Sunday, February 1, 2015

MBUNGE ALLY KEISSY WA NCHI YA TANGANYIKA AWAPA KWELI WABUNGE KUWA UBUNGE UKISHA TU BASI WATAPANDA BAJAJI NA MABASI.


Nchini Tanganyika/Giningi Dodoma. Mbunge wa Nkasi Kaskazini, Ally Keissy (CCM) jana alisababisha tena vicheko bungeni wakati anasema kweli ila wabunge wanachukulia kuwa ni vichekesho wakati aliposema kuwa wabunge wanaomba viwanja vya ndege vijengwe katika maeneo wanayotoka yani mikoa yao wanayotoka, wanafanya hivyo kujifurahisha kwa kuwa baada ya ubunge hawatakuwa na uwezo wa kupanda ndege badala yake watapanda mabasi na bajaji. Akizungumza wakati wa kuchangia hoja ya Kamati ya Miundombinu jana, Keissy, ambaye amekuwa akitumia mifano inayokera kwa wabunge wasaka tonge matumbo makubwa wasio shiba na kufurahisha kwa wabunge wanaotaka kweli maendeleo kwa rai wa nchi ya Tanganyika, alisema wananchi wanataka kusikia habari za barabara na reli kwa kuwa ndiyo usafiri wanaoutegemea.
“Nani anapanda ndege...?? Mh Ally Keissy alihoji Ni baadhi ya wabunge ndiyo wanapanda ndege hapa, baada ya ubunge hata fedha ya kupanda ndege hawatakuwa nayo. Reli ndiyo kitu muhimu na barabara. Kila mtu anaomba kiwanja cha ndege kwenye mkoa wake kujifurahisha, baada ya ubunge anapanda mabasi na bajaji. Lazima muwafikirie wananchi kwanza,” alisema Keissy. Hata hivyo, kauli hiyo ilipingwaa na Spika Anne Makinda aliyemtaka Keissy kuendelea kuomba fedha kwa ajili ya ujenzi wa barabara na kuwaacha wanaotaka ndege waendelee kufanya hivyo inaonyesha kuwa Spika Anne Makinda yeye ni moja katika hao wanaomba viwanja vya ndege vijingwe kwenye mikoa yao wakati mpaka leo hii wananchi hawana hata maji ya kunywa safi wala umeme wao ndio kwanza wanafikiria kujengewa viwanja vya ndege CCM Oyeeee.
Akizungumzia hali ya ubovu wa barabara jimboni kwake, Keissy alisema wiki iliyopita alitembea kilomita 35 kwa miguu wakati akifanya ziara kwa wananchi wake kutokana na ukosefu wa barabara. “Nimetembea kwa mguu na mtu anayepinga hapa, ushahidi ninao… Nimetoka Chongo mpaka Kolongwe kwa mguu kupitia Isaba kupitia Kazobu kupitia Bumanda… Hawana barabara. Nchi ina miaka 55 ya uhuru lakini wananchi hawana barabara,” alisema.Mbunge huyo alisema kwa mara ya kwanza alimuunga mkono mbunge wa Kasulu Mjini (NCCR-Mageuzi), Moses Machali aliyelieleza Bunge kuwa Serikali katika baadhi ya sehemu nchini inabandua lami na kuweka nyingine wakati wapo wananchi ambao hawajawahi kuliona hata gari.
Alitoa mfano Barabara ya Sumbawanga kwenda Mpanda ambayo alisema ilianza kujengwa miaka mitano iliyopita, lakini bado haijakamilika, makandarasi wameamua kuanza kuuza kokoto kwa sababu hawajalipwa fedha wanazodai. Pia, mbunge, alizua kioja tena wakati akizungumzia hali mbaya ya usafiri Ziwa Tanganyika, akisema inawezekana Serikali haitoi fedha za kutosha kwa kuwa ziwa hilo bado linatumia jina la Tanganyika na siyo Tanzania ambalo baadhi ya viongozi wanapenda kulisikia.“Kinawauma sana kusikia bado kuna Ziwa Tanganyika katika nchi hii. Nipo hapa kwenye Bunge wiki moja boti mbili zimezama, hakuna mzigo uliookolewa na baadhi ya watu wamefariki kwa sababu hakuna miundombinu. Liemba (MV) imebaki Liemba,” alisema.

KILA MZANZIBARI ATAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

No comments:

Post a Comment