Friday, January 16, 2015

MARAISI WENGI WA AFRIKA WANABADILI KATIBA ILI WABAKI MADARAKANI ILA NCHI YA TANGANYIKA INABADILI KATIBA ILI IMEZE NCHI YA ZANZIBAR NA KUIPOTEZA KATIKA RAMANI YA DUNIA.


 BENDERA YA NCHI YA TANGANYIKA KATIKA UWANJA WA TAIFA  ZILIPOFANYIKA SHEREHE ZA UHURU WA NCHI YAO YA TANGANYIKA.


Leo tunalazimika kuzungumzia utamaduni ambao sasa unaendelea kuota mizizi barani Afrika, utamaduni wa viongozi  au Maraisi wengi barani Afrika kubadili katiba za nchi zao ili kujiongezea muda wa kubaki madarakani.
Vyombo vingi vya habari zimekuwa vikitawaliwa na habari za Maraisi wa nchi mbalimbali barani Afrika kutumia mbinu za kila aina kubadili katiba kwa kisingizio kwamba wananchi wengi wanawataka waendelee kubaki madarakani kwa sababu ya ‘uongozi na utumishi wao uliotukuka’.lakini ukweli wa mambo ni kuwa utamu,uluwa wakuwa madarakani umewalevya mpaka wanakuwa na hali ngumu ya kuwachia ngazi. Utamaduni huo wa Maraisi kutumia hila na ghiliba kuendelea kubaki madarakani kumelifanya bara letu la Afrika kuwa kichekesho mbele ya jumuiya ya kimataifa. Kati ya Maraisi hao, wengi wametumia ujinga na umaskini wa wananchi wao kubaki madarakani huku wao wakijitajiri kwa kuiba serekalini na kujinemesha wao na wake zao na watoto wao na mahawara wao na kila waziri au mbunge na jeshi na polisi wanao msapoti yeye kubaki madarakani basi nao wanakula mpaka wana nenepeyana.
Wametumia kila njia kufifisha demokrasia kwa kukwaza asasi za kiraia zinazosaidia wananchi kutambua haki zao za msingi. Matokeo yake uchumi katika nchi hizo umekwama, kwani demokrasia na maendeleo ya kiuchumi haviwezi kupatikana katika mazingira yanayowanyima wananchi haki hizo. Matokeo ya Maraisi kubadilisha katiba ili kubaki madarakani ni maafa, kwa maana ya vurugu, umwagaji damu na wakati mwingine vita ya wenyewe kwa wenyewe. Pengine ni vyema tukajikumbusha matukio yaliyosababisha vurugu kama hizo hivi karibuni katika baadhi ya nchi barani Afrika. Nchini Burkina Faso, iliyopo Afrika Magharibi, Rais Blaise Campaore ambaye alitawala nchi hiyo kwa miaka 27, hivi karibuni aliondolewa madarakani kwa nguvu ya umma alipotaka kubadili katiba ili aendelee kubaki madarakani.
Pamoja na kuondolewa madarakani kwa aibu na kukimbilia nchi jirani ya Ivory Coast, aliacha nyuma maafa makubwa, kwani wananchi wengi walipoteza maisha, majengo na miundombinu muhimu kama Bunge na Ikulu yaliteketezwa, huku maelfu ya wananchi wakijeruhiwa na kuachwa bila makazi. Kwa upande wa kusini mwa Afrika, ni Rais Yoweri Museveni wa Uganda na Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe ndio pekee wamefanikiwa kubadili katiba za nchi zao na kuendelea kuwa madarakani. Museveni ametawala kwa miaka 25 na Mugabe miaka 29 sasa. Lakini aliyekuwa Rais wa Namibia, Sam Nujoma alijaribu kubadili katiba kiujanjaujanja bila mafanikio, kama ilivyokuwa kwa waliokuwa Maraisi wa Zambia, Kenneth Kaunda na Frederick Chiluba.
Itakumbukwa kwamba aliyekuwa Rais wa Malawi, Bakili Muluzi naye alijaribu kufanya hivyo, lakini akakabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa wananchi na asasi za kiraia. Hivi sasa hali imezidi kuwa siyo shwari nchini DRC, ambako Rais Joseph Kabila anataka kubaki madarakani wakati muda wa utawala wake utakapomalizika, huku nchini Burundi tayari kukiwako machafuko na hali ya wasiwasi kutokana na Rais Pierre Nkurunziza kutaka kubadilisha katiba ili aendelee kuwako madarakani. Hali ni kama hiyo nchini Rwanda ambako Rais Paul Kagame pia anataka kubadili katiba ili aendelee kutawala, wakati aliishatamka kwamba ataachia madaraka baada ya miaka 14 ya utawala wake kwa mujibu wa Katiba. Maraisi wengine wengi barani Afrika wamejaribu kubadili katiba ili wabaki madarakani.
Pamoja na aliyekuwa Rais wa nchi ya Zanzibar, Salmin Amour kujaribu kubadili Katiba bila mafanikio, dunia na Wazanzibari bado wanaiangalia nchi ya Tanganyika kama nchi ambayo viongozi wake wanaheshimu ukomo wa madaraka. Raisi wa nchi ya Tanganyika wa kwanza Nyerere aliwambia viongozi kuheshimu Katiba kwa kupokezana kijiti cha uraisi. Hili ni jambo zuri kwa nchi zote za afrika linatakiwa kulindwa na kuendelezwa kwa kuwa litaendelea kulinda amani na umoja katika nchi za afrika pia ni vizuri kwa Watanganyika na Wazanzibari kwa maingiliano tuliao nayo na kwa nchi ya Tanganyika iliojijengea kwa miaka 53 ya Uhuru.
Athari za vitendo hivyo tumeziona na Ni jambo jema kwamba Rais Jakaya Kikwete amesema amejiandaa kukabidhi madaraka atakapomaliza muda wake baadaye mwaka huu wa nchi yake ya Tanganyika ila bado kuna kamchezo kanachezwa ili kulazimisha katiba mpya ili ije imeze nchi ya Zanzibar na hilo Wazanzibari washalijuwa vizuri sana kuwa hii katiba sio katiba bali ni mpango mzima wa kutaka kuipoteza nchi ya Zanzibar katika ramani ya dunia nchi nyingi zinabadilisha katiba ili Raisi aliyekuwepo abaki madarakani ila nchi ya Tanganyika inabadili katiba ili imeze kabisa nchi ya Zanzibar na ndio maana wamesusa mpaka leo hawataki kujadili huo wanaita Muungano na kila anaepaza sauti kuhusu hilo anaishia jela au anapotea katika mazingira ya kutatanisha je ndio Demokrasia hiyo....???

KILA MZANZIBARI ATAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

No comments:

Post a Comment