Sunday, June 7, 2015

CUF NA NYINYI MSHAKUWA CCM...??? MGOMBEA WANAE MTAKA WANANCHI MNAWAWEKA PEMBENI MNAWEKA MAKUMBI MNAYOTAKA NYINYI SIO HAYA KOJANI KWA FUTUKA


KISIWA CHA KOJANI PEMBA NCHINI ZANZIBAR MAJI YA CCM POMBA MOJA MJI AU KIJIJI KIZIMA MNACHOTA MAJI KATIKA BOMBA MOJA NA HII NI 2015

Kufuatia uteuzi wa wagombea nafasi za Ubunge na Uwakilishi kupitia Chama cha Wananchi CUF ambao wamepitishwa na Baraza Kuu kumezua sokomoko kubwa miongoni mwa wanachama na viongozi. Jimboni Kojani hali sio shwari. Vumbi linaanza kutimka baada ya mgombea aliyeshinda kura za maoni kuekewa pembeni na kupitishwa mgombea ambaye aliyepata ushindi wa pili. Jimbo la Kojani limejumuisha maeneo ya Kisiwani Kojani na maeneo mengine ya juu. Kikawaida eneo la Kisiwani hutoa Mwakilishi na eneo la juu hutoa Mbunge. Hayo ni makubaliano baina yao. Nafasi ya uwakilishi inashikiliwa na Wakojani kindakindaki.
Yaliyoko ni Wakojani kugawika na kujipanga kupinga uteuzi wa Uwakilishi wakidai Mteuliwa ambaye ni Mwakilishi kwa sasa hawafai kwani hakufanya kitu katika miaka 5 iliyopita. Pia kashindwa kwenye kura za maoni. Vilevile hakutowa ahadi zinazoeleweka nini atawafanyia miaka 5 ijayo. Alikuwa akitumia fedha zote za mfuko wa jimbo kwa maslah yake binafsi. Yapo matawi 28 ndani ya jimbo la Kojani hakuna hata tawi moja alilojenga. Ameshindwa kumaliza jengo la ofisi ya Jimbo la Kojani, lililopelekea kusababisha kifo cha mtoto wa miaka 8 baada ya matufali yake kumuangukia mtoto huyo. Kutumia fedha kutafuta kurudi tena kwenye kiti. ripoti zote za Jimbo na Wilaya zilionyesha kutoridhishwa na utendaji wake. Mwisho ni kuwa hakubaliki kwa Wakojani wenzake.
Kwa upande wa Mgombea aliyeshinda kura za maoni na hakupata kuteuliwa yeye yuko juu kwa kukitumikia chama, pia ameonyesha CV zake za majukumu aliyokuwa nayo. Ametowa ahadi za uhakikiwa ikiwa ni pamoja na kumaliza jengo la ofisi ya Jimbo la Kojani. Kutumia fedha za mfuko wa jimbo kwa kuwakabidhi wenyewe wananchi ili zitumike ipasavyo. Ameahidi kuchangia chama ndani ya jimbo lake kwa kuwapatia mgao maalumu utakao saidia kuendesha shughuli za chama jimboni hapo. Pia kumaliza matawi ya chama yale yaliokwisha aanza kujengwa.
Kumetayarishwa Wakojani waliopo Unguja, Jimbo la Mtoni kwenda kumuona Naibu Katibu Mkuu Mh Nassor Ahmed Mazrui na kumuelezea kadhia yao juu ya uteuzi chama waliofanya. Timu nyengine ya Wakojani inafanya inawasubiri Katibu Mkuu, Naibu Katibu Mkuu na Mkurugenzi wa Uchaguzi. Kuna baadh ya juhudi zimeanza kuchukuliwa ikiwa ni pamoja na ofisi ya Wilaya ya Wete kutakiwa kusuluhisha mzozo huu. Kiukweli moto unafukuta na mwisho wake haujulikani wapii utaripuka.
((cuf msitulete upumbavu au na nyinyi mushakuwa CCM kuweka makumbi kisha watu walipigie kura...? mgombea walio taka wananchi ndio mgombea anaye stahiki kupitishwa na kuwa mgombea sio wananchi wanamchaguwa mgombea huyu nyinyi akifika unguja mnamkata je unguja ishakuwa Giningi kama Dodoma musilete upumbavu mnataka kushinda oktoba au ndio yale ya CCM mwaka huu CUF tunakizika. Acheni mambo ya upendeleo mgombea anaye changuliwa na wananchi ndio mgombea nyinyi mumpitishe bila ya kigugumizi ikiwa hata wafanyia kitu wakilalamika mutawambia heee huyu mulimchanguwa wenyewe kwa hiyo miaka mitano ikimalizika mnajuwa vyakumfanya musimpitishe tena ndio dawa yake. Huyo aliyekuweko miaka mitano washakuambiyeni hana moja alilolifanya kwa nini nyinyi mnampitisha tena....? huyo huyo na wao hawamtaki. Hali yakuwa wananchi wanataka mgombea mwengine kama ni hivyo ilikuwa hakuna haja yakuwauliza wananchi basi. Mulikuwa tu mujichanguliye wenyewe kisha mukawapigia kura wenyewe wananchi tutaka nyumbani pumbavu kabisa musitulete mambo ya CCM hapa tunakata ya hitler mnataka kutuletea ya firauni nyinyi vipi kila jimbo mgombea aliye changuliwa na wananchi ndio mgombea halali sio muliomchaguwa nyinyi au kama nyinyi ni Giningi Dodoma basi twambiyeni tujuwe.))
KILA MZANZIBARI ATAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO

No comments:

Post a Comment