Thursday, April 2, 2015

NCHI YA TANGANYIKA INAENDELEA VIZURI JAPO KUNA UFISADI NCHI YA ZANZIBAR INAZIDI KUDIDIMIA NA NJAMAA ZA VIONGOZI KUFIKIRI VIPI WATAUWA WATU ILI WAZIDI KUKA MADARAKANI


HUU NDIO MUONEKANO WA NDANI YA TRENI YA KISASA KUTOKA DAR HADI KIGOMA NCHINI TANGANYIKA
Nchini Tanganyika Dar es Salaam. Treni ya kisasa (Delux), kwenda Bara yenye mabehewa 22 ilianza safari yake ya saa 30 kutoka Dar es Salaam kwenda Kigoma ikiwa ni tofauti ya saa sita ikilinganishwa na safari ya treni ya zamani.
Kutokana na tofauti hiyo, abiria walioanza safari kwa furaha na matumaini jana saa tano asubuhi wanatarajiwa kufika Kigoma leo saa 11 jioni badala ya saa tano usiku.
Hata hivyo, abiria hao watalazimika kuingiza mikono yao zaidi mifukoni, kutokana na kiwango kipya cha nauli kuwa kimepanda Sh79,400 badala ya Sh75,700 za awali kwa daraja la kwanza.
Huku nauli za daraja la pili ikishuka kutoka Sh55,400 hadi Sh,47,600 zile za daraja la tatu zimepanda kutoka Sh27,700 hadi Sh35,700.
Kwa mtazamo wa haraka, mabehewa hayo yanavutia yakilinganishwa na yale ya awali yaliyokuwa yamekithiri kwa uchakavu na uchafu pia kunuka harufu isiyo julikana, yaliyokuwa yamejaa mende na yenye milango na madirisha mabovu.
Mabehewa hayo yana viti vya kutosha na vya kisasa kama unavyo viona katika picha, kuna huduma ya intaneti Wifi kwa walewenye smart phone tablet na laptop, swichi za umeme za kuchajia simu za aina yoyote na kuunganisha kompyuta na safari zake zimeongezeka kutoka mbili hadi tatu kwa wiki.

KILA MZANZIBARI ATAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO

No comments:

Post a Comment