Sunday, March 1, 2015

SHAKA KIPOFU WA AKILI KUSAKA TONGE NA KUJIJENGEA MAJUMBA KWA MATUSI SIASA HIZI HAPA ZANZIBAR ZIMEKWISHA UMECHELEWA SHAKA KIPOFU WA AKILI.


SHAKA KIPOFU WA AKILI ULIANZA HAPA NA UMATI WA WATU KUKUSIKILIZA UNAVYO ROPOKWA.

SASA SHAKA KIPOFU WA AKILI  UPO HAPA KWENYE BANDA LA KARAFU WEWE UNAITA OFISI YAKO NA WANDISHI WA HABARI WAWILI MPAKA SABA WAKIKURIKODI NA KUKUANDIKA KATIKA HABARI HAUJAJUWA TU KUWA UMEISHIWA...?? KUTOKA KWENYE UMMA WA WATU KUKUSIKILIZA NA SASA WAJIFUNGIA NA WANDISHI BADO KIJANA WEWE BADILIKA HUJA CHELEWA BADO NCHI YA ZANZIBAR INAHITAJI VIJANA KAMA WEWE NGUVU KAZI ILA SIO MDOMO MCHAFU BALI AKILI TIMAMU NA MANENO YA MAANA YA KUITETEA NCHI YA ZANZIBAR BADILIKA KABLA WAKATI HAUJAKUBADILISHA.

•Asema ni ajabu kiongozi wa CUF kwenda kinyume na ahadi zake
Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana ya CCM (UVCCM), Shaka Hamdu Shaka amesema uchumi wa Zanzibar ungekuwa mbovu, Serikali isingeweza kumlipia Sh80 milioni kila safari moja, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad kwenda kutibiwa India.(( kama maalim kwenda akitibiwa India umeliona kubwa mbona SHEIN,MKEWE NA WATOTO WAKE wanakwenda uengereza na operation zinafanyika kwani hatuyajui...?? unajua ni kiasi gani matibabu uengereza...?? gharama zake waweza kutibiwa watu 5 INDIA kwa matatizo hayo hayo.))
Shaka alitoa tamko hilo jana katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika kwenye Ofisi Kuu ya UVCCM Zanzibar, na alitumia muda mwingi kujibu hotuba ya Maalim Seif na viongozi wengine wa CUF ya kwenye mkutano wa hadhara wa uzinduzi wa Kamati za Ushindi kueleka Uchaguzi Mkuu mwaka huu.
Shaka alisema UVCCM imesikitishwa na kauli ya Maalim Seif akibeza kuwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) ni ya kidhalimu na haijajenga uchumi imara.(( wewe Shaka kipofu wa akili habu jiulize kama nchi hii imejengwa kiuchumi mbona mpaka leo 50 na ushaiya nchi imeka kama pori au kichaka kilicho sahauliwa kufeykwa....???
Alisema ni jambo la kushangaza kumuona kiongozi huyo wa CUF akienda kinyume na ahadi zake alizotoa kwa wananchi za kutibiwa nchini, lakini anaongoza kwa kusafiri nje ya nchi, kwa matibabu kuliko kiongozi mwingine, huku akitumia kiasi kikubwa cha fedha za umma.((Ni kweli maalim aliahidi kutibiwa hapo hapo lakini apatapo urais, maana angeibadilisha hospital na wataalamu wakutosha sio nyinyi CCM kazi mwaajiri vikosi tu mwisho hamuna pakuwapangia munawaeka Hospital kupoteza watu muda wakutizama wagonjwa, hata hamuoni CCM kuwa mumeishiwa hospital ndio pakuweka watu na virungu.....?? hamuna hata ubinaadamu hamujuwi kuwa mwenye kuuguliwa na yeye pia huuguwa....? vipi utampiga kirungu mgomjwa......? 
“Tumeshtushwa na matamshi ya Maalim Seif akibeza kuwa uchumi wa Zanzibar umezorota, takwimu zinaonyesha uchumi umekuwa kwa asilimia 7.4 mwaka 2013/14, hakuna mtoto anayetembea zaidi ya kilomita tano kufuata skuli au kukosekana kituo cha afya.”((SHAKA KIPOFU WA AKILI TUNAKULIZA HIVI....Pia humalizi hata kilomita 6 kuna mahakama na wanasheria.. Mbona mumewapeleka masheikh wetu kwa Mkoloni Mweusi Tanganyika...?? Mbona husemi ilo..si moja kati ya udhalim huo SHAKA KIPOFU WA AKILI....??))
Aliongeza: “Kuna barabara za lami, vifo vya mama wajawazito na watoto vimepungua na malaria imebaki historia,” alisema Shaka. Pia, aliponda uzinduzi wa kampeni za CUF na kusema ni mbwembwe na mikogo ambayo haiwezi kukisaidia chama hicho kushinda katika Uchaguzi Mkuu na kuingia Ikulu.
Shaka alisema kwa sababu kina mgombea mmoja wa kudumu, kina viongozi wenye tuhuma za ufisadi na ubadhirifu, hakina uzalendo wala mipango ya kisera.(( Shaka na wenzako munatera, kila mukisikia Maalim ndie mgombea wa urais CUF. Kwa kweli munamuogopa sana Maalim Seif, nasi CUF na Wazanzibari kwa ujumla tunao taka mamlaka kamili tushajuwa kuwa munamuogopa ndio tunawafanyia shindi zaidi hatusimamishi mwengine mpaka mufe kwa chuki zenu na uhasidi wenu. Kumuimbia kote mulikokufanya hakujasaidia kitu, inshallah November 1, 2015 tunamuapisha Maalim kama Rais wa Znz huru, yenye mamlaka kamili.Kufeni kama hilo hamulitaki. Wenzenu waliokuwa hawalitaki hilo washaanza kutangulia, akina Salmin Awadh na Komba.))
“Sherehe na mbwembwe siyo vigezo vya kushinda uchaguzi, huwezi kuwa na chama cha siasa chenye mgombea mmoja wa kudumu…hiyo siyo demokrasia ya kweli na hakiwezi kukubalika kitaifa na kimataifa,” alisema Shaka. Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Umma CUF, Salum Bimani alisema madai ya Shaka hayana msingi wowote. Alisisitiza kuwa hali ya uchumi wa Zanzibar, chini ya uongozi wa sera za CCM, ni mbovu, huku akisema wananchi wanakabiliwa na maisha magumu.
Bimani alisema vijana hawana ajira, wamepoteza matumaini, wanashinda vijiweni, huku vigogo wa CCM wakila nchi na kufuja rasilimali…watoto wao wakisoma na kufanya kazi nje ya nchi, wakati viwanda vyote vimekufa na hawaonyeshi kuleta utatuzi. “Uchaguzi wa mwaka huu…CCM itafute mahali pa kutokea, tumewabana mbavu na wananchi hawawataki, hatutakubali kuibiwa kura zetu, ila tukishindwa kihalali tutakubali, lakini kwa kura moja mtu mmoja,” alisema Bimani.
KILA MZANZIBARI ATAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

No comments:

Post a Comment