Wednesday, June 24, 2015

IKIWA WANANCHI HAWAKUPATA MAENDELEO CCM KWA MIAKA 50 WATAYATAFUTA KWENYE VYAMA VINGENE MAENDELEONi yupi katika hawa atakuwa mwizi mpya wa kuiba na kuwahifadhi majambazi wenzake na kuwaleya mafisadi vizuri ili wandelea kufanya ufisadi wao na kuwakandamiza wananchi kwa kutumia jeshi na polisi ili wao wakae madarakani kwa utulivyo na familia zao na mahawara wao na kuwazidishia wananchi unyonge na umasikini kwa miaka mengine 5..........??? huku wakinadi Amani na Utulivu Maendeleo yanakuja miaka 5. Miaka mitano itakwisha utasikia tena Amani na Utulivu Maendeleo yanakuja miaka 5 ukizinduka miaka 50 mengine imekwisha wewe mwananchi unanuka kwa maisha magumu wao maneno ya vijana wanapeta na kula bata.


Ni kweli kuwa ndani ya CCM mambo si shwari tena,viongozi waandamizi na makada wa mbalimbali wanaumiza vichwa wakihaha ni kwa namna gani watainusuru CCM yao na matumbo yao kwa miaka mengine mitano maana wanaona CCM ina anguko tena anguko lenyewe ni la milele. Ziara anayoendelea nayo kinana ya kujaribu kuwahada wananchi na kujidai kuwapa moyo wa uwongo maana miaka mitano imepita mbona hakututembelea mpaka sasa wakati wa kura ndio kila mahali anapita kwa wananchi. imedhihirisha jinsi wanainchi walivyoichoka CCM ,ni ukweli usio na shaka kuwa CCM imekwisha kwisha kabisa na kwa sasa imebakia kuwa ya wanachama viongozi,wake zao,watoto wao,mahawara wao na watoto wao wa nje ya ndoa na wale wachache wanaolinda maslahi yao, wengi wa hawa wako mguu ndani mguu nje. Ziara ya kinana ktk mikoa yote aliyopita imeshuhudia utitiri wa malalamiko na kutokuridhika kwa wananchi kwa namna watumishi wa serikali wanavyotumia nyadhifa zao kuwakandamiza na kuwapora haki zao wananchi wanyonge wasio na pa kukimbilia,manung’uniko ya wazi yameonekana na ni ukweli usio na shaka kuwa uwezo wa CCM kutatua kero za wananchi ni ama haupo au ni mdogo sana usio na tija na hautoi nafasi kwa wananchi kuendelea kukiamini tena chama hiki, na wazi wazi wananchi wamewaambia hadharani kuwa CCM YA SASA SI ILE YA WAKULIMA NA WAFANYAKAZI. Haisimamii wala kuwakilisha maslahi mapana ya wakulima na wafanyakazi wa nchi hii bali ni kuwakandamiza na kuwaibia.

bungeni wana maji ya kurusha rusha na kumwangika pembezoni lakini wananchi hawana hata maji ya kupigia mswaki wachilia mbali kupikia na kuoga miaka 50 ya ccm na maendeleo ya domo tupu. 
KINANA amesikika katika maeneo mbali mbali akikiri hadharani kuwa ni kweli CCM IMEWAKOSEA WANAINCHI KUPITIA WATENDAJI wake na anaomba Watanganyika na Wazanzibari atii waisamehe CCM anachekesha kweli miaka 50 swali watawalipa vipi wananchi miaka yao 50 iliyo pita....??, pia atii anasema kwamba CCM itajirekebisha huyu jama anachekesha sana. Wanaohudhuria mikutano na wanaoitazama kupitia vyombo vya habari wanashikwa na bumbuwazi kuwa hivi kinachosemwa kina mantiki ipi....? Haiingii akilini hata siku moja chama kinachounda serikali iliyoshindwa kutimiza matakwa ya umma kirudi kwa umma kuuomba msamaha kana kwamba umma huo hauna chaguo jingine.....??

