Sunday, March 15, 2015

UJUMBE WA BANGO ULIO MPOKEA ZITTO KABWE KIGOMA UNASEAMA CHAMA SIYO BORA, UBORA NI UTENDAJI KAZI.


Nchini Tanganyika Kigoma. Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe amesema kutimuliwa uanachama na Chadema ni dhoruba inayomkumba mwanasiasa yeyote anayefanikiwa na kwamba iko siku atashika “nafasi kubwa ya uongozi ya kuwatumikia Watanganyika”. Zitto aliwasili mjini hapa juzi, ikiwa ni siku chache baada ya Chadema kutangaza kumfukuza uanachama kwa kosa la kupeleka mgogoro wa ndani ya chama kwenye mahakama.
Alifungua kesi Mahakama Kuu akitaka imuamuru katibu mkuu wa Chadema kumpa nyaraka za mwenendo wa vikao vya Kamati Kuu vilivyomvua madaraka yote na baadaye kukizuia chama hicho kumjadili. Hata hivyo mahakama ilitupilia mbali shauri lake na Chadema ikatangaza mara moja kumtimua. Akihutubia mamia ya watu kwenye Kijiji cha Nyarubanda ambako alikabidhi gari la wagonjwa, Zitto aliwatoa hofu wananchi hao walioonyesha shauku ya kujua hatma yake na kuwaeleza kuwa hajawatupa, ataendelea kuwahudumia.
“Hakuna kiongozi aliyefanikiwa kisiasa bila kupitia misukosuko ya kupingwa,” alisema Zitto ambaye anamalizia kipindi cha pili cha ubunge wake kwenye jimbo hilo. “Waziri Mkuu wa zamani wa nchi ya India, Indira Gandhi alifukuzwa na chama chake na aliamua kuunda chama kipya na baadaye kuwashinda waliomfukuza katika uchaguzi. Kwa hiyo nawatoa hofu kwa maana ninajengwa zaidi kisiasa.
“Nipo kwenye dhoruba ambayo inanijenga kisiasa na ipo siku nitawatumikia Watanganyika katika nyadhifa kubwa za uongozi.” Katika mkutano huo ambao wananchi walimpokea wakiwa na mabango yenye ujumbe mbalimbali kama “Mheshimiwa Zitto tulikuchagua wewe na siyo chama,” huku mengine yakiandikwa “chama siyo bora, ubora ni utendaji kazi”. Viongozi mbalimbali wa CCM na vyama vingine vya siasa walijumuika kwenye uwanja huo kumpokea Zitto na kushiriki naye kucheza ngoma za asili.

KILA MZANZIBARI ATAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

No comments:

Post a Comment