Friday, March 13, 2015

MAASKOFU JUKWAA LA WAKIRISTO; KATAENI KATIBA MKIPIGA KURA NI YA HAPANA-KIFICHO,MWINYHAJI,MWANASHARI MKUU WA ZANZIBAR SIKILIZENI MANENO HAYA NYINYI MADALALI WAKUBWA

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT), Askofu Dk Alex Malasusa
 MWENYE KITI WA JUMUIYA YA KIKIRISTO NCHINI TANGANYIKA (CCT) ASKOFU DR ALEX MALASUSA

Nchini Tanganyika Dar es Salaam. Jukwaa la Wakristo nchini Tanganyika limewataka waumini wake kujiandikisha kwa wingi katika Daftari la Kudumu la Wapigakura, kuisoma Katiba Inayopendekezwa na kujitokeza kuikataa kwa kupiga kura ya “HAPANA”.
Taarifa iliyotolewa na Jukwaa hilo jana na kusainiwa na mwenyekiti wa Jumuiya ya Kikristo huko nchini Tanganyika (CCT), Askofu Dk Alex Malasusa, mwenyekiti wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki nchini Tanganyika (TEC), Askofu Tarcisius Ngalalekumtwa na mwenyekiti wa Kanisa la Pentekoste nchini Tanganyika (CPCT), Askofu Daniel Awet, imetaja sababu mbili za uamuzi wake kuwa ni muswada wa Mahakama ya Kadhi kukiuka misingi ya Taifa kuwa na Serikali isiyo na dini, na Kura ya Maoni kusababisha mgawanyiko.
“Hivyo basi, Jukwaa linawataka waumini wake wote wajitokeze kwa wingi kujiandikisha katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura, waisome Katiba Inayopendekezwa na kushiriki kikamilifu vipindi vya elimu juu ya Katiba Inayopendekezwa na kisha wajitokeze kwa wingi kupiga kura ya HAPANA kwa Katiba Inayopendekezwa kwa sababu zilizotajwa hapo juu,” linasema tamko hilo la kurasa nne.
Taarifa hiyo imekuja siku moja tu baada ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda MR Zanzibar si Nchi kutangaza kuwa muswada wa uanzishwaji wa Mahakama ya Kadhi uliokuwa umeondolewa kwenye mkutano uliopita wa Bunge kwa ajili ya mashauriano zaidi, utawasilishwa katika vikao vya chombo hicho vinavyoanza Jumanne ijayo baada ya kufikiwa kwa maridhiano baina ya viongozi mbalimbali wa dini.
Pia tamko hilo limekuja siku chache baada ya Rais wa nchi ya Tanganyika Jakaya Kikwete kuiagiza Hazina itoe fedha kwa Tume ya Uchaguzi (Nec) kwa kadri inavyohitaji ili kuiwezesha kukamilisha mchakato wa Kura ya Maoni.
Viongozi wa Jukwaa la Wakristo walikutana Machi 10, mwaka huu kujadili kwa kina kuhusu hali ya usalama wa nchi ilivyo sasa na mustakabali wake, Katiba inayopendekezwa na uanzishaji wa Mahakama ya Kadhi.
Taarifa hiyo ya maneno 712 inasema: “Katiba Inayopendekezwa imeleta mgawanyiko mkubwa katika Taifa kwani imepatikana kwa njia zisizo za kiadilifu na mchakato wake umeendeshwa kwa hila na ubabe.
“Pia haijajibu matakwa na malalamiko ya wananchi kwenye masuala mbalimbali kama muundo wa Serikali, miiko na maadili ya viongozi wa umma, haki za binadamu, madaraka ya rais na uwiano wa mihimili ya dola.
“Ikumbukwe Katiba Inayopendekezwa ilipitishwa kwenye Bunge Maalumu la Katiba kwa ahadi ya Serikali kuipa dini ya Kiislam Mahakama ya Kadhi. Inashangaza kuwa hata Serikali inatoa rushwa ili kufikia malengo yake. Kwa hali kama hii, Kanisa haliwezi kuunga mkono kupitishwa kwa Katiba Inayopendekezwa,” ilisema sehemu ya tamko hilo.
Kuhusu uanzishwaji wa Mahakama ya Kadhi, taarifa hiyo inasema, “Suala la uanzishwaji wa Mahakama hii nchini kama tulivyotoa maoni yetu kwa Kamati ya Bunge ya Katiba na Sheria (Januari 16, 2015); barua yetu kwa Waziri Mkuu na matamko mbalimbali yaliyokwisha kutolewa kuhusu jambo hili; Mahakama ya Kadhi inakiuka misingi ya Taifa hili kuwa na Serikali isiyokuwa na dini wala mfumo wa sheria unaobagua raia wake kwa misingi ya dini.”
KIFICHO,MWINYIHAJI,MWANASHARI MKUU NA MI CCM NJAA MULIO IWEKA KWENYE KICHWA MADALALI WAKUBWA ANGALIENI WATU WANAVYO TETEA HAKI ZAO SIO NYINYI MNAUZA NCHI KWA VISENTI MADALALI
KILA MZANZIBARI ATAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

No comments:

Post a Comment