Wednesday, April 8, 2015

HAKUNA KIONGOZI YOYOTE WA CCM CHAMA CHA MKOLONI MWEUSI TANGANYIKA HAPA NCHINI ZANZIBAR ALIYEFIKIA HATA ROBO ALICHOFANYA MZEE KARUME. LABDA MATUSI NA UBAGUZI


Nchini Zanzibar. Wakati Taifa likiadhimisha kumbukumbu ya miaka 43 ya kifo cha Rais wa Kwanza wa nchi ya Zanzibar, Sheikh Abeid Amani Karume, wananchi wa Zanzibar wamesema awamu saba za Maraisi na Viongozi waliomfuatia wameshindwa kabisa kufikia hata robo ya maendeleo aliyoyafanya Rais wa Kwanza wa nchi ya Zanzibar, Sheikh Abeid Amani Karume. Wakizungumza kwa nyakati tofauti jana, baadhi ya wananchi walisema maendeleo yaliyopatikana katika kipindi cha miaka minane ya uongozi wa hayati Karume aliyeuawa mwaka 1972 ni makubwa ikiwemo kuanzisha sera ya makazi na kuwajengea nyumba za kisasa wananchi wake wa nchi hii ya Zanzibar.
Pia ujenzi wa viwanda, kutekeleza kwa vitendo sera ya elimu bila malipo na huduma za maji safi kutoka katika kila nyumba sio bomba moja au mfereji moja kijiji kizima na afya kutolewa bure leo hata kuingi mnazi moja basi utowe pesa. Mkazi wa Michezani, Said Ali Mohamed alisema Karume alianzisha vituo vya kuwahifadhi wazee wasiojiweza na yatima kwa kuwajengea nyumba za kisasa na kuwapatia huduma muhimu ikiwa ni utekelezaji wa sera ya maisha bora kwa kila mwananchi wake wa nchi ya Zanzibar.Akiendelea kusema hayati Karume alijenga barabara za kisasa za njia mbili na kuwa nchi ya kwanza kuwa na barabara za aina hiyo Afrika Mashariki na Kati na alianzisha kituo cha televisheni ya rangi na kuwa ya kwanza kusini mwa Jangwa la Sahara hii nchi sio yakuwa hivi kabisa katika hali hii sasa itabani.
Mkazi wa Mkunazini, Suleimani Ali ‘Sukari’ alisema malengo ya Mzee Karume yametupwa ndiyo maana viwanda vyote vimekufa kutokana na kukosekana kwa mipango mizuri ya uchumi. Akiendelea kusema nchi hii ya Zanzibar ilikuwa na kiwanda cha kutengeneza viatu, maziwa, magodoro, mafuta ya kupikia, soda, sigara, masufuria, nguo pamoja na viwanda vidogovidogo lakini sasa vimebakia historia na kusababisha ongezeko kubwa la vijana wasiokuwa na kazi.“Kama mambo aliyokuwa ameyapanga yangelikuwa yakifuatwa na viongozi waliomfuatia, nchi ingebadilika na kujenga uchumi imara,” alisema Suleiman.Alisema Karume alipiga vita rushwa kwa vitendo na kusimamia haki za wananchi wake bila ya kujali rangi kabila na kuwaunganisha Wazanzibari baada ya Mapinduzi ya mwaka 1964.
Mkazi wa Mbweni, Juma Makame Mcha alisema: “Karume aliwapenda wananchi wake na mambo aliyoyafanya katika kipindi cha miaka minane ya uongozi wake hakuna kiongozi hata mmoja aliyefikia hata nusu yake.” Mkazi wa Jang’ombe, Mwajuma Juma Suleiman alisema, Karume alifanya mambo mazuri kwa wakati mdogo kwa sababu mali ya wananchi ilitumika kuwaletea maendeleo badala ya kujinufaisha na familia yake.
Alisema Zanzibar ingepiga hatua kama sera za marehemu Karume zingesimamiwa kwa nguvu… “Karume alipenda nchi na wananchi wake, kila jambo zuri anawasogezea wananchi wake, leo wananchi waliopewa ardhi na Karume sasa wananyang’anywa na baadhi ya vigogo katika Serikali.”

KILA MZANZIBARI ATAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO

No comments:

Post a Comment