Sunday, June 14, 2015

MAALIM SEIF SHARIFF HAMAD PEMBA NCHINI ZANZIBAR VIJANA MUKISHA PIGA KURA HAKUNA KULALA WALA KURUDI NYUMBANI LINDENI USHINDI WENU. ((MAALIM AULIZA TANGANYIKA HAIWEZI KWENDA BILA ZANZIBAR...KWANI KUNA NINI HAPA...??))

Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad mara baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa Pemba kwa ajili ya mkutano wa hadhara kumtambulisha rasmi kuwa mgombea Urais wa Zanzibar kupitia chama hicho
Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Shariff Hamad mara baada ya kuwasili uwanja wa ndege pemba nchini Zanzibar kwa ajili ya mkutano wa hadhara kumtambulisha rasmi kuwa mgombea Uraisi wa nchi ya Zanzibar kupitia Chama Cha CUF.

Nchini Zanzibar kisiwani Pemba/Dar. Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Shariff Hamad ameitaka CCM kujiandaa kisaikolojia kukabidhi madaraka kwa chama chake baada ya Oktoba, akisema katika chama chake hakutakuwa na neno “kushindwa”. Maalim Seif Shariff Hamad, ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa nchi ya Zanzibar, aliwataka vijana popote walipo kujiandikisha kwa ajili ya uchaguzi ili kujitayarisha na ushindi aliouita mkubwa. Alitoa kauli hiyo katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Viwanja vya Tibirinzi, Chake Chake Pemba nchini Zanzibar na kuhudhuriwa na maelfu ya wafuasi wa chama hicho kikuu cha upinzani humo nchini Zanzibar.
Wafuasi wa CUF wakinadi picha za mgombea Urais wa Chama hicho Visiwani,  Seif Shariff Hamad katika mkutano wa hadhara wa kumtambulisha  mgombea huyo uliofanyika kwenye  Viwanja vya Tibilinzi- Chake chake Pemba jana. “Hakuna kushindwa CUF, kwa hivyo mawazo yenu yawe na kushinda tu. Vijana, hakuna kukaa ukasema ushamaliza kupiga kura, unakwenda kwako unasubiri ushindi. Hakuna hilo mwaka huu, lazima mjitahidi kulinda ushindi wenu,” alisema Maalim Seif Shariff Hamad. Katibu huyo wa CUF alisema wananchi wa Pemba walioko Arusha, Mwanza na sehemu nyingine warudi kujiandikisha kwenye Daftari la Wapigakura na kuwataka kutoacha fursa hiyo ambayo ni haki yao ya kidemokrasia. Akitilia mkazo suala hilo, aliyekuwa waziri wa SMZ, Mansoor Yussuf Himid Jeneral alimtaka Maalim Seif Shariff Hamad baada ya kupiga kura yake kurudi nyumbani na kuwaachia vijana kumkabidhi ushindi wa chama hicho. Mansoor Yussuf Himid Jeneral ambaye ni mshauri wa Maalim Seif Shariff Hamad, alisema vijana wasitarajie kuletewa ushindi katika kisahani cha chai, washiriki kikamilifu katika kupatikana ushindi wa chama hicho.Wanachama na wafuasi wa cuf wakiwa wamebeba mabango yenye picha za Maalim Seif wakati wa mkutano wa hadhara kumtambulisha mgombea wa CUF, katika nafasi ya Urais wa Zanzibar, Maalim Seif huko uwanja wa Tibirinzi, Chakechake PembaMansoor Yussuf Himid Jenerel alisema hatima ya ushindi wa Zanzibar ipo mikononi mwa vijana, hivyo wanapaswa kuhakikisha ushindi wa Zanzibar unapatikana katika mikono yao. Akihutubia mkutano huo, Mwanasiasa Hassan Nassor Moyo alisema kazi ya Maalim Seif na aliyekuwa Rais wa Zanzibar, Amani Abeid Karume kuleta umoja wa kitaifa si jambo jipya kwa kuwa lilianzia kwa Mzee Karume ambaye alitunga sheria kuondosha ubaguzi na kuwaweka wananchi wote wa Zanzibar kuwa kitu