Friday, March 20, 2015

SHEIN UNAMUOGOPA BORAFYA AU UNAONA RAHA ANAVYO TUKANA MCHANA KWEUPE MLEVI HUYU


BORAFYA NA MATUSI SHEIN UPO AU NDIO DEMOKRASI
DEMOKRASI YA CCM HIYO INALETA MAENDELEO 
SI HABA MIAKA 50 NA USHAIYA SASA
BORAFYA NA MATUSI SHEIN UPO AU NDIO DEMOKRASI
DEMOKRASI YA CCM HIYO INALETA MAENDELEO 
SI HABA MIAKA 50 NA USHAIYA SASA
SIKILIZA VIDEO HII CCM INAVYO ELEZA TATIZO LA UMEME LETAONDOLEWA VIPI NA SEREKALI PAMOJA NA TATIZO LA MAJI NA VIPI NCHI INASAFISHWA NA KUWA NA MAZINGIRA MAZURI
SIKILIZA VIDEO HII CCM INAVYO ELEZA VIPI ITAWEZA KUONGEZA ELIMU KUWA NZURI NA YA JUU KULIKO YA NCH YA UENGEREZA PIA CCM INAELEZA VIPI ITAWASAIDIA VIJANA AMBAO HAWAKUBAHATIKA KUFAULU ELIMU YA JUU NA PIA INAELEZA VIPI ITAOGEZA AJIRA ILI VIJANA WASIKAE MABARAZANI NA KUVUTA MAUNGA NA MABANGI CCM INAENDELEA KUWAELEZA VIJANA VIPI ITAPUNGUZA BEI ZA VYA KULA ILI KILA MZANZIBARI AWEZE KUPATA MILO YAKE MITATU KILA SIKU BILA YA SHIDA CCM KTK VIDEO INAENDELEA KUSAMA ITAJENGA HOSPITALI MPYA ZA KISASA KATIKA KILA MKOA KUTAKUWA NA HOSPITALI YAKE YANYA KUWEZA KUFANYA KILA KITU PAMOJA NA UPASUWAJI NA UPERESHINI ZA MACHO NA KUWEZA KUSAIDI NCHI NYENGINE ZOTE ZA AFRIKA MASHARIKI ILI WASENDE TENA INDIA NA ULAYA KUTAFUTA MATIBABU.

