Saturday, March 21, 2015

NCHINI ZANZIBAR KISIWANI PEMBA SHEHIA YA MAKANGALE WILAYA YA MICHEWENI MAGRET MARTIN ANAUZA POMBE ZOTE UNAZOZIJUWA WEWE NA MADAWA BILA YA LESENI KWA MIAKA SABA NA KUSABABISHA USUMBUFU MKUBWA KWA WAZALIWA WA MICHEWENI


ASKARI HAWACHUKUWI HATUWA YOYOTE MAANA NDIPO WANAPO PONA

WANANCHI wa shehia ya Makangale wilaya Micheweni Pemba, wamemlalamikia aliekuwa naibu sheha wa shehia hiyo Magret Martin, kutokana na kufungua baa lisilo na kibali, na kuuza ulevi kwa muda wa zaidi ya miaka saba sasa. Wamesema katika kipindi hicho chote, tayari wameshakwenda ngazi mbali mbali ikiwa ni pamoja na Jeshi la Polis, ofisi ya wilaya na bado mwananchi huyo anaendelea na biashara hiyo haramu. Wananchi hao walieleza kuwa, amekuwa akiuza vinjwaji mbali mbali vya ulevi ikiwa ni pamoja na konyagi, bia, viroba, gongo na hata madawa mengine ya kulevya. Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi kwa masharti ya kutotajwa majina yao, walisema wanapotoa taarifa kituo cha Polisi, hufanyiwa upekuzi na wanapokuta ulevia kama vile bia na konyagi huachiwa. Walieleza kuwa Polisi wanapofika huwaeleza wananchi kwamba ulevi uliomo ndani ya baa hilo, umeruhusiwa kisheria na wanachotafuta wao ni gongo, bangi na madawa mengine yaliokatazwa na serikali.
“Polisi hutueleza kuwa ndani ya baa la Magret hawakukuta unga, gongo wala bangi, bali ni bia na pombe nyengine zinazotengenezwa kiwandani’’,alidai mwananchi mmoja. Aidha walieleza kuwa, mwananchi huyo amekuwa akifikishwa kituo cha Polisi mara kwa mara, na huachiwa kwa madai hana kazi nyengine ya kufanya. Baadhi ya wazazi na walezi wa shehia hiyo, walisema kutokana na kuwepo kwa baa hiyo kwenye kijiji chao, baadhi ya vijana wao wameanza kutumia vinywaji vinavyolewesha. Mkuu wa Polisi Jamii Zanzibar, Hasina Ramadhan Tawfik, ambae hivi karibuni alikutana na viongozi mbali mbali wa wilaya ya Micheweni na shehia, na alitoa agizo kufanywa kwa doria mara kwa mara eneo hilo. Alisema endapo agizo lake litafanyiwa kazi anaamini mwananchi huyo aliefungua baa ambalo lisilo na kibali, atakosa wateja na anaweza kusimamisha biashara hiyo. “Mimi nilivyozungumza na watendaji inaonekena mwananchi huyo hana hata kibali cha kufanya biashara hiyo, sasa lazima taratibu zitumike kumuondoa na moja ni doria ya mara kwa mara”, alisema. Hata hivyo alisema sio sahihi hata kidogo, kama kweli Polisi wa kituo cha Konde wanafanya upekuzi na wanapokuta bia na konyagi kuziwacha, kwani baa hiyo haipo kisheria.
Sheha wa shehia hiyo Mohamed Juma Ali, alisema kutokana na mmiliki wa baa hilo kuendelea na usugu wake wa kutoacha kazi hiyo alilazimika kumtoa kwenye wajumbe wa kamati yake. “Ni kweli Magret alikuwa mjumbe wangu, lakini kutokana na kadhia yake ya kuuza ulevi, niliamua kumtoa na sasa juhudi za kuondoa baa hilo zinaendelea taraibu’’,alifafanua Akizungumza kwa njia ya simu mmiliki wa baa hilo Mgret Martin alisema kuwa yeye awali alikuwa akinunua viwanywaji hivyo ni kuwauzia wenye hoteli kwa njia ya jumla. “Ni kweli nauza konyagi na viroba na sina kibali, lakini mimi huwataka watu wanunue tu na kwenda kunywa sehemu nyengine, na wala siuzi gongo na bangi kama wanavyodai wengine’’,alisema. Hata hivyo alisema ameshangaikia sana kwenye mamlaka husika ili apatiwe kibali, lakini ameshindwa na hana budi kuachiwa kuuza ulevi huo kwa vile ni kazi anayojipatia kipato. Katika hatua nyengine amekana kwamba wapo wanawake wanaojiuza kwenye baa hilo, na kusema kuwa wapo wengine wanaofanya biashara kama vile maandazi na supu.
“Watu wanacho fuata hapa sio ulevi wala ngono, watu wanapendezewa na supu ninayouza, sasa akionekana mtu ameingia hapa kwangu anaonekana amekuja kunywa ulevi’’,alilalamika. Miaka miliwili iliopita, baa sita zilizripotiwa kuchomwa moto kisiwa Unguja kutokana na sababu mbali mbali ikiwemo mengine kuendesha biashara pasi na kuwa na kibali.Zipo sheria hapa Zanzibar tokea enzi za ukoloni zikipinga kuanzishwa kwa baa pasi na mmiliki huyo kuwa na leseni inayotambulika

KILA MZANZIBARI ATAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

No comments:

Post a Comment