Friday, February 20, 2015

INNAA LILLAAHI WAINNAA ILAYHI RAAJIU;UUN CCM GOGO SALMIN AWADHI KUWA AMEFARIKI DUNIA GHAFLA


Salmin Awadhi wakati wa uhai wake akihutubia katika mkutano wa CCM nchini Zanzibar CCM gogo.

Mwili wa marehemu Salmin Awadhi ukipakiwa katika gari tayari kwa taratibu za mazishi, katika makaburi ya makunduchi Mkoa wa Kusini Unguja,  mwili wa marehemu unategemewa kuagwa kesho saa tano katika ukumbi wa baraza la wawakilishi Chukwani nchini Zanzibar na kusaliwa katika Masjid Muhammad kwa mchina na kuzikwa Kijiji kwao Makunduchi nchini Zanzibar.  

Naibu Katibu Mkuu wa CCM nchini Zanzibar Vuai Ali Vuai, akizungumza na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali waliofika nyumbani kwa marehemu mtaa wa mpendae kupata habari ya msiba huo. Naibu Katibu Mkuu wa CCM Vuai Ali amesema marehemu alifika Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui akiwa katika kazi zake na kuhudhuria Kikao kilichofanyika asubuhi ofisini hapo Vuai akiendelea kuzungumza na wandishi wa habari pamoja na muandishi wetu wa Free Zanzibar People From Mkoloni Mweusi Tanganyika Vuai Alisema marehemu ametoka chumba cha mkutano na kwenda kwenye Afisi yake ya Mnadhimu wa CCM Baraza la Wawakilishi, ndipo matatizo yalipojitokeza na kusema anasikia vibaya na kukimbizwa hospitali ya Rufaa ya Mnazi mmoja kwa matibabu , kufika huko hali ilibandilika na kufariki dunia. Marehemu ameacha pigo kwa Chama na wananchi wa jimbo lake Alisema Vuai.

Mwakilishi wa Jimbo la Kikwajuni Mhe Mahmoud Mussa , akiwa katika eneo la msiba akizungumza na ndugu na jamaa wa marehemu katika kupanga taratibu za Mazishi na mambo mengine muhimu. 
Habari iliotufikia muda huu Mnadhimu wa CCM Baraza la Wawakilishi nchini Zanzibar na Mwakilishi wa Jimbo la Magomeni nchini Zanzibar Salmin Awadh, Salmin amefariki dunia hafla baada ya kuanguka akiwa katika kazi za Chama Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui nchini Zanzibar.

