Wednesday, May 6, 2015

KATIBA NCHI ZA AFRIKA NI KUDAGANYA RAI WAKE TU NA VITI VYA URAISI VYA NCHI ZA AFRIKA VINA LAANA NDIO MAANA KILA ANAE KAA HATAKI KUKIACHA MPAKA ATIMULIWE AU AULIWE


MARAISI WA AFRIKA HAWANA LAO JAMBO KUWALETEA MAENDELEO WANANCHI WANACHO JALI WAO NI KUVA VIZURI NA KILA KITU KINATOKA NCHI ZA NJE SHABASH
Viongozi wakuu wa nchi za Afrika NA HASWA  SASA AFRIKA MASHARIKI wanapotaka kuendelea kukaa madarakani zaidi ya vipindi vilivyokubaliwa kikatiba, hutumia mbinu mbalimbali. Baadhi hutumia wananchi waanze kufanya ushawishi katiba zirekebishwe ili viongozi husika waendelee kuka madarakani hata kama hawawaletei maendeleo wananchi; wengine hutumia kisingizio cha sensa, kucheza na tafsiri ya katiba na baadhi hutumia mbinu ya kuchelewesha uandikishaji kwa makusudi imekuwa kama wana LAANA VIONGOZI HAWA.
Aliyekuwa Rais wa Burkina Faso, Blaise Compaore alicheza na Katiba. Kiongozi huyo aliyeingia madarakani mwaka 1987 kwa kuiangusha serikali ya kijeshi ya rafiki yake, Thomas Sankara, naye alipinduliwa kwa nguvu ya umma Oktoba 30, 2014 mwaka jana sote tukishuhudia siku ambayo Bunge lilikuwa lipitishe mabadiliko ya katiba ili kiongozi huyo aliyetawala miaka 27 kuanzia Oktoba 15, 1987 aendelee kutawala hii nisomo tosha kwa viongozi wengine wa afrika lakini wapi kama nilivyo sema pale juu ni kama WANALAANA siku zote hufikiri limempata Raisi yule mimi halitanipata kwa utamu w madaraka ulivyo walevya. Compaore amekimbilia uhamishoni kabahatika haku uwawa kama Gaddafi.
DRC na sensa 


Nchi nyingine iliyokaribisha machafuko ni Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) ambako Rais Joseph Kabila amefikia ukomo wa uongozi wake. Joseph ametawala DRC tangu Januari 26, 2001 baada ya kuuwawa baba yake Laurent Desire Kabila. Mazungumzo ya amani yalipokamilika mwaka 2002, iliandaliwa katiba pendekezwa iliyopigiwa kura ya maoni mwaka 2005.
Kabila alichaguliwa kidemokrasia mwaka 2006 na mara ya pili ilikuwa mwaka 2011. Lakini alipoona muhula wake wa pili ukikaribia kumalizika Serikali yake ikabuni sensa ya watu ili idadi ya watu ijulikane kwanza ndipo ufanyike uchaguzi mkuu. Hii ina maana sensa hiyo ikianza mwakani na mchakato wake ukachukua miaka minne, kama walivyopandekeza kutokana na miundombimu mibovu ya nchi, Kabila atakuwa amekaa madarakani muhula wa tatu kinyemela kabisa hana wasi wasi anakula tu kuku ikulu bure wananchi wanateseka wananuka. Wananchi walikataa na siku Bunge lilipotaka kupitisha sheria hiyo yalifanyika maandamano makubwa.

