Saturday, April 4, 2015

TAIRENI POLISI, JKU. JIBUNI HAYA MASWALI KWANZA.


Baadhi ya askari wa jeshi la kujenga uchumi nchini Zanzabar (JKU) 
Kwa takribani wiki tatu sasa kumetokea visa na mikasa katika medani za kisiasa hapa nchini Zanzibar, na kama ilivyo ada vyombo vyetu vya ulinzi viko katikati vinaendeleza tabia yao mbaya.Mara hii kwa kuanzia vyombo vyetu viwili vimejitokeza wazi wazi kufanya kazi za chama cha siasa na kukisaidia zaidi chama cha MKOLONI MWEUSI TANGANYIKA.
Tukianza na JKU. Hili ni jeshi la Kujenga Uchumi wa nchi ya Zanzibar ambalo lina wajibu wa kuhakiksha linatoa mafunzo na kuhamasisha vijana katika kujenga uchumi imara je linafanya hayo.....? maana kila kukicha vijana waameja mabarazani hawana la kufanya mwisho wengi wao huishia kuvuta bangi na unga ((drugs)), kazi haswa ya jeshi hili ilikuwa ni kutoa stadi za maisha katika mwelekeo wa kukuza uchumi na kuandaa rasilimali watu kushiriki kujenga uchumi wao.Kama mwezi mmoja uliopita kulikuwa na zoezi la uandikishaji wa nafasi mpya za JKU kwa vijana na kulikuwa na tetesi kote mitaani kuwa UTARATIBU ulikiukwa wa kuwapata vijana. Ilitarajiwa Tume ya utumishi serikalini itangaze hizo nafasi na bila ya UPENDELEO wenye sifa wachaguliwe lakini sivyo ilivyokuwa.Nafasi zilipitia wilayani na kwa masheha ambao wanajulikana kwa upendeleo wao wa kisiasa kwa chama cha CCM. Kutokana na kadhia hiyo ndipo MAKAMO WA KWANZA WA RAIS NCHINI ZANZIBAR na Katibu Mkuu wa CUF bila kupepesa alihutubia mkutanoni pale mnazi mmoja na akalisemea hilo na alisema anazo TAARIFA. Cha kushangaza na kustajabisha siku ya pili alijitokeza mkuu wa utawala wa JKU na mwanasheria wake kutishia kwenda mahakamani ikiwa hawatoombwa radhi atii kwa kudhalilishwa hahahaha bora ni cheke kwanza hahahaha kuthalilishwa....?? Yaani wakamshataki Makamo wa Kwanza kwa madai atii ya kuwadhalilisha. wengine hatukushangaa ingawa tulipigwa na butwaa. Hivi JKU hawajuwi wajibu wao.....????
JKU tujibuni haya maswali.
Kwanza tujibuni zile Taarifa za makamo wa kwanza mlizifuatilia na kupata uhakika wake....?? na jee kama zilikuwa za kughushi jee mahakamani mtakwenda lini....?? na ikiwa si za kughushi ni zakweli je mtakubali kujiuzulu madara yenu yote...??
Jamii inapaswa kuambiwa nani aliyewaagiza masheha kupeleka majina ya vijana watao jiunga na jeshi la nchi ya walioomba nafasi kule wilayani hivi kweli sio nyinyi.....?? na kama si nyinyi ni nani anayefanya kazi hizi kwa niaba yenu twambieni.....??
Hivi ni toka lini sheha amakuwa ndio mwenye kuandikisha majina ya wanajeshi wa nchi hii na ni nani alimpe madara hayoo..??
Nini kiliwasukuma kutoa kauli za kutishia kwenda mahakamani badala ya kwenda kwa Makamo wa kwanza wa rais kuomba awape mashirikiano ya madai yake badala yake kutishia kumshtaki na kujaribu kumjibu hivi siku hizi JKU ni TAASISI YA SIASA.....??
Tunaomba mtupe maendeleo ya zoezi lenu la kwenda mahakamani jee bado nia ipo....?? na mtwambie vipi huo mchakato wa AJIRA umefikia wapi kwa sasa....??
Toka jeshi hili lianzeshwa mpago mzima ni kuleta maendeleo kwa vijana je maendeleo hayo yako wapi..?? je mnaweza kutuonyesha toka kuanzishwa jeshi hili ni maendeleo mangapi yameletwa na jeshi hili na nivijana wangapi wa Zanzibar walio nufaika nalo jeshi hili....?? ikiwa hakuna maendeleo kwa vijana mtakubali livunjwa ili liundwe upya na wakuu wa jeshi hili wote wajiuzulu....??
Jee JKU ni taasisi ya siasa au ya Serikali na kama ni ya Serikali ni serikali gani.....??
JKU mnamtambuwa Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar kama kiongozi halali wa SMZ.....??JESHI LA POLISI.
Kumekuwa na hujuma za kuchomwa moto ofisi za CUF, kupigwa na kujeruhiwa wafuasi wa CUF waliotoka mkutanoni na kuchomwa bendera.Niliona kwenye vyombo vya habari eti POLISI watazuiya vyama visiwasafirishe wanachama kutoka wilaya moja kwenda nyengine wakati wa mikutano na eti kusiwe na lugha za matusi na mabango ya matusi Aaah” Hivi kwa nini mnalenga kuzuiya shughuli za kisiasa za vyama leo baada ya wafuasi wa CUF kushambuliwa na sio kuja na mkakati wa kupambana na wahalifu....?? jee mmeshindwa nguvu na washambulizi kiasi cha kutaka sasa mikutano isiwe na watu kutoka wilaya nyengine.....??
Siku hizi kazi ya POLISI ni kupanga namna ya kufanya mikutano vyama vya siasa....??  Sio kulinda usalama wa raia na watu wake....?? Ni nani kawabadilishia kazi zenu....? Au hamjuwi kazi zenu....?? Twambieni kwanza nani walishambulia msafara wa CUF na kuumiza watu, nani walichoma moto ofisi za CUF na mmefikia hatua gani au bado uchunguzi Unaendelea...?? Vipi mara hii ile teknolojia ya PICHA ZA KUCHORA 
 mtaitumia au kuna mbinu nyengine za kisayansi wakuu....?? Hayo matusi ya mabango na mikutanoni mmeoteshwa au ndio kwanza yanataka kuanza 2015....?? Na kwa nini msisubiri hayo matusi yakaja kwanza ndio mkayasemea au ndio mmeoteshwa....?? Tusaidieni kujibu hayo kwanza na mtwambie vipi MTAEPUKA kuhusishwa na KUTUMIWA NA CHAMA CHA CCM CHA MKOLONI MWEUSI TANGANYIKA ikiwa mambo yenyewe ndio hayo.
JKU, POLISI , Wazanzibari washachoka na Vitimbi hivi, wanahitaji kupumzika,HEBU WACHENI WAZANZIBARI WAPUMUWE.

KILA MZANZIBARI ATAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO

No comments:

Post a Comment