Nikushukuru ndugu mtoa mada kwa kuligusia hili la ndugu borafya pamoja na lile bango jeusi la maskani ya kisonge ki kawaida lugha zinazo tumiwa na vifaa hivi viwili kuhusiana na wapinzani iwe viongozi wao au chama chenyewe na wafuasi wake wote kwa ujumla ni vya kutia aibu sana kwenye nchi inayo jisibu kuwa iliwahi kuwa ya wastaarabu,la kusikitisha zaidi ni hili la kutukana wazi wazi mchana kweupe sikusema hivi kwa kuwa ukitukana giza giza usiku inakubalika bali ninacho gusia hapa ni ukosefu wa mboni za uso zenye uhusiano na kuona haya huwa hazina hata pazia la kuusitiri uso wakati wakiandika au kuporomosha matusi huku jua likirindima.
Niliwahi kulizungumzia hili hapa kuwa mimi binafsi namjua tu borafya lakini simfahamu kwa kuwa hatuna usuhuba wala simjui ni mtu wa aina gani kama ninavyo wajua wale ambao huwaita wenzangu lakini pia naelewa kwa kumuona akijihusisha na kupika pombe za kienyeji pamoja na kupiga ngoma ya bomu hapo nyuma hayo sio mageni kwa wazanzibari karibu sisi wengi hapa mjini tunajua wasifu wake huo pia alikuwa balozi wa nyumba kumi kumi katika mtaa wake pale raha leo kitu ambacho kilimfanya aweze kuuza pombe hiyo kirahisi bila buguza ya polisi kumkamata kwa kuwa walikuwa wakijua yeye ni balozi msijiulize niliyajuaje haya kama na mimi sio mteja wake la hasha mimi siku wahi kunywa chochote cha kienyeji zaidi ya maji ya bomba na togwa na hilo hakuwa akiuza.
Sasa onyo langu kwa viongozi wetu hasa rais Sheni wa sasa kuwa na yeye awe tayari kutukanwa na bwana huyu.kwani katika watu ambao ana hakikisha mkutano wake haumaliziki bila kuwatukana wa kwanza ni mstaafu rais karume,wa pili ni shemeji yake mheshimiwa bwana Mansour himid na watatu wa kufungia dimba si mwingine bali yule yule adui wetu wa asili na asili anaelindwa na mola wake Maalim seif shariff hamad sasa la kushangaza kwa nini bwana boraafya sijapata kumsikia akimtukana rais karume wakati akiwa bado madarakani au hata bwana Mansour wakati akiwa waziri hakuwahi kumtukana matusi ya nguoni pamoja na kumtukana mama yake mzazi hadharani ambae mimi pia ni mama yangu kwa udugu na heshima za familia zetu na hivi sasa ana mitihani ya mola kwa kuwa ana ugua lakini hilo halijamnyima borafaya kibali cha kumdhalilisha mzee wetu huyu kila apatapo fursa kwenye jukwaa la ccm.
Anacho subiri borafaya kwako umalize muda wako wa urais hapo ulipo hata ukiwa makamo wa pili au wa kwanza basi hatokusubiri ustaafu atakusakama na wewe kwa matusi kwani makamo wa kwanza bwana seif sharrif yana mkuta siku zote cheo hicho hakimzuwii mdomo borafya wala kisonge kufanya kazi zao wala usifarijike kwa kuwa yeye mpinzani kwetu ruksa kuwanyanyasa kwa matusi ya kila aina viumbe wa aina hiyo.
Jee hiyo ndio siasa ya Kiswahili au ya kiarabu kwani hili neno nasikia muandishi anatuambia linatonaka na neno la kiarabu”siyasa” kitu ambacho najua na linahusiana na kuchunga farasi ndio asili yake sasa pengine ndugu borafya na kisonge wao wanalitumia kiarabu kwa kuwa waliokuwa hawako ccm lazima watakuwa farasi watupu,sio binaadamu swali langu au onyo kwa rais sheni lina baki pale pale subiri zamu yako ikiwa unaona haya wanayo fanyiwa rais Amani karume.Mansour na Maalim Seif Shariff matamu nahofia matusi yatakayo kukuta wewe yatakuwa makubwa zaidi kwa sababu huyu mheshimiwa hunihtaji mimi kukujulisha kuwa hana adabu umemsikia kwa masikio na macho yako alivyokuwa akihubiri upemba na uunguja kwenye vikao vyenu na wewe ukiwa mwenyekiti mbona hukutishia kumuweka ndani kama ulivyomfanyia shaka au kwa kuwa shaka alikutaja kwa jina?na kama kuna anae mtukana mpemba wewe basi humo tena kwa kuwa umo chama chetu?
Haya sio mambo ya kuachiwa kwa kutumia visingizio vya kuwa hao ni wana maskani tu na hivyo sio vikao halisi vya chama ni mawazo yao tu, kuna kikao gani muhimu zaidi ya unachokalia na kukiongoza wewe kama mwenyekiti na rais wa nchi ikiwa mtapenda kuiita hii nchi na bado wapemba hatusalimiki? au kuna mkutano gani muhimu unao hutubiwa na mkuu wa mkoa au wilaya wa chama chetu ccm na viongozi wote wa juu bado jukwaa hilo hilo likatumiwa siku hiyo hiyo kuwatukana wazee wetu wasio na hatia na hawaja wakosea kitu? imehusu nini kutaja mahari ya uwongo aliyotoa marehemu brigedia yussuf himid kumuolea mzee wetu kwenye majukwaa ya siasa tunapotakiwa kutangaza sera za maendeleoya nchi hii badala yake tumeyageuza majukwaa ya kusasamburia begi la bi harusi,kama huku sio kufilisika kisiasa katika jamii sijui nitafute jina gani huu ni uhuni ulio barikiwa na baraza la mapinduzi na serekali yako rais Ali Mohamed sheni.
Tafadhali uhuni huu ukome mara moja kwa sababu leo tume amua kusema kwa amani lakini haina maana ikiwa serakali yetu inalifurahia jambo hili tutaendelea kutoa ahadi ya kuwa watiifu hakuna anae kubali kudhalilishiwa mzee wake akakaa kimya hilo mlijue na yatakayo kukuteni msije mkasema mmeonewa au hamkuwa na taarifa..
Tafadhalini kama hakuna la kuwaambia wananchi basi mnaweza kuwasalimia tu na kushuka kwenye majukwaa lakini tabia ya kutukana watu na wazee wao kwa kisingizio cha upinzani hakitoweza kuvumilika siku zote na huo sio utu,ustaarabu wala katika dini hatufundishiwi hayo kiasi ya tukute haya kwa sababu huwezi kumgeuza mpiga bomu na mpika na muuza gongo kuwa mshauri wa rais au msaidizi wake ndio maana hata madaktari humshauri mama mja mzito asivute sigara wala asilewe ili kumnusuru mtoto sasa utaipika, utainywa na kuiuza vipi gongo miaka yote halafu isikudhuru.
naomba tahfif kwenye lugha sikuwa mvumilivu kama desturi kwa sababu matusi yanayoletwa hivi sasa na mheshimiwa borafya kwenye ngumi huitwa “below the belt” yaani huko chini ya ukanda usifike, sina budi kutoa ilani kwa waliojificha mvua ya masika chini ya mpapai wakitegea wao haito wanyeshea.
asanteni.
KILA MZANZIBARI ATAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

No comments:

Post a Comment