weusi Tanganyika alisema hivi:

“…Namuapia Mungu Wallahi laadhim kama hodari … mana mumehamasishwa nyinyi vijana…..hao Masheikh mnaowalilia huko wanavyofanywa wanavyofanywa ……mtakwenda kuwa wasaidizi wao .…”
Nadhani sote ni mashahidi jinsi Masheikh wa UAMSHO wanavyoendelea kusota katika Magereza ya nchi jiran ya Tanganyika Wakoloni Weusi Tanganyika kwa kukabiliwa na kesi atii za ugaidi na mpaka leo wanasuwasuwa mara ushahidi haujakamilika mara kinyoko kinyokoke uwonevu tu pia kwa kila mwenye akili timamu ana kila sababu ya kuamini kuwa wanachofanyiwa Masheikh hawa ni uonevu na kukosekana kwa utashi wa kutofuatwa sheria . Siyo lengo la makala hii kujadili kesi ya Viongozi wa UAMSHO.
Maneno aliyazungumza Haji Omar Kheir , ameyatoa siku chache tu baada ya Mkutano wa Chama Cha Wananchi – CUF kufanyika Tumbatu ambapo vijana 200 waliamua kuchukua kadi za chama hicho pamoja na ufunguzi wa Baraza ya Cossovo hayo yakiwa mambo yaliyomkera  pumbavu hili yana kukera nini hii ndio demokrasi kama watu wanaona chama hakina maslah na wao wanahama ndivyo ilivyo CCM sio QURAN juha wewe. 
Kwa maneno aliyoyazungumza Haji Omar Kheir yanaonesha wazi kwamba vitendo wanavyofanyiwa mashekhe wa UAMSHO vinaratibiwa na chama chake anachokinadi na kwamba yeye Haji Omar Kheir anaelewa vyema vitendo vya kuingiliwa kinyume na maumbile , kutiwa chupa za sehemu za siri,majiti na vyenginevyo vilivyoripotiwa na magazeti na mitandao kuwa wanafanyiwa mashekhe wa UAMSHO anavielewa vyema na kwamba yeye kama waziri wa Serikali ya SMZ kwa kutumia cheo chake na mamlaka yake hashindwi kuwapeleka magerezani vijana wa Tumbatu na Wazanzibari kwa ujumla kufanyiwa mambo ambayo wanafanyiwa viongozi wa dini ya kiislam kutoka nchini Zanzibar na kufanyiwa vitendo hivyo huko nchini Tanganyika kw Mkoloni Mweusi Tanganyika kwa itikadi za kisiasa kwa kuikataa CCM.

Kwa upande mwengine Haji Omar Kheir anamwakilisha vyema raisi aliyemteua kuwa waziri, na pia anawawakilisha vyema mawaziri wa CCM na viongozi wenzake kama tunavyowasikia kina Shaka Hamdu Shaka, Sadifa, Bi Asha Bakari, Salmin Awadh,Vuai ali Vuai,Balozi Mkazi A.K.A.Baloteli,Samia na Nahodha wanavyowakashifu Wazanzibari ; kwamba matokeo ya wananchi kwa muda wa miaka 50 kuipenda CCM, Kuithamini CCM, Kuilinda CCM na Kuiweka madarakani ni kuwadhalilisha wananchi kwa kuwatukana kila uchao na kwamba hawana maana yoyote mbele ya CCM na Serikali yake na zaidi ni kuwa kila asiye ipenda CCM atajumuika na Masheikh huko nchi ya Mkoloni Mweusi Tanganyika.


M.MUNGU AWAPE MOYO WA SUBIRI HUKO HUKO JELA WALIKO.
MZANZIBARI MWENYE MACHO HAMBIWI TIZAMA AMKA MZANZIBARI AMKA MZANZIBARI LA LEO LIFANYE LEO USISUBIRI KESHO.

KILA MZANZIBARI ATAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

No comments:

Post a Comment