Wananchi wanapata majibu sasa kuwa kumbe mgomvi wao siku zote si watumishi wa serikali bali ni CCM na serikali yake maana ndiyo iliyowatelekeza kwa kipindi chote hichi cha miaka 50 hadi wanadhulumiwa ardhi zao,machimbo yao,haki zao,mifugo yao,umeme wao,maji yao,hospitali hakuna kwa wanyonge,mtoto wa nyonge hawezi kumaliza elimu ya juu na akimaliza hapewi kazi n.k. huku viongozi wakiunda utatu mtakatifu na wenyefedha na wawekezaji na kuwaacha wao wakiteseka na kuhangaika bila majawabu kwa matatizo yanayowakumba. Leo hii miezi mitatu kabla ya uchaguzi Msanii kinana anasimama hadharani na kuomba radhi etii wananchi wawasamehe na hawatarudia tena hahahahaha. Kinana na CCM wanapaswa kujua kuwa legitimacy ya kuongoza inatoka kwa wananchi wote,na kwa kuwa CCM iliwakumbatia matajiri na kuwaacha wanyonge huku wakiamini hawataamka,leo wameamshwa na wanajua nani ni mchawi wao,hivyo kwa CCM kukumbuka shuka kukiwa kumekucha ni kuendelea kujianika mapungufu yake na kupigilia msumari kwenye jeneza.

Kama unavyo waona wamefurahi kabisa wakati wananchi wanahaha kutafuta mlo moja tu wa siku wana kazi gani viongozi kama hawa....??? wananchi hawana hata maji ya kupigia mswaki wachilia mbali kupikia na kuoga miaka 50 ya CCM na maendeleo ya domo tupu. 
Naishauri CCM iache kuwahadaa Watanganyika na Wazanzibari maana wameshasema imetosha,kuwarubuni na ahadi mpya ya kuwapa ardhi zao, mashamba yao,mali zao ni kuwakoga na kuwadhihaki na tunaomba kama kweli kinana anajua anachokisema basi na atoke hadharani awaombe Watanganyika na Wazanzibari wote msamaha kwa dhiki na taabu walizozipata kwa miaka 50 kwa matendo hasi yake na viongozi wote mafisadi na wahafidhina , asimame na atangazie umma wote kuwa CCM imechoka,imekosa na isamehewe kwa yote na kila fisadi n wahafidhina walio hujumu nchi hizi mbili watapelekwa jela ya segerea na mali walizo ibaa zote zitarudishwa ili zijenge nchi hizi mbili ya Zanzibar na Tanganyika laa kama sivyo kaene msubiri kabla kutupwa kapuni mwezi oktoba.

Muonekano wa ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa Giningi Dodoma unao jengwa na chama cha Mapinduzi.  wananchi hawana hata maji ya kupigia mswaki wachilia mbali kupikia na kuoga miaka 50 ya ccm na maendeleo ya domo tupu.

maisha bora ya ccm walio wapa wananchi kwa miaka 50 na ushaiya ndio haya rimzi za matairi ya gari ndio majiko ya kupikia chakula 2015.

CCM IMESHINDWA KUHUDUMU,IMESHINDWA KUWASEMEA WAKULIMA NA WAFANYAKAZI,WAKWIZI NA WACHUKUZI,MASKINI NA MALBINO,KIMEKUWA KIMBILIO LA WANYONYAJI NA WASAKA UTAJIRI WA HARAKA,MAFISADI NA WAHADHINA NI LAZIMA CCM IPISHE WENGINE WASHIKE NAFASI BADALA YA KUOMBA MSAMAHA KANA KWAMBA BILA CCM MAISHA HAYATOKUWAPO. ZANZIBAR NA TANGANYIKA BILA CCM INAWEZEKANA NA TANGANYIKA BILA KINANA INAWEZEKANA ZANZIBAR BILA YA ALI VUAI INAWEZEKANA.

KILA MZANZIBARI ATAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

No comments:

Post a Comment