Monday, February 16, 2015

RAISI WA NCHI YA ZANZIBAR MAALIM SEIF SHARRIF HAMAD AMEWASILI NCHINI SALAMA SALMANI AKITOKEA NCHINI QATAR ALIKOKUWA ZIARANI.

 
RAISI WA NCHI YA ZANZIBAR AKIWASILI NYUMBANI NCHINI ZANZIBAR BAADA YA KUMALIZA ZIARA YAKE HUKO NCHINI QATAR AKIVIKWA SHADA LA MAUWA KUKARIBISHWA NYUMBANI NA MABINTI WA KIZANZIBARI.

RAISI WA NCHI YA ZANZIBAR AKISALIMIANA NA BADHI YA VIONGOZI NA DUNGU NA JAMAA BAADA YA KUWASILI NYUMBANI NCHINI ZANZIBAR AKITOKEA ZIARANI NCHINI QATAR.

RAISI AKIENDELEA NA MAPOKEZI MAZURI BAADA YA KUWASILI NYUMBANI NCHINI ZANZIBAR.

RAISI WA NCHI YA ZANZIBAR MAALIM SEIF SHARRIF HAMAD AKIZUNGUMZA NA WANDISHI WA HABARI BAADA YA KUWASILI NYUMBANI NCHINI ZANZIBAR.

Rais wa Nchi ya Zanzibar, Maalim Seif Sharrif Hamad amewasili nchini Zanzibar salama usalimini na amepata nafasi ya kuzungumza na Waandishi wa habari.
Amesema alipokutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi ya Qatar Waziri huyo alimwambia Raisi wa Nchi ya Zanzibar Maalim Seif Sharrif Hamad waziwazi kwamba wananchi au Rai wa kawaida wa Qatar hawaijui (Tanganyika-Tanzania) lakini wengi wanaijua nchi ya Zanzibar kutokana na mahusiano ya kihistoria yaliyopo baina ya nchi mbili hizi.
Maeneo waliyokubaliana kushirikiana ni pamoja na:
1. Qatar kuangalia uwezekano wa kuijengea Zanzibar Environment Resource Centre ili kukabiliana na athari za mazingira.
2. Qatar kuisaidia Zanzibar kuanzisha mfumo wake wa kuzalisha umeme wake wenyewe.
3. Qatar kuisaidia Zanzibar katika mradi wa kumaliza tatizo la maji khasa Mkoa wa Mjini Magharibi.
4. Qatar kuipatia lami Zanzibar kiasi cha tani 10,000 kwa ajili ya matengenezo ya barabara.
5. Qatar kuangalia jinsi ya kuwekeza katika uendelezaji wa Uwanja wa Ndege Pemba ili uweze kutoa huduma za kimataifa.
6. Qatar kuangalia namna ya kuwekeza Zanzibar katika Ujenzi wa Bandari maalum ya kushughulikia utoaji wa huduma kwa sekta ya mafuta na gesi asilia.
7. Qatar kusaidia Zanzibar katika kuendeleza Karume Institute of Science and Technology na Kengeja Technical Secondary School kuwa za kisasa.
8. Qatar kuona uwezekano wa kusaidia madrasa za Zanzibar kwa kuziimarisha na kuzipatia vifaa.
9. Qatar kuwapatia ajira vijana wa Zanzibar lakini kwanza kwa kuanzisha vituo hapa hapa Zanzibar vya kuwapa mafunzo ya aina za kazi wanazoweza kuifanyia Qatar.
10. Qatar Investment Authority na Qatar Development Fund kuleta ujumbe Zanzibar kuona maeneo wanayoweza kuwekeza na kufanya kazi kwa pamoja na Zanzibar.
Amesema kinachofuata sasa ni ufuatiliaji na kuchukua hatua madhubuti kuyafanikisha haya.

KILA MZANZIBARI ATAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

No comments:

Post a Comment