Wednesday, May 6, 2015

HAYA NDIO YALIYO MPATA STAR ADEBAYOR KWA FAMILIA YAKE NDIO YANAYO WAPATA VIJANA WENGI WAISHIO UHAIBUNI KWA FAMILIA ZAO AFRIKA NDIO MAANA HATUENDELEI


Mshambuliaji wa Tottenham, Emmanuel Adebayor ameandika maelezo marefu kwenye akaunti yake ya Facebook keleza visa anavyofanyiwa na familia yake akiwemo mama yake, kaka na dada zake.

Adebayor ameamuwa kzungumzia ukweli kuhusu ndugu zake na tamaa ya mali zake. Licha ya kuwafanyia mambo mengi ikiwemo kuwajengea nyumba, kuwanunulia magari na kuwapa mitaji ya biashara, bado wameendelea kumtupia shutma nyingi. Tumeitafsiri posy hiyo.

SEA, nimezihifadhi habari hizi kwa muda mrefu lakini nadhani leo ni muhimu kuziweka wazi baadhi yake kwenu.

Ni kweli masuala ya kifamilia yanapaswa kusuluhishwa ndani kwa ndani na sio hadharani lakini nafanya hivi ili pengine familia zote zinaweza kujifunza kutokana na kile kilichotokea kwangu.

pia weka akilini kuwa hakuna chochote kati ya haya kinahusiana na pesa.

Nikiwa na miaka 17, kwa mishahara yangu kama mchezaji wa soka, nilijenga nyumba kwa jili ya familia yangu na kuhakikisha kuwa wapo salama. kama nyote mnavyojua, nilishinda tuzo ya mchezaji bora wa Afrika mwaka 2008. Nilimpandisha pia mama yangu jukwaani kumshukuru kwa kila kitu.

Katika mwaka huo huo, nilimleta London kwa jili ya kufanyiwa vipimo mbalimbali. Baada ya mtoto wangu wa kke kuzaliwa, tuliwasiliana na mama yangu kumjulisha lakini muda mfupi alikata simu na hakutaka kujuwa chochote.

Nikisoma maoni yenu ya hivi karibuni, baadhi ya watu walisema mimi na familia yangu tungemtafuta T.B. Joshua. mwaka 2013, nilimpa mama yangu fedha ili amtafute (joshua) nchini Nigeria.

Alitakiwa kukaa kwa wiki; lakini simu mbili akiwa huko, nilipigiwa simu kuwa ameondoka. Pamoja na yote hayo, nilimpa mama yangu fedha nyingi kuanzisha biashara ya cookies' ((biskuti zenye sukari)) na bidhaa zingine. kwa kawaida niliwaruhusu waziweke jina na picha yangu ili wauze zaidi. Nini kingine mtoto wa kiume anaweza kukifanya kuisaidia familia yake..?

Miaka kadhaa iliyopita, nilinunua nyumba kubwa huko East lagon (Ghana) kwa dola millioni 1.2 niliona ni kawaida kumuachia dada yangu, Yabo Adebayoor kukaa kwenye nyumba hiyo. Pia nilimruhusu kaka yangu (half brother) Daniel, kukaa kwenye nyumba hiyo. Miezi michache baadaye, nilikuwa mapumzikoni na nikaamua kwenda kwenye nyumba hiyo. chaa kushangaza, niliona magari mengi getini. Dada yangu aliamua kuipangisha nyumba ile pasipo mimi kufahamu. Pia alimfukuza Daniel kwenye nyumba hiyo.Kumbuka kuwa nyumba hiyo ilikuwa na vyumba 15.

Nilipompigia kutaka kupewa maelezo, alinutukana takriban dakika 30 kunitukana kwenye simu. Nilimpigia mama yangu kumwelezea hali hiyo na yeye pia alifanya kile kile alichokifanya dada yangu. Dada huyu huyu anasema mimi sina shukrani. Muulize kuhusu gari anayoendesha ama chochote anachouza leo..?

Kaka yangu Kola Adebayor, amekuwa akiishi Ujerumani kwa miaka 25 Alisafiri kurudi nyumbani kwa takriban mara nne, kwa gharama zangu. Ninalipia gharama za shule za watoto wake kila kitu. Nilipokuwa Monaco, alikuja kwangu na kuniomba pesa ya kuanzisha biashara. Mungu ndiye anayejua ni kiasi gani nilimpatia. Iko wapi hiyo biashara leo hii..?

Baada ya kaka yetu Peter kufariki, nilimtumia Kola kiasi kikubwa cha fedha ili aende nyumbani. Hakutokea kwenye mazishi. Na leo kaka yangu huyo huyo (kola) anawaambia watu kuwa nilihusika kwenye kifo cha peter.

Kivipi..? Ndio kaka yule yule aliyee enda kuongea habari za uongo kuhusu familia yetu kwenye gazeti la The Sun ili kujipatia pesa. Pia walituma barua kwenye klabu yangu wakati nipo Madrid ili nifukuzwe.

Nilipokuwa Monaco nilidhani ingekuwa vyema kuwa na familia ya wacheza soka. Hivyo nilihakikisha mdogo wangu Rotimi anapata chuo cha football nchini Ufaransa. Ndani ya miezi michache tu; kati ya wachezaji 27, aliiba simu 21!!

sitaweza kusema chochote kuhusu kaka yangu Peter Adebayor kwa sababu hayupo hapa leo. Roho yake ilale mahala pema peponi.

Dada yangu, Lucia Adebayorhuendelea kuwaambia watu kuwa baba yangu aliniambia nimlete ulaya. Lakini nini atakuwa sababu ya kumleta Ulaya..? kila mtu yuko hapa kwa sababu.

Nilikuwa Ghana nilipopewa taarifa kuhusu kaka yangu Peter kuwa mgonjwa mahatuti. Niliendesha gari haraka iwezekanavyo hadi togo ili kukutana naye na kusaidia. Nilipofika, mama yangu alisema nisingeweza kumuona, na nilitakiwa kuwapa pesa tu na yeye angefanya kila kitu.

Ni Mungu tu ndio anayejuwa nilimpa kiasi gani siku hiyo. Watu wanasema sikufanya chochote kumsaidia kaka yangu, Peter. Mimi ni mjinga kuendesha gari kwa masaa mawili hadi Togo bure..?

Niliitisha mkutano mwaka 2005 kusuluhisha masuala yetu ya kifamilia. Nilipowauliza kuhusu maoni yao, walisema natakiwa kumjengea nyumba kila mtu kwenye familia na kuwapa kila mmoja mshahara wa mwezi!! 
Leo bado nipo hai na wameshagawana kila mali yangu, kama ikitokea nimekufa.

Kwa sababu zote hizi, ilinichukua muda mrefu sana kuanzisha taasisi yangu barani Afrika. Kila muda nikitaka kuwasaidia watu wenye shida, walikuwa wakiniuliza maswali na wote walidhani ni wazo baya.

kama naandika hiki, dhumuni halisi si kuwaanika watu wa familia yangu. Ninataka familia zingene zijifunze kutokana na hili

Asanteni

KILA MZANZIBARI ATAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

No comments:

Post a Comment