Wednesday, January 14, 2015

SHEIN AJA NA MPYA YA SKULI ZIANZISHE TENA MIRADI YA KUUZA UROJO,KAIMATI NA UJII ILI ZIPATE PESA ZA KUNUNULIA CHAKI DAAAH AIBU TUPU 2015 AMA KWELI AIBU AIBU


Kwanza Hongera Rais wa Kisonge Shein na Wazanzibari woooote ambao bado hawaja elimika kuwa haya mapinduzi sio mapinduzi bali ilikuwa ni kuliwa Wazanzibari na kuchukuliwa nchi yao na kuwa kijiji katika vijiji vya Serekali ya Kikoloni ya Tanganyika Wakoloni Weusi Tanganyika kw akuadhimisha miaka 51 ya Mapinduzi ya kuwauwa Wazanzibari.
Pili, nimesikiliza kwa makini sana hotuba yote (mara mbili au tatu) aliyoitoa Shein katika kilele cha madhimisho ya sherehe za mapinduzi ya kuwauwa Wazanzibari kutimiza miaka 51, pale Amaan stadium.
Kuna kitu sikukifahamu na nitamuomba Shein atufafanulie – Je, elimu alikuwa inalipiwa hapa nchini Zanzibar....???
Kama ni hivyo, ni lini SMZ ilitangaza kuwa sasa elimu sio tena bure; au kwa lugha nyengine ya mnasaba zaidi – Je, dhana ya elimu bure iliondoshwa (lini) na ilitangazwa wapi; alikuwepo nani..??? au BLM lilipitisha hilo...? Je, wananchi tulijulishwa au…..? huna la kuwambia wananchi unabakia kuropoka tu.
Sasa kinachotolewa na wanafunzi ni kitu gani (ada au michango) iliyobuniwa na walimu wenyewe bila ya hata kupata ridhaa ya wazee au hata wizara inayohusika (yaani serikali).....?? Naomba ufafanuzi wenzangu dungu zangu.
Ninacho kifahamu mimi ni kuwa walimu walianzisha hili (kuchangia) baada ya kushindwa hata kuwa na chaki za kuandikia maskulini,na hili sio kosa lao wao ni walimu tu ni kosa lenu nyinyi viongozi musio juwa kutimiza wajibu wenu munacho juwa ni kufitinisha watu na kutisha watu na utamu wa kuiba na kujijengea maisha mazuri na familia zenu basi walio baki kufeni. Hawa walimu pesa hawana, na wizara kushindwa kutimiza haya mahitaji muhimu kwao. Hapo ndipo ilipoanza hicho kitu kinachoitwa ‘michango’ au Shein anasema ‘ada’. Ilikuwa lazima mpaka leo wanafunzi wachangie hili, nafikiri kuanzia 3000 mpaka 5000 shs….skuli nyengine kwa mwaka mpaka elfu 12, na ushei. Almuradi michango au ada zitaendelea; na walimu sifikiri kama wataridhia kauli hii ya Shein maana yeye anaropoka kisha anakwenda ikulu kuchezea biriani halitafuti ufumbuzi unafikiri walimu watafanya nini......??
Huko nyuma, Shein aliwahi kutoa amri kuwa ‘waja wazito wanaokwenda kujifungua hosp.pale mnazi mmoja – wasilipishwe’. Kauli hii pale pale ilipingwa na waziri wake mdogo wa afya, bi.sira ubwa mwamboya. Mpaka leo waja wazito wakija lazima waje na pesa tunalipa kuanzia huduma ya kunua daftari (cheti) 2015 bado tunatumia madaftari aibu tupu mpaka X-ray au utra sound, na hata kuingia pale hosp unalipia, imekuwa kama vile kuigia disco tech/ukumbi wa muzik —na ni jirani na ikulu pale hapana bure tena.
Ninavyoona ni kuwa hii ni siasa ya Shein kuelekea 2015, ili watu wamchague tena na tena. Hilo si tatizo, wewe utapata tu, ukishinda au usishinde siunajuwa jeshi la machogo la Mkoloni Mweusi Tanganyika linakulinda ndio maana pesa zote za nchi ya Zanzibar zinachukuliwa na kuinemesha nchi ya Tanganyika na Wazanzibari wanaumia na maisha na kuufa kwa thiki ya maisha wewe Shein huna wasi wasi unakula tu uluwa wako —Pia tumeshaaambiwa na akina Salmin Awadh Salmin kuwa ‘hata kama tutapiga kura mpaka vidole vikatike basi Zanzibar haitoki mikononi mwa CCM’. na lugha kama hizo……..na mengine mengi waliyosema akina Shaka, Haji Omar Kheri, Balozi Iddi n.k.
