Sunday, March 29, 2015

VIDEO-GARI LA MAJANJAWIDI LAVAMIA MSAFARA WA WANANCHI CUF NA KUSABABISHA MAJERUHI

Miongoni mwa majeruhi wa mkasa wa kushambuliwa na ‘watu wasiojuilikana’ wakati wakirudi mkutano wa CUF Makunduchi tarehe 29 Machi 2015.

MUNGU ALIUMBA DUNIA NA NCHI YA ZANZIBAR TANGU NA TANGU


Jioni ya tarehe 29 Machi 2015, msafara wa wafuasi wa Chama cha Wananchi (CUF) waliokuwa wakitoka Makunduchi, kusini Unguja, kuelekea Mjini Magharibi, ulishambuliwa njiani na ‘watu wasiojulikana.’ Hilo neno ‘watu wasiojuilikana’ tuliwache hivyo hivyo kwenye alama za mashaka, maana ni mtazamo wangu kwamba ni kinyume chake, yaani ni ‘watu wanaojuilikana’ na wale wanaopaswa na wenye wajibu wa ‘kujuwa’ mambo kama haya.
Kwa mujibu wa mmoja wa watu waliokuwamo kwenye msafara huo “gari ya ‘majanjawidi’ ikiwa katika mwendo wa kasi iliupita msafara wao na kisha kuwarushia watu waliokuwemo katika gari hiyo visu na nondo.”
Tunajaribu kufuatili kwa kina habari ili tuzidi kujuwa kunani....?

KILA MZANZIBARI ATAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO

No comments:

Post a Comment