Friday, January 16, 2015

SHEIN AMRISHA SHAKA ATOLEWE KATIKA VIKAO VYA CCM NA AEKWE CHINI YA ULINZI


Habari za mwaka mpya ndio hizi mupo salama wazenji ulimwenguni kote......bukheri wa afya........Mtu wangu karibu zaidii amenijuza haya yaliyojiri katika Kikao cha kwanza CCM kisiwandui ambapo mwekiti wake alikuwa Rais wa Maskani ya Kisonge Shein. Kikao hichi ni kufuatia vikao 2 ambavyo vimefanyika huko huko nchini Zanzibar baada ya sherehe za Mapinduzi ya kuuwauwa Wazanzibari kuadhimishi miaka 51 ya mapinduzi ya kuwapinduwa  Wazanzibari na kuingeuza nchi ya Zanzibar kuwa kimoja cha kijiji katika vijiji vya nchi ya Tanganyika Mkoloni Mweusi Tanganyika ambapo vikao hivi 2 Mwenyekiti wake alikuwa Raisi Jakaya mrisho Kikwete Raisi wa nchi ya Tanganyika.
Shein ambaye ni Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi alimtoa nje ya ukumbi Shaka Mwenyekiti Vijana CCM nchini Zanzibar na Raisi wa Maskani ya Kisonge Shein kuagiza awe chini ya ulinzi. Hii ilitokana na kikao hicho Baada ya Mwenyekiti wa Kikao hicho Rais Shein kuanza kutaja matarajio na tathmini ya chama chao 2015 kuelekea uchaguzi mkuu. Shein alisema “Napenda nipongeze juhudi zinazochukuliwa na chama chetu kwa viongozi wa chama chetu kukiimarisha chama hichi na kua imara zaidi kuliko changuzi za miaka iliyopita mara hii kukuwa kwa kasi zaidi na kuwa na matarajio makubwa ya ushindi mkubwa wa chama chetu. Ambapo Shein alisema matarajio ya chama Cha Mapinduzi kushinda katika uchaguzi ujao ni kuanzia 52% hadi 58% kwa Zanzibar hivyo ni faraja kubwa. Baada ya kusema hayo alisema kikao kimefunguliwa na mkutano uko wazi wajumbe kuchangia’’.
Akaanza kusimama Dr Hussuen Mwenyi Waziri wa Afya na kumtaka Shein pia afafanue mpasuko uliopo ambao unaonekana wazi kukiathiri chama cha Mapinduzi nchini Zanzibar kuhusu Katiba Feki mpya na kuhusu viongozi wa Jumuia ya Uamsho ambao wamefunguliwa mashtaka nchi jirani Tanganyika kwa Mkoloni Mweusi Tanganyika Baraza jambo ambalo kwa kiasi kikubwa limeonekana kukiathiri chama chao kwa watu walio wengi kuchukizwa na jambo hilo kwa upande wa nchi ya Zanzibar.

Baada ya hapo alisimama ndugu Shaka Mwenyekiti vijana wa CCM na neno la kwanza alisema ‘’Mhe Rais chama chetu kimekufaaaa. Akaendelea kusema ‘’Chama chetu kimekufa na aliyekiuwa chama hichi weweeee. (poleni wasomaji lakini inabidi nicheke kidogo hahahahaha)
Ndio aliposimama Shein na kumwambia Shaka mbona wewe huna heshima maneno gani hayo unayosema kuniambia mimi. Unapaswa kuniheshimu na viongozi na maraisi wote wa Zanzibar mumekuwa mukiwa na heshima lakini mimi munakuwa munanivunjia heshima. Na ndio nyinyi mnaosema mimi sigombanii tena Uraisi wa Zanzibar na hali mimi mwenyewe sijatamka jambo hilo. Maraisi wote waliopita wa Zanzibar haijawahi kutokezea mtu CCM kusema kiongozi huyo hagombanii tena baada kumaliza kipindi cha miaka 5 isipokuwa mimi tu.
Naomba mara moja utoke nje na nitakuchukulia hatua kwa kunivunjia heshima na nitakuweka ndani.  ndipo Shaka alipotolewa nje chini ya ulinzi. Ndipo sasa Aliposimama Asha Bakari kutaka kumtuliza na kumburudisha Shein mjumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar akaanza kumpongeza raisi kwa juhudi za chama zilipofikia na kupiga hatua zaidi katika kuleta Maendeleo, na pia kumtaka Rais aweze kumsamehe Shaka amchukulie kama mtoto amekosea na mtoto akikosea kiganja hakikatwi bali huoshwa na akachukua ahadi watamwita ndugu Shaka ili kumuonya mara ya pili asirudie tena.  ((KIMENUKA CCM CHAMA CHA MKOLONI MWEUSI TANGANYIKA HAPA ZANZIBAR KIMENUKA MTAKE MSITAKE))

KILA MZANZIBARI ATAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

No comments:

Post a Comment