MWAKILISHI wa Magomeni nchini Zanzibar, Salmin Awadhi Salmin (CCM), amefariki dunia ghafla baada ya kuanguka katika kikao cha Chama Cha Mapinduzi (CCM), kilichokuwa kinafanyika katika ofisi kuu ya chama hicho, Kisiwandui mjini Magharib nchini Zanzibar.
Taarifa hiyo ilianza kuenea mjini saa 6 mchana, na hata kuzua maswali kutoka kwa wananchi kuhusu utata wa kifo chake.
Salmin mwenye umri wa miaka (57) ambaye pia alikuwa ni mnadhimu wa wawakilishi wa CCM na mjumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho (CC), alikuwa mmoja wa wawakilishi wanaopingaa vikali mfumo wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK) kwa kutaka wananchi atii waulizwe kama bado wanahitaji muundo huo wa Serikali ya (SUK) nchini Zanzibar.
Akizungumza na Mwandishi wetu Free Zanzibar People From Mkoloni Mweusi Tanganyika kuhusu kifo cha mwakilishi huyo, Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vua Ali Vuai, alisema kabla ya kufikwa na mauti, alianguka ghafla wakati akitoka katika kikao hicho cha kawaida.
Alisema baada ya kuanguka viongozi na wanachama walimnyanyua na kumkimbiza Hospitali ya Mnazi Mmoja kwa ajili ya matibabu.
“Baada ya Salmin kuanguka, baadhi ya viongozi na wafanyakazi kwa haraka walimbeba na kumpeleka katika Hospitali ya Mnazi Mmoja kwa ajili ya matibabu na baada ya kufikishwa alipelekwa katika chumba cha wagonjwa mahututi (ICU), ambako baada ya muda mfupi madaktari walithibitisha kuwa amefariki dunia kwa maradhi ya shinikizo la damu.
“CCM imepokea kwa mshtuko mkubwa kifo cha kiongozi wetu ambaye alikuwa ni kiongozi na mtendaji wa kuigwa ndani na nje ya chama chetu, ila kazi ya Mungu haina makosa, jambo la kusikitisha amefariki akiwa katika utendaji wa kazi za chama hapa ofisi kuu Kisiwandui,” alisema Vuai.
Naibu Katibu Mkuu huyo wa CCM alisema kwa sasa taratibu za mazishi zinaandaliwa na Serikali kwa kushirikiana na chama nyumbani kwake Mpendae na anatarajiwa kuzikwa leo kijijini kwao Makunduchi Mkoa wa Kusini saa 7 mchana.
Kwa upande wake, Katibu wa Baraza la Wawakilishi (BLW), Yahya Khamis Hamad, alisema baraza hilo limeondokewa na kiongozi mahiri ambaye muda wote alikuwa na kazi ya kuimarisha umoja kwa Wazanzibari.(kweli.............????)
Salmin Awadh Salmin pia amewahi kushika wadhifa mbalimbali ndani ya CCM ikiwamo ujumbe wa NEC, Kamati Kuu na Mnadhimu wa Wawakilishi wa Kambi ya CCM ndani ya Baraza la Wawakilishi.
Machi 2, mwaka jana wakati wa mkutano wa Bunge Maalumu la Katiba mjini Dodoma Giningi, Salmin aliwaongoza wawakilishi wa CCM kupinga hatua ya Spika wa Baraza la Wawakilishi, Pandu Ameir Kificho, kuwasilisha maoni kwa iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba ya kutaka Serikali tatu na kuyaita ni maoni ya baraza hilo.
Katika mkutano huo, Salmin alisema mapendekezo hayo ni kinyume na msimamo wa CCM na wao hawako tayari kuliona hilo huku akiahidi suala hilo kufikishwa katika vikao vya ngazi za juu.
Salmin alisema Spika Kificho hakuwashirikisha wenzake katika mapendekezo ya Serikali tatu aliyoyawasilisha kwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, wakisema Baraza la Wawakilishi, kama taasisi, halikutoa msimamo wa pamoja.
Mei 4, mwaka jana, Salmin alisema wawakilishi wa CCM wanajiandaa kuwasilisha hoja binafsi kwenye Baraza la Wawakilishi ili kuwapa nafasi wananchi waulizwe iwapo wanataka kuendelea na Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK), au laaaa.(daaah!!)
Kauli hiyo aliitoa wakati akihutubia mkutano wa hadhara wa chama hicho ulioongozwa na Katibu Mkuu wake, Abdulrahman Kinana kwenye viwanja vya Kibandamaiti, nchini Zanzibar.
Salmin alisema wajumbe hao wamefikia hatua hiyo kwa kuwa wanaona kwamba lengo na matumaini ya kuundwa SUK yamefutika na hayana dalili njema katika siku za usoni.
Alisema ni vyema wananchi wakaulizwa kama bado wana hamu na mfumo huo au ule wa zamani urejeshwe.(kwa nini hakusema wuulizwe kama Wanautaka Muungano au Hautaki Muungano...??)
Katika mkutano huo, alimwomba Rais wa Maskani ya Kisonge, Shein, kuunga mkono hoja hiyo itakapowasilishwa ili kutoa nafasi mpya ya kidemokrasia kwa wananchi wake kujua kama wanataka
mfumo wa sasa au wa zamani.

SHUGHULIKA SANA NA DUNIA WAKATI HAPA NI PAHALA PAA KUPITA TU NA KUTENGEZA AKHERA.

Innaa Lillaahi wainnaa ilayhi raajiu'uun

KILA MZANZIBARI ATAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

No comments:

Post a Comment