Tafsiri ya Katiba


Mzuka wa kutaka muda zaidi wa uongozi umeingia nchini Burundi ambako Rais Pierre Nkurunziza anataka muhula wa tatu kinyume cha katiba na kinyume cha makubaliano ya Arusha yaliyoleta amani ya Burundi.
Makubaliano ya makundi mbalimbali ya wanasiasa yanasema itakuwa marufuku kwa kiongozi mkuu wa nchi kutawala zaidi ya vipindi viwili vya miaka mitano. Makubaliano hayo ndiyo yaliingizwa kwenye katiba ambako iliandikwa rais aliyechaguliwa na wananchi hataongoza Burundi kupindukia vipindi viwili.
Utata; Nkurunzina alipoongoza kipindi cha kwanza kwa kuzingatia makubaliano ya Arusha alichaguliwa na Bunge lakini kipindi cha pili alichaguliwa na wananchi. Yeye mwenyewe, mwaka 2010 alipoteuliwa na chama chake kuwania muhula wa pili aliwaambia wananchi kuwa “sitawaangusha Warundi, hiki ni kipindi changu cha pili na cha mwisho”.
Hata hivyo, baadaye alianza kutafsiri makubaliano ya Arusha na kilichoandikwa katika katiba akidai kuwa kwa kuzingatia ‘rais aliyechaguliwa na wananchi’ yeye ni wa kwanza hivyo muhula huu utakuwa wa pili.
Rwanda na KatibaJapokuwa Rais Paul Kagame wa Rwanda amewahi kutangaza, mara kadhaa, kwamba ataheshimu katiba inayotaka rais akae madarakani vipindi viwili vya miaka saba saba, hali ni tofauti. Ushawishi umeanza kufanyika ili agombee kipindi cha tatu cha miaka saba baada ya 2017 kwa madai kwamba ameipatia maendeleo makubwa Rwanda.
Kila alipoulizwa kuhusu suala hilo amekuwa akisema “wananchi wa Rwanda watasema muda ukifika” hivyo kujiweka kando na fununu hizo. Lakini wafuasi wa chama tawala cha RPF wanadai kubakia madarakani kwa muhula mwingine kwa Rais Kagame kutasaidia kuzuia mivutano na machafuko na kutaimarisha hali ya kisiasa na kiuchumi.
Uganda na KatibaYanayofanyika Rwanda ndiyo yanafanyika Uganda. Rais Yoweri Museveni alipoingia madarakani mwaka 1986 aliahidi kuongoza vipindi viwili na kuachia damu changa, lakini hadi leo, haonyeshi dalili za kung’atuka madarakani. Museveni anadai kuwa mchakato wa ukombozi haujakamilika. Na kuthibitisha kwamba chama chake cha NRM kiko tayari kubadili Katiba, kimempitisha mpigania mabadiliko huyo wa Uganda kuwa mgombea urais uchaguzi mkuu utakapoitishwa mwaka 2016.
Tanganyika na Zanzibar na mashine za BVRRais Jakaya Kikwete wa nchi ya Tanganyika ameanza kuagaaa yeye na kibaraka wake Shein. Hata hivyo, anachoongea ni tofauti na yanayofanyika serikalini. Pamoja na kauli ya Rais Kikwete wa nchi ya Tanganyika kwamba anataka kupumzika na kwamba uchaguzi utafanyika kama ilivyopangwa, kusuasua kwa uandikishaji wapigakura katika Daftari la Kudumu la Wapigakura kwa mfumo wa BVR kumeamsha hofu na hasira za wapinzani kuwa kuna njama za mkuu huyo wa nchi kutaka kukaa zaidi madarakani kwa utamu wa madaraka.
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetangaza mara kadhaa kwamba hakuna Uchaguzi Mkuu bila ya daftari hilo kufanyiwa marekebisho, kwa vile la zamani limeharibika. Kazi ya kuandikisha ilianza Februari 23, 2015 katika Mkoa wa Njombe wenye wapigakura wapatao 300,000.
Huo ndiyo mkoa pekee ambao uandikishaji umekamilika tena baada ya miezi miwili. Je, kazi hiyo itakamilika lini nchi nzima ya Tanganyika...? Bado na nchi ya Zanzibar hata hatusiki harufu Tume itawafikia lini wapigakura wapatao milioni 20 ili uchaguzi ufanyike kama ilivyopangwa Oktoba mwaka huu...? Nini kitatokea endapo uandikishaji utakuwa haujakamilika.....?
Kushindwa kwa Tume ya Uchaguzi kukamilisha uandikishaji wa wapigakura kumesababisha kuahirishwa, kwa muda usiojulikana, kwa Kura ya Maoni kwa Katiba Inayopendikizwa iliyopangwa kufanyika Aprili 30. Waliosababisha Tume kushindwa kukamilisha kazi yake ni Serikali iliyoshindwa kuwapa fedha zinazohitajika kwa ajili ya kununua mashine za BVR 8,000 baada ya mamillioni yote walio ibaa ya EPA na ESCROW ila wanazo pesa za kusherehekea sherehe za Muungano feki.
Tume ilikuwa na mashine 250 na hivi karibuni ziliongezwa na kufika 3,000. Je, wananchi waamini kuwa zitakamilisha kazi hiyo mapema ili uchaguzi ufanyike kama ilivyopangwa........? Je, haziwezi kufikiriwa kuwa kutoipa Tume fedha ni mbinu za Serikali ili ishindwe kazi na hivyo tarehe ya uchaguzi isogezwe mbele jambo ambalo litamaanisha Rais Kikwete atakaa hadi hapo uchaguzi utakapofanyika....? Madarakani yeye na kibaraka wake Shein.

KILA MZANZIBARI ATAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

No comments:

Post a Comment