Sunday, March 15, 2015

HAJI OMAR KHEIR NA FITNA ZAKE ZA MWISHO MWISHO


Haji Omar Kheir Kulia 

Kwa mujibu wa taarifa ya habari kutoka kituo cha ZBC leo nikuwa kulikuwa na mkutano wa CUF uliopangwa kufanyika huko kisiwa cha Tumbatu. Taarifa zinasema mkutano huo umekataliwa na Polisi kwa sababu wao wenyewe wanazozijuwa wamekata kuzitaja. Kubwa lililotokea nikuwa atii matawi mawili ya CCM ya Chama Cha Mkoloni Mweusi Tanganyika yamechomwa moto mkesha wa kuamkia leo. Ikinasibishwa na kufutwa kwa mkutano wenyewe wa CUF uliopangwa kufanyika huko katika kisiwa cha Tumbatu.
Ila Wazanzibari wote wanajuwa kuwa Hizi ni njama na Mipango ya Haji OMar Kheir ambaye kwa muda mrefu sasa anajifanya yeye kuwa atii amekuwa stadi, mbunifu, na msimamiaji wa mipango ya kikhalifu na mbinu chafu na maovu kuwafanyia wananchi wa Zanzibar na haswa jimbo lake la Tumbatu, Wazanzibar na wananchi wengine. Ikumbukwe hivi karibuni kuna clip iliyomuhusisha huyu na njama za kuivuruga nchi kwa kuwakamata vijana wa Kizanzibar na kuwafanya kama vile Masheikh walivyofanyiwa kule nchini Tanganyika.
Fitna nyengine ni ile ya kutayarisha database ya vikosi na kuanza kuwafuatilia wale wote wasiounga mkono mipangop yao ya kinyama ya kuwatesa watu kwa kuwa hawataki tena kuwa katika CCM Chama Cha Mkoloni Mweusi Tanganyika. Huyu bwana sasa hivi ni wa kupigwa X dhidi ya fitna zake hizi ambazo kila leo amekuwa engineer kwanza na mchimba fitna mkubwa. Huyu Haji Omar Kheir ni nani....? ni mtu gani.....? je ilimu yake ni ipi....? ni mjinga asiye juwa nini maana ya cheo au uwongozi, ni mtu ambaye darasani siku zote nafasi yake ilikuwa anashika mkia,tiro,wamwisho, fani yake ilikuwa gwaride la paunia miaka ile iliyo pita, na nyimbo za miaka ile za ” mtoto wa nyoka kamata chinja.” Haji Omar Kheir hajawahi kuwa General Trader and Business man kama watu wanavyo sema au kifikiri.
Kwa sababu hata kama angeuzwa yeye na kila alichokuwa nacho kwa wakati huo hakuwa na uwezo hata waa kufungua biashara ya kuuza genge la nyanya kwa wakati huo. Alipofeli form 3 Tumbatu mwaka 1979, alichukua mkoba wake wa ukili akapanda kidau/ngalawa akawa anapapatua soko la samaki Msasani Dar nchini Tanganyika akachanganya na utapeli na kulangua kanga za Mombasa kutokea Kenya. Mambo yalivyomuendea vibaya Msasani, akapanda Ras Nungwi akawa anabangaiza na kutapeli katika kanda inayoanzia Miembeni mpaka Gulioni. Vugu vugu la siasa la vyama vingi lilipoanza miaka ya 1992, alivaa gwanda la kijani akawa mnazi wa maskani za CCM Chama Cha Mkoloni Mweusi Tanganyika, na akanywa maji ya kijani. Haji Omar Kheir kama ilivyo kwa wagombea wote wa kiti cha urais wa Zanzibar kwa kiti cha CCM tokea 1995, hajawahi kushinda kiti cha jimbo la Tumbatu kihalali.


KILA MZANZIBARI ATAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

No comments:

Post a Comment