Monday, March 30, 2015

VIDEO-ATI WANATAKA KUSHINDANA NA KOMPYUTA NA TEKENOLIGIA AMAA KWELI MUMEISHIWA

HILI NDIO JIBU LA HAO WANAOTAKA KUZIBA MIDOMO BLOG NA WANDISHI WA HABARI TUNAWAJUWA NYOTE WEZI WAKUBWA

WAHALIFU wa mtandao pamoja na wasambazaji wa picha za utupu na ngono, wasambazaji wa taarifa za uwongo, za kibaguzi na matusi na watu wengine ambao wanafanya udanganyifu unaohusiana na kompyuta wametungiwa sheria kali ambayo itawafanya kwenda jela hadi miaka 10 au kulipa faini isiyopungua Sh milioni 50.
Miongoni mwa miswada ya sheria utakaowasilishwa bungeni na Serikali wiki hii mjini Dodoma, ni Sheria ya makosa ya mtandao ya mwaka 2015 ambayo imeainisha makosa mbalimbali yanayofanywa na wananchi katika kipindi hiki ambacho matumizi ya mtandao wa kompyuta yameongezeka.
Baadhi ya makosa yaliyoainishwa kwenye sheria hiyo ni kughushi kunakohusiana na masuala ya kompyuta, udanganyifu unaohusiana na kompyuta, ponografia za watoto, picha za utupu, matusi na ngono, makosa yanayohusiana na utambuzi, uwongo, ubaguzi, matumizi ya kibaguzi, mauaji ya kimbari na unyanyasaji kupitia mtandao wa kompyuta.
Katika sheria hiyo, mtu atakayesambaza ponografia ya watoto kupitia mtandao wa kompyuta atawajibika kulipa faini isiyopungua Sh milioni 50 au mara tatu ya faida iliyopatikana kinyume cha sheria au kifungo kisichopungua miaka saba jela au vyote kwa pamoja.
Mkosaji pia ataamriwa kumlipa mwathirika fidia. Kwa upande wa kusambaza picha za ngono, matusi, uasherati atalipa faini isiyopungua Sh milioni 30 au kwenda jela miaka 10 au vyote.
Lakini mtu atakayesambaza picha za utupu atalipa faini isiyopungua Sh milioni 20 au kwenda jela miaka saba au kutumikia adhabu zote kwa pamoja.
Pia kweye muswada huo mtu ambaye atatoa taarifa, data au maelezo kwa njia ya picha, maandishi, alama au aina nyingine yoyote zikiwa ni za uongo akipatikana na hatia atalipa faini isiyopungua Sh milioni 3 au kutumikia kifungo jela kisichopungua miezi sita au vyote.
Kwa upande wa ubaguzi, sheria hiyo inakataza mtu kutumia mtandao wa kompyuta kutozalisha vitu vya kibaguzi kwa madhumuni ya kuvisambaza na iwapo atatiwa hatiani atalazimika kulipa faini ya Sh milioni tatu au kifungo cha mwaka mmoja jela.
Pia mtu akimdhihaki mtu mwingine kwa kupitia mfumo wa kompyuta kwa mwelekeo wa ubaguzi wa rangi, kabila, asili, utaifa au dini fulani akitiwa hatiani atatozwa na Mahakama faini ya Sh milioni tatu au kifungo cha mwaka mmoja jela au vyote kwa pamoja.
Pia sheria hiyo inakataza mtu kuchapisha au kusababisha kuchapishwa vitu vinavyochochea au kuhalalisha matendo yanayopelekea mauaji ya kimbari na makosa dhidi ya binadamu kwa kupitia mtandao wa kompyuta.
Mtu atakayefanya hivyo atakuwa ametenda kosa na akitiwa hatiani atawajibika kulipa faini isiyopungua Sh milioni 10 au kutumikia kifungo kisichopungua miaka mitatu au vyote kwa pamoja.
Pia muswada huo wa sheria unakataza mtu kutoanzisha usambazaji wa taarifa zinazotumwa bila ridhaa na ukitiwa hatiani utatozwa faini ya Sh milioni 3 au mara tatu ya faida iliyopatikana kinyume cha sheria au kutumikia kifungo kisichopungua mwaka mmoja au vyote kwa pamoja.

KILA MZANZIBARI ATAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO

No comments:

Post a Comment