kimoja. Katika hotuba yake ya takriban saa moja iliyorushwa moja kwa moja na kituo cha televisheni cha Star TV, Maalim Seif Shariff Hamad alisisitiza nia yake ya kuifanya Zanzibar kuwa na mamlaka kamili ili iondokane na adhabu ambazo siyo stahiki kwake.Wanachama wa CUF wakiandamana katika mitaa ya Chakechake Pemba wakimsindikiza mgombea Urais wa chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad baada ya kuwasili Pemba. Picha: Salmin Said Wananchi wa Chama Cha CUF wakitembea kwa furaha katika nchi yao ya Zanzibar huko Pemba katika mitaa ya ChakeChake huko Pemba huku wakimsindikiza kwa furaha na amani na utulivu Mgombea Uraisi wao, Maalim Seif Shariff Hamad baada ya kuwasili Pemba nchini Zanzibar.
Maalim Seif Shariff Hamad alisema Wazanzibari wamekuwa wakiadhibiwa kutokana na ufisadi unaofanywa na baadhi ya viongozi wa Tanganyika kutoka Bara. “…Leo watu wanafanya ufisadi huko, tunanyimwa fedha na wahisani halafu sisi ndiyo tunaadhibiwa kwa makosa ambayo siyo ya kwetu. Hatuwezi kukubali,” alisema Maalim Seif Shariff Hamad na kusisitiza kuwa hali hiyo imesababisha bidhaa kupanda bei na kuwaumiza zaidi Wazanzibari. “Zanzibar haina mamlaka kwenye nchi nyingine, hatuwezi kufungua ubalozi kwenye nchi nyingine. Hatuwezi kusaini mkataba na nchi yoyote, hatuna maamuzi juu ya sera, hatuna sera za kiuchumi. Sera zote zinatungwa Dar es Salaam… hii siyo sawa,” alisema Maalim Seif Shariff Hamad.
“Leo tukizungumzia suala la gawio tunapata asilimia 4.5 badala ya asilimia 11.5…ndiyo maana nasema Muungano uliopo hautusaidii. Tutapata kufaidika pale tutakapo pata mamlaka kamili. Zanzibar iwe na mamlaka yake na Tanganyika iwe na mamlaka yake. Halafu tukae pamoja tuangalie pale tunapoweza kushirikiana tushirikiane. “Kwani Tanganyika haiwezi kwenda bila Zanzibar… kwani kuna nini hapa.......?????,” alihoji Maalim Seif Shariff Hamad huku akishangiliwa na umati wa watu waliohudhuria mkutano huo. “Eti wanaokuja Zanzibar kutafuta wadhamini wanasema watawadhibiti wanaovuruga Muungano. Watawadhibiti hao CCM wenzao siyo sisi… tunataka uhuru wetu. Tunataka tupate mamlaka kamili.”
Maalim Seif Shariff Hamad, ambaye alikuwa na furaha kubwa kuwa ameteuliwa kwa mara ya tano kuwania urais kuwa anaaminika, alisema mpango wake ni kuboresha Bandari ya Zanzibar ndani ya mwaka mmoja na kuitangaza kuwa huru. Alisema atahakikisha Zanzibar inakuwa na viwanja viwili vya kimataifa vya ndege. Alisema ushindi wa chama hicho utakuja na mabadiliko ya kiuchumi yatakayowezesha kuimarishwa bandari huru katika kisiwa cha Pemba katika maeneo ya Mkoani na Wete akifafanua kuwa Pemba imekosa maendeleo tangu wakati wa ukoloni hivyo kuna haja ya kuimarishwa kiuchumi na kuendelezwa ili vijana waweze kufaidika na matunda ya nchi yao kwa kupatiwa ajira. “Maalim Seif Shariff Hamad alisema ni Lazima tuwe na meli za kisasa za kasi ili kuimarisha usafiri na miundombinu kuwawezesha wananchi kuvusha biashara zao, alisema Maalim Seif Shariff Hamad ambaye safari hii anawania urais wa nchi ya Zanzibar. Katika mkutano huo wanachama 400 walichukua kadi za Chama Cha CUF baada ya kuhama kutoka ADC.
KILA MZANZIBARI ATAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

No comments:

Post a Comment