Hebu tuangalie – hali halisi ya maskuli yetu…..idadi ya wanafuzni ni kuanzia 60 na ushei, pale mwanakwerekwe, mabanda ya zamani ya maonyesho, sasa yamegeuzwa kuwa skuli — kuna mwanakwerekwe A, B, C,D….lakini kila darasa moja linasoma madarasa mawili (wanaolekea huku ni darasa la sita B, na kinyume chake wanasoma darasa la sita A — mfano). Desk moja na watu wawili, wanakaa wanne mpaka watano…..na hali ndio kama hiyo. Je, hii tutalitatua vipi Shein.............??? miaka 4 upo madaraka lipi umefanya zaidi ya mnara wako pale kisonge......????
Chengine ujenzi wa skuli — SMZ imeamua kujenga skuli kubwa hata kama hakuna wanafunzi wa kusoma, mfano — makunduchi, lakini wilaya ya magharibi pekee inahitaji skuli kama 15, ni wilaya yenye wakaazi wengi kuliko zote hapa nchini Zanzibar kwa mujibu wa sensa ya watu 2012.Nimetaja Makunduchi kwa sababu wakakti wa Maalim Haruna, kama waziri wa elimu, alilazimisha ujenzi wa skuli huko just kuvutia ‘maendeleo’ katika jimbo lake ilhali hakuhitajiki skuli. na kuzipiga panga pesa zote ambazo zilihitajika kwa wahitaji wa skuli, kwa mfano, wilaya ya magahrib. SMZ ilimuachia kukamilisha interests zake wakati nchi inaumia.
Hii ndio hali halisi ya hapa nchini kwetu Zanzibar, ubinafsi, kuvirigiza maneno (ada au michango) ya kuwazuga zuga wananchi kwa kuambiwa kuwa ‘serikali inawaonea huruma ilhali inazidi kuwaumiza na kuwamaliza kabisa huku viongozi wakijitajirisha wao na mahawara wao na kuvimba matumbo yao. Kwa fikra zangu mimi, kauli hii ya Shein kuhusu kulipia mitihani, na kufuta ‘ada/michango’ ni ya kisiasa zaidi ni turufu ya kutaka kuchaguliwa 2015, kulainisha mitambo, kuwalainisha wananchi ili wamuone ‘hodari na mwema’ baada ya mtafaruk wa maisha na kuwasafirisha Masheikh wetu na Dungu zetu kwenda kuwafunga jela ya nchi jirani ya Mkoloni Mweusi Tanganyika. Ukisikiliza ile hotuba yake, utapata picha kuwa Zanzibar ni nchi tajiri sana, na hakuna umasikini kumbe washaimaliza mpaka Mwezi Mtukufu Wa Ramadhani watu Walifuturu Ugali hapa haijapata kutokea lakini Shein mashaa allah.
Sheni alisema skuli zianzishe tena miradi ya kuuza urojo, kaimati na uji ili zipate pesa za kununulia chaki na matengenezo madogo madogo ya skuli ambazo zilitokana na michango hiyo iliyofutwa sasa ngoja tukulize katika utawala wa Mzee Karume miaka hiyo ya sitini na sabiini alipokuwa madarakani ni lini alitangaza kuwa maskuli sasa muuze urojo na kaimati na uji ili mununuwe chaki na matengenezo madogo madogo......?? Mzee Karume kajenga Nyumba za Michenzani,Kilimani N.K. kwa ajili ya wananchi masikini  je wewe Shein  unajenga Nyumba zipi kwa ajili ya masikini.....?? au ule mnara pale Kisonge.........? wakati wa Mzee Karume maji yanatoka 24 7 katika nyumba zenye mifereji leo hii nchi ya Zanzibar imerudi nyuma mpaka inatumia maji ya visima 2015 maendeleo yenu ya mdomo tu miaka 51 ya kuwanyonyo wananchi na kujitajirisha nyinyi Viongozi na Mahawara wenu na matumbo yenu basi ndio faida ya miaka 51 ila kwa rai wakawaida kwa kiswahili cha maskani tunasema KIMENUKA BABA kwa rai wa kawaida.
mengine nimeyawacha kiporo, na hasa sijajua kama ada hii ni ya ‘umma au …..’kama vile Escrow tu.
TOKA AFE KARUME TUNAYUMBA YUMBA TUNASAGA RUMBA HATUNA HATA MAJI ZANZIBAR
WAZANZIBARI HATUTAISAHAU SIKU HII
KILA MZANZIBARI ATAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

No comments:

Post a Comment