Monday, April 13, 2015

PINDA AMUWA KUIPINGIA DEBE KATIBA PANDIKIZWA KWA WATANGANYIKA WAISHIO UGHAIBUNI NCHINI TANGANYIKA KATIBA HAWAITAKI NCHINI ZANZIBAR NDIO KABISA.


MR ZANZIBAR SI NCHI MIZENGO PINDA

Waziri Mkuu wa nchi ya Tanganyika Mizengo Pinda amesema Watanganyika waishio ughaibuni hawataweza kupiga kura wakiwa nje ya nchi yao ya Tanganyika wakati wa Uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba, mwaka huu.
Alisema pamoja na kwamba Watanganyika hao wanatakiwa kupiga kura wakati wa uchaguzi huo, jambo hilo halitawezekana kwa sababu kuna mambo kadhaa ambayo Serikali inabidi iyatekeleze kabla ya uchaguzi huo.
Waziri Mkuu Pinda wa nchi ya Tanganyika alitoa kauli hiyo jana kwenye makazi ya Balozi wa Tanganyika nchini Uingereza, Peter Kallaghe, wakati akizungumza na baadhi ya Watanganyika waishio nchini humo.
Akizungumza na Watanganyika hao ambao baadhi yao walitoka miji ya Leicester na Manchester, alisema mambo makuu ambayo yanahitaji kuzingatiwa kabla hawajaweza kupiga kura ni pamoja na marekebisho ya Sheria ya Uchaguzi namba moja ya mwaka 1985 pamoja na uandikishwaji wa Watanganyika wana-Diaspora kwenye Daftari la Kudumu la Wapigakura.
“Najua suala kubwa ambalo mnatamani kulisikia ni hili la Watanganyika kuweza kupiga kura kutokea huku mliko. Hili inawezekana lisifanikiwe wakati huu kwa sababu kuna mambo muhimu ya kuzingatia, kubwa likiwa ni marekebisho ya sheria na hili zoezi la uandikishaji wa wapigakura kwenye Daftari la Kudumu la Wapigakura.
“Ili mwananchi aweze kupiga kura ni lazima awe ameandikishwa kwenye daftari hilo.
“Itabidi tuangalie kama mashine za BVR nazo zitapaswa kupelekwa kwenye kila ubalozi ili watu wetu waweze kujiandikisha au itafutwe njia nyingine ya kufanikisha hilo jambo… lakini watu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi wanaamini kwamba jambo hilo linaweza kufanikiwa kwenye uchaguzi wa mwaka 2020,” alisema.
 
MR ZANZIBAR SI NCHI MIZENGO PINDA

Waziri Mkuu wa nchi ya Tanganyika ambaye aliwapatia Watanganyika hao nakala zisizopungua 40 za Katiba Inayopendekezwa, alitumia fursa hiyo kuwasisitiza waisome kwa makini ili wawe na uelewa mpana na kisha wailinganishe na Katiba ya mwaka 1977 ambayo inatumika hivi sasa ili waweze kubaini kama kweli haina kitu kama ambavyo watu wengine wanadai.
“Moja ya changamoto zinazotukabili huko nyumbani ni mjadala kuhusu Katiba Inayopendekezwa… wako watu wanaosema kwamba hakuna kitu kipya kabisa kwenye Katiba Inayopendekezwa, lakini mimi nasema hayo ni mawazo yao binafsi,” alisema Pinda.

KILA MZANZIBARI ATAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO

No comments:

Post a Comment