Friday, May 22, 2015

VIDEO-TUNDU LISSU A.K.A. RONALD ASEMA RAISI KIKWETE NA MAWAZIRI WAKE WAMEKITHIRA NA AHADI HEWA NA VIONGOZI WA DINI NA WAUMINI WAO KUFANYIWA UKATILI.


MSEMAJI wa Kambi Rasmi ya Upinzani na mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu, ameichachafya serikali akidai imekithiri kwa ahadi hewa ambazo zimekuwa zikitolewa na Rais Jakaya Kikwete na mawaziri kuhusiana na Kura ya Maoni ya Katiba Pendekezwa. Lissu alitoa kauli hiyo jana katika Mkutano wa 20 wa Bunge unaoendelea mjini Dodoma wakati akiwasilisha mapendekezo ya kambi pinzani kuhusu makadirio ya matumizi ya Wizara ya Katiba na Sheria.

Lissu alisema Rais Kikwete wakati akikabidhiwa katiba pendekezwa aliwaahidi Tanganyika ((Watanzania)) kuwa katiba hiyo ingepigiwa kura ya maoni Aprili 30, mwaka huu lakini hadi sasa ahadi hiyo haijatekelezwa. Alisema leo ni wiki ya 3 tangu Rais Kikwete awaahidi Watanganyika ((Watanzania)) juu ya upigaji wa kura ya maoni lakini mpaka sasa haijulikani siku wala tarehe ya kura ya maoni kutokana na ubabaishaji uliopo ndani ya Serikali.

Lissu alisema ni dhahiri hakuna uhakika wowote kufanyika kura ya maoni juu ya katiba mpya kutokana na sheria iliyopo ya kura ya maoni ya mwaka 2015. Alisema kwa sasa kuna uhakika wa Rais Kikwete kuondoka madarakani bila ya katiba mpya aliyowaahidi Watanganyika ((Watanzania)) kupatikana katika kipindi cha takribani miaka mitano iliyopita.

Mbunge huyo machachari alisisitiza; "Ndani ya utawala wa Rais Kikwete unaonesha dhahiri kuwa ameshindwa kukamilisha mchakato huo pamoja na chama chake CCM. "Hata kama tume ya uchaguzi itaweza kukamilisha jukumu lake la kuandikisha wapiga kura nchi nzima bado hakuna uhakika wa kufanyika kwa kura ya maoni kutokana na matakwa ya sheria ya kura ya maoni 2015."
Alisema Sheria hiyo iliweka utaratibu mgumu wa uendeshaji wa kura ya maoni ambapo kila hatua inayotakiwa kuchukuliwa haiwezekani kuahirishwa kwa kuongezewa muda. Akizungumzia haki za binadamu, Lissu alisema kwa kiasi kikubwa ukiukwaji wa haki za binadamu umeongezeka kwa Watanganyika na Wazanzibari ((Watanzania.)) Alisema mauaji na mashambulizi dhidi ya viongozi wa kidini na waumini wao kufanyiwa ukatili sehemu zao za ibada hakuna mtu yeyote aliyeadhibiwa katika kesi hizo.
"Serikali haijatoa taarifa yoyote juu ya wahusika na wauaji wa mashambulio mbalimbali yaliyofanyika nchini, yakiwemo ya Daud Mwangosi pamoja na shambulio la Dkt.Ulimboka hadi sasa hayajajulikana hatma yake,"alisema Lissu.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Muhambwe Kigoma, Felix Mkosamali alisema ni aibu kwa nchi katika kura ya maoni kwani sheria yake bado haitekelezeki na haiwezekani kwa mazingira ya sasa yalivyo inashangaza waziri wa sheria kutangaza kuwepo kwa kura hiyo. Mkosamali alisema hii ni aibu kwa nchi kuendeshwa bila ya kuwa na uhakika nayo wala kuwa na ratiba au sheria inayoeleweka kwani hata katiba hiyo ikilazimika kupigiwa kura inakuwa haina umuhimu kwa wananchi wake.

"Kwa hili serikali imeshafeli tangu mwanzo mchakato huu wa katiba ni mchakato ambao ukiutakari unashangaza hasa kwa chama cha CCM kushauriana na vyama vingine kwani katiba za wenzetu ni nzuri na zenye mashiko kwa jamii yao,"alisema Mkosamali.

Akizungumzia Sheria iliyopo sasa nchini, Mkosamali alisema  Sheria zinazotekelezwa nchini ni asilimia 30 mambo mengi yanaendeshwa kiholela bila kufuata sheria. Alisema hali ya watu kutumia sheria mikononi imeweza kuongezeka kutokana na jamii kutoamini serikali ambapo mara nyingi wanapowafikisha watuhumiwa polisi wanaachiwa.

KILA MZANZIBARI ATAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

No comments:

Post a Comment